Makapuku Forum

Makapuku Forum

Zaburi 141

1 Ee BWANA, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.


MCHANA MWEMA WAPENDWA MBARIKIWE
barikiwa pia
 
Zaburi 141

1 Ee BWANA, nimekuita, unijie hima, Uisikie sauti yangu nikuitapo.

2 Sala yangu ipae mbele zako kama uvumba, Kuinuliwa mikono yangu kama dhabihu ya jioni.

3 Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

4 Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.


MCHANA MWEMA WAPENDWA MBARIKIWE
Ameen Mama
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 13
ILIPOISHIA:
“YULE uliyekuwa umekaa naye kwenye basi ni nani?”
“Ni rafiki yangu.”
“Unamjua wewe? Na hicho alichokupa una uhakika gani kama ni simu? Ujinga wako utaiponza familia nzima,” alisema maneno ambayo yalinishangaza sana.
SASA ENDELEA…

“NI simu baba!”
“Sitaki kukuona naye tena na hiyo simu lete,” alisema huku akinipokonya ile simu. Nilizidi kumshangaa baba, nikaona kama anataka kunikosesha bahati ya bure. Kwa mara ya kwanza nilijikuta nikipandwa sana na hasira juu yake. Hata hivyo sikuwa na cha kufanya, tuliondoka Ubungo huku kila mmoja ndani ya gari tulilokuwa tumepanda, akiwa anashangaa mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Japokuwa tulikuwa tumebanana sana kwenye ile teksi kwa sababu ya wingi wetu, kila mmoja alikuwa akitamani yeye ndiyo akae dirishani. Tulikatiza mitaa mingi na hatimaye tukaiacha barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya vumbi. Baada ya muda, tulitokeza kwenye nyumba moja nzurinzuri, baba akawa wa kwanza kuteremka kwenye gari, na sisi wengine tukafuatia na kuanza kushusha mizigo.
Wakati tukiendelea kushusha mizigo, geti kubwa lilifunguliwa, mwanaume wa makamo aliyeonekana wanafahamiana vizuri na baba, alimuita kwa jina lake, baba akaacha kila alichokuwa anakifanya na kwenda kumkumbatia, wote wawili wakionyesha kuwa na furaha kubwa kwa kukutana.
“Hii ndiyo familia yangu, shemeji yako na watoto,” alisema baba huku akituonyeshea sisi, akatusogelea na kusalimiana na mama, kisha akaanza kutupa mikono, mmoja baada ya mwingine huku akituuliza majina.
“Naitwa Togolai,” nilimwambia aliponifikia, akanitazama usoni.
“Wewe ndiyo Togo?”
“Ndiyo,” nilisema huku na mimi nikiachia tabasamu hafifu kwa sababu na yeye alikuwa akitabasamu. Baada ya hapo, alitukaribisha ndani, wakati tunabeba mizigo kuingiza, walikuja watu wengine watatu, wasichana wawili na mwanaume mmoja ambao kwa kuwatazama tu, walionyesha dhahiri kwamba ni wanaye kwa jinsi walivyokuwa wamefanana na kupishana umri.
Mkubwa alikuwa wa kike, aliyemfuatia alikuwa wa kiume na mdogo kabisa naye alikuwa wa kike. Hawakupishana sana umri, yule mkubwa alikuwa akilinganalingana na dada yetu Sabina.
Tofauti yao na sisi, ilikuwa kubwa sana, kuanzia jinsi walivyokuwa wamevaa na mpaka muonekano wa miili yao. Walikuwa na mwonekano wa kimjini haswaa wakati sisi tulikuwa na mwonekano wa ‘bushi’, kuanzia sura zetu, mavazi yetu mpaka jinsi tulivyokuwa tukizungumza.
Walitukaribisha mpaka ndani, tukaenda kukaa kwenye sebule kubwa na ya kisasa. Japokuwa tulikuwa wengi, lakini wote tulitosha kwenye masofa ya kisasa. Ushamba wetu uliendelea kujidhihirisha mle ndani kwani tulikuwa tukishangaa kila kitu, kuanzia taa za umeme, feni, mapazia, kuta zilizokuwa zimenakshiwa kwa rangi nzuri na marumaru, kila kitu kilikuwa kigeni kwetu.
Tuliandaliwa chakula na mama wa familia ile ambaye alikuwa mchangamfu na anayependeza kimwonekano kuliko mama yetu. Kilikuwa ni chakula kizuri mno, ambacho ama kwa hakika tulikifurahia. Tukala mpaka kumaliza, mwenzetu mmoja akawa anataka kulamba bakuli la mboga, mama akamkata jicho la ukali na kumfanya aogope.
Baada ya chakula, tulianza kushangaa runinga maana kule hakukuwa kuangalia, ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kuona runinga lakini achilia mbali runinga ya kawaida, ile iliyokuwa mle ndani ilikuwa kubwa sana, tena ya kisasa kabisa iliyounganishwa na spika ndogo za kisasa zilizokuwa zinatoa mdundo mzito.
Mpaka muda wa kulala unafika, hakuna aliyekuwa tayari kubanduka pale sebuleni, kila mmoja alikuwa anatamani kama akeshe palepale akitazama vipindi vizuri vilivyokuwa vinaonyeshwa. Ilibidi mama atumie ukali, kwani kwa muda huo baba ambaye ndiyo tunayemwogopa sana, alikuwa nje kwa mazungumzo na yule rafiki yake.
Kabla ya kwenda kulala, ilibidi kwanza tuende kuoga mmojammoja kuondoa vumbi na uchafu tuliotoka nao kijijini. Mimi ndiye niliyekuwa wa mwisho kwenda kuoga ambapo nilipoingia kwenye bafu hilo la kisasa, nilishangazwa kwa jinsi lilivyokuwa safi. Yaani hata kama ningeambiwa nikae mle ndani kwa siku nzima na kuletewa chakula nilie humohumo ningekubali kwa sababu ya usafi wake.
Kule kijijini tulizoea kwenda kuoga mtoni, wakati mwingine kuogelea lakini mjini mambo yalikuwa tofauti. Nilivua nguo zangu na kuzikung’uta kwanza kwa sababu zilikuwa na vumbi jingi. Kwa bahati mbaya, wakati nikiikung’uta suruali niliyokuwa nimevaa, nilisahau kwamba ile dawa niliyopewa na baba nilikuwa nimeiweka kwenye mfuko, nilipokung’uta ikadondoka chini na kwa kuwa choo na bafu vilikuwa vimeungana, yaani upande mmoja kuna bafu na upande wa pili kuna choo, iliteleza mpaka kwenye sinki la choo.
Kutokana na umuhimu wa dawa hiyo, ilibidi niende kuiokota haraka lakini kabla sijafanya hivyo, niliitundika ile suruali kwenye bomba lililokuwa pembeni. Nikashtuka kuona maji yakianza kumwagika, yakaisomba ile dawa na kuipeleka kwenye shimo la choo, ikapotelea kwenye bomba la kutolea maji machafu.
Nilishangaa sana yale maji nani ameyafugulia lakini nilipotazama vizuri, niligundua kuwa kumbe pale nilipokuwa nimetundika suruali ile ilikuwa ni koki ya bomba ambayo kwa jinsi ilivyokuwa ya kisasa nilishindwa kuitambua.
“Ayaaa!” nilisema kwa sauti kubwa kwa sababu sikutegemea kabisa kile kilichotokea na hata sikujua nitamwambia nini baba kwa sababu wakati ananipa, alinisisitiza kuitunza sana dawa hiyo. Ilibidi nifunge maji kwanza, nikaegamia kwenye marumaru za bafuni, nikiwa na mawazo mengi juu ya nini cha kufanya.
Mwisho nilipiga moyo konde na kujiambia kwamba nitaenda kumweleza baba hali halisi na kwa sababu ananipenda na ananiamini. Nilimalizia kuvua nguo, nikawa nataka nioge maji kwa kutumia bomba linalomwaga maji kama mvua, kama nilivyokuwa nimeona kwenye runinga muda mfupi uliopita.
Kwa umakini mkubwa nilichunguza mahali ilipo koki yake, nilipoiona niliifungua, maji yakaanza kumwagika, harakaharaka nikaingia katikati yake na kuanza kujimwagia.
Ilibidi nifumbe macho wakati najipaka sabuni lakini taratibu nilianza kuona maji yanaanza kuwa ya uvuguvugu kidogo halafu yanakuwa kama mazito kidogo na yana chumvichumvi. Nikawa nikipaka sabuni haiishi mwilini, ikabidi nisogeze kichwa pembeni kidogo na kufumbua macho.
“Mungu wangu,” nilipiga kelele kwa nguvu baada ya kugundua kwamba kumbe kile nilichokuwa nikiamini kwamba ni maji, zilikuwa ni damu zikimwagika kama maji. Uda mfupi baadaye tayari nilikuwa kwenye mlango wa bafuni lakini cha ajabu, licha ya kutoa loki niliyoiweka wakati nikiingia, mlango uligoma kufunguka, nikawa nagongagonga kwa nguvu huku nikiendelea kupiga kelele.
Wa kwanza kufika alikuwa ni yule msichana ambaye alionyesha kuwa ndiyo mtoto mkubwa wa yule mzee, akasukuma mlango kwa nguvu kutokea nje. Nguvu alizotumia, ukichanganya na kwamba miguu yangu ilikuwa na majimaji, nilijikuta nikiteleza na kuanguka chini kama mzigo akaingia na kupigwa na butwaa kutokana na hali aliyonikuta nayo kwani sikuwa na nguo hata moja na bado nilikuwa nikipiga mayowe ya kuomba msaada.
Alichokifanya, haraka alivua khanga aliyokuwa amejifunga juu ya gauni lake na kunirushia ili nijisitiri kisha haraka akageuka na kutoka, nikamsikia akijifungia mlango wa chumbani kwake, nadhani alijisikia aibu sana kwa hali aliyonikuta nayo.
Cha ajabu sasa, wakati nageuka kutazama kule zile damu zilikokuwa zikimwagika, nilishangaa kuona kinachotoka si damu bali maji na wala hakuna dalili yoyote ya damu. Tayari kaka zangu walishafika na kunikuta nikihangaika kujifunga ile khanga niliyopewa, wakataka kujua nini kimetokea
Kelele hizo kumbe hata baba na yule mwenzake walizisikia, nao wakaja haraka kutaka kujua nini kimetokea.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 14
ILIPOISHIA:
“MUNGU wangu,” nilijisemea, mapigo ya moyo yakiwa yananienda mbio kuliko kawaida, nikiwa sijui nini kitatokea, hasa ukizingatia kwamba nilikuwa ugenini na ndiyo kwanza tulikuwa tumewasili.
SASA ENDELEA…

ALINIACHIA huku naye akionyesha kushtuka, akashuka kitandani na kuokota khanga yake, akajifunga kivivu na kunionyesha ishara kwamba niingie kwenye kabati la nguo, nilifanya hivyo haraka, nikamsikia akifungua mlango.
“Baba amesema usije ukafunga mlango mkubwa wa nje, watachelewa kuingia ndani kwani kuna kazi wanaifanya.”
“Haya poa,” nilimsikia akizungumza na mdogo wake, akashusha pumzi ndefu na kuufunga mlango, nikamsikia safari hii akifunga kwa funguo kabisa, akaja pale kabatini na kufungua mlango, akanionyesha ishara kwamba nitoke.
Sikulaza damu, nilitoka harakaharaka nikiwa kama nilivyo, na yeye akauachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, tukawa tunatazama kama majogoo yanayotaka kupigana. Alipiga hatua moja mbele, miili yetu ikagusana, akazungusha mikono yake kwenye shingo yangu, na mimi nikiwa sijiaminiamini, nikaukumbatia ‘mlima’ wake.
Nikiri kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa kwenye hali kama hiyo na nilichokihisi kwenye mwili wangu, sikuwahi kukihisi kabisa tangu napata akili zangu. Ni hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwa nini watu wengi huwa wanayasifia sana mapenzi kwamba ni matamu kuliko asali.
Ni hapo pia ndipo nilipoelewa kwa nini watu wengine hufikia hatua hata ya kutoana roho, baada ya mmoja kugundua kwamba anatembea na mkewe au mpenzi wake. Dakika chache baadaye, nilikuwa nahema kama nataka kukata roho, ufundi wa mikono yake kuvinjari kwenye mwili wangu, ulinifanya mara kwa mara niwe natoa miguno ambayo sikuwahi kuitoa kabla.
Hata sikukumbuka nilifikaje kwenye uwanja wake wa fundi seremala, nilikuja tu kushtukia yeye yuko juu yangu nikiwa nimelala chali, huku nikiendelea kupumua kwa fujo, mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio sana na ‘Togolai’ akiwa anazidi kuongeza hasira kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Kwa ufundi wa hali ya juu, alimuelekeza njia ya kupita, nikajikuta nikianza kuzungumza kama bubu, maneno hayatoki wala hayaeleweki, kucheka natamani lakini muda huohuo natamani kupiga chafya, ilikuwa ni hali ya ajabu mno. Safari iliendelea, mwanzo alikuwa akipiga hatua fupifupi lakini baadaye nikaanza kumuona akinogewa na kuongeza huku akitoa ukelele fulani ulioongeza raha kubwa kwenye masikio yangu.
Baadaye ilibidi tubadilishane magoli kwenye mechi ile ya kirafiki isiyo na refa wala jezi, yeye akawa anapeleka mashambulizi Kaskazini mwa uwanja na mimi napeleka Kusini.
Japokuwa hata danadana sikuwa najua kupiga na siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza, nilijitahidi kuonyesha kiwango kwa sababu nimewahi kusikia kwamba ukicheza chini ya kiwango, huwa unadharaulika mbele ya viumbe hawa.
Akaongeza mno kasi ya mashambulizi kisha akanikaba kwa nguvu shingoni kama wanavyofanya wale watu wanaopora simu au fedha, akanishikilia kwa nguvu na kunibana, na mimi nikaongeza kasi, nikajisikia hali fulani hivi nzuri sana, akazidi kunibana kisha akaniachia na kudondokea upande wa pili, jasho likiwa limemlowanisha chapachapa na mimi nikiwa hoi bin taaban, nilijikuta nikicheka mwenyewe kwa furaha.
Hakuzungumza jambo lolote kwa dakika kadhaa, baadaye aliinuka na kukaa kitandani, akawa ananitazama kama ambaye haamini kitu fulani.
“Una miaka mingapi?”
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Kwa nje unaonekana mdogo lakini wewe ni zaidi ya mwanaume,” alisema na kunikumbatia tena, akaanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu huku akiniambia kwamba ananipenda na anaomba nisimuache ila uhusiano wetu uwe wa siri.
Bado sikuwa naelewa alichokimaanisha, akaendelea na uchokozi wake na hata sijui nini kilitokea lakini muda mfupi baadaye, nilishtukia tukiwa tena dimbani, safari hii kidogo nikawa sina ugeni na uwanja pamoja na mchezo wenyewe.
Mpambano mkali uliendelea mpaka baadaye ambapo ile hali iliyotutokea mwanzo ilitokea tena, tena kwa kila mtu. Safari hii, alipoangukia upande wa pili, haukupita muda mrefu akaanza kukoroma.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, harakaharaka niliinuka na kuvaa nguo zangu nikaenda kufungua mlango na kutoka huku nikinyata, nikaenda mpaka kwenye mlango wa kile chumba ambacho nitalala na ndugu yangu mmoja.
Kwa bahati nzuri, mlango haukuwa umefungwa, nikaingia mpaka ndani, tayari ndugu yangu naye alikuwa akikoroma, nikajilaza kitandani huku nikisikia uchovu wa kiwango cha juu, karibu kila sehemu kwenye mwili wangu ilikuwa inauma.
Tabasamu pana lilikuwa limechanua kwenye uso wangu, hasa kumbukumbu ya nilichotoka kukifanya ilipokuwa inanijia. Sasa na mimi nilijihisi kuwa mwanaume niliyekamilika. Bado nilikuwa siamini jinsi nilivyoweza kuuangusha mbuyu kwa shoka moja, haukupita muda mrefu nilipitiwa na usingizi.
“Motooo! Jamani moto… nakufaaaa,” sauti za mtu aliyekuwa akipiga kelele kuomba msaada, ndizo zilizonishtua kutoka kwenye usingizi mzito, nikakurupuka huku mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida, nikatoka mpaka koridoni.
Sikuamini macho yangu kusikia sauti ile ilikuwa ikitoka kwenye kile chumba ambacho usiku huo mimi na yule dada tulilambishana asali. Moto ulikuwa umekolea kiasi kwamba hata sehemu ya kupita haikuwa ikionekana.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kufika eneo hilo kwa sababu sikumkuta mtu mwingine yeyote, nikaona nikisema niende kuwaamsha baba na mama, dada wa watu anaweza kufa bure, nikapiga moyo konde na kuukanyaga mlango ambao ulikuwa ukiwaka moto, ukaangukia ndani.
Sikujali kuhusu moshi mzito uliokuwa umetanda kwani tayari nilikuwa na uzoefu wa kucheza kwenye moshi kwani kule kijijini ilikuwa kama tunataka kwenda kupakua asali kwenye mzinga, lazima tuwashe moto kwa kutumia miti inayotoa moshi mzito. Nilibana pumzi, nikaenda mpaka pale kitandani ambapo nilimkuta akiwa ameanza kuishiwa pumzi kutokana na kuvuta moshi mwingi.
Kwa kuwa mwili wangu ulikuwa na nguvu, si unajua tena maisha ya kijijini yanakufanya uwe ‘ngangari’ kutokana na kazi ngumu, nilimbeba na kutoka naye mpaka koridoni, moto ukawa unazidi kuwaka lakini kilichonishangaza sana ni kwamba haukuwa ukisambaa kwenye vyumba vingine.
Nikiwa koridoni, mikononi nikiwa nimembeba yule dada ambaye alishapoteza fahamu, nilikutana na baba na mwenyeji wake pamoja na mama na mwenyeji wake.
“Kuna nini tena? Rahma kapatwa na nini?” aliuliza baba yake, ni hapo ndipo nilipojua kwamba kumbe jina lake anaitwa Rahma. Sikuweza kuwajibu kwa sababu walikuwa wanamuona hali aliyokuwa nayo, baba yake na baba wakanipokea na kumkimbiza mpaka sebuleni, feni zote zikawashwa.
“Kumetokea nini?”
“Moto.”
“Motoo?”
“Ndiyo, chumbani kwake kunawaka moto,” nilisema huku nikishangaa kwa nini walikuwa wakiniuliza mara mbilimbili jambo ambalo lilikuwa wazi. Harakaharaka walielekea kule chumbani wakati mama yake akihangaika kumpa huduma ya kwanza lakini muda mfupi baadaye, walirudi mbiombio.
“Umesema chumbani kwake kunawaka moto?”
“Ndiyo, alikuwa anapiga kelele za kuomba msaada ndiyo nikaamka na kwenda kumsaidia, nilisema, nikaona baba na mwenyeji wake wakitazamana, sikuelewa walikuwa wanamaanisha nini. Ilibidi haraka nirudi kule chumbani kwake ili kuangalia moto umefikia wapi.
Cha ajabu, mpaka nafika mlangoni hakukuwa na moto wala dalili za moto isipokuwa mlango ulikuwa umevunjwa na nakumbuka vizuri mimi ndiye niliyeukanyaga kwa nguvu ukavunjika.
Huku nikiwa nimepigwa na butwaa, niliingia ndani ambako muda mfupi uliopita moto mkubwa ulikuwa umetanda kila sehemu lakini cha ajabu kila kitu kilikuwa sehemu yake, nikageuka huku nikiwa siamini, nikakutana na baba na mwenyeji wake ambao kumbe walikuwa nyuma yangu wakinitazama.
“Ulimaanisha chumba hiki au kingine?”
“Hikihiki, nashangaa sijui imekuwaje, kwani nyie hamjasikia kelele za kuomba msaada?”
“Mimi nimesikia kelele za mlango kuvunjwa tu, basi.”
“Mungu wangu,” nilisema kwa hofu kubwa, nikijihisi kama nipo kwenye ndoto ya kutisha.
“Na vipi kuhusu hii?” baba aliniuliza, huku akinionyeshea nguo yangu ya ndani iliyokuwa pale chini ya kitanda cha Rahma. Kumbe wakati muda ule navaa nguo zangu, niliisahau si unajua tena maisha ya kijijini kuvaa hiyo kitu hasa kwa sisi wanaume siyo kitu cha lazima sana? Aibu ya mwaka ilikuwa imenifika.
“Eti kumetokea nini kwani?” sauti ya mama yake Rahma ilisikika, akiwa ameongozana na binti yake ambaye sasa fahamu zilikuwa zimemrudia, wakiwa pamoja na mama. Nilishindwa hata cha kujibu, mate yakanikauka ghafla mdomoni.
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 15
ILIPOISHIA:
“ETI kumetokea nini kwani?” sauti ya mama yake Rahma ilisikika, akiwa ameongozana na binti yake ambaye sasa fahamu zilikuwa zimemrudia, wakiwa pamoja na mama. Nilishindwa hata cha kujibu, mate yakanikauka ghafla mdomoni.
SASA ENDELEA…

“ETI Rahma, nini kimetokea?” “Nilikuwa nimelala, ghafla nikaanza kuhisi kama naungua hivi, sijui tena kilichotokea mpaka nilipokuja kuzinduka kule sebuleni,” alisema na kunifanya nimtazame kwa macho ya mshangao.
Ni yeye pekee ndiye ageweza kuthibitisha kilichotokea lakini kwa maelezo yale, japo alizungumzia kidogo kuhusu kuhisi anaungua, bado yasingetosha kumfanya mtu aamini nilichokuwa nakizungumza. “Na hii nguo imefikaje huku?”
“Niliposhtuka usingizini, sikuwa nimevaa nguo kwa hiyo katika zile purukushani za kuwahi kuja kumuokoa dada nikasahau kuivaa na nadhani ilikuwa kwenye nguo zangu ndiyo maana ikaja kuangukia humu ndani,” nilisema.
Sijui nilipata wapi akili za kutunga uongo mkubwa kiasi hicho. Baba alinitazama usoni, nikakwepesha macho yangu kwa sababu baba alikuwa na uwezo wa kumgundua mtu anayezungumza uongo kwa kumtazama na kwa sababu sikuwa na kawaida ya kudanganya, nilijua anaweza kunigundua kwa haraka.
Namshukuru Mungu uongo wangu ulipita, baba akaisukumia ile nguo kwangu kwa kutumia mguu wake wa kushoto. Niliinama haraka na kuiokota, nikaisunda mfukoni, kiukweli nilijisikia aibu sana kwa sababu mama alikuwepo, mama yake Rahma alikuwepo na hata Rahma mwenyewe.
Licha ya kulimaliza hilo la kwanza kwa kuongea uongo, bado mjadala mkubwa ulibaki kwenye ishu ya mimi kusema chumba cha Rahma kilikuwa kikiwaka moto huku kukiwa hakuna dalili zozote za moto. Niliwaona baba na baba yake Rahma wakinong’onezana jambo, kisha baba yake Rahma akamnong’oneza mkewe, baba akanishika mkono na kunitoa nje, baba Rahman naye akafuatia, kwa lugha nyepesi wanaume tukatoka na kuwaacha mama Rahma, mwanaye na mama.
Tulienda mpaka nje kabisa, tukakaa kibarazani mimi nikiwa katikati, baba akanigusa begani na kunipigapiga. “Hebu sema ukweli, nini kilichotokea mpaka ukaenda kuvunja mlango na kumtoa dada yako mzobemzobe.” “Moto ulikuwa unawake, tena moto mkubwa kwelikweli.”
“Lakini wewe si unafahamu kwamba moto ukiwaka lazima uache ishara yoyote na unavyosema kwamba ulikuwa ni moto mkubwa, inawezekanaji muda huohuo sisi tuende chumbani na tusikute moto wala dalili zozote za moto?” “Aaah… eeh hata mimi ndiyo nasha…ngaa,” nilisema kwa kubabaika, maji yalikuwa yamenifika shingoni na hata sijui ningetumia lugha gani ili nieleweke.” “Umeanza kuvuta bangi kama kaka zako?” baba aliniuliza swali ambalo lilinifedhehesha sana.
Sikuwahi kutumia kilevi cha aina yoyote tofauti na kaka zangu ambao kule kijijini walikuwa na tabia ya kutembea na vijana wahuni wa kijiji ambao ilikuwa inaaminika kwamba wanavuta bangi ndiyo maana walikuwa na uwezo wa kulima mashamba makubwa bila kuchoka au kufanya kazi ngumu za migodini kwa muda mrefu. Nilitingisha kichwa kukataa, akaniambia kwamba ananiamini sana ndiyo maana ananipa upendeleo kuliko mtu yeyote kwenye familia yetu, akanitaka nisimuangushe na kama nina tatizo lolote nimwambie kuliko kumficha. Baba yake Rahma naye aliongeza kwamba wananiamini na kuna kazi kubwa mbele yetu ambayo walishakubaliana kwamba watashirikiana na mimi kwa hiyo lazima niwe makini sana.
“Haya nenda kalale,” alisema baba, nikainuka kinyonge na kuanza kutembea kuelekea ndani, huku nikijisikia vibaya sana kwa sababu niliamini nilichokifanya ilikuwa ni kwa nia njema kabisa lakini kibao kilinigeukia, nikaonekana eti mimi ni mvuta bangi! Nilijisikia vibaya sana kiukweli.
Nilipitiliza moja kwa moja mpaka chumbani, nikaingia na kujitupa kitandani na kuanza kutafakari kwa kina juu ya kilichotokea. Mambo yalikuwa yametokea kwa kasi mno, yaani siku moja ilikuwa na matukio chungu nzima, yaani kama ingekuwa ni filamu, basi nina hakika ingependwa sana.
Kutokana na uchovu wa safari na matukio yote yaliyotokea kutwa nzima, kuanzia alfajiri tulipoianza safari ya kutoka Makongorosi mpaka muda huo, tukiwa tayari ndani ya Jiji la Dar es Salaam, nilipitiwa tena usingizi mzito. Safari hii sikushtuka mpaka asubuhi na kilichoniamsha zilikuwa ni kelele za mafundi waliokuwa wakitengeneza mlango wa chumba cha Rahma.
Nikaamka na kukaa kitandani, kumbukumbu za matukio yaliyotokea jana yake zikaanza kurudi kichwani mwangu, ndugu yangu niliyelala naye alishaamka muda mrefu tu na hakuwepo chumbani kwa hiyo nilikuwa peke yangu.
“Kaka Togo! Kaka Togo,” sauti ya kike ilisikika nje ya mlango wa chumba kile, kabla sijajua cha kufanya mlango ulifunguliwa, nikakutana na sura nzuri ya Rahma, tabasamu pana likiwa limechanua usoni mwake. Aligeuka nyuma kama anayetazama kama kuna mtu anayemuangalia kisha nikamuona akiingia na kufunga mlango kwa ndani.
“Nimekuja kukuita tukanywe chai lakini pia nimekuletea zawadi,” alisema huku akinipa ‘apple’ la rangi ya kijani. Niliachia tabasamu na kulipokea, nikaanza kulila kuchangamsha mdomo kwani tangu nimeamka hata mswaki sikuwa nimepiga. Alikuja na kukaa pembeni yangu pale juu ya kitanda, akawa ananitazama kwa macho yake mazuri wakati nikilila lile tunda alilonipa.
“Samahani, eti kwani jana usiku kulitokea nini? Naomba nisamehe kama nimekusababishia matatizo.”
“Aah, kawaida tu wala usijali.” nilimjibu kwa mkato, sikutaka kujadiliana naye sana kuhusu kilichotokea, akaendelea kuniuliza maswali lakini nikawa namkatisha, nikamwambia tutazungumza vizuri kuhusu suala hilo muda muafaka ukifika.
“Samahani kama nimekuudhi,” alisema huku akiinuka na kunibusu kwenye shavu langu kisha akanikumbatia na kunibusu tena. “Usijali kabisa, wala hujaniudhi,” nilisema huku mapigo ya moyo wangu yakianza kwenda mrama.
Nikiri wazi kwamba Rahma alikuwa mzuri sana, kitendo cha kunikumbatia, kumbukumbu za tulichokifanya jana yake zilianza kujirudia ndani ya kichwa changu. Na mimi nilimkumbatia na kushika kiuno chake, nikamuona akijinyonganyonga huku akinitazama kwa macho kama vile bado alikuwa na usingizi. Hamasa niliyokuwa naipata, ilinifanya nisiogope chochote, nikaamua kuyavulia tena maji nguo, tayari kwa kuyaoga.
Muda mfupi baadaye, tulikuwa msambweni na Rahma lakini safari hii tulikuwa tukijizuia kutoa aina yoyote ya kelele kwani tulikuwa tunajua kwamba watu wote wameshaamka. Yaani ndani ya muda mfupi tu, Rahma alishaingia ndani ya moyo wangu na kunifanya nimpende sana na kuwa tayari kwa chochote.
Tuliendelea kupigiana pasi fupifupi, wakati mwingine Rahma akawa anashindwa kujizuia na kutoa miguno ya hapa na pale, tukiwa tunaendelea, tulishtuka baada ya kusikia minong’ono dirishani kwa upande wa nje. Kwa ilivyoonyesha, kuna watu walikuwa wakifuatilia kila kilichokuwa kinaendelea.
“Togo,” nilisikia sauti nzito ya baba ikiniita, harakaharaka nikamtoa Rahma, kila mmoja akawa anahaha kujiweza vizuri. “Togooo,” alirudia kuniita, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio mno huku mdomo ukiwa mzito kufunguka. Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 16
ILIPOISHIA:
“TOGO,” nilisikia sauti nzito ya baba ikiniita, harakaharaka nikamtoa Rahma, kila mmoja akawa anahaha kujiweza vizuri.
“Togooo,” alirudia kuniita, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio mno huku mdomo ukiwa mzito kufunguka.
SASA ENDELEA…

“NAAM!”
“Hebu sogea hapa dirishani,” alisema baba, harakaharaka nikavaa nguo zangu, Rahma naye akawa ameshavaa nguo zake na bila kujali atakutana na nani nje, alitoka kwa kasi.
“Wewe Togo, si nimekwambia sogea hapa?” alisema baba, safari hii akigonga kioo cha dirisha. Kwa kuwa tayari nilishavaa, nilisogea pale dirishani na kufunua pazia pamoja na dirisha moja, nikamuona baba amenikazia macho.
“Unafanya nini?”
“Nilikuwa nafanya mazoezi ya kupiga pushapu.”
“Kweli?”
“Kweli baba.”
“Hebu funua pazia lote,” alisema baba, kwa kuwa nilikuwa na uhakika Rahma ameshatoka, nilifunua pazia lote, akatazama huku na kule kisha akarudi kunitazama usoni.
“Mwanangu Togo, mbona tangu tumeanza safari umekuwa ni mtu wa kututia aibu kila sehemu? Una nini kwani wewe?”
“Mama sasa kwani mi nimefanya nini? Ina maana hata kufanya mazoezi ndani nako ni makosa?” nilimjibu mama ambaye kumbe alikuwa na baba kule nje, nikavaa uso wa huruma ili kuwafanya waniamini kile nilichokuwa nakisema.
“Hivi unatufanya sisi wote ni watoto wadogo kama wewe?” alisema baba huku akiwa amekazia macho suruali niliyokuwa nimevaa, ikabidi na mimi nijiangalie. Cha ajabu, suruali niliyokuwa nimevaa nilikuwa nimeigeuza nje ndani, aibu niliyoihisi ilikuwa kubwa mno, ikabidi niliachie pazia na kurudi kitandani huku nikikosa cha kujibu.
“Nitasema wakati wa kuvaa nimevaa harakaharaka, bado nitaendelea kukataa kwamba sijafanya chochote,” nilijisemea huku nikiivua ile suruali na kuivaa vizuri. Kwa kuwa mwanzo Rahma alipokuja aliniambia kwamba chai ipo tayari, ili kuzidi kupoteza ushahidi, niliamua kupitia kwanza bafuni kabla sijaenda sebuleni.
Nikanawa uso harakaharaka na kutoka kuelekea sebuleni, bado wale mafundi walikuwa wakiendelea kutengeneza mlango na nahisi walikuwa wanajua kilichokuwa kinaendelea kati yangu na Rahma kwa sababu wakati natoka bafuni, wote waliacha kila walichokuwa wanakifanya na kunitazama usoni, wakionyesha dhahiri kwamba walikuwa na shauku ya kunijua.
Sikuwasemesha kitu, hata salamu sikuwapa, nikapitiliza moja kwa moja mpaka sebuleni ambako niliwakuta karibu watu wote wakiwa wanakunywa chai isipokuwa wazazi wa pande zote mbili, kwa maana ya baba na mama yetu na baba na mama yao akina Rahma, kila mmoja akiwa na kikombe chake na vitafunwa vyake.
Kabla hata sijakaa, Rahma aliinuka na kunichukulia kikombe, akanimiminia chai na kunisogezea pale nilipokuwa nimekaa pamoja na vitafunwa. Watu wote walikuwa kimya kabisa, macho yakiwa kwenye runinga kubwa ya kisasa.
Wakati akinisogezea chai, Rahma alinitazama kwa macho ya kuibia, na mimi nikamtazama, macho yetu yakagongana ambapo nilimuona akiachia tabasamu pana huku aibu za kikekike zikiwa zimetawala kwenye uso wake.
Hakutaka kurudi kukaa pale alipokuwa amekaa awali, alichukua kikombe chake cha chai na kuja kukaa pembeni yangu, nikawaona ndugu zangu, akiwemo dada Sabina wakinitazama kwa macho ya chinichini.
Ukimya uliendelea kutawala, tukaendelea kunywa chai na baada ya kumaliza, Rahma na dada Sabina waliinuka na kuanza kutoa vyombo, tayari kwa ajili ya kwenda kuviosha lakini ghafla mama aliingia akiwa ameongozana na mama yake Rahma. Kwa kuwatazama tu sura zao, ilionyesha kuna jambo halikuwa sawa.
“Togo, njoo huku,” alisema mama, mama yake Rahma naye akamuita Rahma, ikabidi aache kutoa vyombo, wote tukaelekea kule nje ambako tulikuta wazazi wetu wakiwa wamekaa kwenye viti vilivyokuwa pale nje, wote wakionyesha kutokuwa na furaha kwenye nyuso zao.
“Hebu tumbieni, hivi Togo na Rahma mlikuwa mnafahamiana kabla?” aliuliza baba yake Rahma, muda mfupi tu baada ya sisi kufika.
“Hapana,” nilisema huku nikitingisha kichwa.
“Mbona ndani ya muda mfupi tu tangu mkutane mmekuwa na nyendo zinazotutia mashaka? Hivi mnajua kama nyie ni ndugu?” alisema baba yake Rahma na kunifanya nishtuke.
Alichokuwa ametuambia baba, ni kwamba baba yake Rahma alikuwa ni rafiki yake wa siku nyingi ambaye walishirikiana vitu vingi pamoja na ndiyo maana hata alipoona mambo hayaendi vizuri kule Chunya, majirani na wanakijiji wakiituhumu familia yetu kuwa inajihusisha na Imani za kishirikina aliamua kuondoka na sisi mpaka jijini Dar es Salaam.
“Sikuwa nimewafafanulia mwanzo lakini ukweli ni kwamba ukiacha urafiki wetu, sisi ni ndugu, mama yangu kwa maana ya bibi yenu na mama mzazi wa baba Rahma ni mtu na mdogo wake, kwa hiyo sisi ni ndugu na nyie ni ndugu, tena wa damu kabisa,” alisema baba, kauli ambayo ilinishtua mno.
“Msije mkatuletea aibu ya mwaka hapa maana naona mmeshaanza kuonyesha kupendana, nyie ni ndugu na kwa ukoo wetu sisi ndugu wakifanya dhambi kama hiyo, husababisha mabalaa makubwa sana kwenye ukoo mzima,” baba yake Rahma alizidi kupigilia msumari.
Japokuwa ilikuwa ni asubuhi, nilijikuta kijasho chembamba kikinitoka, lilikuwa ni jambo ambalo sikulitegemea kabisa, nikageuka na kumtazama Rahma, nikamuona akiwa amejiinamia kwa aibu.
Sikuwahi kuwa na skendo yoyote ya mapenzi na hata wazazi wangu hawakuwahi kusikia jambo lolote baya kuhusu mimi lakini cha ajabu, ndani ya muda mfupi tu niliokutana na Rahma na kunionjesha ulimwengu wa kikubwa, tayari kila mtu alikuwa na wasiwasi na mimi. Nilijisikia aibu sana.
“Mmeelewa?” alihoji baba, nikajibu kwa kutingisha kichwa, wakatuambia tukaendelee na tulichokuwa tukikifanya, wakati tukiondoka tukawasikia wakipiga stori na kucheka, nadhani baba alizungumza kitu kuhusu mimi kilichowavunja mbavu wote.
Tulipoingia sebuleni, tulikuwa kama tumemwagiwa maji ya baridi, afadhali mimi kidogo niliweza kujikaza, Rahma alionyesha kuchoka mno, macho yakawa mekundu kama anayetaka kulia.
Hakuweza kuendelea kukaa pale sebuleni, nilimuona akiinuka kwa unyonge, akaelekea chumbani kwake ambapo tayari mafundi walikuwa wamemaliza kutengeneza mlango wa chumba chake, akaingia ndani na kujifungia.
Sikumuona tena akitoka mpaka muda wa chakula cha mchana, mimi na ndugu zangu tukawa tunaendelea kushangaa runinga na vitu vingine vya kisasa vilivyokuwa mle ndani.
Baada ya chakula cha mchana kuiva, mama yake Rahma alimtuma mdogo wake kwenda kumuita chumbani kwake wakati chakula kikipakuliwa. Muda mfupi baadaye, alikuja na majibu kwamba dada yake alikuwa amelala chumbani lakini alipojaribu kumuamsha, hakuamka.
“Unasema?” mama yake Rahma aliuliza kwa mshtuko, huku akiacha kila alichokuwa anakifanya. Haraka akakimbilia chumbani kwa mwanaye, huku akionyesha kuwa na wasiwasi mkubwa moyoni mwake, mama naye akamfuata, na mimi uzalendo ukanishinda, nikainuka na kuwafuata.
Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 17
ILIPOISHIA:
“UNASEMA?” Mama yake Rahma aliuliza kwa mshtuko, huku akiacha kila kitu alichokuwa akifanya. Haraka akakimbilia chumbani kwa mwanaye huku akionyesha wasawasi mkubwa moyoni mwake, mama naye akamfuata, na mimi uzalendo ukanishinda, nikainuka na kuwafuata.
SONGA MBELE...

TULIPOINGIA chumbani, mama yake Rahma akaanza kumuamsha kwa kumwita lakini hakuitika wala kutikisika, akasema; “mwanangu umepatwa na nini?” Hata hivyo, Rahma hakuitika wala kufumbua macho, jambo hilo lilitushtua sana, mama naye alipojaribu kumwita hali ikawa vilevile, Rahma alitulia kimya.
Sikukubaliana na hali hiyo, nilijongea kitandani alipolala Rahma, nikamshika begani na kuanza kumtikisa huku nikimwita, kama ilivyokuwa kwa mama yake na mama, kipenzi changu Rahma hakuitika. Kilichofuatia ni kila mmoja wetu kuanza kulia kwani tulijua alikuwa ametutoka, kufuatia vilio vyetu baba yake Rahma alisikia akaja mbio kujua kilitokea nini, akina mama wakiwa wanalia walishindwa kumweleza chochote zaidi ya kulia.
“Eti Togo, kimetokea nini?” akaniuliza. Nilimfahamisha kilichotokea, akiwa amepata mshtuko, mzee huyo alimshika Rahma kifuani akagundua mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa mbali, akawauliza akina mama alipatwa na nini. Mama ya Rahma akamweleza kila kitu, mzee huyo aliwaambia wanyamaze kwani Rahma alikuwa hajafa, mzee huyo aliniambia niende haraka kwa jirani aliyekuwa na usafiri ili amkimbize Rahma hospitali.
Nikiwa nimechanganyikiwa na tukio hilo, nilikwenda kwa jirani huyo ambaye alikuja na gari lake tukampakiza Rahma na kumkimbiza hospitali, alipofikishwa huko alifanyiwa uchunguzi na kuibainika alikunywa dawa mchanganyiko ili ajiue. Madaktari walimuwekea dripu ya maji kisha antpoison kuondoa sumu hiyo, wakati akipewa matibabu hayo alikuwa hajitambui, madaktari walituambia tusiwe na wasiwasi kwani baada ya muda mfupi hali yake ingetengemaa.
“Kati yenu ni nani wazazi wa huyu binti?” Daktari aitwaye Jason aliwauliza akina mama na akina baba! “Mimi mama yake na huyu hapa ndiye baba yake,” mama ya Rahma alimjibu daktari huyo huku akimuonyeshea mumewe. “Oke, naomba twendeni ofisini kwangu tukazungumze kuhusiana na tatizo la binti yenu,” daktari huyo aliwaambia.
“Hakuna shida daktari,” baba ya Rahma alimwambia. “Kwanza nawapeni pole kwa jambo lilitokea kwani najua ni kwa kiasi gani mmepata mshtuko,” daktari aliwaambia. “Tunashukuru dokta, pia tunashukuru kwa jinsi ulivyompokea na kumhudumia kwa wakati,” mama yake Rahma alimwambia daktari. Alipoambiwa, daktari aliwaambia wasijali kwani huo ndiyo wajibu wao kwa wagonjwa kisha akawauliza kilitokea nini nyumbani kilichosababisha Rahma kutaka kujiua!
“Kwa kweli hata sisi tumeshangazwa sana na uamuzi wake, ameamka akiwa mukheri wa afya, tumeshinda naye vizuri hadi mchana mama yake alipomtuma ndugu yake akamuamshe kwa ajili ya kula ndipo akarudi mbio na kumweleza alimwita hakuitika na alipojaribu kumtikisa alitulia tu!” baba ya Rahma alimweleza daktari.
“Oh poleni sana, lakini lazima kutakuwa na sababu kwani katika hali ya kawaida siyo rahisi kwa mtu kuchukua uamuzi wa kutaka kujiua bila ya kukwazwa na jambo f’lani, je, yupo katika uhusiano wa kimapenzi na mtu yeyote?” Daktari aliwauliza. “Hatuelewi maana hatujawahi kumuona na mwanaume yeyote,” mama Rahma alimwambia.
Alipotoa kauli hiyo, daktari Jason aliwauliza tena kama binti yao alikuwa na ugomvi na mtu yeyote hasa marafiki zake, wazazi wake wakamwambia hakuwa na ugomvi. “Labda aliomba mnunulie kitu f’lani mkamkatalia kwa ukali?”
Daktari huyo alizidi kuwabana kwa maswali ili tu kujua sababu ya Rahma kutaka kujiua. “Kwa upande wangu hajaniomba chochote labda mwenzangu,” mama yake alimjibu daktari. “Eh! Baba au alikuomba fedha ukamnyima,” daktari akamwuliza. “Hapana daktari, tena juzi tu nimempatia fedha za kutosha kwa ajili ya matumizi yake,” mzee huyo alimwambia.
Baada ya maswali hayo na majibu, daktari aliwaambia lazima kuna jambo ambalo wazazi hawalifahamu lililosababisha Rahma kutaka kujiua, akawashauri wawe wanachunguza nyendo za watoto wao hasa mabinti kwa sababu wana mambo mengi sana.
***
Wakati kule ofisini kwa daktari Jason akiendelea kuzungumza na wazazi wa Rahma, nje baba yake Togo na mama yake ambao hawakuwa na furaha walikuwa wakizungumza kuhusu tukio hilo. “Hivi mama Togo, kitendo cha kuwauliza hawa watoto kama wanafahamiana tangu zamani na kwamba ukaribu wao unatutia shaka inaweza kuwa sababu ya Rahma kutaka kujiua?” baba Togo alimwuliza mkewe.
“Sidhani, nahisi kutakuwa na jambo lingine tu mume wangu,” mama huyo alimwambia mumewe. Alipoambiwa hivyo, mumewe alimweleza mkewe kwamba huenda tayari walishaanza kufanya utundu na sababu ya kutaka kujiua ni baada ya kuwaambia walikuwa ndugu!
“Ila unachosema naona umenifungua kichwani, huenda ikawa hivyo ili kuficha aibu ya kutembea na kaka yake, lakini tusiwaze sana kuhusu hilo tutajua tu ukweli!” mama Togo alimwambia mumewe.
Hata hivyo, baba Togo alimwambia mkewe kwamba ngoja wamsubiri Togo aliyekuwa amekwenda kununua maji ya kunywa arejee ili wambane kwani walihisi alikuwa anajua sababu za mwenzake kutaka kujiua. “Nakuunga mkono, atakuwa anajua japo anajifanya hajui chochote,” mama Togo alimwambia mumewe. “Mh! Huyu mtoto ana hatari sana, hata kama wameshafanya utundu na kaka yake uamuzi aliochukua siyo mzuri hata kidogo,” baba Togo alimwambia mkewe kwa huzuni.
“Ila mke wangu kama kweli hawa watoto watakuwa wamefanya utundu itakuwa dhambi kubwa ambayo italeta balaa na tutakuwa tumesababisha sisi kushindwa kuwaambia mapema kwamba walikuwa ndugu,” baba Togo alimwambia mkewe.
“Sijui itakuwaje sasa mume wangu, lazima balaa litokee tuombe tu Mungu Togo atuhakikishie kwamba hawafanyi mapenzi na ndugu yake,” mama Togo alimwambia mumewe. Wakati wakizungumza hayo, mara wakawaona baba na mama Rahma wanakwenda walipokuwa wakitokea ofisini kwa daktari, wakaacha mazungumzo yao. Je, kilifuatia nini?
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 18
ILIPOISHIA:
“SIJUI itakuwaje sasa mume wangu, lazima balaa litokee tuombe tu Mungu Togo atuhakikishie kwamba hawajafanya mapenzi na ndugu yake,” mama Togo alimwambia mumewe.
Wakati wakizungumza hayo, mara wakawaona baba na mama Rahma wanakwenda walipokuwa wakitokea ofisini kwa daktari, wakaacha mazungumzo yao.
SASA ENDELEA...

“VIPI anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri, mtoto mjinga sana huyu.”
“Mh! Usimuite mjinga, huu siyo muda wake, uchungu wake naujua mimi, nimembeba kwenye tumbo langu kwa miezi tisa,” alisema mama yake Rahma akionyesha kutofurahishwa na kauli ya mumewe. Walitoka pamoja na kwenda kukaa kwenye benchi lililokuwa nje ya jengo hilo la hospitali, mimi nikaenda kukaa upande wa pili.
“Hivi, mnajua mimi bado sina majibu juu ya haya maswali niliyonayo.”
“Maswali gani yanayokusumbua?”
“Ni kwa sababu gani Rahma amechukua uamuzi wa kuyakatisha maisha yake?”
“Mh! Hawa watoto wetu wa siku hizi, mimi nahisi alikuwa anampenda Togo sasa kitendo cha kuwaambia kwamba ni ndugu ndiyo maana ameamua kufanya aliyoyafanya, tumshukuru Mungu bado yupo hai.”
“Unachokisema ni sawa lakini nahisi kuna kitu zaidi ya hicho, nahisi hawa watoto walikuwa wameshaanza kufanya mapenzi.”
“Mh! Ninavyomjua Togo huwa hana kawaida ya kuwa karibu na wasichana kabisa, ni muoga sana wa wasichana, sidhani kama hilo linawezekana.”
“Hata Rahma naye si mcharuko kiasi hicho, sijawahi hata kumuona akiwa na mwanaume kichochoroni, kama mambo hayo anayafanya basi anafanya kwa siri sana, kwa ufupi anajiheshimu.”
“Sasa kama tatizo siyo hilo, mnafikiri nini kinaweza kuwa chanzo?”
“Mh! Mimi nakuunga mkono rafiki yangu, kuna kitu nimekihisi na kwa kuunganisha matukio, inawezekana ni kweli wakawa wameshaanza kukutana kimwili,” alisema baba na kusimama, akageuka huku na kule, nilishajua ananitafuta mimi na hakuwa akijua kwamba kumbe nilikuwa palepale jirani yao, nikisilikiza kila kilichokuwa kinaendelea.
“Hebu njoo hapa,” alisema huku uso wake ukiwa na jazba, nikasogea huku uso wangu nikiwa nimeuinamisha chini.
Pale kulikuwa na makundi mawili, baba yake Rahma na baba, wao walikuwa waking’ang’ania kwamba lazima mimi na Rahma tayari tumeshavunja amri ya sita wakati mama na mama yake Rahma, wao walikuwa wakitutetea, kila mmoja na mwanaye.
“Ule mzigo niliokupa safarini uko wapi?” nilishangaa baba akiniuliza swali tofauti kabisa na nililolitegemea. Nikaanza kuvuta kumbukumbu anazungumzia mzigo gani, kwa kutumia tafsida akanifafanulia mpaka nikaelewa kwamba kumbe alikuwa akimaanisha ile dawa aliyonipa pale Mlima Nyoka, Mbeya baada ya kunusurika kwenye ajali mbaya ya gari.
“Ipo nyumbani,” nilimdanganya lakini ukweli ni kwamba licha ya kunisisitiza sana niitunze dawa hiyo, ilikuwa imeniponyoka na kutumbukia kwenye shimo la choo, nyumbani kwa akina Rahma wakati nikioga.
“Una uhakika?”
“Ndi... ndi...yo,” nilibabaika. Baba alikuwa akinijua vizuri, nadhani kwa kubabaika huko, alielewa kwamba dawa hiyo haipo salama, akasimama na kunishika mkono, akanivuta kwa nguvu pembeni.
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho, dawa yangu iko wapi?”
“Baba nisamehe, ilitumbukia chooni.”
“Unasemajee?” baba alishtuka kuliko kawaida. Mshtuko aliouonyesha ulinifanya nielewe kwamba kumbe dawa ile kutumbukia chooni halikuwa jambo la kawaida.
“Kwa nini umeniangusha mwanangu? Kwa nini umewapa ushindi?” alisema baba huku akiwa anatingisha kichwa chake kwa masikitiko, nikawa sielewi anamaanisha nini.
“Halafu kwa nini usiniambie mapema ili tujue nini cha kufanya?”
“Nisamehe baba.”
“Nataka uniambie ukweli, wewe umeshafanya mapenzi na Rahma, kweli si kweli?” baba alinihoji, safari hii akiwa amenikazia macho usoni, nikawa nashindwa kama nikubali au nikatae.
“Unaona upumbavu wako? Yaani hili halijaisha umeanzisha jingine, hivi una nini wewe?” alisema baba, akiwa tayari ameshajipa majibu kuhusu swali alilouliza. Nilishindwa cha kusema, nikajiinamia chini kwa aibu, masikitiko na huzuni vyote kwa wakati mmoja.
“Upumbavu ulioufanya utasababisha matatizo makubwa sana kwa watu wasio na hatia, hata sijui itakuwaje,” alisema baba huku akionyesha kuchanganyikiwa kabisa, akaondoka na kuniacha palepale nikiwa nimesimama, na mimi nikiwa nimechanganyikiwa.
Alienda pale alipokuwa amemuacha mama na wazazi wa Rahma, wakawa wanazungumza kitu kisha nikaona wote wamegeuka na kunitazama, hata sijui walikuwa wakizungumza nini.
“Wakiwa bado wananitazama, nesi mmoja alifungua mlango wa wodi aliyokuwemo Rahma na kutoka mbiombio mpaka kwenye ofisi ya madaktari iliyokuwa hapohapo jirani, muda mfupi baadaye akatoka tena mbiombio lakini safari hii alikuwa ameongozana na madaktari wawili ambao nao walikuwa wakikimbia.
Niliwaona akina baba wakikatisha mazungumzo yao na kusimama, huku macho yao yakiwa kwenye ule mlango wa wodi. Mle wodini kulikuwa na wagonjwa kadhaa ila sijui kwa nini akili yangu ilinituma kuamini kwamba walikuwa wakimkimbilia Rahma. Hata akina baba nao nadhani walishajua kwamba mwenye tatizo ni Rahma.
Sikutaka kuandikia mate wakati wino upo, nilitimua mbio kutoka pale nilipokuwa na kukimbilia kwenye mlango wa ile wodi, nikaupiga kikumbo mlango na kuingia mpaka ndani, macho yakiwa pale kwenye kitanda alichokuwa amelazwa Rahma.
Madaktari na manesi walikuwa wamemzunguka, nikasogea kutaka kujionea amepatwa na nini? Nilichokiona sikukiamini. Rahma alikuwa akitapatapa kama anayetaka kukata roho, kibaya zaidi damu nyingi zilikuwa zikimtoka mdomoni na puani, kiasi cha kusababisha mashuka meupe aliyokuwa amelalia yalowe damu.
“Aisee, huruhusiwi kuingia humu, muda wa kuona wagonjwa haujafika,” mlinzi ambaye mkononi alikuwa na rungu kubwa, aliniambia huku akilitingisha lile rungu, akanionyesha ishara kwamba nitoke nje vinginevyo ataniadhibu.
Ilibidi nitoke tu kwani sikutaka matatizo zaidi, ukizingatia na hali niliyomuona nayo Rahma ndiyo nilizidi kuchanganyikiwa.
“Vipi kuna nini?” baba aliniuliza nilipotoka tu, ikabidi nimueleze hali halisi, nikamuona na yeye akishusha pumzi ndefu na kushika kiuno.
“Haya yote ni kwa sababu yako na hawezi kupona kwa kutibiwa hospitali, dawa yake unayo wewe,” alisema baba huku akinitazama kwa macho ya ukali.
“Mimi? Dawa gani?”
“Inabidi ufute makosa ya upumbavu wako wote ulioufanya, hiyo ndiyo itakuwa ponapona yake, mtoto mshenzi sana wewe, wala sikukutegemea,” alisema baba huku akinisogelea mwilini, nikahisi lazima atanizabua makofi kwa sababu anapokasirika sana huwa hawezi kudhibiti hasira zake.
“Itabidi tuwaombe tuondoke naye mpaka nyumbani, nitaenda kukuelekeza nini cha kufanya kumsaidia,” alisema kwa sauti ya kunong’ona, nikahisi kama amechanganyikiwa akili. Yaani kwa hali aliyokuwa nayo, halafu eti akawaombe madaktari tuondoke naye kurudi nyumbani? Niliona ni kitu kisichowezekana.
Baba aligeuka na kuondoka, akasogea pembeni na kuanza kuzungumza na baba yake Rahma. Akina mama wao niliwaona wameshaanza kuchanganyikiwa, mama yake Rahma akawa analia. Nilijisikia vibaya sana ndani ya moyo wangu, hasa kwa jinsi baba alivyokuwa ananishutumu kwamba mimi ndiyo chanzo cha yote yale.
Mara mlango wa wodi ulifunguliwa, daktari mmoja akachungulia nje na kuwaonyesha ishara ya kuwaita baba na baba yake Rahma, mapigo ya moyo wangu yakalipuka mno, sikujua anaenda kuwaambia nini, akilini nikawa nahisi kabisa kwamba mambo yameshaharibika.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na hatia)- 19
ILIPOISHIA:
MARA mlango wa wodi ulifunguliwa, daktari mmoja akachungulia nje na kuwaonesha ishara ya kuwaita baba na baba yake Rahma, mapigo ya moyo wangu yakalipuka mno, sikujua anaenda kuwaambia nini, akilini nikawa nahisi kabisa kwamba mambo yameshaharibika.
SASA ENDELEA...

“Kuna tatizo.” “Nini tena daktari?” “Mgonjwa wenu anaishiwa damu kwa kasi kubwa mno, isitoshe anatapika damu, hatujui tatizo ni nini kwani vipimo havioneshi tatizo lingine lolote zaidi ya kwamba alikunywa sumu kwa lengo la kujiua.”
“Sasa tutafanyaje dokta?” “Inabidi kwanza tushughulikie hili suala la kupungukiwa damu, inabidi wanandugu muitane kwa ajili ya kuchangia damu, mkiwa tayari mniambie ngoja nizungumze na watu wa kitengo cha damu waandae vifaa,” alisema yule daktari na kuingia wodini, nikawaona baba na baba yake Rahma wakitazamana.
“Nahisi kuna nguvu za giza nyuma ya hili suala na kama tusipotumia nguvu za ziada, tunaweza kumpoteza binti yetu,” alisema baba, mwenzake akawa anatingisha kichwa kuonesha kuunga mkono alichokuwa anakisema. “Mimi nina wazo, unaonaje tukiondoka na mgonjwa wetu tukamtibu nyumbani. Kuna kitu tukikifanya mara moja anapona huyu.”
Nilishangazwa sana na uamuzi walioufikia, yaani mgonjwa ana hali mbaya kiasi kile halafu wamuondoe hospitali na kwenda naye nyumbani? Akifa je? Nilijiuliza bila kupata majibu. Muda mfupi baadaye, baba aligonga tena mlango wa wodi, yule daktari akafungua mlango kwa lengo la kusikiliza walichokiamua. “Mmeshakubaliana kuhusu kuchangia damu?”
“Hapana, imani yetu hairuhusu kuchangia damu, tunamuomba mgonjwa wetu tuondoke naye tukajaribu sehemu nyingine,” alisema baba kwa kujiamini, nikamuona yule daktari akiwatazama wote wawili usoni kwa mshtuko. “Ndivyo mlivyokubaliana?”
“Ndiyo,” alisema baba, nikamuona akishusha pumzi ndefu na kuonesha ishara kwamba wasubiri, akaingia ndani nadhani kwa lengo la kwenda kujadiliana na wenzake, muda mfupi baadaye alipotoka, aliwaambia madaktari wenzake wamekataa wazo hilo, wakawaambia afadhali kama wangekuwa wanaomba rufaa kwenda hospitali kubwa lakini kama ni kumrudisha nyumbani, hilo suala haliwezekani.
“Hawa washenzi sana, kwa hiyo wanaamini hatuwezi kumchukua mgonjwa wetu bila ridhaa yao?” alisema baba huku akimshika mkono baba yake Rahma na kuondoka naye, walitoka mpaka nje kabisa ya eneo la hospitali. Nilikuwa na shauku kubwa ya kumsaidia Rahma, nilipohakikisha akina baba wametoka nje, na nilipowatazama mama na mama Rahma kwa mbali ambao walikuwa wakibembelezana pale kwenye
benchi, harakaharaka nilitembea kuelekea kule wodini. “Unasemaje kijana?” “Huyu ni dada yangu, nataka kumtolea damu.” “Ooh! Umefanya jambo la maana sana, twende huku,” alisema yule daktari huku akinishika mkono, tukatoka wodini na kuanza kutembea harakaharaka kwenye korido, tukaelekea mpaka kwenye chumba maalum cha kutolea damu ambapo niliwakuta watu wengine watatu wakiwa wamekaa kwenye vitanda maalum, wakiwa wanajitolea damu.
“Kaa hapo,” alisema yule daktari huku akinionesha sehemu ya kukaa, akapitiliza na kwenda kuzungumza na mwenzake ambaye alikuwa bize akishughulika na mmoja kati ya wale watu waliokuwa wakitoa damu. Akazungumza naye kisha nikaona wote wawili wamegeuka na kunitazama. Muda mfupi baadaye, yule daktari alitoka na kuniaga, akaniambia nikishamaliza niende nikamuone. Alipotoka, yule daktari mwingine ambaye yeye alikuwa amevalia sare za rangi tofauti, alikuja pale nilipokuwa nimekaa, tukasalimiana kisha akaniuliza kama nilikuwa nataka kujitolea damu, nikamjibu kwamba ni kweli.
Alinisogelea na kuanza kunitazama kwenye mkono wangu wa kushoto, akachukua pamba iliyokuwa na spirit, akanipaka sehemu ya ndani ya mkono wangu kisha akanifunga kwa mpira maalum upande wa juu wa mkono, mishipa ikatokeza kwa wingi mkononi. “Huwa unafanya mazoezi?” aliniuliza.
Nilielewa kwa nini ameniuliza swali lile, kazi ngumu za kijijini, ikiwemo kulima na kupasua kuni zilinifanya mimi na ndugu zangu tuwe na nguvu sana mithili ya watu wanaonyanyua vyuma. “Hapana, ni kazi za kawaida tu,” nilimjibu, akatabasamu na kusema wanaume wengi huwa na miili legelege kwa hiyo linapokuja suala la kuchangia damu, inakuwa vigumu kuuona mshipa mkuu wa damu lakini kwangu mimi ulikuwa ukionekana vizuri na ulikuwa mkubwa kama mtu anayefanya mazoezi.
Nikamuona akichukua sindano moja nene iliyounganishwa na mrija kwa nyuma ulioenda hadi kwenye kibegi kidogo cha plastiki cha kuhifadhia damu. Kiukweli sikuwahi kuchomwa sindano hata mara moja kwenye maisha yangu, kule kijijini kwetu mtu ukiumwa zipo dawa za mitishamba kibao. Ukizingatia baba alikuwa mtaalamu wa mambo hayo, alikuwa akizijua dawa za magonjwa karibu yote. Hata hivyo, sikutaka kuonekana mshamba, ikabidi nijikaze kiume, akanichoma taratibu na kuiingiza ile sindano kwenye mshipa, akanifunga na
bandeji kwa juu kisha akafungua ule mpira, damu ikaanza kutiririka kwa kasi kufuata ule mrija mpaka kwenye kile kimfuko. “Mh! Hii damu yako ikoje?” alisema huku akikiinua kile kimfuko cha damu na kuanza kukitazama kwa karibu. Tofauti na damu za watu wengine mle ndani, yangu ilionesha kuwa nyeusi sana mpaka nikawa najishtukia.
“Ina nini kwani?”
“Ni nyeusi sana na inaganda humu kwenye huu mfuko, sijawahi kukutana na hali kama hii,” alisema huku akinitaka nitulie, akaenda kuwaita wenzake na muda mfupi baadaye, walinizunguka, kila mmoja akiwa ananishangaa. “Unaitwa nani?” “Togo.” “Umewahi kuchangia damu kabla ya leo?” “Hapana, leo ndiyo mara ya kwanza.” “Mbona damu yako iko hivi?” aliniuliza daktari mmoja, ikabidi amuelekeze yule aliyenichomeka ile sindano, harakaharaka wakanitoa ile sindano, wakawa wanaendelea kujadiliana kuhusu damu yangu.
“Tunaomba utusubiri pale nje tutakuita,” alisema yule daktari ambaye ndiye aliyenipeleka kwenye chumba kile, nikainuka huku na mimi nikiwa na maswali mengi kuliko kawaida, nikatoka huku nikiwa nimebana pamba pale kwenye jeraha la sindano ili damu isiendelee kutoka. “Ulikuwa wapi tunakutafuta huku?” baba alinidaka juujuu, macho yake yakatua kwenye pamba niliyokuwa nimeikandamiza pale kwenye jeraha la sindano.
“Na hiki ni nini?” alisema huku akinishika mkono kwa nguvu. “Nilikuwa natoa damu.” “Mungu wangu, hivi wewe mtoto una akili timamu kweli?” alisema baba huku akionesha kushtuka mno, akageuka na kumuonesha ishara baba yake Rahma kwamba aje, harakaharaka akaja mpaka pale tulipokuwa tumesimama.Je, nini kitafuatia?
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 20
ILIPOISHIA
“MUNGU wangu, hivi wewe mtoto una akili timamu kweli?” alisema baba huku akionyesha kushtuka mno, akageuka na kumuonyesha ishara baba yake Rahma kwamba aje, harakaharaka akaja mpaka pale tulipokuwa tumesimama.
SASA ENDELEA...

“UNASIKIA majanga ya huyu mtoto aliyoyazua tena?”
“Kuna nini?”
“Eti alikuwa kujitolea damu.”
“Mungu wangu, kwani hujawahi kumwambia ukweli?”
“Ukweli? Ukweli gani?” niliuliza kwa mshtuko.
“Wewe ni mpuuzi sana, yaani hili halijaisha unaanzisha jingine, kwa hiyo tutakuwa na kazi ya kurekebisha makosa yako tu muda wote,” baba alisema kwa kufoka, baba yake Rahma akawa anamtuliza na kumkumbusha kwamba kuna kazi hawajaimaliza.
“Huyu ndiyo ilitakiwa akaifanye hiyo kazi lakini ameshaharibu tena, unafikiri itakuwaje?”
“Twende tu tutajua hukohuko,” alisema baba Rahma huku akinishika mkono, akanipeleka mpaka kwenye gari aina ya Toyota Noah lililokuwa limepaki jirani na geti la kutokea. Kumbe tayari Rahma alishatolewa wodini na alikuwa ameshaingizwa ndani ya gari, mama na mama Rahma wakawa wamempakata.
Tulipoingia tu, gari liliwashwa na kuondoka, mama akageuka na kunitazama kwa uso wa huzuni kama anayeniuliza ‘ulikuwa wapi?’
Nilikaa na kutulia kimya, safari ikaendelea. Watu wote walikuwa kimya kabisa ndani ya gari, sauti pekee iliyokuwa inasikika, ilikuwa ni ya Rahma aliyekuwa anakoroma. Dereva aliendesha gari kwa kasi na baada ya takribani dakika thelathini, tayari tulikuwa tumefika nyumbani.
Siku hiyo hata sikuwa na hamu ya kulishangaa jiji, maghorofa yote ambayo awali nilikuwa na hamu ya kuyatazama jinsi yalivyo marefu na yenye kuvutia, hayakuwa na maana tena kwangu.
Baba na baba yake Rahma walisaidiana kumshusha mgonjwa na moja kwa moja wakampeleka chumbani kwake.
“Nenda bafuni kaoge, usitumie sabuni, utatumia hii badala ya sabuni,” alisema baba huku akinipa kitu kama jiwe laini lenye rangi nyekundu.
Nikageuka na kuanza kuelekea chumbani kwangu kwa lengo la kubadilisha nguo kwanza.
“Unaenda wapi tena? Nimekwambia kaoge, moja kwa moja bafuni nakuja hukohuko,” alisema baba kwa sauti iliyoonyesha kutokuwa na masihara hata chembe. Nilitii alichoniambia, kauli yake kwamba ‘dawa’ ya kumtibu Rahma nilikuwa nayo mimi, ikaanza kujirudia kichwani.
Nilipofika mlangoni, nilivua mabuti yangu, maana siwezi kuita viatu bali mabuti kutokana na jinsi muundo wake ulivyokuwa. Kule kwetu kijijini mabuti hayo yalikuwa yakivaliwa siku za sikukuu au kunapotokea safari kama hiyo tu lakini siku nyingine zote, mimi na wenzangu tulikuwa tukitembea pekupeku, si unajua maisha ya kijijini tena.
Basi niliyavua pale mlangoni na kuvaa ndala, nikaingia bafuni na kuvua nguo, nazo nikazitundika kwenye misumari maalum na kusogea kwenye bomba. Safari hii sikutaka kutumia bomba la mvua kwani tangu niliposhtukia nikioga damu badala ya maji, nilikuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wangu.
Nilichoamua ni kuoga kwa kutumia maji yaliyokuwa kwenye ndoo ya kuogea, nikajimwagia mwilini kwa kutumia kopo kisha nikaanza kujipaka ile dawa aliyonipa baba. Cha ajabu, nilipokuwa nikijipaka, ilikuwa ikitoa povu kama sabuni na ilikuwa na harufu fulani isiyo ya kawaida.
Yote tisa, kumi ni kwamba nilipojimwagia maji tena juu ya ile dawa, nilishangaa maji yaliyokuwa yakitoka mwilini mwangu yakiwa meusi kama maji yaliyochanganywa na mkaa au masizi. Mara ya kwanza nilihisi kama nipo ndotoni, nikakodoa macho lakini ndiyo ulikuwa ukweli.
Ilibidi niendelee kujimwagia maji kwa wingi na kadiri nilivyokuwa nazidi kujimwagia, ndiyo ule weusi ulivyokuwa ukizidi kupungua. Nilijipaka kwa mara ya pili na kujimwagia maji, bado uchafu mweusi ukawa unanitoka kwa wingi, nikawa najimwagia maji kwa wingi mpaka ulipoisha kabisa.
“Ina maana mimi ndiyo nilikuwa mchafu kiasi hiki? Halafu huu ni uchafu gani unakuwa mweusi kiasi hiki?” nilijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu. Wakati naendelea kuoga, nilisikia mlango ukigongwa, ukafuatiwa na sauti ya baba.
Iweje baba anifuate bafuni? Alikuwa anataka kufanya nini? Nikiwa bado najiuliza maswali, nilisikia tena sauti ya baba akinilazimisha nifungue mlango. Ikabidi nifungue kidogo na kumchungulia.
“Umetumia hiyo dawa?”
“Ndiyo.”
“Umeona nini?”
“Maji meusi kama ya mkaa yalikuwa yananitoka.”
“Safi, sasa vaa hii,” alisema baba huku akinyoosha mkono na kupenyeza kitambaa cheupe kupitia ule upenyo mdogo niliouacha. Akanisisitiza kwamba nisiziguse kabisa nguo zangu, nijifunge na yeye ananisubiri nje.
Nilirudisha mlango na kuufunga vizuri, nikawa nakitazama kile kitambaa alichonipa. Japokuwa sikuwa mzoefu wa shughuli za mazishi kiasi hicho, niliweza kukitambua vizuri kitambaa hicho kwamba kilikuwa ni sanda. Ninavyofahamu mimi, sanda huvalishwa maiti, sasa baba alikuwa na maana gani kuniambia nivae sanda?
Sikupata majibu. Nikawa naendelea kuishangaa sanda hiyo huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida. Nikiwa bado katika hali ile, nilisikia baba akigonga tena mlango kwa nguvu, akaniambia ananisubiri.
Ilibidi niivae harakaharaka, kisha nikafungua mlango. Baba alinitazama kuanzia juu hadi chini, akanirekebisha sehemu ambazo sikuwa nimejifunga vizuri, akatoa kipande kingine na kunifunga kichwani, akanisogelea sikioni na kuniambia:
“Upumbavu uliofanya ndiyo uliotufikisha hapa tulipo. Lazima ufanye kila kinachowezekana kuokoa maisha ya Rahma. Kwa hiyo, utalazimika kufanya kile nitakachokwambia bila kuhoji chochote, ukikosea masharti Rahma atakufa na wewe ndiyo utakuwa umemuua, hutakiwi kuzungumza chochote mpaka tutakapomaliza hii kazi,” alisema baba kwa sauti isiyokuwa na masihara hata kidogo.
Nilizidi kutetemeka, yaani mimi ndiyo niwe nimemuua Rahma? Kwa lipi? Hata hivyo, kwa kuwa ndani ya moyo wangu, licha ya yote yaliyotokea nilishatokea kumpenda mno Rahma, nilichojiapiza ni kwamba nitafanya kila kinachowezekana kuhakikisha naokoa maisha yake.
“Nifuate,” alisema baba huku akigeuka, akawa anatembea kwa hatua ndefundefu, alipofika kwenye mlango wa chumba cha Rahma, aliniambia nigeuke na kuupa mlango mgongo.
“Utaingia kinyumenyume mpaka ndani,” alisema baba, bado kidogo nimuitikie ‘sawa’ lakini nikakumbuka alichoniambia kwamba sitakiwi kuzungumza chochote. Alitangulia, akafungua mlango, nikamfuata kinyumenyume kama alivyonielekeza.
“Chumba kizima kilikuwa kimefukizwa ubani wenye harufu kali, alinipa ishara kwamba niendelee kutembea kinyumenyume mpaka aliponipa ishara kwamba nisimame, nikageuka na kutazama pale kitandani. Rahma alikuwa amelala, damu nyingi zikiendelea kumtoka na kulowanisha kitanda kizima.
Hakuwa na nguo yoyote mwilini zaidi ya kipande cha sanda alichokuwa amefunikwa kuanzia juu kidogo ya mapaja mpaka kifuani ambacho nacho kilikuwa na damudamu.
Baba akanitazama usoni, na mimi nikamtazama nikiwa na shauku kubwa ya kusikia kile atakachoniambia. Nilikuwa tayari kwa chochote ilimradi Rahma apone.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
THE GRAVES OF THE INNOCENTS (MAKABURI YA WASIO NA HATIA)- 21
ILIPOISHIA:
Hakuwa na nguo yoyote mwilini zaidi ya kipande cha sanda alichokuwa amefunikwa kuanzia juu kidogo ya mapaja mpaka kifuani ambacho nacho kilikuwa na damudamu. Baba akanitazama usoni, na mimi nikamtazama nikiwa na shauku kubwa ya kusikia kile atakachoniambia. Nilikuwa tayari kwa chochote ilimradi Rahma apone.
SASA ENDELEA…

“Mlichokifanya mkidhani ni siri yenu ndicho unachotakiwa kukifanya hapa,” alisema baba huku akigeuka na kuanza kutoka. Ilibidi nimshike mkono na kumvuta, sikuwahi kumfanyia baba hivyo hata siku moja lakini siku hiyo nilijikuta tu nikifanya hivyo.
“Baba!”
“Ambacho huelewi ni nini? Kama unataka apone fanya nilichokwambia na wakati wa tendo hakikisha hiyo sanda huivui,” alisema baba kisha akatingisha kichwa kuonesha kwamba niendelee, akanifinjia kijicho na kuachia tabasamu hafifu. Nilijikuta nikiogopa pengine kuliko kipindi chochote maishani mwangu.
Yaani mtu anaumwa kiasi kile, yupo kwenye hatua za mwisho za kukata roho, halafu eti naambiwa nifanye naye mapenzi, tena mwili wake ukiwa umelowa damu na mimi nikiwa nimevalishwa sanda! Moyo wangu ulipigwa na ganzi.
“Nakupenda Rahma na sinba cha kufanya zaidi ya kukusaidia, namuomba Mungu anisamehe na akusamehe pia na wewe,” nilisema huku machozi yakinilengalenga. Hali aliyokuwa nayo Rahma pale kitandani ilikuwa ya kuhuzunisha mno, nikaamua kupiga moyo konde na kuivaa roho ya kinyama.
Ilikuwa ni lazima niivae roho ya kinyama kwa sababu vinginevyo ningemuonea huruma Rahma kutokana na hali aliyokuwa nayo na pengine huruma yangu ndiyo ingekuwa tiketi yake ya kuendelea kuzimu.
Niliifunua ile sanda kwa mbele na kuacha uwazi, nikafumba macho na kuanza kuvuta hisia za jinsi mimi na Rahma tulivyokuwa tukiogelea kwenye dimbwi la mahaba, kwa mbali hisia zikaanza kunijia. Sikutaka kufumbua macho kabisa, niliendelea kufumba macho, nikapapasa na kupanda juu ya kile kitanda, mapigo ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida.
Nilipiga magoti na kumuweka rahma katikati yangu, nikakisogeza kile kitambaa cha sanda pembeni, nikaendelea kuvuta hisia huku machozi mengi yakinitoka na muda mfupi baadaye, tayari nilikuwa nikiogelea kwenye dimbwi la damu. Niliendelea kujikaza kisabuni, nikawa napiga mbizi hivyohivyo huku nikiendelea kulia.
Katika hali ambayo sikuitegemea, nilishtuka baada ya Rahma kuzinduka na kunikamata mikono yangu kwa nguvu, ikabidi nifumbue macho, nikamuona amefumbua macho yake huku akijiuma midomo kama aliyekuwa akitaka kuzungumza kitu.
‘Ongeza spidi, dawa inakaribia kufanya kazi,” nilisikia sauti ya baba, sijjui hata ilitokea wapi kwani chumba kilikuwa kimefungwa na hata pazia lilikuwa limefunikwa. Nilijisikia aibu sana lakini sikuwa na cha kufanya, nilizidisha kasi ya kile nilichokuwa nakifanya, nikashangaa Rahma akiniachia mikono na kunikumbatia kifuani huku akianza kuangua kilio.
Sikujali damu zilizokuwa zimeulowanisha karibu mwili wake wote na pale kitandani, niliendelea kufanya kile nilichoagizwa na ghafla, nilimuona Rahma akianza kukakamaa mwili wake, nikazidi kuongeza kasi.
“Kuna kitu kitamtoka mdomoni, hakikisha unakikamata,” alisema baba, nikashtuka maana kauli yake ilimaanisha hicho kitakachomtoka kitakuwa na uhai, sasa tangu lini mtu akatoa kiumbe chenye uhai kutoka mdomoni?
Ghafla rahma alifumbua mdomo huku mwili wake wote ukiwa umekakamaa, nikashtukia kiumbe cha ajabu kama panya mweusi lakini asiye na manyoya mwilini akichungulia kutoka mdomoni, nilishtuka mno kiasi cha kunifanya nishindwe kuendelea kufanya kile nilichokuwa.
Ghafla kile kiumbe kiliruka kutoka mdomoni na kuangukia juu ya kitanda, nikasikia sauti ya baba akinisisitiza kwamba lazima nihakikishe nakikamata. Ilikuwa panya siyo panya, chura siyo chura yaani hata sijui nikielezeeje maana kichwa na kiwiliwili kilikuwa kama panya lakini hakuwa na manyoya wala mkia na hata kutembea kwake hakikuwa akikimbia kama panya bali kilikuwa kikiruka kama chura.
Nilijikuta nikipiga moyo konde, moyo wa kijasiri ukanivaa, nikaruka kutoka pale kitandani mpaka chini, nikakirukia kile kiumbe na kufanikiwa kukidaka kwenye mikono yangu lakini cha ajabu, kilipasukia mikononi mwangu, nikashtukia nimeshika mabonge ya damu.
“Safi sana!” baba alisema huku akiingia akiwa ameongozana na baba yake Rahma ambaye naye alianza kunipongeza, wakawa wananipigia makofi. Bado nilijihisi kama nipo ndotoni, sikuelewa kile kiumbe kimepotelea wapi tena na kuniacha na mabonge ya damu mikononi, nikawa natetemeka kuliko kawaida.
“Harakaharaka baba alitoa kitambaa cheupe, akanifuta yale mabonge ya damu na kukiweka kile kitambaa kwenye mfuko mweusi, akatoa wembe, akanichanja kwenye paji la uso, eneo nywele zinapoanzia na kutoa dawa kwenye kichupa, akanipaka na kuisugua kwa nguvu. Dawa ilikuwa ikiuma mno, akarudia kunipongeza kisha akaniambia kazi imekwisha, nimsaidie rahma kumsafisha na kusaficha chumba chote, wakatoka tena huku wote wakionesha kuwa na furaha kubwa mioyoni mwao.
“Togo!”
“Naam Rahma!”
“Nini kimetokea?” alisema Rahma huku akiinuka kitandani, akawa anashangaa kila kitu.
“Ni stori ndefu, naomba twende kwanza ukaoge,” nilimwambia, harakaharaka nikamuona akiinuka na kukimbilia khanga yake, akajifunga huku akionekana kunionea aibu. Hakuwa Rahma yule ambaye muda mfupi uliopita alikuwa akikaribia kukata roho, alishabadilika na kuchangamka utafikiri hakuna kilichotokea.
Baada ya kujifunga khanga, alisogea kwenye dressing table na kujitazama, nikamuona jinsi alivyoshtuka.
“Mungu wangu, mbona nimelowa damu hivi? Halafu mbona na wewe umelowa damu? Kwani nini kimetokea?” alihoji Rahma, ikabidi nivae tabasamu la uongo ili kumuondolea hofu moyoni. Nakumbuka baba amewahi kunifundisha kwamba njia nzuri ya kuishi na wanawake, ni pale wanapoonekana kulichukulia tatizo kwa ukubwa, wewe lirahisishe.
Hatua hiyo kweli ilifanikiwa sana, kwani licha ya mshtuko aliokuwa nao, aliponiona mimi nikitabasamu, Rahma aliamini kwamba kilichotokea hakikuwa tatizo kubwa, nikamshika mkono na kutaka kutoka naye tuelekee bafuni.
“Hiki nini ulichovaa?” aliniuliza, nikamtazama usoni na kumuomba anipe khanga nyingine na mimi nijifunge.
“Hujanijibu lakini.”
“Mbona una haraka ya kujua mambo yote mara moja? Nimekwambia nitakueleza kila kitu, kuwa mpole.”
“Halafu mimi si nilitaka kujiua?” alisema akiwa ni kama ameanza kurudiwa na fahamu zake, nikachukua khanga mwenyewe na kumshika mkono kumpeleka bafuni maana niliona akili yake bado ina mawenge.
“Utumie ile sabuni niliyokuwa kuogea wewe na yeye,” baba alisema, wote tukageuka na kuwatazama, kumbe walikuwa wakituangalia, wakiwa ni kama hawaamini kama Rahma yule aliyekuwa akikaribia kunusa umauti, ndiyo yule aliyekuwa akitembea mwenyewe.
“Nilifungua mlango wa bafuni, nikamtanguliza Rahma, nikamuona akitaka kujifungia mlango lakini nilisukuma na kuingia.
“Wanatuona, unafikiri baba na mama watatuelewaje?”
“Wao ndiyo wamenipa kazi ya kukusaidia kwa hiyo usiwe na wasiwasi,” nilisema huku nikifunga mlango kwa ndani, rahma akawa ananitazama kwa macho yenye maswali mengi bila majibu.
“Unatakiwa kuoga kwa kutumia hii sabuni,” nilisema huku nikimpa kile kijiwe cha ajabu nilichopewa an baba, ambacho nilikiacha humohumo bafuni, Rahma akawa bado anashangaashangaa, ilibidi nimdogeze kwenye bomba, nikafungulia maji, yakaanza kumwagikia ambapo alionekana kama kuanza kuzinduka.
“Kile nilichokiona mle bafuni na kuhisi kama naoga damu, ndicho kilichokuwa kinatokea muda huo kwani maji yaliyokuwa yakichuruzika kutoka kwenye mwili wa Rahma, yalikuwa damu tupu, nikavuta kumbukumbu na kuhisi labda kile kilichonitokea kilikuwa na uhusiano na tukio hilo.
Nilijifungua ile sanda, na mimi nikabaki kama Rahma, nikasogea pale kwenye bomba, maji yakawa yanatumwagikia, chini damu zikawa zinaendelea kutiririka kuelekea kwenye bomba la kutolea maji machafu. Nilimshika mikono Rahma, nikamvutia kwenye kifua changu, tukawa tunatazamana huku maji yakiendelea kutumwagikia, nikajikuta nikitamani kumbusu mdomoni.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocents (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 22
ILIPOISHIA:
Nilijifungua ile sanda, na mimi nikabaki kama Rahma, nikasogea pale kwenye bomba, maji yakawa yanatumwagikia, chini damu zikawa zinaendelea kutiririka kuelekea kwenye bomba la kutolea maji machafu. Nilimshika mikono Rahma, nikamvutia kwenye kifua changu, tukawa tunatazamana huku maji yakiendelea kutumwagikia, nikajikuta nikitamani kumbusu mdomoni.
SASA ENDELEA...

“Mbona najisikia hivi?”
“Unajisikiaje?”
“Hata sijui nisemeje lakini najisikia raha ya ajabu ndani ya moyo wangu,” alisema Rahma na kabla hata sijafanya kile nilichokuwa nakitamani, yeye alinianza akanibusu kwa midomo yake milaini huku akinikumbatia kwa nguvu, na mimi nikamuonesha ushirikiano.
“Kwa nini ulitaka kujiua?” nilimuuliza, akafumbua macho yake ambayo kwa muda wote alikuwa ameyafumba, akanitazama usoni bila kusema chochote, akajiinamia. Niligundua kwamba hakulipenda swali hilo, nikaamua kubadilisha mada lakini bado hakuzungumza chochote.
Nilimsaidia kumsafisha mwili wake wote mpaka damu zote zikaisha kwenye miili yetu, nikafunga maji na kumpa khanga yake lakini aliikataa kwa sababu nayo ilikuwa na damu.
“Vaa tu kwanza tutaoga tena kwa mara nyingine, inabidi tukafanye usafi chumbani kwako,” nilimwambia, akakubali. Tulichukua ndoo za maji na vifaa vya kufanyia usafi, tukaelekea chumbani kwake ambako kila sehemu ilikuwa imechafuka kwa damu.
Tukaanza kufanya usafi lakini bado Rahma hakuzungumza chochote, muda wote alikuwa kimya kabisa na pale alipohitaji kunielekeza jambo, alikuwa akitumia zaidi ishara.
“Mbona umebadilika ghafla? Nisamehe kama kuna kitu nimekukwaza,” nilimwambia, akanitazama tena.
“Kwani nini kilitokea?”
“Wewe unakumbuka nini?”
“Nakumbuka niliamua kunywa sumu ili nife.”
“Kwa nini?”
“Kwa sababu nakupenda.”
“Sasa ukimpenda mtu ndiyo ujiue?”
“Kwa sababu walituambia kwamba sisi ni ndugu,” alisema Rahma huku akiacha kila alichokuwa anakifanya, machozi yakaanza kumtoka.
“Kumbe walisema vile kututishia kwamba tusije tukaanza kufanya mapenzi lakini siyo kweli, hatuna undugu ila baba yangu na baba yako ni marafiki tangu wakiwa vijana wadogo kwa hiyo ni kama ndugu tu,” nilimwambia.
Hata mimi maneno hayo niliwasikia mama na mama yake Rahma wakiongea kule hospitalini, wakilaumiana kwa maneno waliyotuambia ambayo ndiyo yaliyosababisha Rahma achukue uamuzi wa kuyakatiza maisha yake.
Nilipomueleza maneno hayo, alinitolea macho akiwa ni kama haamini, akanisogelea na kunishika mkono, akawa ananitingisha kwa nguvu akitaka nimhakikishie kwamba ni kweli. Nikarudia tena kumueleza vilevile, jambo lililosababisha anikumbatie na kuanza upya kulia.
“Nisamehe! Niliona bora nife tu kuliko kuishi bila wewe, nimejikuta nikikupenda mno mwenzako, utafikiri tulijuana miaka mingi nyuma,” alisema huku akiendelea kulia.
“Na hizi damu imekuwaje?” aliniuliza, kama nilivyokuwa nikimjibu mwanzo, nikamwambia asiwe na haraka atajua kila kitu kilichotokea. Alinibusu tena, tukaendelea kufanya usafi. Ilibidi nguo zote zilizokuwa zimechafuka kwa damu, tuzikusanye kwa ajili ya kwenda kuzifua, tulitoa kuanzia mashuka mpaka foronya.
Tukasaidiana kupiga deki kwa kutumia sabuni maalum, chumba chote kikawa kisafi kabisa. Baada ya kumaliza, tulibeba furushi la nguo chafu kwa ajili ya kwenda kuzifua kule bafuni lakini wakati tukitoka, baba alikuja kutuambia kwamba nguo hizo hazikutakiwa kwenda kufuliwa bali inabidi zikachomwe moto.
Itabidi mvue hata hizo mlizovaa, zote hizi ni za kuchoma moto, tena inabidi nyie wenyewe kwa mikono yenu. Tulifanya kama baba alivyotuelekeza na muda mfupi baadaye, tulikuwa tumemaliza kila kitu, ikabidi tukaoge tena na safari hii, kila mtu alienda kuoga peke yake. Rahma alinipa fulana yake moja niivae kwani sikuwa na nguo zozote za maana nilizobeba kutoka kule kijijini.
“Baba yako amenipa hii pesa anasema muende sehemu yoyote nzuri mkatembee na Togo, hata kama ni ‘beach’ ila msichelewe kurudi,” alisema mama yake Rahma huku akitoa noti mbili nyekundu na kumpa Rahma.
“Lakini mama, naomba unisamehe!”
“Usijali, tumeshakusamehe Rahma, tunamshukuru Mungu kwa kukuokoa kutoka kwenye bonde la mauti. Jioni mtapenda kula nini?” alisema mama yake Rahma kwa upole wa ajabu.
Hata mimi nilishangaa sana, nilitegemea kwamba baada ya kila kitu kutulia, lazima mimi na Rahma tulikuwa na kesi ya kujibu lakini mambo yakawa tofauti kabisa.
“Nataka tule pilau, si ndiyo Togo,” alijibu Rahma, na mimi nikatingisha tu kichwa. Kule kijijini kwetu, pilau lilikuwa likipikwa sikukuu tu, tena Krismasi, nikajikuta nikijilamba midomo yangu kwa uchu. Baada ya hapo, mama yake Rahma alitoka na kututakia matembezi mema.
“Twende wapi kutembea,” alisema Rahma huku akinikumbatia na kunibusu, nikamwambia mimi sijui sehemu yoyote kwa hiyo yeye ndiyo aniongoze, akacheka sana na kunipiga mgongoni. Yaani kama kuna mtu alimuona Rahma saa chache zilizopitahali aliyokuwa nayo, asingeamini kwamba ndiye yeye.
Harakaharaka alianza kujiandaa, akaenda tena kuoga na kurudi chumbani kwake, mimi nikawa nimekaa kwenye kiti cha pembeni. Niweke wazi kwamba safari hii sikuwa naogopa chochote ikwa sababu baba na baba yake Rahma ndiyo walioniruhusu kuwa karibu na Rahma wakihofia kwamba kama wataendelea ukali juu yetu, anaweza kujidhuru tena.
Na waliniambia natakiwa nisimuache peke yake kule chumbani kwake kwa hiyo nilikuwepo pale kihalali kabisa ingawa waliniambia kwamba sitakiwi kufanya chochote naye kwa sababu kulikuwa na mambo yasiyo ya kawaida wameyabaini na chanzo cha yote ilikuwa ni mimi kufanya naye mapenzi.
“Hebu niambie Togo, unanipenda kweli kama mimi ninavyokupenda?”
“Nakupenda tena sana,” nilimwambia, nikamuona akiachia tabasamu pana, akanisogelea pale nilipokuwa nimekaa, akanishika mkono na kunivuta ili nisimame, nikatii, alinivutia kifuani kwake na kunibusu kimahaba, na mimi nikafanya kama yeye.
“Kama kweli unanipenda nataka unioe,” alisema Rahma kwa sauti ya kunong’ona, akanibusu tena.
“Usijali kabisa, kwako nipo tayari kwa chochote,” nilimwambia. Kiukweli nilimjibu tu kwa lengo la kumfurahisha maana niliambiwa sitakiwi kumuudhi kwa chochote. Baada ya hapo, aliniachia na kwenda kufungua kabati, akaniambia nimsaidie kuchagua nguo ya kuvaa.
Kwangu ulikuwa mtihani mkubwa sana kwani wakati mwingine alikuwa akiiachia ile khanga aliyotoka nayo bafuni na kuufanya mwili wake wenye mvuto wa kipekee ubaki wazi, nikawa na kazi ya ziada. Baadaye aliipata nguo aliyoitaka mwenyewe, akavaa gauni zuri lililompendeza na kujitanda ushungi.
Kwenye suala la mavazi, Rahma alikuwa akijitahidi sana, alikuwa akivaa mavazi ya heshima tofauti na wasichana wengi wa mjini. Mimi sikuwa na cha kubadilisha, vilevile nilivyokuwa nimevaa, tulitoka, nikataka kuvaa mabuti yangu lakini akaniambia kuna raba nzuri huwa anafanyia mazoezi, akaingia tena ndani na kutoka nazo.
Zilinipendeza vizuri, nikawa nachekacheka tu, tulienda sebuleni na kuaga, ndugu zangu waliokuwa wamenogewa na tivii, walinitazama kwa macho ya wivu, tukatoka mpaka nje ambapo Rahma alipunga mkono upande kulipokuwa kumepaki Bajaj, ikaja moja, tukaingia na kukaa.
“Tupeleke Coco Beach, kule wanakouza mihogo,” alisema Rahma, safari ikaanza lakini mita chache mbele, nilishtuka baada ya kusikia mtu akiliita jina langu kwa nguvu, tena sauti yenyewe ilikuwa ya kike, ilibidi Rahma amwambie dereva asimame, tukageuka nyuma kutazama ni nani aliyekuwa ananiita kwa sababu mimi nilikuwa mgeni na hakuna mtu yeyote aliyekuwa akilifahamu jina langu zaidi ya wale tuliokuwa tukiishi pamoja.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 23
ILIPOISHIA:
“Tupeleke Coco Beach, kule wanakouza mihogo,” alisema Rahma, safari ikaanza lakini mita chache mbele, nilishtuka baada ya kusikia mtu akiliita jina langu kwa nguvu, tena sauti yenyewe ilikuwa ya kike, ilibidi Rahma amwambie dereva asimame, tukageuka nyuma kutazama ni nani aliyekuwa ananiita kwa sababu mimi nilikuwa mgeni na hakuna mtu yeyote aliyekuwa akilifahamu jina langu zaidi ya wale tuliokuwa tukiishi pamoja.
SASA ENDELEA...

Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kushuka kwenye Bajaj, Rahma naye akafuatia, nikawa na shauku kubwa ya kumjua aliyeniita kwa bashasha kiasi kile.
“Togo, ni wewe! Ooh siamini macho yangu, sikujua kama nitakupata!” alikuwa ni yule msichana ambaye tulikaa naye siti moja kwenye basi wakati tukisafiri kutoka Mbeya kuja Dar es Salaam. Alikuwa amevaa sketi fupi na nyepesi ambayo ilimfanya maungo yake yajichore vizuri.
Juu alikuwa amevaa blauzi ndogo ambayo iliacha sehemu kubwa ya kifua chake wazi, akawa anatembea kwa maringo akinifuata huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake. Kiukweli na mimi nilishindwa kujizuia kutabasamu, hasa nilipokumbuka wakati mzuri tuliokuwa nao kwenye basi mpaka tulipoachana Ubungo.
“Jamani mbona ile simu niliyokupa hupatikani hewani? Nimehangaika sana kwa kweli,” alisema akiwa tayari ameshanifikia, kufumba na kufumbua nikashtukia amenikumbatia kimahaba na kunibusu mdomoni.
“Dada mambo!” alimsalimia Rahma ambaye alikuwa amesimama pembeni yake, akiwa ni kama haamini kile alichokuwa anakiona. Ilibidi nianze kuvungavunga pale maana kila kitu kilikuwa kikitokea kwa kasi kubwa mno.
“Umepajuaje hapa?”
“Ilibidi nimtafute dereva teksi aliyewabeba wakati mnatoka pale Ubungo, kwa bahati nzuri akawa anakumbuka sehemu alipowaleta, ndiyo amenileta, yule pale kwenye gari,” alisema huku akigeuka nyuma na kuonesha upande teksi alityokuja nayo ilipokuwa imepaki.
“Mnaenda wapi kwani?”
“Tunaenda bichi,” nilimjibu harakaharaka huku nikigeuka na kumtazama Rahma usoni ambaye bado alionesha kutoelewa kinachoendelea.
“Kwa nini tusipande kwenye ile teksi, mi nimeshalipa.”
“Hapana, ahsante,” Rahma alidakia na kunishika mkono, naona uzalendo ulishafika kikomo, akatangulia kuingia kwenye Bajaj na kunivuta mkono na mimi niingie.
‘Kwani mnaenda bichi gani?” aliuliza huku akionesha bado kuwa na shauku kubwa ya kuzungumza na mimi.
Sikuwa nakujua Coco lakini kwa sababu nilimsikia Rahma akimueleza dereva wa Bajaj kuwa atupeleke wanakouza mihogo, na mimi nilijikuta nikijibu hivyohivyo.
“Coco wanakouza mihogo,” baada ya kumjibu hivyo, nilimuona haraka akigeuka na kurudi kwenye teksi aliyokuja nayo. Watu kadhaa waliokuwa eneo lile, waliacha kila walichokuwa wanakifanya na kugbaki wakishangaa muvi iliyokuwa inaendelea.
“Togo, yule ni nani?”
“Mh! Jina lake simjui lakini tulikaa naye siti moja kwenye basi wakati tunakuja.”
“Muongo! Yaani mtu uliyekaa naye siti moja tu ndiyo akuzoee kiasi hiki? Angalia amekupaka lipstiki yake mdomoni,” alisema Rahma huku akionesha kuanza kulengwalengwa na machozi.
“Kweli tena, hata ukimuuliza atakwambia hivyohivyo, hata hatujuani vizuri,” nilisema huku nikijifuta mdomoni, kweli kulikuwa na mabaki ya lipstiki aliyoniachia aliponibusu mdomoni.
“Yeye amenizoea tu lakini hakuna chochote kati yetu.”
‘Mbona nimemsikia akisema alikupa simu? Yaani inawezekanaje mtu akupe simu tu? Halafu umeona alivyovaa, kwa nje tu anaonekana changudoa, ka hiyo kumbe wewe unatembea na machangudoa? Si nakuuliza?” Rahma alizidi kunibana kwa maswali mengi. Sikuwahi kumsikia Rahma anavyozungumza akikasirika lakini siku hiyo alikasirika kwelikweli, akawa anaendelea kufoka na muda mfupi baadaye alianza kulia.
Ilibidi nianze kazi ya kumbembeleza, nikamkumbatia kifuani kwangu na kumbusu sehemu mbalimbali za mwili wake, kidogo nikamuona akianza kutulia, na yeye akanikumbatia kwa nguvu kifuani huku Bajaj ikizidi kukata mitaa.
“Halafu umemuelekeza mpaka sehemu tunapoenda, hujui anaweza kukufuata? Dereva nimebadilisha mawazo, hebu tupeleke Msasani Beach na siyo Coco tena, nitakuongeza hela,” alisema Rahma, dereva akatingisha kichwa kuonesha kwamba amemueleza.
“Unajua mimi nakupenda, kwa nini unanifanyia makusudi lakini?”
“Nisamehe Rahma, hayakuwa makusudio yangu, nimejikuta tu mambo ya ajabu yametokea, nisamehe,” niliendelea kumbembeleza na kumbusu, cha ajabu alitulia kabisa na hakusema neno lingine lolote mpaka tulipofika Msasani Beach. Sikuwa naijua mitaa lakini kiukweli nilifurahia sana mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Alimlipa dereva kisha tukashuka, tukawa tunatembea kuelekea baharini huku nikiwa na shauku kubwa ya kuiona bahari maana nilikua nikisikia tu. Nilitaka pia nikaonje maji yake nihakikishe kama kweli yana chumvi kama ambavyo watu huwa wanasema.
Tulipita sehemu ambapo kuna viti vya kupumzikia, tukawaona watu mbalimbali wakiwa wanapunga upepo, wengine wakila na kunywa. Tulipitiliza mpaka baharini kama nilivyomuomba Rahma na kitu cha kwanza nilichokifanya, ilikuwa ni kunawa usoni na kichwani kwa kutumia maji ya baharini.
Niliwahi kusikia pia kwamba maji ya baharini huondoa mikosi, nikanawa kwa maji mengi na hapo ndipo nilipogundua kuwa ni kweli maji hayo yalikuwa na chumvi, tena nyingi kiasi kwamba huwezi hata kuyanywa. Kiukweli nilifurahi sana kuiona bahari na kuyagusa maji ya bahari, nikawa najisikia kama nimetua kwenye ulimwengu mwingine tofauti.
Rahma muda wote alikuwa akicheka kwa furaha, hasa kwa jinsi nilivyokuwa ‘najitoa ufahamu’ na bahari. Nilifurahi kumuona akicheka mpaka kukaukia, akiwa amekaa kwenye mchanga, jirani na pale nilipokuwa.
Baada ya kucheza sana kwenye maji, nilirudi pale alipokuwa amekaa Rahma, nikakaa pembeni yake na kumuegamia, akanibusu kwenye paji la uso na kuniambia kuwa nimemfurahisha sana. Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale lakini mra kwa mara Rahma alikuwa akipenda zaidi tuzungumze mambo ya kikubwa.
Alikuwa anataka kusikia nina mal;engo gani naye siku za usoni, alitaka kujua napenda kuwa na familia ya watoto wangapi au nitakuwa baba wa aina gani kwa wanangu. Aliniuliza pia kama nina mpango wa kujiendelea kwenye fani yoyote ili mwisho na mimi nije kuwa na uwezo wa kutunza familia.
Kwangu mazungumzo hayo si tu kwamba yalikuwa mageni kwangu, lakini pia mambo mengi sikuwahi kuyawaza. Nadhani hili ndiyo tatizo linalowakumba watu wengi wanaopishana umri wa wenzi wao, hasa kama mwanamke akiwa mkubwa. Kwangu Rahma alikuwa mkubwa, kama nilivyowahi kusema siku za nyuma, alikuwa akilingana na dada yetu mkubwa, Sabina.
Hata mazungumzo yake, alikuwa ni mdada anayejiheshimu, mwenye busara na anayewaza mbali, alionesha kweli kwamba ameanza kukomaa kiakili. Hali ilikuwa tofauti kwangu kwa sababu hata mwanamke mwenyewe, yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kwangu, kwa maana sikuwahi kuwa na mpenzi wala kushiriki sanaa za kikubwa kabla ya kukutana naye.
Sikuwa nikiwaza chochote kuhusu familia, au mke au maisha ya ndoa, nadhani ni kwa sababu ya umri. Hata hivyo, kwa sababu Mungu alinipa uwezo wa kumsoma mtu haraka, sikutaka kumkasirisha mawazo Rahma, kwa hiyo ikabidi na mimi nianze kuzungumza kama mtu mzima flani hivi, tukawa tunaenda sawa.
“Mh, hebu naomba simu yangu mara moja, sijaigusa tangu tumefika,” alisema rahma, nikamsogezea pochi yake ndogo ambapo alifungua na kutoa simu.
“Mh! Baba amepiga sana, sijui alikuwa anasemaje,” alisema Rahma huku akiendelea kubonyezabonyeza simu yake, mara akanigeukia na kunitazama usoni.
“Kulikuwa na ujumbe wako hapa lakini tumechelewa sana, hata sijui itakuwaje,” alisema, hali iliyonifanya na mimi nishtuke kwa sababu ya jinsi yeye mwenyewe alivyoonekana kushtuka.
“Kuna nini kwani?” nilimuuliza, akaniambia baba alikuwa amempigia simu kwa lengo la kutaka kuzungumza na mimi na kubwa alilokuwa anataka kuniambia ni kwamba wamesahau kuniambia kwamba nikienda ufukweni nisiguse kabisa maji ya bahari. Nilishangazwa sana na maelezo hayo, nikajiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
Tayari nilishayagusa na siyo kuyagusa tu bali niliyachezea vya kutosha na kama Rahma asingenizuia au kama siyo woga wa bahari, nilitaka hata niogelee. Tukiwa bado tunashauriana cha kufanya, mara simu ya Rahma ilianza tena kuita, harakaharaka akaipokea.
“Samahani simu ilikuwa kwenye mkoba baba,” nilimsikia Rahma akijitetea, bila shaka aliulizwa kwa nini hakupokea simu.
“Eeeh niko naye,” alijibu tena, nikajua lazima ameulizwa kama yupo na mimi, nikamuona akinipa simu, akaniambia baba anataka kuzungumza na mimi.
“Haloo Togo.”
“Haloo baba.”
“Hebu ongea na mzee,” alisema baba yake Rahma akimaanisha nizungumze na baba, akampa simu. Alimpa simu baba na swali lake la kwanza lilikuwa ni kama nimeshayagusa maji ya bahari. Ilibidi nimjibu kwamba nimeshayagusa kwani sikuwa najua chochote.
“Mungu wangu, kuna mtu anaenda kufa,” alisema baba kisha akakata simu, nikashtushwa mno na kauli yake hiyo. Sikuelewa nini kimetokea au kosa langu lilikuwa ni nini.
“Mbona watu wanachezea maji, wengine wanaogelea bila tatizo, mimi kosa langu nini,” nilijikuta nikijisemea, Rahma akanishika na kunituliza pale chini kwani nilishaanza kuchanganyikiwa kutokana na kile alichokisema baba.
“Amesemaje kwani?” aliniuliza Rahma, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama usoni, sikutaka kumwambia ukweli wa nilichoambiwa na baba, nikamdanganya kwamba baba amenifokea sana kwa sababu nimegusa maji hayo. Aliupokea uongo wangu, akanikumbatia na kunipa pole, nikatulia kifuani kwake.
Ghafla tulishtushwa na kishindo kikubwa ambacho hata sikuelewa kimetokea wapi.
Je, nini kimetokea? Ni kishindo cha nini? Usikose next issue.
 
The Graves of The Innocent (Makaburi ya Wasio na Hatia)- 24
ILIPOISHIA:
Ghafla tulishtushwa na kishindo kikubwa ambacho hata sikuelewa kimetokea wapi. Watu walianza kupiga kelele kwa nguvu huku wale waliokuwa baharini wakianza kukimbia kuokoa maisha yangu. Ilibidi tugeuke kutazama kule kishindo kile kilichotokea ambako bado zile kelele zilikuwa zikitokea.
SASA ENDELEA...

Lahaula! Samaki mkubwa ambaye sikuwahi kumuona ingawa baadaye nilisikia kwamba anaitwa papa, akiwa na meno makali yaliyochongoka, aliipiga kikumbo boti ndogo ya uvuvi iliyokuwa eneo hilo na kusababisha kishindo kikubwa, wavuvi waliokuwa ndani ya boti hiyo wote wakarukia majini na kuanza kuhaha kuokoa maisha yao.
Nikiwa bado namshangaa samaki yule ambaye alijirusha kwa nguvu kutoka majini na sasa akawa anaonekana mzimamzima, wote tulishtukia akimfuata mmoja kati ya wale wavuvi, akafunua mdomo wake uliokuwa na meno makali kama msumeno, akamkamata kiunoni, kufumba na kufumbua akaubana mdomo wake kwa nguvu, yule mvuvi akagawanyika vipande viwili.
Sijui nilipata wapi ujasiri, nilijikuta nikiinuka kwa kasi kubwa pale tulipokuwa tumekaa na Rahma, akabaki anapiga kelele za kuniita huku akiniuliza nakwenda wapi na kufanya nini? Sikuelewa swali lake lilimaanisha nini kwa sababu kila kitu kilikuwa wazi, nilikuwa nakwenda kutoa msaada kwa wale wavuvi.
Nilikimbia mpaka eneo ambalo maji yalianza kunifika kiunoni, kwa kuwa nilikuwa na uzoefu wa kutosha wa kupiga mbizi, nilianza kuelekea eneo la tukio. Kadiri nilivyokuwa nazidi kusonge mbele ndivyo kelele zilivyokuwa zikizidi kuongezeka. Sikuwahi kudhani kwamba samaki ana sauti ya kutisha kiasi kile maana alikuwa akitoa milio ya ajabu.
Nikiwa naendelea kupiga mbizi, nilimshuhudia akikifuata kile kipande cha kichwa cha yule mvuvi, akaanza kukichanachana kwa meno yake makali, akararua minofu yote na kubakiza mifupa michache tu, akahamia kile kipande kingine cha kichwa, akakitafuna na kuacha kichwa tu. Nilijikuta nikipatwa na hofu ya ajabu, hakika sikuamini nilichokuwa nakiona.
Maji yote ya eneo lile yalibadilika rtangi na kuwa mekundu, mimi nikawa nazidi kupiga mbizi nikiwa hata sijui naenda kufanya nini maana uwezo wa kupambana na samaki yule kwenye maji, hakika sikuwa nao, nikasikia kelele za watu wakinizuia na kunitaka nirudi maana tayari wale wavuvi wengine walishapotea kwenye upeo wa macho yangu.
Ghafla nilihisi kama kuna kitu kimenishika kwenye mguu wangu wa kushoto na kuanza kunivutia chini, tayari nilishafika kwenye kina kirefu, nikatumia nguvu kubwa kujaribu kupambana na kile kitu kilichokuwa kimeninasa ambacho bado sikuwa najua ni nini, ghafla nikajikuta nikizama.
Nilipoibuka, nilikuwa nimemeza kiasi kikubwa cha maji ya chumvi na nikiri kwamba unaweza kuwa unajua sana kuogelea kwenye maji baridi lakini maji chumvi ni hatari sana maana yakikuingia puani au ukiyanywa, ile chumvi inakufanya uzidi kuwa kwenye hali mbaya.
Nilijaribu kupiga mbizi kwa nguvu lakini bado kile kitu kilikuwa kimenibana mguu na kuzidi kunivuta, nilitamani nigeuke niangalie ni nini lakini sikuweza kutokana na jinsi nilivyokuwa napambana na mawimbi makali. Nikajikuta nikizama tena na kunywa maji mengi zaidi ya mwanzo, nikaibuka na kuendelea kutapatapa, safari hii mwili ukiwa umeishiwa kabisa nguvu kiasi cha kuanza kuhisi giza nene machoni.
Sikuelewa tena kilichoendelea kwani giza nene lilinizingira usoni huku nikianza kuona picha za majinamizi ya kutisha.
***
“Nisaidieni jamani mchumba wangu anakufaaaa, msaada?” Rahma alipiga kelele kwa nguvu na kuwafanya watu wote waliokuwa ufukweni hapo, wakiwemo wavuvi waliokuwa wakivuta nyavu zao, kuacha kila walichokuwa wakikifanya na kukimbilia kule baharini kwenye kina kirefu.”
“Imekuwaje tena jamani?”
“Mh hata sijui nini kimetokea, hawa walikuwa wamekaa pale ufukweni na mwenzake, mara mwanaume akaanza kukimbilia baharini, tena akiwa na nguzo zake zote.”
“Mimi mwenyewe nimemuona, nikasema huyu jamaa kachanganyikiwa nini? Unaambiwa kakimbia mpaka kule, akaanza kupiga mbizi kwa kasi kubwa kama samaki, mara tunashangaa anaanza kutapatapa, mwisho maji yanamzidi anazama,” alisema mwanaume mmoja, shuhuda wa tukio lile.
“Binti kwani amepatwa na nini?”
“Nisaidie kwanza kumsaidia, mengine tutajua baadaye,” alijibu Rahma huku akilia na kurusharusha miguu kama amekanyaga siafu. Muda mfupi baadaye, wavuvi watatu tayari walikuwa wameshamfikia pale alipokuwa ambapo kwa sababu alishazama na kuibuka kwa mara ya tatu, ilibidi wazame chini kumtafuta.
Kwa bahati nzuri, walifanikiwa kumpata, wakaibuka naye na kupiga mbizi mpaka ufukweni kwenye mchanga ambapo watu wengi walikuwa tayari wameshakusanyika, zoezi la kumsaidia kurejesha pumzi zake likaanza ambapo wale wavuvi walianza kumkandamiza tumboni kwa nguvu.
***
“Kwani ilikuwaje Rahma?”
“Hata sijui baba, siwezi kuelezea maana naona ni zaidi ya maajabu,” nilisikia sauti za watu wakizungumza kwa mbali ambapo nilizitambau vyema sauti hizo kuwa ni Rahma na baba. Bado macho yangu nilikuwa nimeyafumba, nikihisi kila kiungo kwenye mwili wangu kikiwa kizito na kilichokosa nguvu kabisa.
Nilijaribu kufumbua macho mara kadhaa lakini nilikuwa nashindwa, nikawa nimelala tu lakini nikiwa na uwezo wa kusikia kila kilichokuwa kinaendelea.
“Tueleze ili angalau tupate mwanga maana mpaka sasa sote tupo gizani na wewe ndiye uliyekuwa naye kabla hajafikwa na haya matatizo.”
“Tulikuwa salama tu lakini baada ya ile simu mliyopiga ndiyo mambo yalipoharibika, kwa sababu mwanzo tulikuwa tumekaa kwenye mchanga baada ya kuwa Togo ameshacheza sana na maji ya bahari, tena akawa ananichekesha kwa kuniambia eti ukipia chakula hakuna haja ya kuweka chumvi.
“Muda mfupi baada ya kumaliza kuzungumza na simu, nilishangaa kusikia akiniambia kama nimesikia hicho kishindo kikubwa, nikawa nashangaa maana hakukuwa na kishindo chochote, mara akasimama huku akitazama baharini, akawa ni kama ameona kitu ambacho mimi hata sijui ni nini.
“Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilishangaa akianza kukimbilia baharini, alipofika kwenye maji mengi alipiga mbizi kwa kasi kubwa mpaka alipofika kwenye kina kirefu, mara akaanza kutapatapa mpaka akazama, wavuvi wakaenda kumuokoa akiwa hajitambui, tumbo likiwa limejaa maji,” nilimsikia Rahma akitoa ufafanuzi ambao ulinishangaza sana.
Nilijikuta nikipata nguvu za ghafla, nikafumbua macho na mimi nikitaka kutoa ufafanuzi wa kilichotokea. Kitendo cha mimi kufumbua tu macho, kiliwafanya wote waache kila walichokuwa wanakifanya, wakanisogelea na kuzunguka pale kitandani huku nikimsikia Rahma akimuita nesi.
Wakati wao wananishangaa na kuniuliza nilikuwa najisikiaje, mimi bado nilikuwa nikitafakari maelezo aliyoyatoa Rahma ambayo niliyasikia vyema kabisa. Nilishangaa kwa nini akwepeshe ukweli wa kilichotokea? Yaani alibadilisha maelezo kwa faida ya nani?
Kwani yeye hakumuona yule papa mkubwa aliyekuwa akimla mvuvi huku wenzake wakiponea kwenye tundu la sindano? Ina maana hakusikia kile kishindo cha samaki yule mkubwa anayetisha alipoipiga kikumbo kikubwa boti ile ya wavuvi? Kwa nini hawaambii kwamba nilikuwa naenda kuwaokoa wavuvi? Nilijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
Nilianza kuwatazama mmoja baada ya mwingine, kuanzia mama ambaye uso wake ulikuwa na huzuni kubwa, baba ambaye alionesha kuwa katika tafakuri nzito na ndugu zangu wote ambao walikuwa wamekodolea macho, kila mmoja akiwa na maswali mengi yasiyo na majibu.
Mara mlango wa wodi ulifunguliwa, watu wote wakageuka kutazama ni nani aliyekuwa akiingia kwa kasi kiasi kile.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom