MKE JEURI
"we una nini mbona unalia?? ... Afu mbona GPS yangu inanionyesha upo hospitali ya india, umefata nini huko"
Aliongea baba yake huku sheby asijue ajibu nini, lakini papo hapo akapata wazo,.. Lakini kabla hajaliongea ghafla shadya alikohoa, na wakati huo bafo kafunikwa shuka jeupe mpaka usoni, na hata sheby hakumuona...
"mfunueni bado ni mzima huyu"
Aliongea sheby huku simu ya yeye na baba yake ikiwa bado ipo hewani.. Lakini sasa cha ajabu hakuwa shadya, yaani licha ya uzima wa huyo mtu, ila bado hakuwa shadya...
"wewe aheby nani ni mzima hapo... Wewe huko hospitali umefata nini"
Aliongea baba yake sheby
"mzee, kuna mtu aligongwa na gari ambayo mimi nilikuwepo ndani, hivyo tumemleta hospitali"
"ww ndio ulikuwa ukiendesha"
"hapana ni tax za huku"
"sasa kapona huyo mtu"
"aahhh tulimleta hospitali lakini vipimo vilionyesha amekufa, lakini kumbe yupo hai"
"aaahhhh afadhali... Vipi umeiona hio mashine"
"ndio, na kesho saa mbili ndio naondoka"
"hakikisha kazi inakwenda sawa sheby"
"usijali mzee"
"ok kazi njema"
Simu ilikata huku sheby akizidi kumwangalia yule mgonjwa alioletwa kwa kusemekana kafariki dunia..
Alikuwa ni mschana wa Kiafrika tena alikuwa ni Mtanzania kabisa...
"habari yako dada"
Sheby Alimsalimia dada huyo kwa kumpa mkono
"salama... Huku nipo wapi... Uuuuuuuwwwiiiiiiiii jamani zile si maiti zile"
Dada huyo alilia sana baada ya kuona maiti waliokuwepo hapo,.. Basi yule dada alitolewa pale na kuwekwa katika chumba cha matibabu mana hakuwa na ugonjwa wowote sema apimwe tu kwasababu alidondoka na kuzimia...
"lakini ninyi madokta mna kesi kubwa sana ya kujibu.. Kwanini mtu ni mzima afu mnasaini kafa"
"ni kosa lete boss, tunaomba ulinyamazie boss, tutamtibu bure hakuna shida... Ni mawazo tu"
"mawazo kwenye maisha ya watu"
"boss... Msamaha wako unahitajika boss"
Madokta walikuwa wakimlilia sheby ili anyamaze, mana hio ishu ikivuja ni hatari kwao,..
"ivi kwa hali hii, yule mgonjwa wangu atapona kweli"
"bosiiiiii.... Hivi vipimo vilikosewa tu boss"
"ok fanyeni juhudi na huyu awe salama"
"sawa boss, lakini tunakuomba lisivuje hili jambo"
"ok poa"
Sheby alitoka hapo mbio mpaka kwenye chumba ambacho alitakiwa alale shadya,.. Alifungua na kumkuta shadi anabadili nguo..
"ooohhh Sorry, Sorry mamy"
Sheby alitoka mbio baada ya kumkuta shadya anabadili nguo,..
"eeehhh uyu mtoto kaumbika, duuu"
Sheby aliongea hivyo huku akitoka na kuelekea hotelini kwake ambako ndiko alipopangisha chumba chake,.. Alipofika alioga vizuri kisha akalala zake
Kesho yake aliamkia hospitali ili kujulia hali wagonjwa wake, mana anamjua shadya hajui Kingereza hivyo sheby hatakiwi kuwepo mbali, na sijui itakuwaje pale sheby atakapoondoka,..
Alianza kumjulia hali mpenzi wake zai ambae alikuwa bado ana mabendeji katika macho,..
"za saa hizi shadya"
"salama tu, hali yako"
"nzuri... Vipi hali ya mgonjwa"
"aahh tunamshukuru mungu anaendelea vizuri"
"sasa shadya,... Samahani kwa kile kilichotokea jana"
"kitu gani hicho"
Sasa sheby alitaka kuongelea ile ishu ya jana kuingia chumbani bila hodi na kumkuta shadi anabadili nguo..
Sasa baada ya kuona shadya kasahau ikabidi apotezee tu
"au basi tu"
Sheby Aliongea hivyo kisha akaondoka kwenda kumjulia hali na yule mwingine ambaye alisemekana kufa.. Lakini alioofika alimkuta kakaa mahari huku akiwa analia,..
"za saa hizi dada"
"salama tu"
"vipi mbona haupo wodini afu unalia kuna nini"
"aahhhh ni stori ndefu kaka"
"kwanini usiniambie tu kama naweza hata kukuseidia kwa mawazo tu"
Dada huyo alikuwa mzuri sana na mwenye aibu za kipekee, na hakuwa mgumu wa kuongea na sheby..
"tulikuja hapa hospitali toka juzi, lakini madaktari wakataka tuhamishwe hospitali nyingine,... Sasa katika kuondoka, mimi nikawa namalizia kukusanya vitu kule kwenye vyumba vya wauguzi.. Lakini nilipokuwa natoka, nikapishana na mtu aliopata ajali mbaya sana.. Sijawahi kuona nyama za binadamu,.. Kiukweli kitendo kile kilinifanya nizimie papo hapo.. Ndipo nilipozinduka nikajikuta nipo mochwari na ninyi mkiwa pembeni yangu... Hivyo mpaka sasa sijui wamekwenda wapi na sijui wanaendeleaje huko"
"mmmhhh pole sana dada angu.. Naa ni nani wako hao"
"ni shemeji yangu.. Yaani dada yangu kaolewa huko, sasa ndugu yake mume wa dada yangu, kaletwa kwa ugonjwa wa uvimbe tumboni"
"ooohhh pole sana"
"mpaka sasa sijui nawapata vipi ili niweze kurudi nyumbani"
"ooohh pole sana dada angu,.. Lakini kwanini usiendelee kuwepo hapa, mana wanaweza kuja hapa"
"sasa nitawezaje kukaa hapa na wakati mgonjwa alionileta hayupo, ulifikiri nitalipaje bili za watu"
"kwani unadaiwa"
"hapana, ila nikiendelea kuwepo hapa bila sababu"
"sababu ipo..... Sikia nina mgonjwa hapa ndani, nilikuwa naomba ushirikiane na dada mmoja hivi"
"una mgonjwa, mgonjwa gani"
"twende ukamuone"
Dada huyo ambae hata jina hatumjui alichukuliwa na kijana sheby mpaka kenye wodi ya macho na kumwonyesha mgonjwa wake
"alikuwa haoni kabisa au"
Dada huyo aliuliza
"alikuwa kipofu kabisa"
"hhhmmm pole sana.. Ni dada yako ee"
"no, ni mpenzi wangu"
"aahhhhhh wanaume kama ninyi ni wachache sana duniani,... Sijui kama wapo wengine, kwa jinsi wasichana tulivyo na akili mbovu, una moyo kaka angu"
"nampenda sana mpenzi wangu"
"I know"
"Eeeeehhh we unajua kimombo kidogo"
"yes, I know"
"basi naomba ukae hapa na huyu hapa ni dada yangu, utakuwa nae hapa ili uongew na madaktari...... Dada shadi, huyu atakuwa mgeni wetu"
"sawa...... Dada karibu"
"Ahsante.... Naitwa Judith naishi Dar es Salaam"
"ooohhh mi naitwa shadya, naishi arusha"
"ooohhh napenda sana kuishi arusha"
Basi shadya na Judith walianza kupendana ghafla tu na urafiki ukaanza.... Wakati huo madaktari wanaendelea na matibabu juu ya zaituni...
"sasa naombni nitoke kidogo nitarudi nadhani"
"sawa kaka"
"aahhhh Judi, tayari nimeshalipa kila kitu, hivyoo.. Chukueni hii ikae ya mfuko kwa ajili ya vitu vidogo vidogo vitakavyohitajika"
"sawa"
Sheby aliondoka zake ikiwa ni saa mbili kasoro robo,... Alichukuwa tax ilimfikisha mpaka kwenye kampuni ya mr mageshi,.. Alimaliza mambo yote kisha safari ya kuelekea dubai ilianza...
Huku hospitalini judi akiwa anaongea na shadi
"kaka yako mkarimu eee, tena anaonekana anapenda kuseidia watu"
"aahhhh waapi korofi hilo hapana chezea"
"mi napenda wanaume wakorofi, mana mwanaume mkorofi basi lazima kuna mahari ni mzuri... Kuliko kupata mwanaume mzuri kila idara, basi jua kuna siku utalia mpaka ukome"
"kwaio unamaanisha umeshapenda ivyo"
"kupenda sio kazi, kazi kukubaliwa"
"weeeeeeee shauri zako.. Mwenyewe yule pale kalazwa akikuskia huna bahati"
Walikuwa wkiongea huku wakicheka,
"hapana bwana,.. Huyu mkaka namueshim sana japo tumekutana kwa muda mfupi tu"
"hata mimi mwenyewe namueshim weeee"
"we kumueshim ni lazima... Si kaka yako"
"mmmhhh"
"mmmhhhh nini sasa"
Baada ya masaa 9 kupita kijana sheby ndani ya dubai, wakati huo clan linafanya kazi ya kuitoa ile mashine katika ndege,.. Mashine yenyewe ina uzani wa tani 20
"sasa jamani, nadhani mzigo wenu umefika salama"
Sheby aliongea hivyo ili waamalizane aondoke zake...
"kwahio watakaje"
"mkataba wa pesa huu hapa, tusaini kisha mnilipe niondoke"
"hapana, huezi ondoka bila mashine kuwekwa, mpaka mashine iwake ndio uondoke"
"Ati nini we Mwarabu"
Sheby alipanic ghafla kwa kusikia kuwa atatakiwa kukaa mpaka mashine iwake, laa sivyo hatolipwa..
"hio ni moja ya kanuni zetu... Kulipwa utalipwa lakini mpaka mashine iwake, isipowaka utarudi nayo india"
"ayaaaaaaaaaa"
"sikia mr sheby.... Huku tutakugharamia kila kitu, yaani utachagua hoteli uitakayo utakula chakula ukitakacho, yaani maisha yako huku dubai tuachie sisi"
"hamula lolote bwana mbwembwe tuuu"
Sheby kwa hasira alimoigia baba yake
"haloo mzee"
"vipi, Nakuona hapa umeshafika bandarini, na nadhani mnapakua mashine"
"ndio mzee... Lakini mbona wanasema siwezi kulipwa mpaka mashine iwake kwanini"
"ndio kanuni zao, huwa hawatakagi biashara za kona kona"
"sasa itachukuwa muda gani mzee"
"mpaka waunganishe hio meli yao, yaweza chukuwa hata wiki nzima"
"Whaaaat,... Mzee mi nilijua itachukuwa masaa, wiki nyingi mzee hebu ongea nao basi hata siku ziwe chache"
"haiwezekani.. We kaa hapo uone na ulinde, tena ukikaa mbali itakula kwetu, kutatolewa kifaa hapo afu tuambiwe ni sisi wasafirishaji"
"aaakhaaaaa"
"ndio kazi hizo baba tulia"
Sheby alikasirika kweli yani, afu unaambiwa hatakiwi kwenda mbali mpaka mashine iunganishwe kwenye meli,.. Iwake ndio alipwe,.. Sheby alikaa mahari huku akiwaza itakuwaje kule hospitali,... Yaani wasiwasi wake wote ni kule hospitali.
Sasa tukija huku kwa mama yake zaituni, leo tunaiona nyumba ya akina zaituni inakarabatiwa yaani inakuwa nzuri, kwa muonekano wa haraka haraka inaonekana sheby keshainunua hio nyumba, hivyo hapo ilikuwa ikipigwa rangi,
"mama, zaituni kaenda wapi mbona simuoni karibia siku ya tano hii"
"we wamtakia nini mwananguc
"heeeeeeee mamaa, kwani kuna shida gani kumuulizia pacha wangu"
"pacha wako... Pacha wako ungemwagia tindikali kisa wanaume"
"lakini mama si nimeomba msamaha, ilikuwa ni usichana tu"
"mimi sijui hio, afu fanya uondoke kwenye nyumba yangu mshenzi wewe"
"sasa nikiondoka nani atalipa kodi"
"weeeeeeeeee, nyumba imeshanunuliwa hio,.. Mdogo wako ana nyota ya kupendwa, sio wewe mshenzi wewe... Tena staki hata kukuona, nilikuwa nakuchukua sana sema sikuwa na jinsi ya kufanya kwakuwa ulikuwa unalipa kodi lakini nilikuwa sikupendi hata kidogo"
"mamaaaa.... "
"tokaaaa"
BAADA YA WIKI MOJA KUPITA
"Ahsante sana mr sheby,.. Mashine imefanya kazi vizuri na umeifikisha salama"
"sawa hebu tusaini kisha utume pesa kwenye akaunti ya mzee"
"sawa njoo huku ndani"
Kijana sheby alikuwa ana haraka ya hali ya juu, mana wiki nzima yupo dubai, licha ya kulipiwa kila kitu akiwa dubai,...Hali ya hewa ya dubai kwa sheby haikumpenda kiasi flani kwani alikuwa na mafua ya hapa na pale, hivyo hata sauti yake ilikuwa haitoki vizuri,... Basi Pesa zilitumwa katika akaunti ya mzee Rashidy kisha sheby akampigia simu baba yake
"mzee B 5.7 zimefika"
"aaahhhh ngoja niangalie kupitia akaunti ya simuuuuuuuu.. Yes, imefika"
"ok poa... "
"kazi nzuri, safi sana huo ndio ukubwa sasa"
"sawaaaa"
"rudi nyumbani sasa, au huna pesa nikutumie"
"ninayo"
Sheby alikuwa kakasirika sana hakua na raha hata kidogo, hata baba yake hakuwa akimjibu vizuri.. Yaani kakaa wiki nzima dubai bila sababu za msingi...
Basi sheby alimaliza kila kitu kisha akawahi Airport na kupata usafiri wa private,.. Ndege iliokuwa na spidi kali kuliko za kawaida...
Masaa matano tu yupo ndani ya india, hakutaka kuchelewa, mara moja akachukuwa tax, ilimpeleka mpaka hotelini alipopangisha chumba,.. Alibadiri zile nguo zake za kawaida za kimaskini japo zilikuwa safi safi kidogo lakini ni nguo za kimaskini sana... Bila kuchelewa sheby ndani ya tax mpaka hospitali, wakati huo alikuwa na haraka ya kwenda kuwaona wagonjwa wake,... Spidi aliokuwa nayo hata salamu alikuwa hatoi..
"we kaka vipi, ina maana huoni au?"
"Samahani da........ Haaaaaaa zaituni"
"umelijuaje jina langu? ... We vipi wewe"
Alikuwa ni zaituni, tena alimjibu huku akimuangalia juu mpaka chini...
Je? Nini kitaendelea??....