Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 14

Mtunzi..... MoonBoy.
"we kaka vipi, ina maana huoni au?"
"Samahani da........ Haaaaaaa zaituni"
"umelijuaje jina langu? ... We vipi wewe"
Alikuwa ni zaituni, tena alimjibu huku akimuangalia juu mpaka chini...

Kijana sheby anashangaa kuona zaituni anamwangalia kwa dharau ya hali ya juu,...
"mmmhhhh samahani zai, yaani hata hunikumbuki"
Sheby aliongea lakini ukumbuke kuwa kijana sheby alipatwa na mafua kule dubai, hali haikumpenda sana katika nchi hio,.. Sasa kijana huyo hakuwa akitoa sauti yake halisi bali ni sauti ya kubanwa na kifua
"wala hata sikukumbuki"
Sasa kabla sheby hajaongea, ghafla shadya katokea akiwa na judith
"heeeeee sheby umerudi saa ngapi"
Aliongea shadi huku akitamani kunikumbatia lakini kashindwa kutokana na zaituni kuona,...
"nimerudi dada angu"
"heeeeeee sauti yako imepatwa na nini tena"
"we acha tu dada shdi, nimeenda kupigika kikazi huko nimebebana na mizigo mizito"
"mmmhhh pole kaka sheby, lakini umewnda kufanya nini sasa"
"sasa bila kufanya kazi tutapataje nauli ya kurudi Tanzania"
Sheby aliongea huku akishika shingo kuashiria kabeba mizigo mizito, lakini sio kweli sema hataki kujulikana kama ni mtoto wa kitajiri,..
"pole sana kaka"
Aliongea judith huku akiwa na huzuni mana kweli kijana huyo alikuwa anahema kwa spiti afu katoka jasho kwa kukimbia....
"kaka sheby.. Umemuona zai wako"
"nimemuona, lakini yeye hanijui"
"we zai,.. Huyu ndio sheby mwenyewe huyu"
Aliongea ahadi huku akimsistizia zai kuwa huyo ndio sheby,
"mbona sauti yake sio"
"ina mana we hujaskia hapa nikimuuliza kuhusu sauti yake"
Mara na judi na akaongea kuwa
"ndio wewe zaituni, huyu ndio aliomileta huku india"
Huezi amini zaituni alianza kulia kwa kile alichomfanyia sheby kabla ya kumjua,...
"nisamehe baby wangu, sikujua"
"najua sio kosa lako zai... Kwanza pole sana baby"
"Ahsante"
Basi walichukuwana mpaka katika chumba cha hapo hospitali,
"unajua nini sheby... Zai alipoona tu, akaahidi kuanzia siku hio hatokaa kumjua mwanaume yeyote yule zaidi yako, yaani atamdharau kila mwanaume, sasa alipokuona wewe ndio akaanza dharau zake, ila haikumaanisha akudharau wewe"
Aliongea shadya, huku wakiwa wamekaa wote kitandani
"mimi mbona sijakasirika, nipo sawa na najua sababu ya yeye kuwa vile"
Waliongea sana huku wakipanga mipango ya kurudi Tanzania,...

BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA

Na leo ni siku nyingine tena sheby akiwa anaburuza mkokoteni uliojaa viazi mbatata,.. Alifika mpaka pale alipo pangisha, ukumbuke kuwa walisharudi Tanzania na ni mwezi sasa umepita toka waliporudi nchini kwao,... Kijana sheby aliingia katika boma alilopangisha na kumkuta shdiya katika kazi yake ya ushonaji wa nguo,...
"za saa hizi shadi"
"salama tu kaka sheby habari yako"
"safi tu... Vipi uyu mamsapu yupo"
"nadhani atakuwa anachota maji hapo mbele"
"ok.. Ngoja nimuachie viazi kidogo vya kupika mchana"
"sawa"
Sheby aliweka viazi ndani kisha akamfuata shadya...
"we mwanamke, ivi kazi inaendelea"
"ndio, inaendelea wala usijali"
"ok poa"
Waliongea maswala ya kazi lakini hatukujua ni kazi gani waliopeana baina ya shadi na sheby,... Kijana huyo akiwa anaondoka ghafla anakutana na mpenzi wake zaituni
"waooo mume wangu, Asalam aleykh"
"waaleykh msalam hali yako lakini"
"mmmhh swalama tu"
"upo freshi eee"
"ndio, ila... Nina shida kidogo"
"nini tena"
"unajua toka nimefanikiwa kuona, lakini sijaenda hata kumsalimia mama yangu"
"oooohhhh shit, sema bize nyingi.. Lakini kesho Jumapili lazima twende"
"eti eeee"
"Ahsante sana mume wangu"
Basi sheby na zai waliagana, lakini huezi amini kijana huyo hajamgusa zai mpaka leo hiii.... Kiukweli ni ngumu sana kwa vijana wa sasa hivi kuishi na mwanamke bila kumgusa... Sasa sheby kumbe aliazima mkokoteni wenye viazi ili kuendelea kuimarisha uhusiano wao
"Aisee asante sana bwana..."
Kijana sheby alirudisha mkokoteni wa watu kisha akamlipa mhusika wa kago hilo,...
"usijali kaka.... Ila umetoka jasho kwelikweli yani"
"we acha tu,... I think mtakuwa mnapata tabu sana ndugu zangu.. Poleni sana"
Sheby aliwapa pole wasukuma mikokoteni, mana yeye ni mara moja moja tu lakini kachoka ile mno..

Kesho yake mida ya saa nne hivi sheby akiwa katika hali yake kimaskini sana,.. Wakati huo ndio wanawasili katika nyumba ya mama mkwe au mama yake na zai,..
"mungu wangu, sheby ile nyumba yetu imeuzwa, wazazi wangu watakuwa wapi sasa"
Zaituni aliongea hivyo na wakati huo kashika fimbo yake na miwani kavaa ili kumdanganya mama yake kuwa bafo haoni,...
"we twende tu"
Sheby alimwambia zai kuwa wao waende tu,.. Na ukumbuke leo hii ni siku ya Jumapili,.. Sasa ghafla mama zai katika nje, alifurahi sana kumuona mtoto wake, lakini bado hajui kama tayari mtoto anaona.... Sasa mama kujiandaa kumkumbatia mtoto wake lakini ghafla kakwepa, kana kwamba zaituni alikuwa akiona.
"heeeee we umenionaje kama nakuja"
Mama aliongea hivyo bila kujua kuwa kumbe zai anaona,..
"mama, huezi amini nakuona tena mama angu"
Zaituni alimwambia mama yake hivyo huku akitupa mti na miwani, mama zai haamini kwa kile anachoambiwa na mtoto wake kuwa anaona,..
"za... Za.. Zai... Zaituni unasema kweli"
"ndio mama... Sasa hivi naona"
Mama alilia huku akimkumbatia mtoto wake, kiukweli sheby alimpenda sana zaituni, yaani nyumba ya akina zai imependeza mno
"mama nani kafanya hivyo"
Zaituni aliuliza nani kaikarabati nyumba yao,..
Sasa mama akamwangalia sheby, ila sheby akatikisa kichwa kuwa asiseme kuwa ni yeye,.. Mana mama anajua fika sheby ni kijana mwenye pesa, lakini zai hajui
"mwanangu, nimeganga ganga sokoni, nikakusanya na vibati vyangu, nimeikarabati mimi"
"jamani mama.... Pole sana mama angu, nahisi utakuwa umejidhiki sana mpaka kufanya hivyo"
"usijali mwanagu........ Sasa karibuni ndani jamani"
Sasa wakiwa wanaingia ndani, ghafla zainabu pacha wake zaituni katokea kwa mbele,...
"heeeeee ndugu yangu zai... Ulikuwa wapi"
"toka mbele yangu"
Zaituni kapita pembeni baada ya kuona zainabu kasimama njiani..
"heeeeeee mama... Zaituni anaona"
"nani kakwambia"
"sasa mbona kaweza kukata kona bila kuelekezwa"
"kwaio we ulitaka asione... Haya mmwagie tena hio tindikali yako"
"mamaaaaa.... Lakini si nimeomba msamaha mama angu, ilikuwa ni mambo ya kitoto tu"
"mambo ya kitoto kumpofua mwenzio"
Mama na zainabu walikuwa wakichemshana huko nje lakini zaituni na sheby wapo ndani tena kwenye sofa
"mmmmhhh zai kwenu kuzuri eee"
Sheby nae alijifanya hajui kuhusu nyumba hio
"we acha tu mama yangu kajitahidi kweli yani, nampa hongera"
Basi mama alifika hapo sebuleni na kuongea mengi sana kuhusu zai na sheby...
"sasa mnatakiwa mfunge ndoa wanangu... Hakuna kitu kizuri kama kupata mtoto mkiwa ndani ya ndoa"
"ni kweli mama, ila wacha nijipange ndani ya miezi hii miwili mitatu, lazima ndoa itimie"
Aliongea sheby huku akiwa na aibu ya kumwangalia mama mkwe...
"mama, hata mimi natamani niolewe hata sasa hivi, sema mchumba wangu bado hajajipanga vizuri"
Aliongea zaituni huku mama yake akijibu kuwa
"ni kweli mwanangu za,.. Lakini kumbukeni maisha ni haya haya, kama unataka kuwa tajiri ndio uoe, hutoweza"
"ni kweli mama"
"ila zai, nakusihi sana, naomba mpende mchumba wako,.. Huyu kijana sio masiki, huyu kijana sio fukara, lakini huyu kijana ni tajiri wa roho"
Sheby alipasukwa tumbo, mana alijua mama atasema kuwa yeye ni tajiri,...
"mama, mimi nampenda sheby wangu, yaani kumuacha we sahau"
"hata mimi nataka iwe hivyo"
Mara simu ya sheby inaita, kucheki alikuwa ni baba yake...
"haloo zee shkamoo"
"marahaba... We asubuhi subuhi hiii umekwenda wapi wewe"
"aahhh nimetoka kidogo nipo mazoezini"
"mazoezi gani ya saa hizi saa sita hii"
"nipo njiani narudi"
"hebu fanya haraka uje kuna mahari twende"
"sawa mzee nakuja"
Simu ilikata kisha kijana huyo akawa anaaga kuondoka...
"mama naomba tukuage"
"sawa baba... Ila naomba huu mwezi usiishe muoane baba... Maisha ni haya haya sio mpaka upate pesa ndio uoe"
"sawa mama yangu, nimekuelewa"
Sasa sheby ile anataka kutoka tu,.. Zaituni kamuita
"baby... Naomba tuongee kidogo"
Walitoka nje na kuanza kuongea
"mume wangu... Naomba ruksa toka kwako"
"ruksa gani tena"
"nina hamu na mama yangu"
"kwahio inataka kubaki"
"ndio mume wangu"
"haina shida,... Ila ukumbuke una kwako ujue"
"au basi twende tu"
"no, no,... We ondoa hamu na mama kwanza sawa"
"sawa, ahsante mume wangu.. Narudi kesho"
"sawa haina shida"

Sasa tukija huku nyumbani kwa akina sheby
"huyu mtoto akioa ndio atatulia"
Aliongea baba yake sheby huku akitamani hata kijana wake aoe leo
"lakini baba sheby, yule mschana ni mkubwa yule... Ni mzazi mwenzangu yule"
"wewe mama sheby, kwanini unamkuza mtoto wa mwenzio kiasi hiki"
"kiukweli ni basi lakini sijapenda mwanangu aoe pale"
"mtoto kakuwa huyu, na nyumba yake imeshaisha ni yeye kuoa na kuhamia tu"
Aliongea mzee rshidi huku wakiwa wamevaa vizuri sijui walikuwa wanakwenda wapi,..
Ghafla sheby anaingia ndani huku akiwa kavaa kawaida tu..
"wewe umetoka wapi mchana wote huu"
"mzee kwani leo kuna kazi... Mimi nitakaaje ndani mzee nimekuwa godoro"
"umeona majibu ya mtoto wako.. Unayaona sasa... Mi nakuambia keshakuwa huyu, aoe aende kwake"
"baba sheby kuwa mpole basi"
"hebu ajiandae twende"
Sasa sheby anashangaa ajiandae waende wapi,...
"mzee, tunakwenda wapi"
"jiandae twende utajua mbele tu"
Sheby aliingia chumbani kwake na kuoga haraka haraka,.. Dakika chache keshamaliza kuvaa, mzee kawasha gari kisha haooo, sheby hajui wanakwenda wapi,... Safari yao iliwachukuwa nusu saa nzima, walifika katika nyumba moja ya kitajiri, wakafunguliwa geti na kuingia ndani,..
"aaahhhhhh mr rashidi, habari yako bwana"
"swalama tu, hali yako mr Mohamed"
"swalama kabisa...... Aahhhh Mrs Rashidy hali zenu jamani"
"aahh tunamshukuru mungu siku zinakwenda"
"vipi mbona simuoni kijana wako"
"yumo ndani humo...... We Sharbiny hebu shuka basi baba"
Mzee rashidi alimwita mtoto wake kwa heshima ya hali ya juu,.. Sheby alishuka na kutoa salamu kwa wote,. Wakati huo walikuwa wanaingia ndani.. Walipofika ndani waliongea mengi sana, lakini ilifikia hatua mke wa mzee Muhammad anamwita mtoto wake..
"mwanaheri,.."
Mama alimwita mtoto wake kwa heshima
"abeee mama"
"njooo mwanangu"
Mwanaheri alikuja huku akiwa kajitanda mtandio mkubwa, tena alikuwa kavalia kihindi sio kihindi,.. Na huyo mwanaheri sio haba, ni bonge la dada haswa,..
"mwanangu mwana.... Huyu ndio yule kijana tuliokuambia jana, anataka kukuoa"
Sasa sheby kashtuka kwa kuskia hivyo,... Lakini ghafla baba yake sheby nae akasema kuwa...
"mwanangu sheby,... Huyu ndio yule mschana tuliokuchagulia mwanangu, ana heshima nzuri kama unavyoona..... Jamani tupigeni vigelegele kwa furaha ya watoto wetu"
Sasa ile watu wanajiandaa kupiga vigelegele, ghafla mama sheby kastopisha vigelegele vyao
"Eehh eehhh hebu tulieni kwanza.. Naomba kwanza kuuliza umri wa huyu mtoto wa kike, kisha muendelee na hizo kelele zenu"

Je? Nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom