Makapuku Forum

Makapuku Forum

1476cec93a0a5f8b7492cb4b617c7191.jpg
 
TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA:

sehemu ya 07:

Njia hii Mpya ilifanyika mwanzo lkn haikutiliwa mkazo. Sasa Baada ya FBI kuona hakuna mafanikio yoyote ktk misako yao ya maeneo yote ambayo walikesha wakiteseka ikabidi sasa.....

Waamue kuweka nguvu mtaani na kwkua FBI walizipiga picha noti moja moja wakaona wazisake pesa yeye wamuache atazitumia tuu.(lkn wapelelezi wa kimyakimya walikua mzigoni).

Kumbuka walimpa noti 10, 000 za dola 20. Kwahiyo walikua na serial namba za kila pesa. Hapa waliamini km itatumika hata noti moja basi FBI watadetect na kutrece hiyo hela imetoka kw nani.

Lkn wakasubiri miezi mpaka miaka ikakatika bila kupata hata mia mbovu. hoi kabisaaa!!!!.......

Wakasema hataaaaaa, ramani zikachorwa kila sehemu na CCTV mpaka chooni Kua akienda hata kujisaidia wapime DNA lkn holaaaa.!!!

Kitendawili kikazidi Kua kikubwa zaidi. Jamani km alikufa maiti yake ipo wapi?.
Hata nguo au mabaki angalau ya parashuti hakunaaaaaaa, nukta kw nukta holaa, kw Sara na maombi holaaa, UDI na UVUMBA ng'oooooo.

Miaka ikakatika na watu wakaanza kukata tamaa sasa. Ikabidi watu waulizwe vzr ivi nikweli kuna kiumbe alisafiri siku ya tukio?. Ndio nakala za carbon zinaonesha kiumbe huyo alikata tiketi tarehe na siku km ile. Alipanda ndege kila mtu alimuona kabisa tena kw kujiamini alinunua soda na kuvuta sigara na akarudisha chenji.

Pia picha zake zilibaki pale kutokana na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua crips wakati anakata tiketi. na hata ndani ya ndege sura yake hakuificha. DNA inayoonekana ktk soda aliyokunywa na sigara alizovuta zinadhihilisha huyu ni MTU aliesafili siku hiyo na tiketi yake ipo.

Jamani sasa tufanye nini ikiwa mpaka kwa maombi kashindikana?. wakaomba msaada umoja wa mataifa UN. hapo China nao KAZINI.

Km alitua salama kwnn asizitumie pesa zake?. au alitaka umaarufu?. sasa wazee wa huu haaa...chaa.....chii. Mzigoni. Baadhi ya maafisa vitambi vilianza kuporomoka na kukonda kabisaaa.

Hapa sasa hata kw TAI CHII atadakwa tuuu.

Je hawa cha,nchi,chuuu walimdakaa?.



ITAENDELEA........
 
TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA:

sehemu ya 08:

Baada ya UN na wachina kuingilia kati na kufanya msako lkn bado likawa fumbo kumpata huyu MTU. fumbo hili liliwatesa FBI kw miaka 7, mpaka mwaka 1978 ambapo kidogo mwanga ulipatikana.

ILIKUAJE........

Kwanza kabisa vidhibiti vinafanya fumbo la kumpata bwana Dan cooper Kua gumu.

Mwaka 1978, mwindaji mmoja aliokota kikaratasi chenye maelekezo ya namna ya kushusha mlango wa nyuma Wa ndege aina ya Boeing 737,( North orient flight 305. Hapo sasa na ndege wanayoifanyia uchunguzi wa tukio la bwana Dan cooper ni Boeing 727.. Hapo nisawa MTU avute bangi alafu umpe chipsi Kuku kw mlenda.

Utata mwingine km alikiangusha hicho kikaratasi bwana cooper kinawezaje kukaa miaka 7 bila kuchanika na karatasi sio Naironi?. Mtihani Mpya huo. Basi wakaashumu poa alikitupa yeye eheeee inakuaje sasa alikitupa yeye tunaamua nn?.

Hakuna cha kuamua maana ushahidi huu ni sinema tuu,

Bahati nzuri sasa ikaja kupatikana mwaka 1980

Mtoto wa miaka 8, alieitwa BRIAN IGRAM akiwa kwnye vacation na familia yake kwnye Beach ya mto Columbia alikua akichimba chimba chini km ujuavyo tabia za watoto....

...Basi bwana ndugu msomaji naona macho yamekutoka eeee.......

Mtoto alichimba shimo lefu kiasi, hapo ndipo alipokutana na makaratasi.

IKAWAJE?..........

Baada ya kuyatoa aliwaita wazazi wake na waligundua vilikua ni vibunda vitatu vya hela.

Presha baada ya kuzichunguza wakabaini ndizo zile zilizosambazwa serio namba zake mpaka mashuleni. Ole wake akutwe MTU anazo atajua kwnn kolea kaskazini hawavai Jean's za blue.

Wakawasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama na FBI mbiombio wakaja na kuzibaini ndizo zenyewe

SWALI ZILIFIKAJE PALE?.

Msako uliokua ukifanyika tangu pesa zipotee haikua rahisi MTU aende bichi achimbe na kufukia mkwanja bila kuonekana hata usiku wa manane.

Pili ktk begi mbili vije vipatikane vibunda vitatu zingine ziko wapi?.

Basi FBI wakatumia utaalam wao kufumbua juu ya hili, kwnz vibunda vyenyewe vya hela vilikua km ifuatavyo.

..kibunda cha kwnz kilikua pekee kinajitegemea na kilikua na noti 100 zilizofungwa pamoja kw rubber.

Kibunda cha pili kilijitenga cha ajabu kilikua na noti 90.lkn nazo zilifungwa pamoja kw rubber band.

Kibunda cha tatu nacho kilikua na noti 100 zilozofungwa pamoja.

Licha ya Kua noti zilikua zimefungwa kw rubber band lkn zilikua zimekaa hovyo hovyo ktk umbo la mviringo.

Basi FBI wakatoa conclusion Kua zilikaa hivyo kwakua zilisombwa na maji kuletwa hapo. Lkn kwnn vibunda vijikusanye wa pamoja?.

Hayo maji yalijuaje km hizo hela zinaukoo?. Yaani zifungwe vibunda tofauti ila ziletwe pamoja na kufukiwa shimo moja inaingia akilini kweli?.

UTATA MZITO.......

Ufukwe huo wa mto ulifanyiwa marekebisho na kuchimbuliwa chini kabisa kutengeneza ufukwe wa kitalii miaka miwili kabla ya fedha kupatikana.

Kampuni zilizotumia magreda na katapila ziliboresha ufukwe huo na kuuchimbua mpaka chini zaidi, tifua timua wote na kuutengeneza upya.

Swali hizo pesa zimefikaje pale wakati ufukwe ni Mpya?. Km pesa ziliibiwa 1971 na ufukwe umetifuliwa mpaka chini 1978 pesa zipatikane 1980 zimekujaje?. Inamaana zimekuja baada ya ufukwe kutifuliwa. zilitoka wapi?. FBI wakaingia kazini tena mpaka cooper ajisalimishe.

Hapo kazi ikaibuka upyaaaaaaaaaa.



ITAENDELEAAA......
 
TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA:



Sehemu ya 09:

Kilichopitishwa ni kuendelea na msako lkn FBI walikua wanajiuliza kwnn pesa zipatine ktk mazingira hayo?. Basi majibu yalikua almost impossible uchunguzi uendelee.

Kutokana na kesi hii kuviteka vyombo vya habari kipindi hicho hasa kugundulika tena kw zile noti basi kibarua kikaanza upya.

Sasa alitafutwa mtaalam wa JIOLOJIA alieitwa LEONARD PAILMER kutoka ktk chuo kikuu cha Portland.

Sasa uchunguzi ktk beach ambayo vibunda 3 vilipatikana. Hapo kazi ikaanza upya, magazeti sasa weeee. Kila gazeti na kichwa chake cha habari. Wakapiga hela vya kutosha na hakuna RAIA aliekubali kupitwa.

Uchunguzi na utafiti wake sasa Ukashangaza FBI na taifa zima.

Kwanza kumbukumbu sahihi zinaonesha sehemu kubwa ya mto Columbia ikiwemo sehemu vibunda vilipopatikana vilefanyiwa dredging mwaka 1974 kabla ya ile ya 1978. Dredging ni vile wanatumia vifaa maalumu kutoa udongo chini ya mto na pembezoni na kuumwaga kwnye Beach ya mto.

Kitendo hichi hua kinafanyika kuongeza kingo za mto na kuboresha ubora wa beach. Sasa basi alichokigundua huyu mtaalam ktk lile shimo ambalo mtoto alichimba na kukuta vibunda vya mkwanja chini yake kulikua na matabaka 2 ya udongo.

Tabaka la kwanza lilipatikana udongo wa mfinyanzi ambao ndio udongo unaopatikana baada ya kufanya dredging.

Sasa hii inamaana gani?. Maana yake nikwamba hivyo vibunda vya hela za cooper vilikua deposited hapo baada ya Dredging Kua imefanyika .

sasa kumbuka vzr msomaji wng dredging ya kwnz ilifanyika mwaka 1974 na tukio la bwana Dan cooper lilitokea mwaka 1971, kunatofauti ya miaka 3. Sasa je hivi ni kweli inawezekana hela zikukuruke na maji miaka 3 na kw bahati mbaya au nzuri isiyooaminika vibunda 3 vyote vikwame sehemu moja?.

( huu ujinga sasa, kwanza vibunda vinauzito gani vitumie miaka 3 kuja ufukweni?.)

Kama hiyo haitoshi kumbuka mtaalam alisema chini ya shimo alilochimba yule Dogo kulikua na matabaka 2 ya udongo ndipo ufike tabaka la udongo mfinyanzi uliotokana na dredging kufanyika mwaka 1974.

Ilipita miaka kadhaa ambapo yale matabaka mawili mengine yakajitengeneza kw juu ya udongo mfinyanzi ndio hivyo vibunda vya hela za cooper zikawa deposited.

Pia huyo mtaalam alikisia hivyo vibunda vimekua deposited hapo baada ya miaka 2 tuu iliyopita yaani baada ya yale marekebisho ya 1978 na hela kupatikana mwaka 1980, miaka 2 nyuma maana yake 1978 na kumbuka vilikwama sehemu moja vibunda vyote. Hizo sasa ntunguli sio bure. (Kaziweka nani?)

Hapo sasa walianza kukata tamaa kabisaaa. kitendawili kikawa nani alizichimbia pale beach?, kwnn ziwe vibunda vitatu tuu ktk mabegi mawili yote?.

kwnn kibunda kimoja kulikua na noti 90 badala ya noti 100 kila kibunda?.
kwnn atusumbue kichwa huyu binadam?.

Baadhi wakaona huo ni ujinga na kupotezeana muda. MTU hata km ulikua umeanza kutoka kitambi kinashuka choote.

Mawazo km vile mtu anaeishi na mama wa kambo. sasa wakaanza kulowana maana sasa maji yamefika shingoni huyu binadam mpaka apatikane itagarimu pesa zaidi ya alizoiba na atatukondesha taifa zima.

Endapo atapatikana na garama za kumtafuta zimezidi alizoiba adhabu yake ni kumuweka makumbusho akiwa hai.

watu waje kumuona mpaka alipe fidia ya deni alilotia hasara mataifa kibao yaliyoingilia kati kumtafuta, ( hiyo ni nadharia yng mwandishi).

Aibu aliyoitia serikali yake pia ilikua so ya inchi hii. RAIA uijambishe serikali mpaka umoja wa mataifa wakushindwe we nani?????????....

ITAENDELEa
 
TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA:

Sehemu ya 10:

Baadae FBI nao waliunga mkono kupitia kikosi kazi maalum kilichoundwa baadae na FBI kilichojulikana km Cooper Research Team, kua wanasaport alichokisema yule doctor.( walichoka kuteseka bila mafanikio)

Ugunduzi uliwapa maswali na kuwachanganya zaidi FBI badala ya kuwasaidia kwasababu haingii akilini hela zikukuruke na maji miaka 7 yaani tangu ziibiwe 1971, changanya umbali Wa kilometa zaidi ya 20. Kutoka anapozaniwa aliruka huyu binadamu mpaka mtoni ni umbali Wa hizo kilometa 20.

Hivyo basi hata km maji yangekua yananyata isingechukua miaka 7 yaani kuanzia 1971 mpaka 1978 ufukwe ulipochimbuliwa na pesa zikaokotwa mwaka 1980. Maji hata yatembee mdogomdogo yangechukua dakika 40 tuu na sio miaka yote hiyo.

Pia km nilivyosema hivyo vibunda kwnn hata km vililetwa na maji vitakaaje shimo moja?.

Ktk ofisi ya FBI maswali ambayo yalikua mengi kuliko majibu kuhusu fedha kufikaje pale ufukweni ilikua utata?.

Zilifikaje pale?, zililetwa na nani? Alikua na malengo gani?. haya kwnn azichimbie pale km ni mtu kaziweka?.

Basi ikapita miaka 6 bado wanatokwa jasho na swala hili la bwana Dan cooper. Mpaka waliokua vijana sasa wakaanza Kua wahenga na watoto wakaanza kupevuka sasa.

Hatimae ilipofika mwaka 1986 FBI wakanyoosha mikono na kusubiri MUNGU ajibu maombi tuu. (maombi hayawahi wala kuchelewa. Uvumilivu unatakiwa)

. .Rasmi kabisa maafisa Wa FBI mikono juu mwendo Wa mateka wakasalim amri. Fedha zilizookotwa wakaona hazina maana zinawachoresha tuu na kuwatia aibu kila siku.

Walizikalia vikao na wakakubaliana wazigawe angalau wanywe hata bia mojamoja kuchamba koo maana sio mchezo( hii utani Wa mwandishi, Ila walizigawa).

Wakakubaliana wazigawe Ila waachie noti 14 km ushaidi linaweza kutokea zali siku moja mtu akalala maskini na kuamka tajiri kw kumuona bwana Dan cooper.

Walimpa noti zilizobaki kijana alieziokita yule Dogo IGRAM ( hapo sio Dogo tena). umri umeenda kidogo ujana kw mbaliii.

....pesa zingine walipewa KAMPUNI ya Bima waliolipa fidia Norther west Oriental Airlines.

Yule dogo igram aliziuza ( alizichenji maana zilikua dola tupu). kiasi kidogo cha baadhi ya noti zake mwaka 2008 ktk mnada Wa hadhara kw thamani ya dola 37,000.

Zilizobaki kazitunza mpaka Leo huenda akapata zali la kumuona muhusika bwana Dan cooper maana hajakamatwa.

Takribani noti 9700 hazijulikani zilipo lkn FBI wakaja na dhana labda kupitia ile timu iliyoundwa mwaka 1987 itafanikiwa kupata chochote.

FBI walioteseka kuanzia 1971 wakainua mikono km vyeo bora wakose, na baadhi waliokua na uchu wakakomaa na kuunda timu Mpya mwaka 1987.

Je hawa watamnasa bwana Dan cooper?.

Je fedha zitapatikana au?.

Huyu binadam baada ya FBI kutangaza wamenawa km pilato atajitokeza?.

Fatilia sehemu inayofata utajua kumbe huyu bwana Dan cooper sio MTU Wa spotispot. akili mingimingi sana.

Usikose ITAENDELEA.....
 
TUKIO HALISI LA WIZI LILILOISHANGAZA DUNIA.


sehemu ya 11:

Kamati Mpya ya FBI iliyoundwa mwaka 1987 wakaanzisha COOPER RESEACH TEAM.

Nadharia zao ilikua SAIKOLOJIA YA MKAKATI WA COOPER*
Lkn miaka mingi ikapita bila chochote kupatikana huku upelelezi ukianza kupwaya sasa. hatimae mwaka 2007 FBI walitangaza kw umma bila kumung'unya maneno baadhi ya mambo waliyobaini ktk mkasa mzima Wa D. B COOPER, kiboko yao.

*1* siku ya tukio cooper alihitaji parachuti 1 tuu ili aweze kuruka lkn akawaagiza 4, FBI wanaamini Kua cooper alitoa maagizo hayo ya dizaini hii ili kupandikiza wazo vichwani mwa maofisa Wa FBI Kua kulikua na uwezekano ataruka na mateka ambao watatumia zile parachuti 3 na yeye moja.

Hii iliwalazimu kumpatia parachuti 4 ambazo hazina hitilafu wala ubovu wowote, kwamana hiyo nao walishiriki kumfikisha salama. Pia hawakujua Kua alicheza na akili zao bila wao kujua.

*2* Pia uchunguzi Wa kuiteka northwest orient flight 305 haukua Wa bahati mbaya alijipanga na kwa bibi yake aliaga. FBI wanaamini kua cooper alifanya uchunguzi Wa kina na kuchagua kuiteka ndege hiyo.

. kumbuka kua orient flight 305 ilikua ni aina ya ndege ya Boeing 727. Kwa kipindi hicho Boeing 727 ndio zilikua ndege pekee zenye uwezo Wa kufunguliwa mlango Wa nyuma mkiani ikiwa bado angani.

Kitu hiki kilikua hakijulikani kw RAIA na hata wamiliki wenyewe Wa ndege hawakuruhusiwa kujua labda ingekuja kutokea dharula ndipo makao makuu wanaohusika kuongoza ndege(radar) ndio wanakwambia bonyeza wapi mlango furani ufunguke. sasa yeye alijuaje hayo yote na hahusiki na utengenezaji Wa ndege?.

Ilikua ni siri kubwa kujua mlango huo Wa dharula Wa nyuma ya ndege mkiani.
Nataarifa hizi zilifichwa maana kw kipindi hicho kulikua hakuna ndege ya abiria kua na ubunifu Wa aina hiyo.

Watu pekee walioruhusiwa kujua siri hii na kupata advantages ya ubunifu huu ilikua ni CIA ambao walitumia ndege km hii kudondosha mizigo na maafisa wao ktk maeneo husika ktk vita ya Vietnam. Na hao walikua na viapo vikali wasitoe siri.

*3* Pia injini za Boeing 727 zilikua juu kidogo tofauti na ndege nyingine za abilia ambazo injini zake zilikua chini. Umeona bwana ........

Muda huo RAIA wanasikiliza tuu wanavyochambuliwa na hayo yalikua majibu yaliyoendelea ktk hadhara hiyo. Kila mwananchi alihitaji kujua hitimisho sio kuwachambulia mambo wasiyoyajua sijui injini Mara mafuta, sijui spoku na breck za ndege ( wao walimtaka cooper)

Kumbuka kua injini ya ndege ikishawashwa na kuanza kuzunguka, kitu chochote kikipita karibu au mbele yake kinavutwa na kumezwa kwnye injini na kuharibiwa au injini kupata hitirafu.

Hivyo basi uchunguzi Wa haraka kutoka kwny Boeing 727 ilimaanisha kua ilipunguza hatari ya mrukaji kuvutwa na kumezwa na injini. Nadharia zitaendelea ila bwana cooper wakampa SHIKAMOOOO. Mikono juuu....
 
Aha ha ha ha ha ha kwani nyie ngao ya hisani mmeshinda mara ngapi na mwisho wenu umekuwajeee....
Mimi niliangalia mechi nzima kwa ujumla, Arsenal wanamapungufu mengi tu, ila Chelsea walipwaya zaidi, ni kama mechi ya tatu hivi Chelsea hawachezi vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom