Makapuku Forum

Makapuku Forum

4698e73a86515976b50aef48b6c70635.jpg
 
"Don't correct the correct corrections corrected by the correct corrector because the correct corrections corrected by the correct corrector are correct"

"Usiyasahihishe masahihisho sahihi yaliyosahihishwa na msahihishaji sahihi kwa sababu masahihisho sahihi yaliyosahihishwa na msahihishaji sahihi ni sahihi"
 


Stay true to yourself. You are not what people think or say you are.

You are not other people's opinion. You are you! And you owe your life to you. So, stop trying to please everybody with your life. That is dangerous.

You can't please everybody unless you have nothing to stand for. The truth is some people don't even care what is happening to you.

Look, the day you were formed, none of these people was close by; God didn't seek anybody's approval before He molded you. They don't know your past; they don't even know how you came this way! And they can never understand you.

Be yourself because, life is too short to waste it living someone else's life. You can do it.

I BELIEVE IN YOU!

Good morning &
Have a Great day!


 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 29

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"unawekaje michaneli yako na wakati mi naangalia chereko chereko, Ebu yoa ITV yako niwekee send off zangu niangalie mimi..... Afu kesho hakuna kwenda kazini,... Kesho ni sherehe ya mtoto wetu kufikisha miezi miwili tumboni"
Sheby alimuangalia sana huyu mwanamke na asimpatie jibu.. Sasa sheby kuna CD alikuja nayo kutoka kazini, aliinunua mida ya mchana hivi sasa aliiweka kwenye gari sasa alipofika nyumbani akaitupia mezani
"hiii ni cd gani.. Ya Bongo movie au ni ngumi zako tu"
Mwai aliongea hivyo huku akiichukuwa hio cd na kuifungua kava ili atoe ile cd yenyewe,... Lakini sasa ile anafungua tu, kuna karatasi ilidondoka mezani, kana kwamba ilikuwa ndani ya lile kava....
Sheby nae alishangaa mana aliponunua hio cd alifungua na hakukuwa na karatasi, yeyote sasa nani kaweka hio karatasi.. Lakini sheby hakuwa na wasiwasi sana kana kwamba huenda ni karatasi ya maelezo ya hio cd....
"heeeee cd za siku hizi zina maelezo"
Aliongea mwai huku akiifungua ile karatasi
"mbona una Kiherehere we mwanamke, kwani nimekuletea wewe hio cd
"hata kama, kwani si umeiingiza ndani... Haaaaaaaaaa"
Sasa ghafla mwai anastuka kwa kusoma hio karatasi, hata sheby akapatwa na wasiwasi juu ya karatasi hio....
"ina mana kumbe ulikuwa unatafuta mke mwingine???"
Sheby alishtuka kuskia mwai kasema hivyo,..

ENDELEA........

Katika maisha unaweza kufanya kitu bila kujua kuwa kinaweza kumuathiri mtu mwingine, kumbuka unapofanya jambo angalia na mbele kutakuja kutokea nini,... Kijana sheby mchana wa leo aliingia katika Library ya kuuza CD ili ile siku ya sherehe ambayo ni kwsho awe ndani tu anaangalia zake muvi, mana hajaipenda na hatamani kuhudhuria,.. Sheby alinunua cd moja iliomvutia sana iitwayo THE BEST WIFE... Aliiweka kwenye gari yake kisha huyo kaelekea kwenye mizunguko yake,... Sasa muda huu ndio anashangaa kumsikia mke wake anasema mambo ya kutafuta mke mwingine,..
"ina mana kumbe ulikuwa unatafuta mke mwingine???"
Sheby alishtuka kuskia mwai kasema hivyo, mana kwake analifanya kama siri na hataki hata wazazi wake wajue kama anatafuta mke mwingine, ili siku akimbwaga mwai aje mwingine,...
"we umeikuta wapi hio karatasi"
"si huku ndani ya cd uliokuja nayo"
"yaani umekosa cha kuniongelesha sasa umeona uandike upumbavu wako afu ujifanye ilikuwa kwenye cd"
Aliongea kijana sheby huku akiwa na hasira mno,
"heeeeeeee ina maana mimi ndio nimeandika hivi"
"hebu lete hio karatasi"
Sheby aliichukua ile karatasi tena kwa kumpokonya mwai,... lakini sasa sheby anazidi kushangaa mbona mwai siku hizi kapunguza ukali, yaani ni tofauti na mwanzoni mwa ndoa yao mana kuna muda sheby anashikwa tai kabisa na kutaka kupigwa, lakini sasa hivi ukali umepungua,... Sasa sheby kuangalia ule muandiko ulioandikwa pale, ni muandiko anaoufahamu kabisaa...
"ina maana yeye ndio kaandika hivi,.. Na nilimpakia lini"
Sheby alikua anajiuliza huyo myu alimpakia lini mana hajawahi kumpakia kwenye gari hio
"zaituni nilimpakia lini mungu wangu, mana huu ni muandiko wake kabisa huuu... Au ni huyo demu wa saidi ndio mwenye muandika kama wa zaituni"
Sheby alizidi kujiuliza sana kimoyomoyo na wakati huo mwai ndio anaondoka kwenda kulala zake mana siku hizi kapunguza ukali na alijua tu huo ujumbe huenda haujui na ndio mana kaacha, na pia mpaka hapo sio tabia yake, kapunguza sana tu.... Sheby alijua kabisa huo ujumbe haukuwa ukimuusu yeye japo hata yeye anatafuta mke mwingine... Ujumbe uliandikwa hivi...

SAWA NASHUKURU KWA KUNIFANYIA HIVYO,... KWANZA SIAMINI KAMA UNA MKE... ILA NISAMEHE SANA MANA HUENDA NIMEKUPOTEZEA MUDA NA PESA ZAKO,... HATA MIMI NILIKUWA NAKUPENDA SANA, ILA TAMAA YA MAISHA... BINAFSI NI KWAMBA TAYARI NIMEKUKOSA,.. LAKINI NAKUOMBEA KWA MUNGU UPATE HUYO MKE WA PILI,... MANA SIAMINI KAMA NINGELIKUJA KUWA MKE WA PILI.... SAMAHANI SANA, NAJUTA KUKUHISI FUKARA.... NAKUOMBEA UPATE MKE MWENYE HESHIMA KULIKO MIMI,.. NA PIA NAOMBA UENDELEE KUUZA VIAZI ILI UPATE MKE BORA... AHSANTE SANA.... NAKUTAKIA BAHATI NJEMA

Sasa sheby ndio kajua sababu ya mke wake kuachana na ujumbe huo ni kwasababu ya pale aliposema, usiache kuuza viazi ili upate mke bora.... Mwai akajua hio sms wala haimuusu mana sheby sio muuza viazi, lakini sasa sheby kajua fika huo ujumbe unamuusu yeye, sema alikuwa anazuga zuga tu... Ila kichwa chake kinatafakari sana, je huyu zai kapanda lini gari yake? Kila akifikiria juu ya zaituni kupanda gari yake hapati picha kabisa.... Sheby aliangalia simu yake haoni, akajua kaiacha chumbani,.. Aliamka na kwenda chumbani,... Alipofika alimkuta mke wake anachati Instagram yupo na laptop yake,.. Sheby kaka kwenye kitanda chake na kumpigia saidi...
"oya saidi vp hali"
"safi boss, vp saa hizi kuna nini tena"
Saidi alipata hofu baada ya kuona simu ya boss mdogo usiku...
"ivi mke ulioenda kutambulishwa kwao anaitwa nani"
"hahahahahaha, mtoto wa Kiislamu mtoto anaitwa zaituni"
Sheby alishtuka lakini hakuonyesha kama kashtuka... Ila akatumia maneno ya kawaida ya kumchombeza saidi ili atume picha ya huyo zaituni
"waapi wewe usikute umeoa kimbaumbau hana hata nyama"
"aaahhhh weweeee, boss ivi mi unanionaje vile... Ngoja nikuonyeshe mtoto,.. Nilimpiga picha akiwa kwenye vazi la kimjini mjini"
Sheby hivyo ndivyo alivyotaka picha itumwe na ni kweli inatumwa... Sheby kwa uchokozi akamchokoza mke wake mana siku izi kapunguza ukali
"vipi umeujua huo ujumbe ni wa nani, mana umeniacha ghafla tu"
"niliposoma tu neno usiache kuuza viazi nikajua sio wewe wala haikuusu hio"
Ghafla simu ya sheby ikaingia meseji, kuangalia alikuwa ni saidi kamtumia picha.... Laaaaa Haulaaaa alikuwa ni zaituni kweli, tena mtoto alivaa tishet kubwaa zile za kike ambayo imefika mpaka mapajani, tena ilikuwa imembana, hivyo umbo lake lote unaliona kwa ramani tu ya ile tishet mana ilimchora haswa,... Sheby alishikwa na hasira sana, yaani kumbe saidi ndio katongoza demu ambaye sheby alimtazamia kuwa mke, ila kwa mapepe ya mwanamke huyo ikashindikana,...

BAADA YA USIKU HUO KUPITA

Na leo ni asubuhi sheby akiwa anajiandaa kwenda kazini
"hee hee hee, unakwenda wapi"
Aliongea mwai huku akiwa kasimama mlangoni,...
"ina maana nikae nyumbani kama wewe si ndio eee"
"ina maana hii sherehe ya mtoto wetu haikuusu"
"mtoto wenu na nani"
"jamani, kwaio mimi nimejitia mimba mwenyewe si ndio"
"jiulize mwenyewe usiniulize mimi"
"sasa hutoki hapa, na ninapiga simu kwa baba mkwe"
Sheby kiskia simu inapigwa ikabidi awe mpole, mana baba yake sheby akiskia mwai katutuluguswa na sheby, kinachofata kwa sheby ni kufokewa bila sababu za msingi... Hivyo sheby akawa mpoleee,...

Watu walizidi kuingia katika jumba hilo lenye uwanja mkubwa sana,... Mwai alikuwa akikaribisha wageni, chakula chenyewe hakipikiwi hapo chakula kinaletwa spesho kwa ajili ya watu kula... Sheby kwakuwa kazuiwa kwenda kazini hivyo alitoka kidogo nje, wakati huo inaendea mchana, na jukwaa linapambwa, na hio yote ni sifa ya mke wake, sasa kama mimba tu ni hivi, je akizaliwa itakuwaje??... Watu walizidi kumiminika kutoka sehemu mbali mbali walizoalikwa kwa sherehe hio, wengine walibeba zawadi nyingi sana, kama unavyojua mambo ya mjini ni kujishebedua tu... Wakati huo wamama wa uswahilini walikiwa wakicheza muziki taratibu kabisa.... Sasa sheby kutembea kwake alifika mpaka barabarani, alikutana na vilema wengi sana, mana toka ahamie kwenye huo mtaa hajawahi kuuzunguukia na kujua hata majirani, yeye na gari gari na yeye..... Vaa yake tu iliwajulisha wale vilema kiwa huyu ni mtu mwenye wadhifa fulani katika hii dunia....
"seidia ndugu yangu"
Aliongea maskini mmoja aliokuwa hana hata vidole,... Sheby ana huruma sana na watu hao, akiangalia wamama wenye watoto juani,.. Watoto wanalia kwa jua kali
"kwanini msitafuta mahali kwenye kivuli"
Aliongea sheby huku akiwa kainama ili kwenda sambamba na wao,..
"baba, sasa tukikaa kwenye kivuli, nani atatuseidia"
Sheby alitamani hata kulia mana kila kilema hapo ana matatizo yake,..... "Hakuna shida, nitawaseidia ila kwanza mkapate chakula kwanza"
"wapi baba"
"hapo nyumbani kwangu kuna sherehe, na kuna chakula kingi tu kwanini msiende kula"
"ni mbali?"
"wala, ni hapo tu"
Ghafla kuna wengine wakatoa kauli ya kwamba
"na sisi vipofu tutapajuaje baba, tuna njaa"
Aliongea mwanamke mmoja wa makamo, sheby alishindwa kuvumilia, vimachozi vilimtoka kwa kiasi fulani..
"ninyi ambao mnaona mtawaseidia wenzenu kuwashika hata mikono sawa,... Afu mimi nakwenda huku juu nikirudi mmeshakula nawapa pesa kila mmoja pesa yake sawa"
"sawa kijana Tunashukuru sana baba"
Waliongea hivyo huku wakitaka kujiandaa kwenda kula katika nyumba ya sheby ambako kuna sherehe ya kukua kwa mimba ya mwai,.. Sasa ile sheby anataka kuondoka aliona gari ya saidi ikiwa inakuja huku alipo sheby,...
"huyu saidi kaambiwa na nani kiwa nina sherehe huku kwangu"
Aliongea hivyo huku akiwa karibu na wale omba omba.... Sasa wale omba omba walipoona gari wakaamka na kuanza kuomba, vipofu nao waliomba kwa kusikia sauti ya gari,.. Vilema walijikongoja mpaka kwenye gari, lakini sasa cha ajabu na cha kishangaza sheby alishangaa kuona vioo vya gari vinafungwa kabla hajafika eneo la omba omba... Sheby alikasirika sana yaani saidi leo ni wa kufunga vioo vya gari..... Lakini sasa kadri gari inavyozidi kusogea sheby ndio anazidi kumuona dereva.... Laaa haulaaa kumbe hakuwa saidi,.. Dereva alikuwa ni zaituni, sheby haamini macho yake leo anamuona zaituni, mana ni miezi miwili hajawahi kumuona ila leo anamuona tena akiwa na gari ya saidi... Sasa zai kutahamaki mbele anamuona sheby kasimama mbele ya omba omba, tena akiwa kavalia mavazi yake ya kitajiri.....
"haaaaaaaaaaaa.... Huyu ni sheby au macho yangu"
Aliongea zai na kushika breki ya ghafla,.... Zai yeye aliambiwa tu kiwa sheby ni tajiri mkubwa, lakini hajawahi kumuona kwa macho yake akiwa kwenye hali hio, sasa leo ndio anamuona live bila chenga... Yeye sheby hajashtuka kumuona zai,... Sasa zai aliposhika breki, omba omba nao wakajua kasimama kwa ajili yao,.. Sasa wakalizunguka gari ya zaituni na kuanza kuomba, lakini zai macho yake yalikuwa kwa sheby tu... Sheby yeye alikuwa anatabasamu tu muda wote toka alipomuona zaituni..
"ivi huyu ndio yule muuza viazi kweli??? Siamini macho yangu.... Sasa nitamwambia nini sheby mimi... Naona hata aibu kushuka kwenye gari..."
Zaituni alitamani kuondoka lakini alishindwa kwasababu mbele kulikuwa na omba omba.... Alipiga honi ili watoke lakini wapi, yaani walikuwa kama wametumwa vile
"piiiiiiiii piiiiiiiii... Piiiiiiiii..... Piiiiiiii"
Omba omba waliokaa mbele walikuwa ni wale viziwi na mabubu kabisaa, hivyo hawakiwa wakiisikia honi... Waliosikia honi waliondoka lakini ambao hawajasikia waliendelea kukaa mbele ya gari kwa kidhani kuwa boss huyo angeshuka na kuwapatia chochote kitakachokidhi mahitaji yao ya kimaisha....
Huezi amini kijana sheby alikuwa analia kabisa... Hali aliomkuta nayo zai, leo ni mtu wa kupiga honi ili omba omba waondoke,.... Na hoa masikini walijua gari imesimama kwa ajilo yao kumbe ilisimama kwa ajili ya sheby.... Sasa zai baada ya kuona kuna ambao hawaondoki mbele ya gari yake.... Zaituni aliamua ku

Je? Nini kilitokea hapo.... Zaituni atashuka au ataondoka... Na sheby atamwambia nini zaituni... Na zai atajibu nini pale atakapoulizwa na sheby?
 
"Don't correct the correct corrections corrected by the correct corrector because the correct corrections corrected by the correct corrector are correct"

"Usiyasahihishe masahihisho sahihi yaliyosahihishwa na msahihishaji sahihi kwa sababu masahihisho sahihi yaliyosahihishwa na msahihishaji sahihi ni sahihi"
What a word .....my qoute of a day
 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 30

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsA

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

Yeye sheby hajashtuka kumuona zai,... Sasa zai aliposhika breki, omba omba nao wakajua kasimama kwa ajili yao,.. Sasa wakalizunguka gari ya zaituni na kuanza kuomba, lakini zai macho yake yalikuwa kwa sheby tu... Sheby yeye alikuwa anatabasamu tu muda wote toka alipomuona zaituni..
"ivi huyu ndio yule muuza viazi kweli??? Siamini macho yangu.... Sasa nitamwambia nini sheby mimi... Naona hata aibu kushuka kwenye gari..."
Zaituni alitamani kuondoka lakini alishindwa kwasababu mbele kulikuwa na omba omba.... Alipiga honi ili watoke lakini wapi, yaani walikuwa kama wametumwa vile
"piiiiiiiii piiiiiiiii... Piiiiiiiii..... Piiiiiiii"
Omba omba waliokaa mbele walikuwa ni wale viziwi na mabubu kabisaa, hivyo hawakiwa wakiisikia honi... Waliosikia honi waliondoka lakini ambao hawajasikia waliendelea kukaa mbele ya gari kwa kidhani kuwa boss huyo angeshuka na kuwapatia chochote kitakachokidhi mahitaji yao ya kimaisha....
Huezi amini kijana sheby alikuwa analia kabisa... Hali aliomkuta nayo zai, leo ni mtu wa kupiga honi ili omba omba waondoke,.... Na hao masikini walijua gari imesimama kwa ajilo yao kumbe ilisimama kwa ajili ya sheby.... Sasa zai baada ya kuona kuna ambao hawaondoki mbele ya gari yake.... Zaituni aliamua ku

ENDELEA........

Wakati huo huku nyumbani kwa sheby sherehe zilikuwa zikizidi kupamba moto,... Watu walikuwa wanazidi kumiminika tena watoto wa kitajiri walikuwa ni wengi mno,... Mana mke wa sheby ni mtu anaependa sifa sifa sana hivyo hata waalikwa wake ni watu wenye uwezo na wanaoweza kutoa mchango fulani juu ya sherehe hizo.... Siku ya leo akina rose na mary nao walifanikiwa kufika katika sherehe hizo japo wao walikosa kwenye harusi lakini kwenye sherehe hawakuwa nyuma kabisa,... Mana leo kampuni ya akina sheby imefungwa kwa siku hio mana wazazi wote wapo kwenye sherehe, wamama wakwe nao wapo ndani ya nyumba, uzuri wa nyumba za kitajiri zina nafasi kubwa sana inayoweza kuingiza hata watu 100 mpaka 200,...yaani ni sehemu kubwa kiujumla na imefanikiwa kuingiza waalikwa karibia wote..
"we mumeo yupo wapi"
Aliuliza mama mkwe ambae ni mama yake mwai,
"katoka tu sjui kaelekea wapi"
"au kaenda kazini"
"no, katoka na track na sendo yaani ni kama mtu aliokuwa anaangalia madhingira"
"mumeo nae aahh, sasa wageni ndio hao"

Wakati huo huku barabarani tunamwona sheby akiwa na omba omba wake,... Muda huo zai yupo ndani ya gari akiwa anapiga honi ili kiwaondoa omba omba wale... Na hao masikini walijua gari imesimama kwa ajilo yao kumbe ilisimama kwa ajili ya sheby.... Sasa zai baada ya kuona kuna ambao hawaondoki mbele ya gari yake.... Zaituni aliamua kushuka kwenye gari, kila maskini aliongea maneno yake
"saidia dada,.... Seidia mama.... Mama tuseidie maskini"
Huezi amini zai kabadirika kwa kiasi kikubwa sana,.. Na hajui kama alishayapitia maisha hayo,..
"sina jamani heeee.... Kwani kutoa lazima nyie vipi??... Ebu sogeeni uko"
Sheby kuskia hivyo roho ilimuuma sana, haamini kama zai ndio anaetoa maneno yote hayo....
"zai... Zai... Ivi ni wewe zai ninaekujua au mnafanana tu"
"najua nilipotoka lakini sina"
"siamini kama ni wewe... Ivi kumbe nilikuwa nioe shetani kiasi hiki"
Sheby aliingea kwa hasira huku akiwa kasimama vile vile bila hata ya kumsogelea zai...
"tuanchane na hayo, nina maongezi na wewe"
Aliongea zaituni huku akimtaka sheby apande kwenye gari waondoke, sheby aliwaangalia sana wale binaadamu waliokuwa wanaomba pesa za kujikimu maisha yao
"kwahio umekosa hata elfu 20 ya kuwapa hawa watu"
"sasa kama sina mie nifanyeje, au nivue nguo wanifanye ili waridhike"
"sijakwambia uvue nguo... "
"ok nimekuelewa, i Know unapenda kuseidia watu na ndio mana hata mimi ni mmoja kati ya watu uliowaseidia, ila naomba tuongee kwenye gari"
Sheby hakutaka kukataa kuingia kwenye gari, mana hata yeye ana maswali ya kumuuliza kwanini aandike ujumbe wake na kuuweka kwenye cd...
Sheby alipanda kwenye gari hilo huku akitoa shingo na kusema
"sasa nyie nendeni mkale kwanza pale kwangu kisha nitakuja kiwatoa kibingwa"
"sawa sawa mkuu... Ila kama huyo ni mke hafai"
Maneno hayo yalimfanya zaituni atake kushuka na kuwatukana,...
"tulia basi hasira za nini?... Au wamekosea waliposema hivyo"
"sheby, naomba tueshimiane na hawa omba omba wako"
"wewe mbona ulikuwa omba omba, ivi hujui kuwa ulikuwa unaudhi watu"
Zaituni aliondoa gari eneo hilo lakini alikuwa na hasira sana.... Walikwenda umbali wa kama kilometa tatu hivi kwenye uwanja wa mpira, kisha zaituni akasimamisha gari na kutoka nje, na sheby nae akatoka nje...
"mimi sina maneno mengi na wewe... Ila nilitaka kujua tu kwanini ulikuwa na nia ya kunioa na wakati una mke"
Aliongea zaituni huku akiwa na mapozi ya ajabu ajabu.. Yaani ndani ya miezi miwili tu zai kawa mwanamke wa tofauti sana....
"mwanamke nilienae nilichaguliwa na wazazi wangu,... Kiufupi ni kwamba sikumpenda na simpendi mpaka leo... Nia yangu ni kuoa mwingine ninaempenda katika maisha hayo... Lakini kutokana na wasichana wa siku hizi mlivyo na akili mbovu,... Mnashindwa kujua ni mwanaume yupi mwenye uwezo wa kukuoa wewe... Kwa miaka ya hivi karibu wasichana wengi walibadirika na kupenda kuolewa na wanaume wachapa kazi, yaani ajulikane tu ana uwezo wa kuacha kodi ya meza.. Lakini wasichana wa sasa hivi, mnapenda pesa sana.... Tamaa ndio imekuponza zai.. Na ndio mana nikawaza kufanya hivyo, kuuza viazi ili ujue kuwa nafaa au sifai.. Na vile vile nikamtuma shadi akuchombeze kama utakubaliana na akili yake... Kumbe kweli,.. Unashindwa kumpenda mwanaume anaefanya kazi, ati unaangalia yule alievaa kiatu cha bei ghali... Sasa wewe utakula viatu huko ndani... Zai... Binafsi nilikupenda sana.. Milioni 10 ziliisha juu ya macho yako.. Lakini vyote hivyo huvijui, ulishindwa kufikiria muuza viazi kama huyu kapatia wapi pesa ya kumpeleka mtu nje na kumtibu kisha kumrudisha... Umeshindwa kujiuliza kabisa yani... Ukakubali kufata akili ya shadi, na shadi sio kuwa alikuwa malaya, bali alikuwa spesho kwa kukushawishi wewe, ili nijue mke bora tukiwa katika shida... Kiukweli mpaka sasa bado natafuta mke na sikati tamaa ila sintouza viazi tena... Ila sina hasira saaana, kwasababu anaekuoa ni mfanyakazi wangu, hivyo wacha nifanye kama nimemsaidia tu... Lakini ndani ya miezi hio miwili umebadirika sana zaituni... Badirika sana t.

Sheby aliongea bila hata ya kumeza mate,... Aliongea mengi sana juu maisha alioyataka kuishi na zaituni.. Wakati huo mtoto wa kike kakaa kimya huku machozi yakimlenga lenga,...
"lakini sheby, ulichokifanya wewe sio kizuri, japo kimekuseidia, kwa njia hio hutopata mke kwa karne ya sasa wasichana wengi wanaangalia pesa.. Na kama sio huo mchezo wako wa kuuza viazi, basi nami ningelikuwa mmoja kati ya wake zako..."
"mimi sina kosa... Shida yangu ni kupata jiko bora"
Sheby alikuwa akiongea huku akitabasamu tu, ila wakati huo zai machozi yalikuwa yakimtoka mfululizo...
"ok... Kisicho riziki hakiliki... Ila nakushukuru kwa yote ulioyafanya juu yangu, pamoja na familia yangu... Nakushukuru sana tena sana... Ila kwa kupata mke kwa staili hio hutopata kiukweli.. Jaribu njia nyingine"
Aliongea hivyo zai huku akitamani kulia kwa sauti kubwa........

Kiukweli wanawake wa sasa hivi wamebarikiwa kupewa sura nzuri... Maumbo mazuri,.. Wanavutia vizuri, lakini wamekosewa kupewa staha ile ya kimwanamke... Miaka inazidi kwenda huolewi, unamlaumu mwenyezi Mungu kwanini huolewi,... Hutoolewa kwasababu unataka mwanaume mwenye gari na nyumba nzuri ya kitajiri.. Au mwanaume mwenye uwezo.... Ukiona mwanaume kavaa nguo za gharama kubwa basi unaona pale ndipo penye pesa kumbe mwenzio kaazima au kajipiga kanunua ili akupate kiulaini, mana keshajua unapenda pesa, hivyo nasi tukaa spesho kipesa pesa, tunajipiga tunapata pamba ili tukupate kiulaini mana si unapenda wanaume wasafi wenye pesa, lajini kutafuta hawajui.. Unaenda kuchezewaaaaa, baadae ndio unagundua kumbe mwanaume hana hata hela.. Mnaachana,.. Mkishaachana mwenzio anatafuta mpenda hela mwingine, na watafuta mpenda hela mwingine,... Mnajikuta manachezeana tu... Sasa umri unapoona unazidi kwenda ndio unakumbuka kuolewa hapo una miaka 28 - 30 - 35, eti ndio unakumbuka kuolewa.. Na hapo sasa hakuna kijana mwenye miaka 35 kwenda mbele ambae hajaoa, na hata kama kaoa we bado unakuwa mchepuko tu.... Kiukweli wasichana wa siku hizi wanachezewa sana tena, na mtaishia hivyo hivyo... Mana hata sisi wavulana mmetuzoesha kupenda pesa, hata ukiwa unanipenda kwa dhati mimi nakua sijui mana asilimia kubwa manapenda pesa....

NAOMBA KUTOA USHAURI KWENU KWA WALE MNAOPENDA KUOLEWA

Usxxxxxzhauri wangu ni hivi..... Usitake kuhangaisha kiuno chako buure kukichosha kipapuch chako... Angalia mwanaume wa kukuoa ana vigezo gani.... Vigezo unavyotakiwa kumuangalia kama atafaa kuwa mumeo...

1)...awe na kazi ya kudumu, haijarishi inaingiza kiasi gani.. Hata kama anaingiza 1000 kwa siku, bado una nafasi ya kuishi nae, mana mnazitafuta mkiwa mafukara wote

2)....awe ana uwezo wa kukulisha milo mitatu... Nadhani akiwa na kazi ataweza

3)...anaependa kazi, mchapakazi.. Asie mvivu kutafuta pesa...

4)...usiangalie mavazi, mavazi yanadanganya katika maisha... UMARIDADI HUFICHA UMASIKINI sasa umeona mtu katia jinzi ya elfu 50 ukaona huyo ndio kidume, kumbe utashinda njaa mwenzio ananunua nguo kali kila siku, utafikiri mpiga show...

5)... Kingine na cha mwisho... Usipende mwanaume aliokwisha tafuta pesa zake, mana naye ana tabu yake katika ndoa.. Mana umemkuta na nyumba yake, umemkuta na gari yake, umemkuta na miradi yake... Mwanaume kama huyo usione tu anakufaa, utakuja kujuta na kuona bora ungeolewa na masikini mzitafute wote... Lakini umemkuta Kidume kakamilisha kila kitu, wewe ni kuingia na kuzaa tu.. Afu baada unaachwa eti unataka mali pasu kwa pasu... Na wakati ulizikuta zote.. Akili zenu mbofu mnashindwa kufikiri kwa ukaribu... Mpende fukara wako umwambie ukweli, usimpe papuchi yako mpaka mkatambulishane au muoane kabisa.. Na akikuacha kwasababu hujampa papuchi yako, basi jua huyo hakuwa akikupenda, alikuwa akuinje kisha akuache... Je? Mtaweza kukaza papuchi isiliwe??... Hamuezi ng'oooo
Kikubwa ni kutafuta mwanaume ulimpenda na akupende mtafute pesa mkiwa wote ni mafukara, lakini mmoja akiwa tajiri kuna tabu zitakuwepo ndani ya ndoa... Utajuta kuolewa na tajiri...

Sasa wakati huo sheby akiwa kasimama na zaituni... Na zai alikuwa akilia mana alikuwa awe mume wake lakini kwa tamaa alijikuta anamsahau na kutokumbuka msaada aliompa...
"binafsi mimi nakutakia maisha mema na saidi wako... Ila kuwa makini sana, kama saidi nae utamchezea utakuwa kama dada yako Zainabu"
Aliongea kijana sheby kisha huyoo akaondoka zake.. Hata lile swala la kwanini aliandika ujumbe hakutaka kumuuliza, mana zaituni alikuwa akilia sana.. Na lawama zote alimshakizia shadi, mana ndio aliomshawishi kuingia kwenye ujinga na kumsahau sheby...... Zaituni aliingia katika gari huku akifuta machozi ya uchungu.... Sheby yeye alichukuwa toyo impeleke nyumbani mana walikuja umbali wa kilometa tatu hivi... Sheby alikuwa akiwahi kule nyumbani ili kuiwahi sherehe japo hapendi kuwepo kwenye sherehe hio...

Baada ya dakika kadhaa sheby anakaribia nyumbani kwake, alishangaa kuona wale omba omba wanatolewa nje ya geti tena walikiwa wakifukuzwa haswa.... Sheby alitoa macho kwa kitendo kile kilivyokuwa kikiendelea pale getini kwake.. Kijana alishuka kwenye pikipiki na kwenda mpaka getini kwake, na kukuta baadhi ya vipofu waliokuwa wakisukumwa na wengine wasioweza kutembea walitolewa kama maji taka.....
"heee hawa nao walialikwa na nani hawa laana kum"
 
Zaburi 146

1 Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.

2 Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Ameni barikiwa sana
 
Zaburi 146

1 Haleluya. Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.

2 Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

3 Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.

4 Pumzi yake hutoka, huurudia udongo wake, Siku hiyo mawazo yake yapotea.
Asante mlisha kondoo wa Bwana.....
7114881060f5ce4c2b7fff3da2272daa.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom