Makapuku Forum

Makapuku Forum

The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na hatia)- 25
ILIPOISHIA:
Nilianza kuwatazama mmoja baada ya mwingine, kuanzia mama ambaye uso wake ulikuwa na huzuni kubwa, baba ambaye alionesha kuwa katika tafakuri nzito na ndugu zangu wote ambao walikuwa wamenikodolea macho, kila mmoja akiwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Mara mlango wa wodi ulifunguliwa, watu wote wakageuka kutazama ni nani aliyekuwa akiingia kwa kasi kiasi kile.
SASA ENDELEA...

“Shikamooni! Samahani naomba kuuliza eti hii ndiyo wodi aliyolazwa Togo?” alisema mtu huyo lakini kabla hajajibiwa, tayari alikuwa ameshasimama sehemu ambayo ilinifanya mimi na yeye tutazamane.
Moyo wangu ulinilipuka mno kugundua kuwa kumbe alikuwa ni yule msichana tuliyekutana naye kwenye basi na kujenga naye urafiki utafikiri tumejuana miaka kumi iliyopita.
Sikuelewa amejuaje kwamba nilikuwa hospitalini hapo kwa sababu mara ya mwisho alipokuja nyumbani na kunikuta nikiwa na Rahma, tukiondoka kuelekea ufukweni, nilimueleza kwamba tunaenda Coco lakini baadaye tukabadili uelekeo na kuelekea Msasani Beach kwa lengo la kumkwepa.
Kwa harakaharaka, isingewezekana mtu ambaye ametufuata Coco ajue kwamba kumbe tulienda Msasani na kama hiyo haitoshi, ajue kwamba kuna tatizo limetokea na kujua mpaka wodi niliyokuwa nimelazwa. Kengele ya hatari ililia ndani ya kichwa changu.
“Ooh! Ahsante Mungu, Togo... umepatwa na nini baba?” alisema huku akinisogelea pale kitandani lakini baba alimzuia.
“Binti, sidhani kama nakujua. Wewe ni nani?”
“Togo alisema hawafahamiani ila walikaa siti moja kwenye basi tu, hata sijui amefuata nini,” alidakia Rahma na kuzungumza kwa chuki, moyoni nikajisikia vibaya sana kwa sababu kama mtu alikuwa amekuja kwa ajili ya kuniona, achilia mbali utata mkubwa uliokuwa nyuma ya tukio la yeye kujua mahali nilipo, hakupaswa kufanyiwa vile.
“Mruhusuni. Ni rafiki yangu!” nilitamka kwa sauti dhaifu ya kukwamakwama, yakiwa ndiyo maneno yangu ya kwanza kuyatamka tangu niliporejewa na fahamu. Baba akageuka na kunitazama kwa sekunde kadhaa, akageuka na kumtazama yule dada usoni, akageuka na kumtazama Rahma ambaye utulivu ulimuisha.
Akamruhusu anisogelee pale kitandani, huku uso wake ukilengwalengwa na machozi, aliniinamia pale chini kwa heshima.
“Pole baba, nimeona picha ya tukio la wewe kuokolewa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, nikajaribu kuulizia ndiyo nikaambiwa umelazwa hapa. Pole sana,” alisema huku safari hii machozi yakiwa yanamtoka. Nadhani kwa jinsi alivyoonesha kuguswa na hali yangu, hata baba alianza kumkubali kwani nilimsikia akishusha pumzi ndefu.
“Najua hakuna anayeweza kukuelewa ukieleza kilichotokea, nakuombea upone haraka,” alisema msichana huyo na kunifanya nikodoe macho kama fundi saa aliyepoteza nati. Alijuaje kwamba hakuna atakayenielewa nikieleza kilichotokea? Alijuaje kwamba maelezo ya Rahma yalikuwa tofauti kabisa na kile nilichoamini kwamba ndiyo ukweli? Nilijikuta nikichanganyikiwa.
Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, alinibusu kwenye mkono wangu uliokuwa na sindano ya dripu, akageuka na kuwashukuru watu wote kisha kwa heshima kubwa akaondoka zake. Japokuwa mavazi aliyokuwa amevaa yalimtafsiri katika picha nyingine tofauti kabisa, alionesha nidhamu ya hali ya juu mno.
“Huyu ni nani?” swali la baba lilinizindua kutoka kwenye dimbwi la mawazo, akanikazia macho akionesha kuwa na shauku ya kutaka kusikia nitamjibu nini.
“Ni rafiki yangu.”
“Huyu ndiyo mliyekuwa naye kwenye basi?”
“Ndiyo.”
“Na ndiyo aliyekupa simu si ndiyo?”
“Ndiyo.”
“Amejuaje kama umelazwa hapa?”
“Anasema kuwa ameniona kwenye mitandao.”
“Mitandao? Wewe umefikaje kwenye mitandao?” baba alinihoji, huku na yeye akionesha kutokuwa na uelewa wa mambo ya teknolojia kama mimi. Nilimuona baba yake Rahma naye akisogea na kuja kuungana na baba pale pembeni ya kitanda changu.
“Eti anasema amemuona kwenye mitandao,” alisema baba huku akimgeukia baba yake Rahma.
“Inawezekana, unajua hawa vijana wa siku hizi ni wepesi sana wa kutumia mitandao ya kijamii kama Facebook, WhatsApp na Instagram kwa hiyo tukio lisilo la kawaida likitokea tu, haraka wanapiga picha kwa kutumia simu zao na kuliweka mtandaoni kwa hiyo habari zinasambaa kwa kasi,” alisema baba yake Rahma.
Na mimi nikawa nimepata elimu kidogo maana kiukweli sikuwa najua chochote kuhusu hayo mambo maana kule ‘bush’ kwetu tulichokuwa tunakijua ni redio tu. Muda mfupi baadaye, madaktari waliingia na kuwataka watu wote wawapishe ili waweze kuendelea kunipa huduma.
Madaktari walifurahi kuniona nikiwa na hali ile, wakaanza kuniuliza jinsi nilivyokuwa najisikia. Niliwaambia kwamba nahisi mwili wote umekuwa mzito, kila kiungo hakina nguvu. Waliniambia ni kwa sababu ya kiwango kikubwa cha chumvi nilichokuwa nimekula na mwili kukosa hewa safi kwa muda.
Hata hivyo, waliniambia kwamba hali hiyo ni ya muda tu, mwili utapata nguvu hasa baada ya kumaliza kiwango cha dripu walichonipangia, ambazo zilikuwa zikiendelea kutiririka kwa kasi kuingia mishipani mwangu.
“Kwa hiyo leo naweza kuruhusiwa kutoka?”
“Leoleo utatoka wala usiwe na wasiwasi.”
“Kwani saizi ni saa ngapi?”
“Ni saa moja za jioni,” alisema daktari huku akinipima mapigo ya moyo kwa kutumia kifaa maalum, akarekebisha kasi ya dripu kuingia mwilini mwangu kisha akawa anaandika jambo kwenye faili huku akijadilianana wenzake.
“Kwani wewe hujui kuogelea.”
“Najua vizuri tu.”
“Sasa mbona maji yalikuzidi nguvu? Si vizuri kucheza na maji kama hujui kuogelea vizuri, sawa kijana?” alisema daktari huku akinitazama. Niliamua kukaa kimya maana hata ningeeleza kilichotokea, hakuna ambaye angenielewa. Kwa kifupi ni kwamba ilionesha eti mimi nilikuwa nachezea maji ya baharini ndiyo maana nikazama na kutaka kupoteza maisha.
Hicho ndicho walichokuwa wakikiamini watu wote lakini ukweli nilikuwa nao moyoni mwangu, nikaona njia nzuri ni kunyamaza tu kwa sababu sikuwa napenda kukaa hospitalini, isitoshe hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kulazwa. Kule kijijini kwetu, mtu ukiumwa ilikuwa hakuna kwenda hospitali, baba anamaliza kila kitu yeye mwenyewe.
Kwenye majira ya kama saa tatu za usiku, nilimuona baba na baba yake Rahma wakiingia wodini wakiwa wameongozana na wale madaktari waliokuwa wakinitibu, wakapewa baadhi ya maelekezo kisha wakaja pale kitandani kwangu, daktari mmoja akanichomoa dripu na kuniambia nijaribu kusimama.
Nilifanya hivyo, japokuwa kwa mbali nilikuwa nasikia kizunguzungu, niliweza kusimama vizuri. Wakaniambia nijaribu kutembea hatua chache, nilifanya hivyo na wote waliridhishwa na maendeleo yangu. Yule daktari akawaelekeza akina baba sehemu ya kwenda kulipia, baba yake Rahma akanishika mkono na kuanza kuniongoza kuelekea nje.
Nguo nilizokuwa nimevaa hazikuwa zile nilizovaa wakati nilipotokewa na tukio lile, hata sikukumbuka nani alinibadilisha na alinibadilisha saa ngapi. Nilipotoka nje, niliwakuta ndugu zangu wote wakiwa wamekusanyika, wote wakainuka baada ya kuniona nikitembea kwa kujivuta, wakaja na kunizunguka.
“Unaendeleaje mwanangu,” alisema mama huku akija na kunikumbatia, nikamwambia naendelea vizuri, akaja mama yake Rahma ambaye naye alinikumbatia, akaja dada Sabina, Rahma na wengine wote, kila mtu akawa ananikumbatia na kunipa pole kwa kilichotokea.
Wote wakageuka na kuanza kuniongoza kwenye gari aina ya Toyota Noah lililokuwa eneo la mapokezi, mimi nikasaidiwa kukaa siti ya mbele, pembeni ya dereva, ndugu zangu wengine wote wakakaa nyuma. Kwa sababu ya wingi wao, hawakutosha, ikabidi mama na mama Rahma pamoja na baba zetu wao wapande kwenye teksi iliyokuwa imepaki mbele ya ile Noah tuliyopanda.
Muda mfupi baadaye, dereva aliingia, akanisabahi na kunisaidia kufunga mkanda, kabla hajaondoka nilimuona yule msichana akitokea upande wa pili, akamuonesha dereva ishara kwamba asiondoe kwanza gari, akaja pale kwenye dirisha la siti niliyokuwa nimekaa.
“Togo, vipi unaendeleaje?”
“Naendelea vizuri, namshukuru Mungu.”
“Pole sana mpenzi wangu,” alisema, nikiwa bado nashangaa kwa nini ameniita hivyo, alinivuta na kugusanisha mdomo wake na wangu, nikabaki nimeganda kama nimepigwa na shoti ya umeme. Aliponiachia, harakaharaka niligeuka kuangalia kama Rahma hakuwa ameona kitendo hicho, kwa bahati nzuri alikuwa akipiga stori na dada Sabina, kiufupi hakuna aliyeona zaidi ya dereva ambaye naye alizuga kama hajaona kitu.
“Hii ni zawadi maalum kutoka kwako,” alisema huku anikipa bahasha kubwa ya rangi ya pinki, akanibusu kwenye paji la uso kisha akaniachia na kunipungia mkono, akampa ishara dereva kwamba aondoke. Wakati hayo yakiendelea, kumbe baba aliyekuwa amekaa siti ya mbele ya ile teksi iliyokuwa imeshaanza kutoka pale eneo la maegesho, alikuwa akishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea.
Nilipomtazama, macho yangu na yake yaligongana, akanikazia macho, ikabidi nikwepeshe macho yangu, safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku mara kwa mara baba akichomoza kichwa na kunitazama, jambo ambalo sikulifurahia.
Bado nilikuwa na maswali mengi kuhusu huyu msichana, sikuwa najua ndani ya ile bahasha kuna nini na kwa sababu gani anaonekana kunijali kiasi hicho. Baada ya dakika kadhaa, tukawa tumeshawasili nyumbani.
Magari yaliposimama tu, baba alishuka haraka na kunifuata, kabla hata dereva hajanisaidia kufungua mkanda, baba alifika na kunitazama kwa macho ya ukali, safari hii nikaona kama ananionea, na mimi nikamkazia macho, tukawa tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, huku nikiificha ile bahasha asiione maana angeweza kunipokonya kama alivyofanya kwenye simu.
“Kwa nini unakuwa huelewi unapoonywa jambo? Unataka mpaka nini kitokee ndiyo ujue kwamba yule msichana ni mtu hatari kwako na kwetu sisi sote?”
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocent (makaburi ya Wasio na Hatia)- 26
ILIPOISHIA:
Nilipomtazama, macho yangu na yake yaligongana, akanikazia macho, ikabidi nikwepeshe macho yangu, safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku mara kwa mara baba akichomoza kichwa na kunitazama, jambo ambalo sikulifurahia.
SASA ENDELEA...

Bado nilikuwa na maswali mengi kuhusu huyu msichana, sikuwa najua ndani ya ile bahasha kuna nini na kwa sababu gani anaonekana kunijali kiasi hicho. Baada ya dakika kadhaa, tukawa tumeshawasili nyumbani.
Magari yaliposimama tu, baba alishuka haraka na kunifuata, kabla hata dereva hajanisaidia kufungua mkanda, baba alifika na kunitazama kwa macho ya ukali, safari hii nikaona kama ananionea, na mimi nikamkazia macho, tukawa tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, huku nikiificha ile bahasha asiione maana angeweza kunipokonya kama alivyofanya kwenye simu.
“Kwa nini unakuwa huelewi unapoonywa jambo? Unataka mpaka nini kitokee ndiyo ujue kwamba yule msichana ni mtu hatari kwako na kwetu sisi sote?”
Magari yaliposimama tu, baba alishuka haraka na kunifuata, kabla hata dereva hajanisaidia kufungua mkanda, baba alifika na kunitazama kwa macho ya ukali, safari hii nikaona kama ananionea, na mimi nikamkazia macho, tukawa tunatazamana kama majogoo yanayotaka kupigana, huku nikiificha ile bahasha asiione maana angeweza kunipokonya kama alivyofanya kwenye simu.
“Kwa nini unakuwa huelewi unapoonywa jambo? Unataka mpaka nini kitokee ndiyo ujue kwamba yule msichana ni mtu hatari kwako na kwetu sisi sote?”
“Sasa baba, unajua mimi kuna mambo mengi sana sielewi, halafu nikikuuliza hata hunipi majibu ya kuridhisha.”
“Hilo siyo jibu, umeanza kuwa na kiburi,” alisema baba kwa sauti ya chini lakini akionesha kama alikuwa amepania kuniadhibu. Sikumjibu chochote, akauma meno kwa hasira na kuelekea pale alipokuwa amesimama baba yake rahma, wakawa wanazungumza jambo. Nadhani walikuwa wananijadili.
Kiukweli, uhusiano wangu na baba ulikuwa umeingia doa kubwa na sababu ya yote, ni mambo ya ajabu yaliyokuwa yakinitokea ambayo yeye alionesha kwamba anajua kila kitu na pengine ndiyo chanzo cha yote. Bado nilikuwa na maswali mengi ambayo alipaswa kunijibu.
Swali la kwanza, nilitaka aniambie kwa nini wanakijiji wenzake kule kijijini kwetu, Chunya walikuwa wakimtuhumu kwamba ni mchawi na ndiye aliyeshiriki kwenye vifo vya watu wawili katika mazingira ya kutatanisha. Kwa macho yangu nilishuhudia akipambana na watu hao kabla ya baadaye kubainika kwamba wamekufa vifo vya ghafla.
Nilitaka aniambie ukweli, yeye ni mganga kama mwenyewe alivyokuwa akijinadi au alikuwa ni mchawi? Nilitaka pia anieleze, aliwezaje kusafiri kutoka Chunya mpaka Dar es Salaam bila kuwemo kwenye basi tulilokuwa tumepanda lakini muda wote akawa anatoke apale panapotokea tatizo, kama alivyotusaidia kuepukana na ajali mbaya zilizotaka kutokea wakati tukisafiri kutoka Chunya kuja Dar, ya kwanza ikiwa ni kwenye eneo hatari la Mlima Nyoka na la pili likiwa ni kwenye Mlima Kitonga.
Nilitaka anieleze vizuri aliwezaje kuniokoa nisigongwe na gari, lakini wakati huohuo watu wengine wote wakawa hawamuoni wala kumsikia zaidi yangu. Nilitaka aniambie, ile dawa aliyonipa niwe namnyunyizia dereva, ilikuwa na maana gani na iliwezaje kutuepusha na ajali?
“Nataka kujua nini kimetokea hapa kwa akina Rahma maana nasikia kabla sisi hatujafika walikuwa wakiishi kwa amani, mbona tangu tuingie, japo ni muda mfupi tu lakini tayari kuna mambo mengi ya ajabu yametokea? Kwa nini naona mambo ambayo watu wengine hawayaoni?”
“Mbona unaongea peke yako Togo?” sauti ya Rahma ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye dimbwi la mawazo machungu, nikashtuka sana kugundua kwamba kumbe nilikuwa nikizungumza kwa sauti huku mwenyewe nikidhani nawaza.
“Umesikia nini kwani?” nilimuuliza huku mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio sana. Kwa bahati nzuri, kumbe sikuwa nimetamka kwa sauti mambo mengi zaidi ya kujiuliza kwa nini tangu tufike nyumbani kwa akina Rahma mambo mengi ya ajabu yalikuwa yakitokea.
“Kwani unafikiri ujio wenu ndiyo chanzo cha haya yote?” aliniuliza Rahma kwa upole huku akinishika mkono na kunielekeza tuelekee ndani maana nilikuwa nimesimama, nikiwa nimepoteza kabisa mwelekeo.
“Sisi ndiyo chanzo na pengine mimi ndiyo chanzo hasa,” nilisema kwa sauti ya unyonge, Rahma akaniambia kuna jambo zuri anataka tukazungumze chumbani kwake. Nilimkubalia, tulipoingia ndani tulipitiliza mpaka chumbani kwake.
Akina mama ilibidi waanze kuchakarika kwa sababu hata chakula cha usiku hakikuwa kimepikwa siku hiyo kwa sababu ya majanga yaliyonitokea ambapo baada ya kupata taarifa kwamba nipo hospitali nikiwa sijitambui, ilibidi nyumba nzima ije kunijulia hali. Waliingia jikoni huku ndugu zangu na wadogo zake Rahma wakikaa sebuleni kutazama runinga.
Baba na baba Rahma, kama kawaida yao wao walibaki nje wakiendelea na mazungumzo yao.
“Unataka kuniambia nini Rahma,” nilimuuliza kwa upole baada ya kumuona akifunga mlango wa chumbani kwake kwa komeo. Hakujibu kitu zaidi ya kuvua blauzi yake kisha ‘bra’, akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu.
Japokuwa mwili wangu haukuwa na nguvu, nilijikuta nikisisimka mno. Rahma alikuwa amejaliwa kifua kizuri mno, ambacho kwa mwanaume yeyote aliyekamilika, ilikuwa ni lazima atokwe na udenda kama fisi aliyeona mfupa.
Rahma aliendelea kunikumbatia huku akinibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu kimahaba, hali ambayo ilinichanganya kabisa kichwa changu. Taratibu alinirudisha nyuma mpaka tulipofika kwenye uwanja wa fundi seremala, akanisukumia juu yake kisha akamalizia na za chini zilizokuwa zimesalia.
Akionesha kuwa na papara za hali ya juu, alihamia kwangu na kuitoa ya juu, nikabaki kifua wazi, akahamia na ile ya chini na muda mfupi baadaye, tulikuwa ‘saresare’ maua. Bado mwili wangu haukuwa na nguvu kwa hiyo nilimuachia yeye ndiye awe ‘dairekta’ wa filamu ile ya kusisimua na kweli alikitendea haki cheo nilichompa.
Itaendelea...
Kwa ufanisi wa hali ya juu, Rahma aliitii kiu yangu, mpaka anashuka kutoka juu ya mnazi, alikuwa ameshaangua madafu kadhaa, akajitupa upande wa pili huku akinishukuru, na mimi nikawa namshukuru. Hatukuchukua raundi, kila mmoja akapitiwa na usingizi mzito.
Nadhani wangu ulikuwa mzito zaidi kwa sababu kuichwa changu kilikuwa kimebeba mambo mazito mno na alichonipa rahma ilikuwa sawa na dawa ya usingizi. Tulikuja kushtuka baadaye baada ya kusikia mlango wa chumba cha Rahma ukigongwa. Mimi ndiye niliyekuwa wa kwanza kuzinduka, nikamuamsha Rahma ambaye aliamka kichovu na kusogea karibu na mlango.
Safari hii hatukuwa na hofu tena kwani tulikuwa na ruhusa ya kukaa pamoja karibu, mimi kazi yangu ikiwa ni kuhakikisha rahma harudii tena kujaribu kuyakatisha maisha yake na Rahma kuhakikisha ananisaidia mimi mgonjwa.
“Unasemaje?”
‘mama anauliza kama mtakula na sisi au mletewe chakula chenu huku.”
‘Ngoja nakuja mwenyewe,” alijibu Rahma wakati akizungumza na mdogo wake aliyetumwa na mama yao kuwaulizia.
‘Eti mpenzi wangu, we unapenda tukakae sebuleni au tulie hukuhuku chumbani.”
‘Utakavbyosema wewe hamna shida ila napenda zaidi tukikaa peke yetu,” nilimjibu, akanitazama kwa macho yake ambayo yalikuwa yameelemewa na usingizi kisha akaachia tabasamu la kichovu.
“Ngoja nikaonge kwanza,” alisema na kuchukua kitenge, akaelekea bafuni na muda mfupi baadaye, alirudi akiwa amechangamka kidogo. Ilibidi na mimi niende kuoga wakati yeye akihangaikia chakula.
Niliporudi kutoka bafuni, tayari rahma alikuwa ameleta chakula kizuri kule chumbani. Tofauti ya vyakula tulivyozoea kula kijijini na mjini ilikuwa kubwa mno. Chakula kilipikwa vizuri, yaani kwa kukitazama tu ilikuwa ni lazima mate yakutoke. Tulinawa vizuri lakini nilipotaka kuanza kula, Rahma alinikatazana na kusema anataka anilishe kidogo.
Yalikuwa ni mambo mageni kabisa, nilizoea kuona watoto wadogo au wagonjwa ambao wako mahtuti ndiyo wanalishwa, lakini eti dume mimi nilishwe? Hata hivyo sikumkatalia. Akaanza kunilisha kwa upole, huku mara kwa mara akinitazama machoni. Sijui nini kilimtokea Rahma lakini alionesha kunipenda sana, tena sana.
Mara kwa mara alikuwa akinibusu na kuniambia kwamba ananipenda sana, mpaka nikawa najisikia aibu. Sikuwa najua kabisa mambo ya kikubwa na wala sikuwa na uelewa wowote wa mahaba. Nilikuwa nikisikiasikia kwamba watu wa pwani ndiyo wataalamu wa hayo mambo.
Japo Rahma alikuwa akinilisha matonge madogo tofauti na niliyozoea lakini kiukweli nikiri kwamba nilijisikia raha ya ajabu ndani ya moyo wangu. Tulipomaliza kula, alitoa vyombo, akaja kufanya usafi kisha akafunga tena mlango.
“Itabidi mimi nikalale chumbani kwangu,” nilimwambia Rahma lakini akakataa katakata, akaniambia tutalala wote humo chumbani kwake na tutajifunika shuka moja. Japokuwa kwa nje nilikuwa navunga, ukweli ni kwamba hata mimi nilikuwa napenda sana kuwa karibu na Rahma hasa kutokana na mapenzi ya dhati aliyokuwa ananionesha.
Ile tofauti ya umri kati yetu sikuiona tena, namimi nikawa najiona mkubwa kama yeye, hata ile harufu ya undugu kati yetu nayo ilitoweka kabisa, ndani ya muda mfupi tu tuliokaa pamoja ikawa utafikiri tumeishi pamoja kwa miaka mingi tangu zamani.
Tulipiga stori za hapa na pale, baadaye muda wa kulala ulipofika, kama ilivyokuwa mara ya kwanza, Rahma aliniganda kama ruba, tukapeana tende na halua kwa mara nyingine kabla ya kupitiwa na usingizi mzito, akiwa ameniganda kifuani kama ruba.
Nilikuja kuzinduka usiku wa manane baada ya kuhisi hali isiyo ya kawaida. Kilichoniamsha, zilikuwa ni kelele za paka waliokuwa wakipigana juu ya paa, huku wakitoa milio ya ajabu kama watoto wachanga.
Sikutaka kumuamsha Rahma, nilimtoa kifuani kwangu taratibu kisha nikashusha miguu chini, nikawa nimekaa huku nikitazama huku na kule. Sikuweza kuona chochote kutokana na giza lililokuwa limetanda usiku huo. Mara nikasikia kishindo kizito kama cha kitu kilichodondoka kutoka darini mpaka sakafuni, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kuliko kawaida.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 27
ILIPOISHIA:
Sikutaka kumuamsha Rahma, nilimtoa kifuani kwangu taratibu kisha nikashusha miguu chini, nikawa nimekaa huku nikitazama huku na kule. Sikuweza kuona chochote kutokana na giza lililokuwa limetanda usiku huo. Mara nikasikia kishindo kizito kama cha kitu kilichodondoka kutoka darini mpaka sakafuni, mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio kuliko kawaida.
SASA ENDELEA...

Nilikaza macho kwenye giza kujaribu kuangalia ni kitu gani hicho kilichodondoka, kwa mbali nikaanza kuona kama mtu amepiga magoti kwenye kona ya chumba hicho, taratibu akaanza kuinuka, nikazidi kumkazia macho na kadiri muda ulivyokuwa ukizonga ndivyo nilivyozidi kuiona vizuri taswira yake.
Nilimtambua kwamba ni mwanamke kutokana na maumbile yake ingawa alionesha kuwa ni mzee kwani niliweza kuiona ngozi yake ilivyokuwa imekunjamana, nikamkazia macho usoni nikitaka niione sura yake. Hata hivyo eneo la usoni lilikuwa na giza sana, nikamuona akiinua mikono juu kama anayetoa ishara fulani, akageuka na kuanza kujisugua makalio yake ukutani.
Mara nilisikia kishindo kingine, hofu ikazidi kutanda ndani ya moyo wangu, kijasho chembamba kikawa kinanitoka huku nikiwa nimekodoa macho kwa nguvu zote.
Nilitamani niamke nikawashe taa lakini ujasiri huo sikuwa nao, nilitamani niingie chini ya kitanda lakini mwili wote haukuwa na nguvu, nilitamani kupiga kelele kuwaamsha nyumba nzima lakini sikuwa na uwezo huo, nikawa natetemeka kuliko kawaida.
Nilipotazama kwa makini pale chini, nilimuona mtu mwingine kama yule wa kwanza naye akiinuka taratibu lakini tofauti yake, huyu alikuwa mwanaume kutokana na jinsi mwili wake ulivyokuwa na alionesha pia kuwa mzee zaidi maana mpaka mgongo wake ulikuwa umepinda.
Alipoinuka, naye alisogea ukutani na kuanza ‘kusonta’ ukutani kwa kutumia makalio yake kisha akasogea mbele na kushikama mikono na yule mwanamke wa kwanza, wakaiinua juu na kutoa ishara ambayo sikuielewa, mara nikasikia vishindo mfululizo.
Vilisikika vishindo kama sita hivi, ikimaanisha kwamba watu wengine sita walikuwa wameingia, uzalendo ukanishinda. Sijui nilipata wapi ujasiri, nikasimama wima kisha nikapaza sauti, ‘tokeni hapa washenzi nyie, hata mimi baba yangu ni mchawi vilevile’.
Kauli yangu ni kama iliwashtua watu wale wa ajabu ambao hata sielewi niwaelezeeje, wote wakashtuka na kunitazama, nikazidi kushtuka baada ya kuona wote macho yao yalikuwa yakiwaka kama mnyama mkali gizani.
Kwa wale ambao wameishi maeneo ya maporini watakuwa wananielewa kwamba mida ya usiku, wanyama kama simba, chui, mbwa mwitu au hata mbwa wa kawaida na paka, wakiwa kwenye giza totoro kisha wakakukodolea macho yao, huwa yanatoa mwanga fulani wa kutisha.
Kwa jinsi walivyonitazama, hofu ilinizidi maradufu lakini nikaona hakuna kingine cha kufanya zaidi ya kuendelea ‘kugangamala’. Sikuwa najua kama wakinigeukia nitafanya nini, sikuwa najua mbinu zozote za kupambana nao na eti nilijikuta nikijilaumu kwa nini baba hakunifundisha au hakunipa mbinu yoyote ya kukabiliana na wachawi.
Yule mwanamke aliyekuwa wa kwanza kuingia mle ndani, nilimuona akinisogelea huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya woga. Nilihisi haja ndogo ikitaka kunitoka lakini nilijikaza kiume na kusema liwalo na liwe, akanisogelea jirani kabisa huku akiendelea kunitazama kwa macho yake makali, cha ajabu, licha ya kunisogelea, sikuweza kabisa kuitambua sura yake.
Nimewahi kusikia kwamba wachawi wana kawaida ya kula nyama za watu, nikahisi na mimi usiku huo nakwenda kuliwa huku nikijiona. Niliujutia uamuzi wangu wa kusimama na kuwafokea watu hao, nikiwa bado natetemeka, nilisikia kofi moja zito likitua kwenye shavu langu la kushoto, maumivui niliyoyasikia yalikuwa hayaelezeki, nikapiga kelele kwa nguvu nikimuita baba.
Sikumbuki kama nimewahi kutoa sauti kubwa kama hiyo maishani mwangu, mara mlango ukaanza kugongwa kwa nguvu nje, nikasikia kibao kingine kikitua kwenye shavu la upande wa pili, likafuatiwa na misonyo mingi kisha wale watu wakayeyuka wote na kupotea kama moshi upoteavyo angani.
“Togo! Nini kimetokea?” alisema baba baada ya kuwa amefanikiwa kufungua mlango na kuwasha taa. Jambo la aibu ni kwamba baada ya ule mchezo wa kikubwa niliocheza na Rahma, hakuna aliyekumbuka tena kuvaa nguo zake kwa hiyo nilikuwa kama nilivyozaliwa, baba akanitazama kwa mshangao.
Najua alishangazwa na mambo mengi kwa wakati mmoja, kwanza kwa nini nilikuwa chumbani kwa Rahma mpaka usiku huo wakati makubaliano yalikuwa ni kwamba kila mmoja atalala kwake, kwa maana kwamba baada ya c hakula ilitakiwa mimi nitoke na kwenda kwenye chumba nilichopangiwa lakini sikufanya hivyo. Yote tisa, kumi ni kwamba nilikuwa kama nilivyozaliwa, na Rahma naye ambaye bado alikuwa kwenye usingizi mzito, akikoroma bila kujua chochote kilichokuwa kinaendelea, hakuwa na chochote mwilini, nikamuona baba akishusha pumzi ndefu na kunipa ishara kwamba nivae kwanza nguo, akatoka na kuurudisha mlango.
Kumbe sekeseke hilo lilisababisha nitokwe na haja ndogo bila kujua, ikabidi nichukue tambara la kufanyia usafi na kufuta harakaharaka huku nikigeuka kumtazama Rahma asije kuwa ameamka na kuona nilichokifanya. Nilipomaliza kufuta, harakaharaka nilivaa nguo zangu huku nikitetemeka kuliko kawaida.
Baba alikuwa pale mlangoni akinisubiri, nilipomaliza aliingia na kunionesha ishara kwamba nisizungumze kwa sauti ya juu, akaniuliza nini kilichotokea.
“Wachawi baba, wachawi wengi wamekuja, angalia walivyonifanya,” nilisema huku nikimuonesha mashavu yangu ambayo nilikuwa nahisi kama yanawaka moto. Awali niliona baba hataki kuamini kama ambavyo imekuwa kawaida yake mara kwa mara ninapotokewa na mambo kama hayo lakini nashukuru safari hii kulikuwa na ushahidi wa moja kwa moja.
“Mungu wangu, umefanya nini?”
“Wamenipiga,” nilisema huku nikianza kutokwa na machozi.
“Hebu niambie ukweli, umefanya tena mapenzi na Rahma?”
“Ndiyo.”
“Lakini si tumeshawakataza nyie na kuwasisitiza kwamba msirudie ujinga wenu?” baba alizungumza kwa hasira lakini kwa sauti ya chini. Sikujua kwa nini alikuwa akizungumza kwa sauti ya chini, akanishika mkono na kufungua mlango, akatazama huku na kule na alipojiridhisha, alinipeleka mpaka kwenye chumba ambacho ndicho nilichotakiwa kulala.
“Hutakiwi kumwambia yeyote kuhusu hiki kilichotokea, umenielewa?” baba aliniambia, nikatingisha kichwa lakini nilijiuliza, kama yeye ameweza kusikia zile kelele nilizopiga, si ina maana nyumba nzima wamesikia? Na kama wamesikia, kwa nini wengine wote hawakuamka isipokuwa yeye tu?
“Lakini kwa nini haya yanatokea?” utajua tu lakini unachoniudhi ni kwamba ukiambiwa jambo fulani usilifanye, wewe ndiyo unalifanya. Hukuwa na mambo ya wanawake kabisa lakini tangu tumefika hapa ndiyo umekuwa mchezo wako... utasababisha vifo vya wasio na hatia kwa nini unakuwa mgumu kuelewa?” baba alisema, safari hii siyo kwa ukali bali kwa hisia za ndano kabisa, kauli yake ikanishtua mno.
Yaani mimi ndiyo nisababishe vifo vya wasio na hatia? Kivipi? Halafu kulikuwa na uhusiano gani wa mimi kulala na Rahma na hayo yaliyokuwa yanatokea? Katika yote, jambo ambalo nilijiapiza, ni kwamba kamwe sitamuacha Rahma maana alikuwa amenionesha dunia ya tofauti mno.
Baba alitoa kichupa kilichokuwa na unga mweusi lakini kabla hajafanya chochote, aliniambia nikajitazame kwenye kioo kilichokuwa humo chumbani.
“Mungu wangu,” nilisema kwa mshtuko usio wa kawaida.
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 28
ILIPOISHIA:
Baba alitoa kichupa kilichokuwa na unga mweusi lakini kabla hajafanya chochote, aliniambia nikajitazame kwenye kioo kilichokuwa humo chumbani.
“Mungu wangu,” nilisema kwa mshtuko usio wa kawaida.
SASA ENDELEA...

Uso wangu ulikuwa umebadilika na kuwa mweusi tii kama mkaa. Kilichoonekana ilikuwa ni macho na meno tu. Nilishindwa kuelewa kwa nini mimebadilika na kuwa vile, sikujua kama ni yale makofi ya nguvu niliyopigwa au ni nini.
“Usishtuke, na huo mchezo wako ukiendelea nao yatakufika makubwa zaidi, yaani unaonekana umeonja asali na sasa unataka kuchonga mzinga kabisa. Hukuwa na mambo ya kupenda wanawake, nini kimekusibu?” alisema baba lakini maneno yake yaliingilia sikio moja na kutokea jingine.
Akili yangu ilikuwa ikiwaza kuhusu mabadiliko yaliyotokea kwenye uso wangu. Nilishindwa kuelewa itakuwaje kama nitaendelea kuwa hivyo, nilijikuta nikiishiwa nguvu kabisa, nikakaa chini huku hofu kubwa ikiwa imetanda moyoni mwangu.
“Si naongea na wewe?” alinihoji baba huku akiwa amekishika kile kichupa, sikumjibu chochote kwa sababu akili yangu ilikuwa ikiwaza mambo mengine tofauti kabisa. Suala la kuacha kufaidi penzi la Rahma halikuwepo kabisa kichwani mwangu, kwa sababu hata wao wenyewe walijaribu kulizuia lakini kilichotokea kila mmoja akawa shahidi.
“Hebu inuka,” alisema baba kwa jazba, nadhani ni baada ya kuona simpi ushirikiano. Nilisimama, akatoa wembe kwenye mfuko wa mbele wa shati yake, akanichanja kwenye paji la uso, juu kidogo ya sehemu nywele zinapoanzia.
Akanipaka ile dawa, yaani kwa jinsi ilivyokuwa inauma, nilishindwa kujizuia, nikawa napiga kelele, baba akanikamata na kuniziba mdomo huku akinionesha ishara ya kunyamaza.
“Inatakiwa ujikaze, halafu hakikisha asubuhi hakuna mtu yeyote anayejua kilichotokea, ni mambo ya aibu sana na yatatusababishia matatizo makubwa, si unajua ndiyo kwanza tumefika na hapa ni kwa watu?”
“Nataka kujua wale ni akina nani na wametoka wapi? Kwa nini wameingia chumbani kwa Rahma?”
“Nitakujibu lakini siyo leo,” alisema baba huku akinisisitiza kwamba nilale na nisiende tena chumbani kwa Rahma. Hakuna jambo ambalo lilikuwa likinikera kwa baba kama kila ninapomuuliza kuhusu mauzauza yanayonitokea yeye anakimbilia tu kusema kwamba atanijibu. Alitoka na kurudia kunisisitiza kwamba nisitoke na asubuhi nisimwambie yeyote kuhusu kilichotokea.
“Na huu uso itakuwaje?”
“Hiyo dawa niliyokupaka itakusaidia, mtu yeyote akikuuliza mwambie umeamka tu asubuhi na kujikuta ukiwa hivyo,” alisema. Nikasogea tena kwenye kioo na kujitazama. Yaani hata sikujua kama asubuhi kukipambazuka halafu nikawa bado kwenye hali hiyo itakuwaje maana kiukweli nilikuwa natisha.
Kwenye upande wa shavu la kushoto na kulia, kulikuwa na alama za vidole za yule bibi kizee sehemu aliponipiga makofi, nikaapa siku nitakayomjua halafu nikakutana naye barabarani, lazima na mimi nimlipizie.
Nilijaribu kujilaza kitandani lakini usingizi haukuja kabisa, mara kwa mara nilikuwa nikisikia vishindo vikubwa juu ya bati kama kuna watu wanapigana, huku wakati mwingine sauti za ajabu zikisikika. Nilikuja kupata usingizi wakati kumeshaanza kupambazuka kabisa.
Kwa kuhofia kwamba ndugu yangu akiamka anaweza kuniona nilivyokuwa natisha usoni, nilijifunika ‘gubigubi’. Nilimsikia akijiongelesha kama aliyeshtuka kuniona nimelala pembeni yake wakati hakumbuki usiku niliingia saa ngapi.
“Unaendeleaje Togo,” aliniuliza lakini nilijikausha na kujifanya nimepitiwa na usingizi.
“Togoo!” aliniita huku akivuta shuka kwa nguvu. Kwa kuwa sikutegemea tukio hilo, alifanikiwa kunifunua na mimi bila hata kufikiri mara mbili, nikaamka kwa hasira, tukawa tunatazamana.
“Mbonaunapenda kunisumbua wakati unajua mwenzio naumwa?”
“Hee... huko usoni umefanya nini?” aliniuliza huku akirudi nyuma kwa hofu, akafungua mlango na kutoka mbio. Nilijikuta nikikosa amani mno, ikabidi nisogee na kujitazama tena kwenye kioo. Bado uso wangu haukuwa umerudi kwenye hali yake.
Japokuwa ule weusi kidogo ulikuwa umepungua lakini bado mtu yeyote asingeweza kunitazama usono bila kushtuka. Pia mashavu yote mawili yalikuwa yamevimba huku damu ikiwa imevilia kwenye zile alama za vidole na kwenye jicho langu la kushoto.
“Eti kuna nini,” baba alisema huku akifungua mlango. Kumbe kutokana na mshtuko alioupata alikuwa amekimbia na kwenda kumuita baba.
“Huyu mjinga eti mimi nimelala yeye ananivuta shuka,” nilisema huku nikikwepa kutazamana usoni na baba. Aliligundua hilo, akanilazimisha nimuangalie.
“hebu ngoja nakuja, na wewe acha ujinga wa kupigapiga kelele, inamaana hujui kama mwenzenu anaumwa,” alisema baba kwa kumkaripia yule ndugu yangu, nikamuona ‘limemshuka’ maana alitegemea baba atashtuka kama yeye.
“Kwanza ondoka muache apumzike,” alisema baba, ikabidi atoke naye, nikajilaza tena kitandani nakujifunika vizuri. Nikawa naendelea kutafakari mambo mengi yasiyo na majibu. Muda mfupi baadaye, baba alirejea akiwa na kimkoba chake kidogo, akaniamcha na kunitaka nifanye kama anavyoniambia.
Kuna kimzizi fulani alikitoa kwenye mkoba wake, akipa na kuniambia nikitafune lakini nisimeze mate. Nilipokitia mdomoni, niligundua kwamba kilikuwa kichungu sana, nikakitafuna huku nikiwa nimekunja sura.
‘Temea mate kwenye mkono wako wa kushoto na ujipake kwenye shavu la kulia,” alisema huku akinisisitiza kuwa makini. Nilifanya hivyo, nikajipaka kwenye shavu na kuhisi kama moto unawaka. Tema mengine kwenye mkono wa kulia na ujipake kwenye shavu la kushoto,” aliniambia, nikafanya hivyo, maumivu yakazidi ikuongezeka, nikawa nahisi kama ngozi ya sura inajaa kama puto.
“Nifuate,” alisema, akafungua mlango na kuelekea bafuni, nikamfuata ambapo alinielekeza namna ya kusimama kisha akafungulia maji na kuanza kunimwagia kichwa kizima huku akinisugua na kunipaka ungaunga mwingine uliokuwa na ladha kama magadi.
Alinisafisha kwa muda mrefu kisha akatoa kipande cha kitambaa na kunifuta, akaniambia nisifumbue macho mpaka atakaponiambia. Alinishika mkono na kunirudisha chumbani, akanilaza kitandani na kuniambia nifumbue macho.
“Inabidi ulale hivyo kwa dakika saba, zikiisha amka halafu ujitazame tena kwenye kioo,” aliniambia baba, akakusanya vitu vyake na kuondoka. Nikawa nasubiri hizo dakika saba ziishe maana aliniambia atakuja mwenyewe kuniambia. Baba alikuwa na mambo mengi sana yenye utata, hasa huo ujuzi wake wa mitishamba na dawa za kiganga.
Nililala pale kitandani lakini kwa mbali nilianza kujihisi hali fulani hivi isiyo ya kawaida. Sikutaka kuitilia maanani kwani bado uso wangu ulikuwa ukiwaka moto kwa maumivu. Dakika saba baadaye, kweli baba alirudi na kuniamsha, nikasogea na kujitazama kwenye kioo. Huwezi kuamini, uso wangu ulikuwa umerudi kwenye hali yake ya kawaida ingawa jicho moja bado lilibaki limevilia damu na zile alama za vidole mashavuni zenyewe hazikufutika.
Alitoka na kuniacha mwenyewe, angalau moyo wangu ukawa na amani. Nilisimama kwa muda pale mbele ya kioo nikiendelea kujitazama. Ile hali sasa ilizidi kunisumbua na kunifanya nijisikie vibaya. Yaani kwa jinsi nilivyokuwa najisikia, ilikuwa ni kama nimeshikwa na kiu kali lakini tofauti na kiu ya kawaida, ilikuwa ni kiu ya kukutana kimwili na mwanamke.
Nilibaki nikijishangaa mwenyewe kwani kadiri muda ulivyokuwa ukisonga mbele ndivyo nilivyokuwa nikizidi kuteseka. Wakati nikiendelea kuugulia ndani kwa ndani, nilishangaa kwa nini rahma mpaka muda huo hakuwa amekuja kuniuliza nimeamkaje na hata sauti yake sikuisikia. Japokuwa baba alikuwa amenikanya sana, kwa jinsi hali ilivyokuwa, niliamini yeye ndiye anayeweza kuwa msaada kwangu kwa sababu tunapendana.
Nilitoka na kusogea kwenye mlango wa chumbani kwake lakini kabla sijashika kitasa, nilisikia sauti ya mdogo wake wa kiume akiniambia kwamba hakuwepo, alikuwa ameondoka na mama yake asubuhi na mapema kufuatilia mambo ya chuo. Ni kweli jana yake alikuwa amenidokeza kuhusu suala hilo lakini sijui kwa nini sikukumbuka. Nilijikuta nikiishiwa nguvu kwani sikujua nini kitafuatia.
Nilirudi chumbani kwangu huku hali ikizidi kuwa mbaya, sijui ni machale gani yalimcheza baba, mara akafungua mlango na kunikuta nikiwa kwenye hali ambayo haielezeki.
“Ule mzizi niliokupa na kukwambia uutafune lakini usimeze, ulifanya kama nilivyokwambia?” baba aliniuliza. Kiukweli baada ya kutema mate kwenye mkono wa kushoto na kulia, mengine yaliyobakia, pamoja na mabaki ya mzizi wenyewe, nilivimeza vyote. Nilipomwambia hivyo baba, alishtuka kuliko kawaida. Sikujua kwa nini ameshtuka kiasi hicho, akatoka haraka.
Nikiwa bado naendelea kuugulia, nilisikia ndugu yangu mmoja akiniita kutokea dirishani, nikafunua pazia na kuchungulia nje. Sikuyaamini macho yangu baada ya kumuona akiwa na yule msichana tuliyesafiri naye, harakaharaka nikafungua dirisha huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 29
ILIPOISHIA:
Nikiwa bado naendelea kuugulia, nilisikia ndugu yangu mmoja akiniita kutokea dirishani, nikafunua pazia na kuchungulia nje. Sikuyaamini macho yangu baada ya kumuona akiwa na yule msichana tuliyesafiri naye, harakaharaka nikafungua dirisha huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wangu.
SASA ENDELEA...

“Mambo Togo?”
“Safi, karibu,” nilisema huku nikitazama huku nakule. Yule ndugu yangu alikuwa amesimama pembeni akikutazama kwa zamuzamu.
“Samahani nina maongezi kidogo na wewe,” alisema. Kwa hali niliyokuwa nayo, nilikuwa nikifikiria jambo moja tu kutokakwake, mapenzi.
“Nisubiri kwa kule mbele,” nilimuelekeza huku harakaharaka nikitoka na kuelekea bafuni. Nilijimwagia maji ya baridi kwa wingi ili angalau nitulie kisha nikarudi chumbani na kuvaa nguo.
Nilijitazama tena kwenye kioo, bado nilikuwa na alama za kuvilia damu usoni lakini sikujali, akili yangu ilikuwa ikihitaji kitu kimoja tu kwa wakati huo. Nilitoka kimyakimya bila kumuaga mtu yeyote mpaka nje.
Nikamfuata yule ndugu yangu na kumwambia kwamba iwe siri yetu nitampa zawadi, nikamsisitiza kwamba asimwambie mtu yeyote. Alikubali, nikamshukuru nakumfuata yule msichana ambaye alionesha kuwa na shauku kubwa ya kuonana na mimi.
Tulitoka mpaka nje kabisa, sehemu ambayo mtu yeyote aliyekuwa ndani asingeweza kutuona, akanikumbatia kwa nguvu na kunibusu shingoni. Nilijikuta nikisisimka mno, nikawa nachekacheka tu mwenyewe.
Aliniambia kuna mahali anataka rtwende pamoja kwa sababu alikuwa na jambo muhimu lililokuwa likimsumbua ndani ya moyo wake. Nilimuuliza amepata wapi ujasiri wa kuingia mpaka kule ndani? Akaniambia ilikuwa ni muhimu sana kuonana na mimi na ndiyo maana hakujali chochote.
“Huwa unakunywa pombe?” aliniuliza, nikatingisha kichwa kumkatalia. Licha ya kujaribu mara kadhaa kunywa pombe za kienyeji tukiwa Chunya, kiukweli kichwa changu kilikuwa kibovu sana, kiufupi sikuwa na uwezo wa kuhimili pombe. Akacheka sana huku mara kwa mara akinipigapiga begani.
“Chagua sehemu ambayo unadhani inaweza kufaa kwa mazungumzo ya mimi na wewe, twende beach, Mlimani City au tutafute ‘lodge’ yoyote nzuri,” aliniuliza l;akini kati ya sehemu zote alizozitaja, ni moja tu ndiyo niliyokuwa naelewa, beach. Sikuwa najua Mlimani City ndiyo wapi na kupoje wala sikuwa najua huko ‘lodge’ ni wapi na kuna nini cha muhimu. Waliosema ushamba mzigo, hawakukosea.
Ilibidi nimuulize ili anipe ufafanuzi, akacheka sana, akaniambia Mlimani City ni kituo maalum cha kibiashara, mahali ambapo kuna maduka makubwa, mabenki, migahawa ya kisasa ya sehemu mbalimbali za starehe. Akaniambia pia kuwa neno lodge ni la Kiingereza lakini linamaanisha nyumba ya kulala wageni. Nikashtuka!
“Unamaanisha gesti?”
“Ndiyo?” alinijibu huku akinitazama kwa macho yake mazuri, ikabidi nijifanye sitaki nataka kwa sababu kule kwetu kulikuwa na stori kwamba watu wanaoingia gesti wakati hawapo safarini ni wale wahuni walioshindikana. Nikamwambia kwamba Mlimani City atanipeleka siku nyingine, akanitazama tena usoni na kuachia tabasamu pana.
Japo jibu langu halikuwa la moja kwa moja, nadhani alinielewa haraka nilikuwa namaanisha nini. Tuliingia kwenye Bajaj, nikageuka huku na kule na nilipohakikisha hakuna aliyeniona, nilimpa ishara kwamba tuondoke.
Kwa makusudi kabisa, aliniegamia kimahaba huku mara kwa mara akiendelea kuniangushia mabusu ya hapa na pale. Yaani kama angekuwa anajua kilichokuwa ndani ya kichwa changu, kamwe asingethubutu kumwagia petroli kwenye moto.
Hatukwenda mbali sana, Bajaj ikaingia kwenye jengo moja la kisasa, getini likiwa na maandishi yaliyosomeka Sideview Hotel, tukashuka kwenye Bajaj, nikawa nashangaashangaa huku na kule, alinishika mkono bila hata wasiwasi, tukaingia mpaka ndani ambapo alimfuata dada wa mapokezi na kuanza kuzungumza naye.
Alimwambia anahitaji chumba kwa siku nzima mpaka kesho yake. Nilishangaa kwa nini anataka tukae mpaka kesho yake wakati anajua mimi ni mgeni na nilikuwa chini ya wazazi wangu. Hata hivyo, sikutaka kumhoji chochote mpaka nipate nilichokuwa nakitaka.
Alitoa pochi yake na kuhesabu fedha, akampa yule mhudumu, akatoka na funguo na kwenda kutuonesha chumba chenyewe. Kilikuwa chumba kizuri mno, yaani pengine kuliko vyumba vya kwenye majumba ya watu wengi sana. Picha niliyokuwa nimeijenga kichwani mwangu mwanzoni, nilitegemea chumba kitakuwa kama vile vya gesti za kijiji, kitanda kidogo chenye kunguni na kilicholegea, godoro chafu na jembamba sambamba na mashuka makuukuu.
Kitanda kilikuwa kikubwa, juu yake kikiwa kimetandikwa kwa mashuka meupe na mito mikubwa mizuri, chini kikiwa kimepigwa marumaru safi nyeupe, huku taa zenye mwanga fulani mzuri zikizidi kuyapendezesha mandhari ya chumba hicho, nikawa nashangaashangaa.
Sikuwa na habari kwamba mwenzangu bila hata kuzungumza kile alichosema tunataka kuzungumza, ameshaanza kufaanya kazi nyingine. Alikuwa tayari ameshavua blauzi yake na kubaki na bra, akawa anahaha kufungua suruali yake iliyokuwa imembanana kulichora vilivyo umbo lake. Nilijikuta nikitetemeka mwenyewe, hata sijui ni kwa nini, nikampa mgongo.
“Togo! Mimi mwenzio na...ku..pe...” alishindwa kumalizia alichotaka kukisema, akagusanisha mdomo wake na wangu huku mikono yake ikiwa imenibana kisawasawa kwenye kifua chake kilichosheheni. Kwa kuwa rahma alikuwa amenipa ‘twisheni’ ya mambo hayo, na mimi sikutaka kubaki nyuma, nilimpa ushirikiano, tukawa tunaelea kwenye ulimwengu tofauti kabisa.
Ile halai niliyokuwa naisikia mwanzo, safari hii ilizidi mno, yaani nikawa naona kama nachelewa. Tofauti na Rahma, huyu yeye hakuwa na aibu kabisa na kila alichokuwa anakifanya, alikuwa akifanya kwa kujiamini. Akaninyonyoa manyoya yote kama kuku aliyechinjwa huku na yeye akifanya hivyohivyo, muda mfupi baadaye, tukawa ‘saresare’ maua.
“Togoo!” aliniita kwa mshtuko huku akiwa amepigwa na butwaa iliyochanganyikana na furaha.
“Kumbe upo hivi,” alisema huku akinitazama kwa macho yake kama anasikia usingizi, sikuelewa kauli yake hiyo ilikuwa ikimaanisha nini, lakini aliendelea kunimwagia sifa lukuki kwamba siku ya kwanza aliponiona tu aligundua kwamba nina sifa za kipekee ambazo wanaume wengine hawana.
Sikutilia sana maanani kile alichokuwa anakisema, akili yangu ilikuwa ikiwaza jambo moja tu. Muda mfupi baadaye, tuliianza safari huku mimi nikiwa ndiyo kiongozi wa msafara. Unajua kama una kiu kali ya maji, hata ukipewa jagi zima unaweza kulifakamia lote mpaka liishe. Hicho ndicho kilichotokea kwangu.
Ghafla nilishangaa akianza kugeuza macho na kutupatupa mikono na miguu kama mtu anayetaka kukata roho, haraka nikashuka chini na kuanza kumtingisha kwa nguvu huku nikishindwa hata namna ya kumuita maana kiukweli sikuwa nalijua jina lake.
Kadiri nilivyokuwa namtingisha ndivyo alivyozidi kulegea, mara akatulia huku macho yake yakiwa yamegeuka na kutazama upande wa juu. Nilijaribu kusikiliza mapigo ya moyo wake lakini hayakuwa yakipiga na hakuwa akipumua.
“Mungu wangu,” nilisema huku nikianza kutafuta nguo zangu, harakaharaka nikavaa huku kijasho chembamba kikinitoka, nikawa najiuliza nini cha kufanya maana tayari ulishakuwa msala. Hakuna ambaye angeamini kwamba msichana huyo amekufa mwenyewe, wangejua kwamba nimemuua, nilijikuta nikitetemeka mno.
Akili niliyoipata, ilikuwa ni kuondoka haraka hotelini hapo bila mtu yeyote kujua. Nilichukua shuka na kumfunika kisha nikafungua mlango. Nilitazama huku na kule, nilipoona hakuna mtu, nilitoka na kuurudishia mlango, harakaharaka nikawa natembea kuelekea nje.
Kwa bahati nzuri, nilipofika pale mapokezi, yule dada hakuwepo, nikatoka kimyakimya mpaka nje, nikaelekea lilipo geti kubwa huku nikijitahidi kuvaa tabasamu la uongo ili walinzi wa hoteli hiyo wasishtukie chochote.
“Aroo! We kijana... Aroo wewe,” nilisikia sauti ya mlinzi wa nje ya geti la hoteli hiyo akiniita, moyo ukalipuka paah!
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na hatia)- 30
ILIPOISHIA:
Kwa bahati nzuri, nilipofika pale mapokezi, yule dada hakuwepo, nikatoka kimyakimya mpaka nje, nikaelekea lilipo geti kubwa huku nikijitahidi kuvaa tabasamu la uongo ili walinzi wa hoteli hiyo wasishtukie chochote.
“Aroo! We kijana... Aroo wewe,” nilisikia sauti ya mlinzi wa nje ya geti la hoteli hiyo akiniita, moyo ukalipuka paah!
SASA ENDELEA...

“Unaenda wapi?”
“Naenda dukani afande.”
“Mwenzako umemuacha wapi?”
“Yupo ndani, narudi sasa hivi, naenda kununua kinga.”
“Mbona kama una wasiwasi?” alisema yule mlinzi huku akinisogelea. Licha ya kujaribu kucheza na akili zake, ni kama alishashtukia jambo kwa jinsi nilivyokuwa na hofu. Mtu kukufia chumbani, usifanye mchezo.
Hata kama ulikuwa jasiri vipi, lazima uchanganyikiwe. Hicho ndicho kilichonitokea. Hofu ilishindwa kujificha kwenye macho yangu, nikawa nakwepesha macho kwa sababu niliamini yule mlinzi kwa jinsi alivyonishupalia, angeweza kugundua kitu. Nilitamani kufanya kitu lakini sikuwa na uwezo, harufu ya jela ikaanza kunukia.
“Mkazie macho usoni,” ile sauti ya ajabu ya baba, ilisikika masikioni mwangu, nikageuka huku na kule lakini baba hakuwepo eneo hilo. Kwa kuwa mara zote ilikuwa ikinisaidia, nilifanya kama nilivyoelezwa.
Nilimkazia macho yule mlinzi, na yeye akanitazama. Ghafla nikashangaa anakuwa mpole ghafla, mwanzo alikuwa amekunja sura lakini ghafla alitabasamu. Niliendelea kumkazia macho.
‘Haya nenda, unajua siku hizi kumekuwa na matukio ya ajabu sana kwenye hizi nyumba za kulala wageni kwa hiyo lazima tuwe makini,” alisema huku akichekacheka, akageuka na kurudi getini. Sikuamini kilichotokea.
Kwa tafsiri nyepesi, baba alikuwa anaona kila kinachoendelea kwa sababu asingeweza kuniambia maneno yale tena katika muda muafaka kabisa. Hofu yangu ilikuwa ni je, anajua nilichokifanya kule gesti? Mara kwa mara alikuwa akinikanya lakini kwa ubishi wangu nikaona kama ananibania nisifaidi.
Sikuwa nalijua Jiji la Dar es Salaam wala sikuwa najua ramani ya kunifikisha nyumbani, kitu pekee nilichokumbuka, ni barabara ile tuliyojua, nikawa natembea harakaharaka huku nikitamani kama ningekuwa na uwezo ningepaa kabisa na kutoweka eneo hilo.
Nilinyoosha na barabara na nilipofika mbali, nilianza kukimbia, hofu kubwa ikiwa imetanda kwenye moyo wangu. Kwa bahati mbaya zaidi, sikuwa nakumbuka sehemu ambayo tulikatia kona na kutokezea kwenye barabara hiyo, nikajikuta nikipoteza uelekeo, nikawa nazunguka huku na kule, kijasho chembamba kikinitoka.
Sikuwa na fedha mfukoni kwamba ningezitumia kukodi bodaboda na kuwaelekeza nyumbani. Nikiwa naendelea kuumiza kichwa, hatimaye nilipata akili mpya. Pale nyumbani, kwa nje kulikuwa na kituo cha madereva wa Bajaj na nimewahi kusikia kwamba wenyewe wana umoja wao na wanajiita City Boys wakimaanisha watoto wa mjini.
Kuna Bajaj ilikuwa ikija mbele yangu, nikaipiga mkono, ikapunguza mwendo na hatimaye ikasimama. Nilimfuata dereva na ikabidi niwe mkweli kwake, nikamwambia kwamba nimepotea na ramani pekee iliyopo kichwani mwangu, ni kituo cha Bajaj cha City Boys.
Alicheka kisha akaniambia niingie kwenye Bajaj yake, nikamtahadharisha kwamba sikuwa na fedha, akaniambia atanisaidia.
“Wewe si unakaa pale kwa akina Rahma, mbona mimi nakujua,” alisema yule kijana kwa uchangamfu, nikamshukuru Mungu wangu na kuelewa kwa nini alicheka nilipomueleza kwamba nimepotea.
‘Mimi nakusaidia lakini na wewe nataka unisaidie jambo, unajua mi nampenda sana yule dada Rahma ila naogopa kumwambia ukweli maana muda wote yupo ‘sirias’, nataka unisaidie kufikisha ujumbe, mwambie Zedi dereva teksi, ukifanikisha ntakuwa nakuja kukuchukua nakutembeza viwanja mbalimbali na Bajaj, hata ukitaka pesa ntakuwa nakutoa,” aliniambia yule dereva Bajaj.
Kwa kuwa nilikuwa na shida kwa wakati huo, nilimkubalia kila alichokuwa anakisema. Hakuwa akijua kwamba mimi ndiye mmiliki wa Rahma. Kumbe sikuwa mbali sana na nyumbani, muda mfupi baadaye tukawa tumeshafika, akanishusha getini na kunisisitiza kuhusu ombi lake, nikazidi kumdanganya kwamba asiwe na wasiwasi.
Niliposhuka niliingia moja kwa moja ndani huku bado hofu kubwa ikiwa imetanda kwenye moyo wangu.
“Ulikuwa wapi?” mama aliniuliza kwa ukali mara tu nilipofika sebuleni. Nikakosa cha kujibu kwa muda, nikawa najiumauma, baadaye nikamwambia kwamba kuna rafiki yangu nilikuwa nimemsindikiza.
“Rafiki? Rafiki gani? Una rafiki hapa mjini wewe?” mama alinihoji huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara. Ilibidi ninyamaze kimya, nikataka nipitilize kwenda chumbani lakini aliniambia nataakiwa kukaa nao hapohapo sebuleni kwa sababu ninapopewa muda wa kuwa huru nashindwa kuutumia uhuru wangu vizuri.
Huo ulikuwa mtihani mkubwa sana kwangu, ikabidi nimwambie mama kwamba bado sijisikii vizuri, akaniambia nitakapotoka tena bila ruhusa yake au bila kuaga, atanisemea kwa baba aninyooshe. Nilifurahi kwa sababu aliniruhusu niende chumbani kwangu.
Nilipoingia tu, nilijifungia kwa ndani, nikakaa kwenye ukingo wa kitanda na kujiinamia, maswali mengi yakiendelea kupita ndani ya kichwa changu. Sikuwa najua nini itakuwa hatima yangu endapo ukweli utafahamika. Hata hivyo, kwa upande mwingine, nilianza kujiuliza mimi kosa langu ni nini kwa sababu, yeye ndiye aliyenifuata hadi nyumbani na ndugu yangu alikuwa shahidi.
Yeye ndiye aliyenishawishi twende kwenye nyumba ya kulala wageni na hata tulipofika, alionesha wazi kwamba alikuwa akinihitaji na kwa vile na mimi nilikuwa kwenye hali mbaya, tulijikuta tukiangua dhambini.
Nilijaribu kujiuliza kwamba labda kuna kitu kisicho cha kawaida nilimfanyia mpaka yakatokea ya kutokea lakini sikukumbuka chochote. Bado niliendelea kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
Nikiwa nimejifungia chumbani, mara nilianza kusikia kelele sebuleni, ndugu zangu wakawa wananiita nikaangalie. Ilibidi nitoke na kwenda mpaka sebuleni. Habari za dharura au Breaking News kama wengi walivyozoea kuita, zilikuwa zikioneshwa runingani moja kwa moja kutoka eneo la tukio.
Zilikuwa ni habari za samaki hatari aina ya papa kuvamia kwenye ufukwe wa bahari ya Hindi na kusababisha vifo vya watu kadhaa, wakiwemo wavuvi na wengine waliokuwa wakiogelea ufukweni huku wengine kadhaa wakijeruhiwa. Nilijikuta moyo wangu ukilipuka kuliko kawaida.
Kilichonishtua ni kwamba, mazingira ya tukio lile, yalikuwa sawa kabisa na kile kilichonitokea nilipoenda ufukweni na Rahma.
Habari zilieleza kwamba wavuvi walaikuwa kwenye boti yao wakivuta nyavu lakini ghafla, samaki huyo aliwashambulia kwa kuvunjavunja boti yao na kuanza kuwala, mmoja baada ya mwingine, hali iliyosababisah maji ya bahari yageuke rangi na kuwa mekundu.
Yaani kilekile nilichokieleza na kila mmoja kuniona kama mwendawazimu, ndicho kilichokuwa kimetokea, taarifa ya habari iliendelea kueleza kwamba polisi na vikosi vya uokoaji, wamefika eneo la tukio na wanahangaika kupambana na samaki huyo mkubwa.
Baada ya habari hiyo kuisha, watu wote pale sebuleni walinigeukia na kunitazama kwa mshangao uliochanganyikana na hofu. Tukiwa bado tunatazamana, mara baba aliingia getini akiwa ameongozana na baba yake Rahma na askari watatu waliokuwa na silaha. Nikajua mwisho wangu umefika, nilishindwa cha kufanya, nikabaki nimesimama palepale, nikitetemeka kuliko kawaida.
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 31
ILIPOISHIA:
Nikiwa bado naendelea kumtazama kwa jicho baya, mara nilishtuka kusikia vishindo viwili vikubwa juu ya bati, kama vile nilivyokuwa navisikia usiku uliopita, moyo wangu ukapatwa na mshtuko mkubwa mno. Mara nilisikia vishindo vingine vitatu mfululizo, nikawa nimepigwa na butwaa huku macho yangu yote yakiwa juu.
SASA ENDELEA...

Kwa jinsi vishindo hivyo vilivyokuwa vikisikika, ilikuwa ni kama kuna watu wanaruka kutoka angani na kudondokea juu ya bati kwani vilikuwa vizito mno. Safari hii nilitaka kuwa makini kushuhudia je, kile ninachokisikia mimi, kila mtu anasikia hivyohivyo maana nilishahisi kuna kitu hakipo sawa kwangu lakini baba hataki kuniambia ukweli.
Baada ya vishindo vile vya kama watu au vitu kutua juu ya bati, mara vilianza kusikika vishindo vya mtu akitembea juu ya bati.
Unajua haya matukio kama hujawahi kutokewa nayo, huwezi kuelewa ile hofu unayokuwa nayo lakini kiukweli, ni bora tu uwe unasikia lakini yasikutokee. Hakuna hofu inayotesa kama hofu ya matukio kama haya yanapokutokea, hasa usiku kama huo.
Nilijikuta nywele zikisisimka vibaya mno, mapigo ya moyo yakawa yananienda kwa kasi maana sikujua safari hii wanakuja kwa mtindo gani. Vishindo viliendelea kusikika kisha kikasikika kishindo kingine ambacho kwa makadirio yangu ya haraka, kilikuwa ni kwenye sakafu ya mle mahabusu.
Nilishindwa kuelewa, inawezekanaje usikie mtu anatembea juu ya bati, tena kwa nje halafu muda mfupi baadaye umsikie akirukia na kudondokea kwa ndani, tena jirani kabisa na pale ulipo! Inatisha sana.
“Humu ndani kuna wanga eeh! Mbona nywele zinanisisimka? Sasa ole wake mtu aniguse,” mmoja kati ya wale mahabusu tuliokuwa nao mle ndani, aliyekuwa amekaa kwenye kona nyingine, alisikika akiongea kilevilevi, akawa anaporomosha matusi mazitomazito.
Kitendo kile kilinifanya niamini kwamba hatimaye sasa sikuwa peke yangu ambaye nilikuwa nikishuhudia mchezo uliokuwa ukiendelea. Niliamini hivyo kwa sababu kwenye kona aliyokuwa amekaa yule mahabusu ambaye alikuwa akiendelea kutukana, ndiko ambapo makadirio yangu yalinionesha kwamba yule mtu aliyekuwa akitembea juu ya bati alidondokea palepale.
Matusi aliyokuwa akitukana, yalisababisha mahabusu wengine ambao bado hawakuwa wamelala, waanze kucheka kwa nguvu na kumtania kwamba amelewa lakini kelele zote zilizimika ghafla bila mtu yeyote kutoa amri, ikatokea tu kwamba watu wote wapo kimya.
Katika ukimya huo, ulisikika msonyo mkali ambao japokuwa wale mahabusu wengine waliamini kwamba umetolewa na yule mahabusu aliyekuwa akitoa matusi mazito kwa wale aliowaita wanga, mimi nililitazama tukio hilo katika sura nyingine tofauti.
Haikuwa mara ya kwanza kusikia msonyo wa namna hiyo ingawa safari hii ulionekana kutoka kwa mtu tofauti ambaye sijawahi kuisikia sauti yake. Unajua kuna watu wamezaliwa wakiwa na uwezo fulani wa kipekee, sijui niuiteje lakini kwa kifupi mtu anakuwa na uwezo wa kufikiri na kuyaona mambo kwa utofauti na wengine.
Yaani kuna baadhi ya watu, nyie wengine wote mnaweza kuamini kwa mfano ajali iliyotokea barabarani imesababishwa na uzembe wa dereva kukimbia kwa mwendo kasi akiwa hajafunga mkanda, lakini mtu mwingine hapohapo akalitazama tukio na kutoa jibu tofauti kabisa ambalo pengine halikutegemewa.
Baba amewahi kunifundisha kwamba japokuwa watu wa namna hii huwa wanachekwa au kuzomewa na kuonekana wanaishi kwenye ulimwengu wa ndoto, lakini wao ndiyo huwa sahihi kwa sababu wanautazama ulimwengu kwa jicho tofauti na watu wengine wote.
Ndicho kilichotokea mle mahabusu, wakati watu wote wakilichukulia tukio la yule mahabusu kudai kule ndani kuna wachawi kisha akaanza kuporomosha matusi, wengi walimuona kama mlevi tu lakini mimi nilimtazama kwa jicho tofauti.
Hata uliposikika ule msonyo na watu kuanza kumtuhumu kwamba anawavurugia usingizi wao, mimi nilikuwa nikiamini kwamba hakuutoa yeye na alichokuwa akikisema kwamba mle ndani kulikuwa na wanga, ulikuwa ni ukweli mtupu.
“Sikilizeni, sikilizeni,” alisema yule mahabusu, kwa msaada wa mwanga hafifu uliokuwa ukipenya kutokea nje, nilimuona akiinua kichwa chake juu kutazama darini, lakini kelele za mahabusu wengine zikamfanya ashindwe kusikia alichokuwa akitaka kukisikia.
“Au naye ana nguvu kama mimi?” nilijiuliza kwa sababu wakati akiwataka watu wote watulie ili wasikie, ni kweli juu ya bati kuna mtu alikuwa akitembea kwa vishindo kabisa kisha naye akasikika akidondokea ndani ya ile mahabusu.
Baada ya hapo, vilianza kusikika vishindo vya watu wakirukia mle mahabusu mfululizo, nikawa natetemeka nikiwa sijui nini kitatokea maana kama unavyojua, milango ya mahabusu huwa muda wote imefungwa na haiwezekani ikafunguliwa kwa muda ule. Nilichokuwa nakiomba, ni wachawi hao wasije wakawa wamekuja kwa shari kama ilivyotokea kwangu na safari hii, nilijifunza kuufyata mkia, sikutaka kuzungumza chochote zaidi ya kuzidi kukodoa macho yangu gizani kama nitaona kitu chochote.
Nilishangaa mfuko wa suruali yangu ukianza kutetemeka kama ndani kulikuwa na kitu ‘kinacho-vaibreti’, sikukumbuka kama niliweka kitu chochote mfukoni na hata kama ni simu, wala sikuwa nikimiliki baada ya baba kunipokonya ile niliyopewa na yule dada ambaye ndiye aliyesababisha muda huo nikawa nyuma ya nondo.
Kwa hofu kubwa niliingiza mkono mfukoni huku nikiwa bado nimekodoa macho, nikagundua kwamba kulikuwa na kitu kwenye mfuko wangu ambacho sikuwa najua ni kitu gani.
Mbaya zaidi, sikujua ni nani aliyekiweka kwenye mfuko wa nguo yangu kwa sababu wakati naingizwa na wale askari, waliniambia pale kaunta nitoe kitu chochote nilichokuwa nacho mfukoni na wala sikuhitaji kujisachi kwa sababu nilikuwa najua sina chochote.
Cha ajabu, nilipokigusa kitu hicho tu, kiliacha kutetemeka lakini yote tisa, kumi ni kwamba nilianza kuona vitu vya ajabu mno. Japokuwa mle ndani kulikuwa na giza, niliweza kuwaona watu wote vizuri, mpaka sura zao utafikiri ilikuwa mchana, ila tofauti yake ni kwamba hakukuwa na mwanga wenye uangavu kama wa mchana bali ulifanana kwa mbali na nuru ya mbalamwezi.
Kwa wale tuliokulia vijijini nadhani wanaelewa vizuri usiku wa mbalamwezi unavyokuwa, yaani unaweza kusema ni mchana kabisa kwani vitu vyote vinaonekana japo siyo vizuri kama vile nilivyokuwa naona mimi.
Nilianza kuwatazama mahabusu wenzangu mmoja baada ya mwingine maana kama unavyojua, niliingizwa giza likiwa limeshaingia na kwa sababu mle ndani hakukuwa na taa, watu pekee niliowaona vizuri ni wale waliokuwa jirani na mimi.
Cha ajabu, wakati nikiendelea kuwatazama mahabusu hao ambao wengi walishaanza kusinzia kutokana na uchovu, niligundua kwamba kulikuwa na watu wengine wasio wa kawaida mle ndani, nao wakiwa wamejichanganya na mahabusu lakini tofauti yao ilikuwa moja.
Karibu wote walikuwa na macho mekundu sana na walikuwa wakinitazama kama wanaosubiri kuona nitafanya nini lakini kubwa, wote walikuwa watupu kabisa. Nilipopiga jicho harakaharaka na kujaribu kuwahesabu, walikuwa kama saba hivi, tena wengine wawili walikuwa ni wanawake na kama unavyojua mahabusu huwa hawachanganywi wanawake na wanaume.
Wote waliacha kila walichokuwa wanakifanya, wakawa wananitazama kwa macho makali. Sikuelewa nini hasa kimetokea, wakati nikiendelea kuwatazama vizuri kwa mara ya pili, kuna jambo moja lilinishtua mno mpaka nikajikuta nimetoa mkono mfukoni, giza likarudi kama lilivyokuwa mwanzo.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 32
ILIPOISHIA:
Wote waliacha kila walichokuwa wanakifanya, wakawa wananitazama kwa macho makali. Sikuelewa nini hasa kimetokea, wakati nikiendelea kuwatazama vizuri kwa mara ya pili, kuna jambo moja lilinishtua mno mpaka nikajikuta nimetoa mkono mfukoni, giza likarudi kama lilivyokuwa mwanzo.
SASA ENDELEA...

Japokuwa kulikuwa na giza, niliweza kuonamacho ya wale watu yaking’ara kama wanyama wakali wa porini, nikawa najilaumu kwa kile nilichokifanya. Hata sijui nini kilitokea kwani kuanzia mwanzo nilikuwa nimejiapiza kwamba siku hiyo sitaleta ujuaji wowote mbele ya watu hao lakini cha ajabu, ndani ya muda mfupi tu, tayari nilishakuwa nimewekwa mtu kati.
Sikujua safari hii wataniadhibu vipi lakini niliamua kupiga moyo konde, liwalo na liwe. Bado nilikuwa najiuliza maswali mengi kuhusu kile kilichokuwa kwenye mfuko wangu, sikujua ni nini na kilikuwa na uhusiano gani na ule mwanga uliotokeza ghafla mle ndani ya mahabusu.
Sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilijikuta nikiingiza tena mkono taratibu mfukoni, nilipokigusa tu kile kitu mle mfukoni, ule mwanga ulirudi tena vilevile, wale watu ambao safari hii walikuwa wamejikusanya na kutengeneza kama nusu duara hivi, waliinua wote shingo zao na kunigeukia tena, nikakishika kile kitu kwa nguvu huku na mimi nikiwa nawatazama.
Katika hali ambayo sikuitegemea, nilishangaa wa kwanza akisimama na kukimbilia kwenye ile kona alipokuwa amekaa yule mahabusu ambaye awali alikuwa akipiga kelele. Safari hii alikuwa amelala, tena kwa kuinamisha kichwa mbele, katikati ya miguu yake.
Nikamuona yule mtu wa kwanza, mikono yake akiwa amejiziba sehemu nyeti, akisogea mpaka kwenye kona, alipoikaribia, aligeuka na kuanza kutembea kinyumenyume, akamkanyaga yule mahabusu kisha nikashangaa akipotelea kwenye ukuta.
Ni hapo ndipo nilipoamini yale maneno niliyowahi kuyasikia kwamba wachawi wanao uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya nyumba hata kama milango imefungwa. Nilishindwa kuelewa ni nini hasa kilichofanya iwezekane kwa yule mtu kupotelea kwenye ukuta.
Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilimuona mwingine naye akiinuka, akaanza kutembea kuelekea kwenye ile kona, wengine nao wakasimama, wakawa wanatembea huku wote wakiwa wananitazama kwa macho mabaya. Ni kama nilikuwa nimewavurugia mipango yao, nikazidi kukishikilia kile kitu mfukoni.
“Hiyo ndiyo nafasi yako ya kutoka mahabusu, hakikisha unamshika mmoja kati yao na kumvua usinga aliovaa shingoni kisha na wewe utatoka kama hao wengine walivyotoka,” nilisikia sauti masikioni mwangu ambayo niliitambua vizuri kwamba ni ya baba.
Bado sikuwa nimeelewa ni mbinu gani anayoitumia baba kuwasiliana na mimi kwa sauti ambayo hakuna mtu mwingine yeyote anayeisikia. Hata hivyo, sikutaka sana kuhoji, nilichokifanyailikuwa ni kufuata maelekezo.
Cha ajabu, wale watu walipoona nawafuata, walianza kukimbia lakini kwa sababu ya nafasi ndogo iliyokuwepo, walishindwa kutoka wote kwa mkupuo, nikafanikiwa kumkamata mmoja ambapo moja kwa moja nilipeleka mkono shingoni ambapo alikuwa amevaa kitu kama kamba nyembamba lakini iliyosokotwa kwa nywele, ikakatika na kubaki mkononi mwangu.
Kitendo hicho kilisababisha alie kwa sauti kubwa lakini cha ajabu sasa, sauti yake ilitoka kama zile sauti zinazotolewa na mapaka yanayolia usiku, akadondoka chini na kuendelea kulia kwa sauti kubwa kama paka.
Cha ajabu, wakati nikiwa nimeshageuka na kuupa mgongo ukuta, tayari kwa kufanya kile baba alichoniambia nikifanye, yule mtu aliinua uso wake huku akionesha ishara kwamba nimsamehe. Kilichonishtua ni kwamba sura yake ilikuwa ikifanana na mimi kwa kila kitu wakati awali hakuwa vile.
Nikiwa bado naendelea kumshangaa, nilisikia sauti ya baba ikinisisitiza kutoka haraka. Sikuwa nimewahi kushiriki uchawi mkubwa kiasi hicho, nikawa natetemeka nikiwa siamini kama kweli naweza kupita ukutani. Nilipiga hatua kurudi nyuma mpaka nilipoufikia ukuta.
Cha ajabu, nilipouegamia ulilainika kama pazia, nikapiga hatua nyingine na kujikuta nusu ya mwili wangu tayari ipo nje, nikapiga hatua nyingine, nikawa nimetoka nje kabisa. Nilibaki nimesimama kwenye maua yaliyopandwa pembezoni mwa ile mahabusu nikiwa bado siamini.
Niligeuka na kutazama huku na kule, hakukuwa na mtu yeyote eneo hilo, harakaharaka nikatembea na kupotelea kwenye kota za askari wa kituo kile, nikawa nazidi kutembea nikiwa sielewi naelekea wapi. Nilizimaliza kota hizo, kwa mbali nikawa nawasikia mbwa wakibweka, nikaongeza mwendo na muda mfupi baadaye, nilitokeza kwenye barabara ya lami.
Siwezi kuficha jinsi nilivyofurahi kutoka mle mahabusu. Hapohapo nikajikuta eti na mimi nikitamani kuwa mchawi ili nipate nafasi ya kufaidi mambo mengi kwenye hii dunia ambayo binadamu wa kawaida hawawezi.
Hebu vuta picha, hata kama ni wewe, yaani ndugu yako yupo gerezani anateseka halafu leo ukiambiwa kuna ujuzi ukifundishwa ndugu yako anaweza kutoka kiulaini, tena bila kutumia nguvu wala fedha, huwezi kutamani kweli?
Labda kamauna imani kali ya dini ndiyo unaweza kuukwepa mtego huo lakini kwangu mimi, siwezi kuficha kwamba nilifurahi sana na kutamani kuwa mchawi, tena niliyebobea. Nilijiapiza kwamba nitakapopata nafasi ya kuzungumza na baba, nitamueleza nia yangu bila kujali atanichukuliaje.
Niliendelea kutembea kufuata ile barabara ya lami huku muda mwingi tabasamu likiwa limechanua kwenye uso wangu. Tafsiri ya kile kilichotokea n kwamba asubuhi polisi wangeingia na kufanya ukaguzi mle mahabusu wangekuwa na imani kwamba bado nipo, labda watashtuka kwa nini sijavaa nguo kwa sababu yule mchawi hakuwa amevaa nguo.
Nilielewa kwa nini baba aliniambia nisitoe maelezo yoyote kwa sababu kama yule mtu niliyebadilishana naye na kumuacha mle ndani mahabusu atahojiwa, maelezo atakayoyatoa yatakuwa hayaungi chochote na tukio lililotokea kwa hiyo uwezekano wa baadaye kuja kuachiwa kwa sababu ya kukosekana ushahidi ulikuwa mkubwa.
Sikujua atasota kwa muda gani mle mahabusu, tena kesi yenyewe ikiwa ni ya mauaji lakini niliona kama anastahili maana ni uchawi wa aina gani watu wanaenda kuufanyia sehemu hatari kama mahabusu? Niliendelea kutembea huku mara kwa mara nikicheka mwenyewe maana nilijiona bonge la mjanja kuukwepa msala ule.
Nikiwa naendelea kutembea nikiwa sijui naelekea wapi kwa sababu kama nilivyoeleza, sikuwa naijua mitaa ya Jiji la Dar es Salaam, nilisikia vishindo vya mtu akija huku akikimbia akitokea nyuma yangu. Baba amewahi kuniambia kwamba ukiwa unatembea usiku, ni mwiko kugeuka nyuma.
Alizidi kunikaribia, nikawa najiuliza kama atakuwa ni mtu mbaya itakuwaje? Niliendelea kujikaza kisabuni, vishindo vikazidi kunikaribia na alipofika usawa wangu, nikasikia akipunguza mwendo. Kilichonifanya niamini kwamba hawezi kuwa mtu mbaya, ni jinsi manukato aliyokuwa amejipulizia mwilini yalivyokuwa yakinukia vizuri.
“Mambo,” sauti ya kike ilisikika, safari hii ikiwa usawa wangu kabisa, ikabidi nisimame, nikageuza shingo yangu upande wa kulia alipokuwepo mtu huyo aliyenisalimu. Muda huo kwa makadirio ilikuwa ni kama saa nane za usiku maana kuna sehemu nilipita nikasikia redio kwa mbali ikitangaza kwamba ni saa nane kasoro za usiku.
“Mbona umeshtuka Togo!” alisema huku akinisogelea. Siwezi kuficha, mshtuko nilioupata nusura nidondoke na kuzimia.
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of the Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia) - 33
ILIPOISHIA:
Muda huo kwa makadirio ilikuwa ni kama saa nane za usiku maana kuna sehemu nilipita nikasikia redio kwa mbali ikitangaza kwamba ni saa nane kasoro za usiku.
“Mbona umeshtuka Togo!” alisema huku akinisogelea. Siwezi kuficha, mshtuko nilioupata nusura nidondoke na kuzimia.
SASA ENDELEA...

Alikuwa ni yule msichana ambaye mchana wa siku iliyopita alinifia gesti tukiwa kwenye mechi ya kirafiki na kunisababishia matatizo makubwa mpaka nikapelekwa mahabusu nikikabiliwa na kesi kubwa ya mauaji.
Nilitaka kukimbia nikahisi mwili wangu ukiishiwa nguvu, nilitaka kupiga kelele lakini sauti ikawa haitoki, nikabaki nimesimama palepale nikitetemeka kama mbwa mbele ya chatu, akawa ananishangaa usoni kama anayejiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Wewe si ulikufa wewe?” nilisema huku safari hii miguu yangu ikiwa imeanza kupata nguvu, nikawa narudi nyuma nikiangalia upenyo wa kukimbia. Ni kama alishagundua ninachotaka kukifanya, akacheka na kunisihi nisikimbie bali kuna jambo la muhimu anataka kuniambia.
Maneno yake yaliingilia sikio moja na kutokea la pili, akili yangu ilinifanya niamini kwamba hakuwa yeye bali mzimu wake, akawa anazidi kunisogelea mwilini.
“Najua unafikiri labda mimi ni mzimu, siyo, nipo hai wala sijafa na leo nitakutajia mpaka jina langu,” aliniambia huku akizidi kunisogelea. Mazungumzo yake hayakuonesha kama alikuwa mzimu au alikuwa na nia mbaya na mimi lakini bado niliendelea kurudi nyuma, naye akawa anazidi kunifuata.
“Jina langu naitwa Isrina au wengi huwa wanapenda kuniita Isri. Nakuomba unipe japo dakika chache nikueleze kilichotokea leo na historia fupi ya maisha yangu, pia nataka nikueleze kitu ambacho hukijui kuhusu wewe ambacho kitakusaidia sana,” alisema kwa sauti ya upole.
Sijui nini kilitokea lakini nilijikuta nikishawishiwa na maneno yake matamu, nikasimama, akazidi kunisogelea mwilini na kunikumbatia kimahaba. Kitendo hicho kilisababisha hofu yote niliyokuwanayo iyeyuke ghafla kwa sababu nimewahi kusikia kwamba tofauti ya mtu na mzimu, ni kwamba mzimu unakuwa na mwili ambao japo unauona, hauwezi kuushika ukashikika.
Nimewahi kusikia kuwa miili ya mizimu inakuwa kwenye mfumo wa hewa, kwamba unamuona mtu lakini ukitaka kumkumbatia anakuwa kama hewa, hashikiki. Ili kuwa na uhakika, na mimi nilimshika kiuno chake, kweli kikashikika vizuri kabisa, tukawa tunatazamana usoni.
Tukiwa bado tunaendelea kutazamana, alinibusu kwenye shavu langu la kushoto, nikajikuta mwili mzima ukisisimka na ndani ya sekunde chache tu, ile hali iliyokuwa inanisumbua sana, ya kuwa na kiu kubwa ya kucheza mchezo wa kikubwa ilinianza tena.
Ni kama Isri alielewa nilichokuwa nakihitaji, alichokifanya ilikuwa ni kuendelea kunitoa hofu huku akiendelea kunichokoza hapa na pale, hali ikazidi kuwa tete kwa upande wangu.
Usiku huo kulikua kimya kabisa, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akuipita barabarani, kelele pekee zilizokuwa zinasikika zilikuwa ni za mbwa waliokuwa wakibweka mitaani. Ilibidi tusogee pembeni ya barabara, hakukuwa na muda wa kupoteza, kila mmoja alijiweka kwenye mkao wa kula na kazi ilianza palepale.
Kwa jinsi nilivyokuwa na ‘kiu’, nilimsambaratisha vilivyo Isri mpaka ikabidi aweke mpira kwapani. Hata hivyo, angalau kidogo nilianza kujisikia vizuri, akili yangu sasa ikahamia kwenye kutaka kuujua ukweli kwa sababu nilishahakikisha kwamba Isri hakuwa amekufa.
“Haya niambie kilichotokea.”
“Kwanza nashukuru,” alisema huku akinikumbatia na kunibusu huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
“Usijali, ahsante na wewe,” nilisema, akazidi kucheka. Alivuta pumzi ndefu na kunitazama usoni, Japokuwa ilikuwa ni usiku, kwa msada wa mbalamwezi niliweza kumtazama vizuri jinsi alivyokuwa ananiangalia kwa macho yaliyojaa ujumbe.
Alishusha tena pumzi ndefu kisha akanikumbatia na kujilaza kifuani kwangu, akaniambia kama sitajali, tutafute sehemu na kukaa kwa sababu alikuwa amechoka sana. Nilimkubalia, tukasogea kwenye nyumba ambayo ilikuwa ikijengwa lakini bado haijakamilika, tukakaa kwenye msingi na kuanza kuzungumza.
Aliniambia kwamba aligundua kwamba nina kitu fulani cha kipekee siku ya kwanza tulipokutana ndani ya basi, wakati tukisafiri kutokea Mbeya kuja Dar es Salaam. Aliniambia kwamba yeye amezaliwa katika ukoo wa kichifu kwani babu yake mzaa baba, alikuwa ni kiongozi wa mila wa Wanyakyusa waliokuwa wakiishi kandokando la Mlima Rungwe na alikuwa akiheshimika sana. Aliniambia kwamba hata babu yake huyo alipofariki, alimrithisha mikoba yake baba yake ambaye licha ya kuwa msomi, akiwa ni daktari kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia alikuwa akiendelea na shughuli za kimila na ndiyo maana yeye alikuwa na uwezo wa tofauti na watu wengine kwani ndani kwao yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzaliwa.
Maelezo hayo bado hayakuwa yamenisaidia kuelewa chochote, niliona kama ananizungusha tu lakini sikutaka kumkatisha, nikatulia na kuendelea kumsikiliza.
Aliniambia kwamba kwa kuwa yeye ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yao, na kawaida zile kazi za kimila huwa zinarithishwa kwa mtoto wa kwanza, baba yake alikuwa amefanya kitu kimoja kibaya sana kwenye maisha yake ndiyo maana siku aliponiona mimi alifurahi sana.
“Unamaanisha nini?”
“Mimi ni kaburi la wasio na hatia Togo, nimeamua kukueleza ukweli kwa sababu wewe ndiye mwanaume pekee ambaye umeweza kuuvuka mtego wa kifo,” aliniambia, nikawa simuelewi kabisa. Sikuelewa anamaanisha nini anaposema yeye ni kaburi la wasio na hatia na anamaanisha nini anaposema mimi nimeweza kuuvuka mtego wa kifo?
Nikiwa bado na shauku kubwa ya kutaka kumsikiliza alichomaanisha, nilipoinua uso wangu na kutazama upande wa barabarani, nilishtuka sana kuona kulikuwa na watu wengi wamekusanyika, wote wakiwa wanatutazama.
“Mungu wangu,” nilisema kwa mshtuko kwani ilionesha kuna jambo halikuwa sawa kwetu na ndiyo maana walikuwa wakitutazama. Tofauti na mimi, yeye alipowatazama wala hakushtuka, akaniambia ni haki yao kushangaa kwa sababu hatukuwa tukionekana wa kawaida.
“Unamaanisha nini?”
“Umewahi kusikia stori za majini?” aliniuliza, nikamgeukia na kumtazama usoni kisha nikawatazama tena wale watu, walikuwa wakizidi kuongezeka kwa wingi, safari hii baadhi yao wakawa wanatupiga picha kwa kutumia simu zao. Niliweza kuligundua hilo kwa sababu ya mwanga wa flash uliokuwa ukitumulika.
Nilimtaka tuondoke lakini akasema wala nisiwe na wasiwasi, hawawezi kutufanya jambo lolote na hawana uwezo huo. Alipoona situlii, aliniambia nimpe mkono wangu wa kushoto, nikafanya hivyo, akashika kidole changu cha mwisho kisha akaniambia na mimi nifanye hivyohivyo, nikamshika.
“Nahesabu mpaka tatu, nikifika tatu fumba macho na usifumbue mpaka nitakapokwambia,” alisema, nikatii kile alichoniambia. Alipofikisha tatu, nilifumba macho, nikashtukia ghafla tumehama pale tulipokuwa na kwenda upande wa pili, kule barabarani ambako watu wengi walikuwa wamesimama wakishangaa, tukajichanganya na wale watu.
“Hebu angalia wanachokishangaa,” alisema huku akinitaka nitazame pale tulipokuwa tumekaa awali. Macho yalinitoka nikiwa ni kama siamini.
Je, nini kitafuatia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom