Muziki: Uaminifu Usiuchulie Poa
U khali gani Kapuku mheshimika, mimi niko poa na kama unavyojua ratiba yangu ya Jumamosi ni kwenda kupasha viungo na maveterani wenzangu baadaye tunakutana pale pale kubugia supu na kinywaji kidogo kisha nasoma magazeti ndo najipanga kuiangalia jioni inaendaje na sasa ni usiku wikend inaenda kuisha.
Jmosi kama ujuavyo huwa sina maneno mengi maana Ijumaa huwa inakuwa imenimaliza yaani niko fried kabisa maneno hayatoki na hata kidole pendwa hakina nguvu ya kuandika ninayotaka yaandikwe.
Hujui nini kuhusu uaminifu, tupo Makapuku waaminifu, wapo watejja waaminifu, wapenzi waaminifu , raia waaminifu na kadha wa kadha. Uaminifu ni kuaminiana na kama hamuaminiani, uaminifu ukawa wa upande mmoja basi kama ni kazi haiwezi kuwa na tija. Mwajiri amuamini mtumishi wake na mtumishi amwamini mwajiri wake. Wasipoaminiana, yaani mmoja akachukulia poa basi ndo inakuwa ni mambo ya kuoteana.
Muziki sasa, naendelea na Shaggy bado na labda utamchoka kwa wiki hii yote maana nitacheza sana nyimbo zake. Burudika na hii nikikutakia mmaliziko mzuri wa wikend