Makapuku Forum

Makapuku Forum

1 Nalimngoja Bwana kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.
Zaburi 40 :1

2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.
Zaburi 40 :2

3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumaini Bwana
Zaburi 40 :3

4 Heri aliyemfanya Bwana kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
Zaburi 40 :4

5 Ee Bwana, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Zaburi 40 :5

6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
Zaburi 40 :6

7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)
Zaburi 40 :7

8 Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Zaburi 40 :8
 
MUHUBIRI 12;1 1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.‍♂‍♂

Sifa na utukufu ni Mungu wetu aliyejuu tunasema Asante kwa kutuamsha salama si kama sisi ni wema Sana Bali ni upendo wako tu utulinde,utuongoze na kutuekimisha tuwapo barabarani, mashuleni na maofisini simama nasi teta nasi utusamehe tulipoenda kinyume na wewe kwa mawazo maneno matendo na kutotimiza wajibu tunaomba baraka zako tuanze na Bwana tumalize na Bwana siku iliyonjema sana kwetu wabariki

Wabariki yatima,wajane,na wasiojiweza ukawe faraja kwao ukawe nao muda wote maana wewe ni faraja ya kweli na uzima Wewe ni Alfa na omega tuna imani tupo mikononi mwako kuanzia sasa Ameen
Amen

Ubarikiwe dadake na mimi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom