Muziki: Kumbuka Mazuri Utabasamu
Makapuku hiki si kipengele cha siku zote ulichokizoea toka kwangu kuja kwako yaani kama Chakachaka, from me to you. Kipengele chenyewe kitakuja katika muda wake wa kawaida maana mimi kuwahi sijui na kuchelewa sio kwamba sijafika.
Tumeumbwa na hulka moja ambayo si nzuri kiafya ya roho na mwili, mara nyingi huwa tunapenda kukumbuka mambo ya jana na juzi ambayo yalitunyong'onyeza kwa kuwa tu leo na muda huu tumejikwaa kidogo. si wanasemaga majaribu ni mtaji na dhahabu ili iwe dhahabu lazima ipitishwe kwenye moto na kwa msemo wa anko wangu pombe nzuri lazima ichache kwanza na maziwa yakichacha yanakuwa mtindi ambao mimi naupenda sana. Mimi na mtindi na shanga kwa kweli ninapenda hadi natamani kumpa rushwa muadhini anirushe mida ya kuamka.
Muziki huu umeombwa na aunt yangu mnayemfahamu
Shunie ambaye ni mke anayejulikana wa anko wangu. Kwa sasa anapambana ana hali yake na akisikiza muziki huu atatabasamu na kuachana na kulamba ndimu