Muziki: Tumbo Si Kipimo Cha Furaha
...u khali gani Kapuku mheshimika, mimi niko sawa sana na usawa huu nikisema niko sawa na nimekuwa na siku nzuri basi niamini. Kila wakati napenda kukusalimia maana wewe ni mtu mzuri sana (inawezekana usiwe mzuri wa sura-oh, uzuri wa mtu uko machoni mwa mtu, beauty is relative) na unapendeza kuwa hapa kwa muda wako unaokufaa maana hakuna anayekulipia bando la kuperuse mtandao na hasa kujikita JF. Mimi huwa naingia usiku maana anko wangu huwa anawasha Wi-Fi yake nami napata cha kusemea. Tuna tofautiana ujue.
Leo kwanza kabisa ni siku ya kuzaliwa anko wangu, ngao ya kidonge na ngao ya maji zote ni zile zile usidanganyike na umbo. Anko wangu huyu ni kaka kabisa wa mama sema tabia za anko ni tofauti na za dada yake. Si huwa wanasema mtoto hufuata akili za wajomba basi inaweza kuwa sawa maana kwa ujasiri wa anko wangu ninastahili kuwa jasiri pia. Anko wangu ana ile kitu tunasema 'stomaching facts' unavumilia mengi na mazito ili ufanikiwe. Wengi wetu tunakikosa hiki, tunapenda mikato, 'short cuts'. Wengi wetu tumekuwa watu wa ajabu tunaipima furaha kwa tumbo, jiangalie tumbo lako na ndipo utaipima furaha yako (measuring happiness by the belly).
Muziki sasa, nimesema anko ni mvumilivu na hjipanga sawia ili afanikiwe, tumuige ila sio tuige ile tabia yake kipindi anamfukuzia teller, alikaa anapigwa jua tangu la utosi hadi la kichogo anasubiri mrembo atoke. Aliniambia mvumilivu hula mbivu, kilichoendelea aunt yangu atakuja aseme.