Muziki: Siku ya Sayansi KF
Ni imani yangu kabisa, kila mtu ana imani yake FYI, kuwa leo uliianza wiki kwa hatua nzuri kabisa na usiku huu umeingia unajitafakarisha nini ukiendeleze na nini usikiendeleze maana kila mmoja anajijua hatua anazopitia kufanikisha kila anachoamini. Hivi ninaandika nini, maana hata mimi najikuta naandika tu bila hata kukusalimia Kapuku wewe mheshimika na kukuuliza wikend yako ilikuwaje.
Leo humu tumeanza na sayansi, asante sana anko mdogo
Lyon Lee na
makaveli10 kwa kutusayansisha yaani kutuonjesha ufahamu wa kisystematic unaojenga na kuorganize ufahamu katika hali ambayo unaweza kujaribisha (testability) na ukatabiri mambo makubwa. Heh, na
Transcend nimekutambua uwepo wako. Sisi wengine mlipokuwa mnaongelea masuala ya K na msuguano, hasa mimi nikatamani akili zangu nizipeleke napopenda lakini ndo muhali tena nilikuwa na kiongozi mmoja wa dini anayeamini mimi ni mtakatifu sana. Na alinishangaa nilipomwambia mimi sitapenda kwenda mbinguni ikiwa marafiki zangu wa Makapuku hawatakuwepo. Na kwa vile nilikuwa nimepiga mtungi kidogo nikamwambia ' I would rather not to go to heaven if nobody is there but me. I want to go because my great Makapuku members will be there'. Sina hakika kama aligundua sikuwa sober.
Muziki sasa, jana hamkuniona humu, rafiki wa anko kateuliwa kuwa waziri, sasa ndo anko akanipa mwaliko wake wa kujipongeza hata kabla hajatawazwa, well, sio kutawazwa unakokujua ukiwa umeshiba kiporo, namaananisha uapisho uliofanyika leo. Burudika na gitaa na sauti ya chuma ya mwanamama ninayemuhusudu bila husuda