Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 15

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsAp



Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"vipi mbona simuoni kijana wako"
"yumo ndani humo...... We Sharbiny hebu shuka basi baba"
Mzee rashidi alimwita mtoto wake kwa heshima ya hali ya juu,.. Sheby alishuka na kutoa salamu kwa wote,. Wakati huo walikuwa wanaingia ndani.. Walipofika ndani waliongea mengi sana, lakini ilifikia hatua mke wa mzee Muhammad anamwita mtoto wake..
"mwanaheri,.."
Mama alimwita mtoto wake kwa heshima
"abeee mama"
"njooo mwanangu"
Mwanaheri alikuja huku akiwa kajita

ENDELEA......

Kila mtu alishangaa kwa kuskia sauti ya mama sheby ikisema, baada ya kujua umri wa mschana huyo, basi waendelee na kelele zao.....
Unajua hakuna raha ya ndoa katika maisha kama wanandoa wote mtakuwa mmeridhiana, ndoa yenye furaha ni ile ya kupendana wenyewe na sii kuchaguliana wake au waume, mama sheby aliona mbali sana kuhusiana na mtoto wake sheby kuoa kwa kuchaguliwa mwanamke,..
"mama sheby, mtoto wetu keshakuwa sasa, kwanini ahangaike mwishowe tutakuja kumpoteza kwenye mijumba ya starehe huko"
Aliongea baba yake sheby, mana ile kauli ya mkewe ilimfanya ajue kuwa mkewe hajaridhika na jambo hilo,
"nataka kujua umri wa huyu mtoto wa kike"
Alirudia tena mama sheby
"ok, mtoto wangu ana miaka... "
Sasa aliokuwa anataka kuongea ni mama wa mschana, lakini baba wa mschana akamkatisha mkewe ili aseme yeye
"ana miaka 21 huyu"
Baba mwai au baba mwana aliongea hivyo huku wakicheka na baba yake sheby,..
"hapana mimi siamini... Kwasababu mimi namzaa mwanangu wa kwanza ambae ni Rehema, huyu mtoto wenu alikuwa mkubwa tu, yaani hata halingani na mtoto wangu wa kwanza"
Sasa baba sheby akaona mambo yataharibika hapo, ikabidi amchukue mke wake mpaka nje ili aongee nae..
Waliongea mambo mengi sana lakini sisi hatujasikia maongezi hayo
"lakini baba sheby tutamtesa mtoto wetu lakini"
"mama sheby....... "

Baada ya dakika kadhaa hivi walirudi lakini mama sheby alionekana kutoridhika na hali hio lakini alikubali, sasa sijui kaambiwa nini na mume wake, lakini kakubali sheby aoe, na sheby nae hana ujanja mana ni wazazi wake hawezi kuwakatalia, japo ana mchumba wake ambae ni zaituni,
"kilichobaki ni kupanga siku ya harusi yao"
Aliongea baba yake mwai au mwana au mwanaheri,...
"aahhh sio mbaya kama itakuwa Jumapili"
Alijibu baba yake sheby huku wakipeana mikono ile ya kiutu uzima, ila mzee Mohamed alikua akitoa shukrani nyingi sana kwa jambo hilo kufikia wakati wake...
Sasa kwa sheby na mwai, wakati huo wazee wanaagana sheby akamfunua mtandio huyo mchumba aliochaguliwa na wazazi wake,.. Kweli sii haba, yaani sema ni kuzidiwa kiumri tu, lakini mwai alikuwa ni mzuri wa kila kiungo, na hata umbo lake lilikuwa kubwa kiasi, kifua alijaaliwa mshalah, sasa kijana alivyomfunua ule mtandio akawa anamkagua sana tu, kisha akampa mkono kwa kumsalimia, mana haina jinsi na ili usioe basi cha kwanza uwakane wazazi wako na cha pili uhame na usijuane na wazazi wako, kitu ambacho hakipo...
"mambo"
"safi tu"
Mwai aliitikia ile kiaibu aibu, lakini huezi amini sheby alikuwa ana hasira ya ndani kwa ndani iliokuwa ikimla taratibu, yaani haamini kama anachaguliwa mke,..

Sasa wakiwa katika gari lao wanarudi nyumbani,...
"lakini mzee mbona mnanifanyia hivi lakini"
Aliongea sheby huku akilia kabisa
"nini tena... Wewe umeshakuwa sasa uoe utulie"
"sikatai kuoa baba... Lakini kwanini mnichagulie mke, jitu nene lile hamlioni"
Wakati huo mama sheby katulia tu hana usemi, mana tayari nae kesha shawishiwa na mume wake,..
"mwanangu, acha kunitia aibu kiasi hicho, wewe ni mwanaume bwana"
Sheby hakuwa na ujanja zaidi ya kukubali kuoa

Baada ya siku hio kuoita na leo ni siku nyingine tena ikiwa ni siku ya Jumatatu mida ya saa nne hivi,.. Mary na rose wakiwa kazini
"heeeee mary ibi umeipata hio"
Aliongea rose huku akipanga panga mafile yake vizuri
"nini tena"
"mwai ndani ya ndoa keshokutwa tu"
Kwa mshangao mary kajikuta kaamka kwenye kiti
"weeeeee mwai huyu huyu shost wwtu au kuna mwai mwingine"
"huyu huyu shost yetu"
"eeeeehhhh maajabu haya, mana mwai hapendi kuolewa sijui imekuwaje kwakweli... Enheee harusi ni lini"
"Jumapili ijayo"
"nitaikosaje hioooo, ni kitu kisichowezekana kabisa"
"nakwambia naskia anaolewa na kijana mdogo mdogo"
"weweeeeeee acha utani"
"ndio"
"au ndivyo alivyokuwa akitaka nini"
"labda" +255714419487
Akina rose na mary walikuwa wakimwongelea rafiki yao mkubwa ambae ni mwai, afu hawajui nani anamuoa mwai....
"dada rose... Natamani ingelikuwa mimi na boss sheby"
Aliongea mary bila kujua sheby huyo huyo ndio anaemuoa rafiki yake,
"tatizo lako una haraka sana, kila kitu ni taratibu tu"
"sawa nimekuelewa jamani"
Wakati huo kijana sheby yupo ofisini kwake akiwa na mawzo mengi sana juu ya zaituni, atamuambia nini na wamesha ahidiana ndoa yeye na zai, na mbaya zaidi hata mama yake zai anajua kabisa ni siku chache tu ndoa ifungwe baina ya sheby na zaituni,...
"ngo, ngo, ngo"
Ilikuwa ni sauti ya mlango uliokuwa ukigongwa katika ofisi ya kijana huyo
"karibu"
Aliingia rose huku akiwa kashika baadhi ya mafaili flan hivi..
"boss kuna kazi hapa"
"Samahani, naomba umpelekee mzee"
Aliongea kijana sheby kuwa hatoweza kuifanya, bali ampelekee mzee wake...
"lakini boss... "
"Rose??..."
"abeee boss"
"niliongea Kingereza au Kiswahili"
"ok sorry boss"
Rose aligeuka na mafaili yake mpaka kwa mzee
"boss... Kuna document za kutia saini hapa"
"sheby kashindwa"
"aahhh kiukweli hayupo vizuri na ndio mana kasema nilete huku kwako"
"ok ziache hapo nitazifanyia kazi"
Mzee alinyanyuka kwenda ofisini kwa mtoto wake, lakini huku ofisini kwa akina rose
"mary"
"abeee"
"mpenzi wako anaumwa"
"Unasemaje wewe"
"nahisi kitu kama hicho, nimemkuta ana mawazo mwanzo mwisho"
Mary kweli alimpenda sheby, yqani alijikuta tu anakurupuka na kwenda ofisini kwa kijana huyo... Lakini huku nyuma rose akajisemea kuwa
"wacha akakutane na boss mkubwa huko mana kazidi kiherehere sana"
Rose ameshaanza kumchukia mwenzake kisa ni mapenzi tu, yqani kitendo cha mary kumpenda sheby imekuwa tabu kwa rose,.. Sasa mary ile kufika tu na kufungua mlango, aliongea neno moja tu
"boss..... "
Aliongea mary baada ya kuingia ndani, lakini alishindwa kuendelea kwasababu alimkuta mzee rashidi kakaa na mtoto wake,..
"sema kuna shida"
"hapana boss... Samahani kwa hilo"
Mary alitoka lakini alijiskia vibaya sana, na yote hayo ni kwasababu ya upendo tu, yaani anampenda kuoita maelezo sema aibu ndio inayomsumbua...
"wee dada rose una dhambi wewe"
"nini kwani"
"kwanini uniambie boss anaumwa afu kumbe haumwi"
"heeeeee boss hana hali nzuri"
"mbona nimemkuta na baba yake"
"labda alienda sasa hivi lakini mimi nilimkuta peke yake"
"ok tuyaache hayo tuendelee na kazi"

Huku kwa sheby na baba yake wakiwa, mzee alikuwa na wasiwasi na mtoto wake
"nini shida baba"
Aliongea mzee rashidi huku akimuangalia mtoto wake, lakini sasa hata mzee rashidi hakupenda mtoto wake aoe yule mwanamke, sasa sijui sababu ya kuoa pale imetokea wapi na wakati hata baba pia roho yake inamuuma.... Tutajua mbele kwanini mzew huyo hapendi mtoto wake amuoe yule bint, na wakati yeye ndio kashinikiza waowane...
"mzee, Samahani lakini... Ivi hata mama angu pia mlichaguliwa"
Aliongea sheby huku akitamani hata kulia
"hapana.. Ila ninachokuomba wewe kubali tu, ila utanielewa nilikuwa nina maana gani"
"yaani Nikubali kuoa mtu ambae sijampenda.. Aiseew mzee unanifanyia nini mwanao"
Huezi amini mzee mwenyewe ikabidi aondoke mana ni kweli huu sio wakati wa kuchaguliana wake au waume...

Tukija huku nyumbani kwa akina zaituni, tunamwona Zainabu kaketi chini ya mti na rafiki yake neema,
"haya ndugu yako kaona tena, vipi utampofua tena"
Aliongea neema kwa kumuuliza Zainabu,
"huo ujinga siwezi kuufanya tena, coz nilijuta sana kwa kile nilichokifanya mwaka ule,.. Yaani sina hata hilo wazo, mana kwa sasa kama unavyonijua nimeshakuwa malaya wa kutupwa, hakuna mwanaume yeyote yule atakaesubutu kunioa.. Hivyo sina haja ya kugombania wanaume"
"lakini mpenzi aliompata sasa hivi wala hana hela kama wale wa mwanzo"
Aliongea neema na kumfanya Zainabu kushtuka
"weeeeeeee, tena sasa hivi ndio kapata tajiri haswa.. Yaani yule mkaka ana pesa"
Sasa kumbe zaituni alikuwa akizisikia zile story.. Mana dirisha lilikuwa wazi, na yeye alikuwa chumbani kwake...
"mmmmhhhh mwanaume yenyewe hata nguo hajui kuvaa yule, yaani katika hasara ya wanaume aliowapata ndugu yako, huyu ni hasara"
"neema wewe hujui... Yule mwanaume mimi ndio mtu wa kwanza kukutana nae"
"ulikutana nae wapi wewe"
"nilikutana nae supamaketi akiwa na mdogo wake wa kiume,... Gari wanayotumia ni gari ya pesa haswa"
"we Zainabu muongo mmmhhh sikuezi"
Sasa zaituni ndio kwanza anatega skio vizuri...
"sasa sikia... Unaiona hii nyumba yetu"
"ndio"
"yeye ndio kainunua, na yeye ndio kaikarabati upyaaa"
Sasa huku ndani zaituni ndio anafungukwa na masikio, kumbe mpenzi wake ni tajiri kiasi hicho afu anaishi kwenye kibanda kina matundu kila kona..
Zaituni bila kuchelewa alimfuata mama yake na kumuuliza
"mama, ina maana kukosa kwangu kuona ndio hata ukweli hutaki kuniambia"
"una nini zai mwanangu, kwani mimi nimekudanganyia nini"
"nani kanunua hii nyumba.. Na kama ni huyu mchumba wangu mbona ni muuza viazi, au ni jambazi afu mnanificha, kwahio mnataka niolewe na jambazi si ndio mama"

Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom