Makapuku Forum

Makapuku Forum

THE DOM

Sehemu Ya 10

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

Sasa sahi yeye kaja kama mwanafunzi lakini kitu alichokiacha katika computer yake, ni kitu kikubwa sana ambacho kilitakiwa kufuatiliwa na mageneral wakubwa ila sio mwanafunukama huyo,... Sasa JJ akawa anakuja katika ofisi ya BB,... Alishangaa sana kwa kile alichokikuta katika skrini ya sahi,...
"hii si DOM hiii??... Huyu anaitafuta kama nani"
Aliongea JJ lakini alikuwa kama anajiuliza mwenyewe,.. Joseph hakuridhika na jambo hilo alitoka na kuelekea chooni kule kule alipo sahi ila Joseph hajui kama sahi yupo huko,.. Sasa JJ ndio anapiga simu lakini haijulikani alikuwa akimpigia nani ila ilionekana ni simu ya siri sana... Na huyu ni mtoto wa rais,..
"halo habari yako mkuu"
"salama.. Vp mbona kama una wasiwasi hivyo"
Sasa sahi anasikia ishu nzima ya JJ anavyoongea na huyo mtu... Kama kawaida ya saa yake kurekodi,..
"kuna kijana ananipa mashaka sana hapa kitengo"
"ana nini"
"Naona ana program ya DOM sasa huyu ni nani na ni mwanafunzi"
"whaaaat?? Unasema ana program ya DOM??.... Kaipata wapi?"
"siwezi kufahamu, ila mkuu nina wasiwasi na wewe, mana kijana huyu ni mgeni katika kitengo hiki, iweje ajue siri hii.... Kwanza niambie hio DOM ipo"
"ndio ninayo... Na yule mnunuzi anakuja kuichukuwa mwezi ujao sasa DOM Codes ndio inatakiwa haraka sana"

ENDELEA.........

Maongezi hayo yalikuwa yakiendelea pasina kujua kuwa palikuwa na mtu akisikia, yaani sahi ana bahati ya kujua vitu kuliko uwezo wake, sasa kitu anachokitafuta na asijue angeanzaje leo anapata njia jinsi ya kukianza... Hapo alipo sahi alikuwa anajiskia furaha sana kwa kujua dom ilipo,... Ila sema hakujua nani aliekuwa akiongea nae
"kwahio sasa mkuu, huyu kijana tumfanye nini, mana tayari anaifuatilia ishu yetu"
"huyo hana shida, tayari yupo upande wetu"
Sasa hapa ndio kama tunapata ufumbuzi juu ya mtu ambe anaongea naye katila simu, ni baada ya kusema kuwa kijana huyo yupo upande wetu
"sasa mbona hujaniambia kabla"
"hapo ndipo nilipofanya makosa, lakini.. Kuhusu ishu ya dom hatujamgusia hata kidogo"
"sasa kwanini anayo programu ya dom"
"hebu mshirikishe, huenda ana elimu zaidi au anaweza kuipata codes za dom"
"hebu ngoja nijaribu kuongea nae mana katoka kidogo"
"sawa... We mshirikishe mwambie mimi na wewe ni kitu kimoja"
"sawa mkuu, nimekuelewa... Afu unaonaje tukamfanya kipaumbele akailete hio codes, na akifa huko atajua mwenyewe"
"sawa pia, ila kuwa makini na hilo"
"usihofu mkuu, tulikuwa tukifikiria chambo tutakitoa wapi sasa ndio hichoo kimejileta"
"na huyo ataiweza kazi mana ni majasiri mno"
"basi tuyaache mkuu"
"sawa"

Simu ilikata kisha Joseph akarufi katika ofisi ya sahi na kukaa, mana tayari keshajua kuwa wana ushirikiano mzuri na sahi,... Sasa hapa tunagundua kuwa hata huyu mtoto wa rais sio mwema, na ndio anaeiumiza nchi kwa cheo alichopo.. Mana hiki kitendo ni zaidi ya CIA (Criminally International Army).. Na kitengo hiki kinaingia sehemu yeyeote ile ndani ya nchi husika, yaani ni kitengo kisichojulikana lakini kinapoingia mahala hakiwezi kukataliwa kutokana na utambulisho wake...

Sahi akiwa ndio anafika katika computer yake lakini alishangaa kumkuta Joseph akiwa kaketi katika kiti cha pembeni, sasa sahi akajifanya kama kakosea sana kuiacha ile programu pale kwenye skrini,...
"Samahani mkuu, ni programu ya kawaida tu"
Aliongea sahi kujifanya ni muoga kama panya, kumbe hakuna mtu mbaya kama yeye,...
"wala usijali... Ila nina maswali kadhaa kuhusu hii programu yako hapa"
"sawa mkuu hakuna shida"
Hawa watu wawili ni lika moja, lakini Joseph yeye ana cheo kikubwa sana cha ugeneral, ila hata kama awe nani hawezi kuukuta uwezo wa sahi,... Sahi kasomeshwa na mtu binafsi na sio serikali, hivyo hapo anaifanyia serikali na sio mtu binafsi,.. Mana mtu aliomsomesha mpaka sasa yupo madarakani,.
"hii programu uliipata wapi"
Aliuliza Joseph huku sahi akijifanya hajui saaana kuhusu hio kitu
"aaa... Hii programu mbona niliikuta hapa hapa kwenye hii computer"
"unasemaje??... Ni kweli, na hata mimi nimeshangaa kwanini ipo hapa, na pia nimeshtuka sana kuiona hapa"
"sio kuwa umekuja nayo"
"hapana, mimi ni mgeni nitawezaje kuja na kitu kama hiki"
"unakijua hicho kifaa"
"yes... Hio ni dom"
"hii dom ainatafutwa sana,.. Na nitakuwa nawe mstari wa mbele"
Aliongea Joseph huku akiangalia pembeni kama hakuna mtu anaesikia, kisha akamuinamia sahi na kumwambia
"sisi sote tupo pamoja... Hio dom sisi tunayo... Ila codes zake ndio hatuna"
Sahi akajifanya kushtuka sana huku nae akisema
"aahhh kwani hizi dom zipo ngapi... Mana mimi ninayo yenye codes zake kabisa"
Joseph alishtuka kuskia hivyo, ilibaki kidogo tu adondoke kwa mshtuko...
"unasemaje"
"ndio... Ninayo dom ina codes zake.. Ngoja nikutafutie programu yake"
"wewe si ulisema hio programu uliikuta hapa wewe"
"nilikudanganya, hii program ni yangu na hapa nilikuwa nacheki information yake ipoje"
Sasa sahi akafanya vitu vyake kwenye computer, kachapia chapia hapoo kisha akamwonyesha codes za dom..
"unaziona hizi... Hizi ndio codes za dom... Alafu dom yenyewe ninayo hapa kwenye begi"
Sahi aliitoa ile dom kisiri siri, na kumwonyesha Joseph ambae ni mtoto wa rais aliopo madarakani,.. Hivyo mtoto anaihujumu nchi ya baba yake,..
"we hii kitu umepata wapi"
"unanitisha tena"
"hapana, nataka tu kujua umetoa wapi"
"niliikuta chumbani kwa baba yangu"
"baba yako anafanya kazi gani serikali"
"Alikuwa ni mtumishi wa BOT"
"sasa, tupe hio dom na hizo codes zake... Tutakupatia bilioni moja tasilimu"
Sahi kusikia neno Bilioni moja, sio pesa ndogo hio, unakula mpaka ucgakae, sasa hapa wamekutana wapelelezi wote, hivyo kikubwa ni kumjua mshindi ni nani na wote ni lika moja, yaa hata umri wa hawa watu ni sawa... Sasa sijui kwanini imekuwa hivyo
"hio ni pesa kubwa sana mkuu... Lakini, nikikupa hii baba yangu ataniletea shida... Sasa tufanyeje ili nisiletewe shida"
Aliongea sahi huku akiingiza dom katika begi lake,...
Joseph alikuwa akiutamani sana mana huenda kule bank alichezewa mchezo siku ile na kuwekewa feki,... Afu mbaya zaidi ile walionayo haina programu,
"huyo baba yako alistaafu mwaka gani"
"mwaka jana"
Sasa kusikia mwaka jana, Joseph akajua lazima huyu baba yake sahi aliondoka na Original kisha akaacha dom feki,.. Na ndio hio wanayoitafutia codes zake, kumbe sio Original...
"sasa sikia, nitakupatia hio tulio nayo.. Kisha utupatie hio"
"sawa... Mimi kitu ninachokitaka ni baba yangu asijue kama dom haipo"
Joseph aliona kapata Zezeta lao la mwaka, yaani bonge la Zezeta... Wasipoangalia watafanywa mazezeta wao...
Joseph hakuchelewa kuoiga simu kwa General Nyange,..
"haloo mkuu..."
"kuna nini tena Joseph"
"mkuu... Huezi amini kumbe sisi tunamiliki dom feki"
"ati unasemaje wewe"
"hio dom ni feki mkuu, yaani tumeingia choo cha kike"
"kama hii ni feki, hio Original iko wapi"
"huyu kijana anayo, tena ina codes zake"
"Whaaaaaat???..... Ati unasema nini"
"ndio hivyo mkuu"
"sasa si umwambie akupe, huyo ni mtu wetu"
"tatizo ni kwamba, anahofia kwa baba yake atajua kuwa dom haipo ndani.. Hivyo angalao tumpe hio feki akamdanganyie"
"una uhakika hio ni yenyewe"
"ndio mkuu, na nimeziona codes zake"
"basi ngoja niitume hii dom nilionayo huku, kisha nawe itume hio... Nampiga simu yule mzungu aje aichukuwe sasa hivi, mana haifai kukaa nayo"

Sasa huku kambini kwa General aliekuwa ofisini kwake pamoja na mr deo General mwenzie
"deo, hatimae dom original yapatikana"
"unasemaje nyange"
"kumbe yule kijana baba yake ni mtumishi wa BOT, na ndie alieondoka na dom original"
Aliongea mr Nyange huku wakiwa na furaha ya hali ya juu,... Na wao wakiipata wanaiuza kwa mzungu mmoja ambae yeye ndie anamiliki mashine ndogo ya kuchapia pesa, hivyo mzungu huyo akifanikiwa kuwa na dom hio atachapa pesa ya Tanzania ambayo ni laki moja ya noti moja, ni hatari sana mtu binafsi kuachia pesa tofauti na serikali...
"kwahio, yule yule kijana tuliekuwa nae jana ndio mmiliki wa dom Original?"
"ndio, na ni dom iliokuwa ndani kwa baba yake"
"anhaaaa, sasa tutaipataje hio original"
"lazima tumpatie hii yakwetu ili baba yake akaendeleee kudanganyika"
"sasa unasubiri nini, ita helikopta hapa uitume haraka"
Harakati za kutuma dom zilianza huku wakijua kuwa watakapo ipata tu wanaiuza yaani hawataki kukaa na mzigo tena, na hata sababu ya kukaa na mzigo kwa muda mrefu ni kwamba hawaku ukamilisha mzigo huo,....
"lakini mr nyange, angalia sana uwepo wa huyo kijana.... Mana kuipata dom sio kitu cha mchezo eti"
"aaahhh hakuna tabu, kama kasema baba yake alikuwa mtumishi wa BOT sasa kuna maswali gani hapo"
"basi haya, itume"

Huku TSS sahi alikuwa akiendelea kumwonyesha kazi ya hio dom, unajua wengi wanaitafuta lakini hawajui inafanyaje kazi, japo wanajua ndio kichapisho cha pesa lakini hawajui kinafanyaje kazi,... Sahi akazidi kumpa Joseph jinsi dom inavyofanya kazi katika mashine...
"sahi, hii mashine upatikanaji wake vipi"
Aliuliza Joseph baada ya kuoneshwa mashine hio
"hii mashine, kuipata sio rahisi, unapaswa kuwa tajiri mkubwa sana katika dunia... Na hata serikali binafsi haiwezi kuimiliki mana kuinunua kwake inaweza kufilisi nchi"
"duuuuuu,... Kwahio yule mzungu ana mashine sio"
Aliongea Joseph, maneno yaliomshtua sahi mana hajui hio dom inauzwa wapi,..
"mzungu??...mzungu gani huyo"
"kuna mzungu anataka kuinunua kwa thamani ya shilingi bilioni 500"
Sasa sahi ndio anajua kuwa hio dom inauzwa kwa mzungu na gharama ni Bilioni 500,...
"sasa mnachelewa nini nanyi"
"wewe si ndio unayo"
"walete hio feki basi nika mdanganyie mzee kama ipo kumbe ni feki"
"inakuja usijali"

Wakati huo helikopta ipo angani kuelekea jijini Dar es Salaam, kuipeleka dom feki,...
"sahi, tutoke nadhani dom inakaribia Airport"
"Twende"
Basi sahi na Joseph walitoka pamoja lakini ni kila mtu na gari yake,...
Sasa wakiwa wapo njiani, sahi alipokea simu ya Mheshimiwa rais GU,
"haloo mkuu"
"habari yako kijana"
"salama tu Gu"
"vipi kazi inakwendaje"
"nakwenda kuchukuwa dom original"
"sawa... Angalia usije haribu mipango, wasije kukushtukia"
"usijali mr GU"
Mazungumzo yao hua sii ya simu ya kawaida, huwa wanatumia transmission iliounganishwa automatically katika sikio la sahi, lakini hio transmission haionekani katika sikio la sahi,...

Sasa sahi alipokuwa barabarani, kuna gari aliiona, na anaijua hio gari, wakati huo Joseph yupo nyuma ya sahi, na sahi yupo mbele, sasa sahi kaona gari ya mama mmoja hivi anamjua vizuri,... Sasa ile gari ya yule mama ikapaki pembeni,... Sahi alishindwa kuvumilia kumpita huyo mama,.... Sasa hata Joseph pia anaijua hio gari ya huyo mama,... Lakini yeye hakutaka kusimama... Ila hofu ilimjia mr Joseph, kwanini sahi kasimama kwa ajili ya huyo mama... Mama huyo ni mke mkubwa wa General Nyange, yaani mama wa yule marehemu itwae Sharbiny,... Sasa Joseph anashangaa, huyu sahi amemjuaje huyu mama.... Sasa sahi anaharibu kila kitu,.... Lakini sasa huyu mama ndio yule alie onekana kwenye simu ya sahi, ndio huyu hapa
"shkamoo"
Sahi alimsalimia mama huyo, mama kwa mshtuko wa sauti ya mtu huyo alijikuta akilia mwenyewe,... Sasa swali linakuja hivi, kwanini sahi anafanana sauti na huyo kijana... Sasa je, hata huyu mama pia hamjui sahi??....
"huyu sahi, anajuana vipi na huyu mama,... Hapana lazima nimtaarifu General Nyange, je huyu ni nani?"
Aliongea Joseph huku akichukuwa simu yake na kutafuta jina la mr Nyange,...... Sasa sahi keshaharibu swala la kwenda kuchukuwa dom original....

Itaendelea......

Je? Nini kitaendelea??.... Sahi atafanikiwa kuchukua dom original

ITAENDELEA.....
 
Heri walio masikini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao

Heri wenye huzuni maana hao watairithi nchi

Heri wenye njaa na kiu ya haki maana hao watashibishwa

Heri wenye rehema maana hao watapata rehema

Heri wenye moyo safi mana hao watamwona Mungu

Heri wapatanishi mana hao wataitwa wana wa Mungu

Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki maana ufalme wa mbingu ni wao

MATHAYO:5:3:10

Mbarikiwe sana muwe na asubuhi iliyo njema kwenu
Nawe pia barikiwa mdogo wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom