Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Jumatano August

U khali gani kapuku mheshimika, inawezekana ikawa muda wa kusalimia umepita sana maana tulisalimiana asubuhi na jioni hii inapaswa tuulizane tu siku yako ilikuwaje. Kwangu siku ilikuwa poa, japo mambo yanakaba lakini hayajaninyima nafasi ya kuja humu kuonana na wewe mtu bora kabisa unayelifanya Jukwaa hili kuwa la kipekee. Unajijua kuwa wewe ni mtu bora kabisa ndo maana KF inapendeza.

Leo 10 kubwa zimechelewa na sio mbaya zikiingiliana na muziki, na muingiliano huu usikupelekee kuwa na mawazo machafu, mawazo bakanifu. Ni suala la muda tu na si unajua KF ndani ya JF ni kama kokoro, likivutwa linaleta kila kitu na bila kusahahu KF ni kama utawala wa malkia, kwingine leo ni Alhamisi watu wanajiandaa na Ijumaa. Asante kwa mliotuamsha kwa magazeti, sala, hadith, BBC, historia na sports. Asante sana wadau.

Leo hakuna ubaya nikisema humu sio kwamba hatuwezi kukosana, umoja wetu naamini unaletwa na mitizamo tofauti tuliyonayo, tofauti zetu ndo umoja wetu. Utashangaa nasema nini, usikonde nitakugusia maana tumeongea na SHIMBA YA BUYENZE na hakuna ubaya kati yetu na hata aliponiita fala nilicheka tu maana hata yeye anajua huko ninakotoka Fala ni jina la mtu tena kabatizwa, hujui, jina Francis linafupishwa kuwa Fala 😀

Muziki sasa, ni ngumu sana kuutambua muziki wa Tanzania, kuna sababu nyingi za hili lakini linaweza kuwa ni kutokuwepo kwa utashi wa kisiasa kuufanya utamaduni usambae maeneo mengi. Ni mada ndefu ngoja tu nikwambie huu muziki wa singeli unaweza kututambulisha endapo utashi utakuwepo kwa sana. Burudika wakati tukiitafuta Alhamisi


Namuona Obe alivoulamba
 
......Na kweli kile alichokifikiria Lady Ninja Asha na ndivyo ilivyokuwa kwani mbali na mbinu, uzoefu na ujanja aliokuwa nao Tyga katika maswala ya upiganaji na uninja lakini kwa Cj4 alionekana bado kabisa hajaiva kutokana na mapigo aliyokuwa anapelekewa hata yeye mwenyewe Tyga alishangaa.
"Nani wewe unaingilia ugomvi usiokuhusu!!?"
alilalama Tyga mara baada ya kuanguka kwa mara ya pili na kutema mate yaliyochanganyika na damu nyingi sambamba na meno mawili ya mbele mara baada ya kupokea nakozi za ajabu kutoka kwa Cj4 aliyakuwa anamchanganyia mapigo matatu kwa wakati mmoja.
"NANI WEWE!!!?"
Aliuliza tena kwa kufoka Tyga huku akijizoazoa tena pale chini damu zikizidi kumvuja baada ya swali la awali kutojibiwa kwa mdomo zaidi ya kupelekewa mateke mfurulizo ya angani ambayo alifanikiwa kuyapanch yote lakini alistaajabu pindi yule mtu ambae hakumjua alipotua chini tu ghafra alimfatua mguu kwa kumchalaza na wire furani uliomvinga na kumchota mtama Tyga na kudondoka kama gunia la viazi.
Alisimama na kujikaza kiume Tyga huku akirudia rudia kuuliza lile swali ambalo Cj4 hakunyanyua mdomo kumjibu zaidi alimjibu kwa mkong'oto wa hali ya juu uliopelekea sasa Tyga kuona nyota nyota.

Wakati mwanaume Cj4 akiendelea kumfunza adabu Tyga kwa kumuonesha vita vya kiume ndipo Lady Ninja Asha alipotumia ule uchawi wake wa Kininja na kufanikiwa kuondoka eneo lile na kutokea upande wa pili ambapo alitembea hivyo hivyo japo alikuwa na maumivu makali sehemu zile alizoumizwa na Tyga hususani pale tumboni kulipokuwa na kile kisu cha kininja.
Huku nyuma bado Tyga alizidi kudhibitiwa na Cj4 na hatimae alizimishwa kwa kupigwa kata ya shingo iliyopelekea kuteguka ule mshipa uliopitia nyuma ya sikio na kupoteza fahamu.
"The Game is start, Mr X you are the Next..."
aliongea Cj4 huku akiwa kamkanyaga kifua Tyga pale chini alipopoteza faham na kuchomoa kijiantena kilichokuwa katika saa yake kubwa ya mkononi ambayo pia ilikuwa kama simu na hapo ndipo alipotuma location za mawasiliano kwa Kamishna Shebby na signal ilipofika tu alipiga simu muda ule ule bila kuchelewa kutokana na yeye kule alipokuwa alikuwa kwenye usingizi wa mawenge kutokana na mawazo ya ndoa yake na Asha pia vile alivyojua kuwa Hussein bubu ni baba mkwe wake.
["Muangalie usoni atakuwa ni mwanamke tu, Nakuja sasa hivi"]
aliongea Shebby kwa njia ya simu mara baada ya kupata signal maalum ya Cj4 na kupewa taarifa kwa ufupi kilichojili.

Na kweli baada ya pale CJ4 alimnyanyua Tyga ambae alikuwa kapoteza fahamu na kutimka nae kwa umakini eneo lile hadi mahala ambapo aliamini pametulia wakati huo signal iliyokuwa inampa mwelekeo Kamishna Shebbyikiwa on.
Nusu saa baadae Shebby alifika pale na gari ndogo akiwa mwenyewe walimpakia Tyga na kuondoka nae kuelekea maeneo ya Kongowe njia iliyoelekea gerezani kwa Shebby na huko walipanga kumuingiza kwenye gofu la nyumba moja ya zamani iliyokuwa haishi mtu yeyote ili wamfungie mule kwaajili ya kumuhoji juu ya Mr X.
"Kumbe walikuwa wawili?"
aliuliza Shebby pindi wakiwa njiani
"Yah! walikuwa wawili ila mmoja nimemuacha aende"
alijibu Cj4
"Kwanini sasa?"
"Kwa sababu alikuwa mwema"
"Mwema?! Kivipi wakati nae ni Ninja"
"Kwa sababu ni Ninja wa kike"
"Cj4 umefanya kosa huyo wa kike ndie nilikuwa namtaka haswaaaaa nina imani ndie aliyetushambulia Mkuyuni"
Alilalalma Shebby baada ya kusikia kumbe walikuwa wawili lakini Cj4 amemzalau wa kike na kumuacha aende.
Aliumia Shebby kwani hasira zake kuu ni kumjua yule Ninja wa kike ili amuue kwa mkono wake kama alivyomuahidi siku ile endapo atamuacha hai.
Lakini kwa Cj4 alishagundua kitu kutokana na kusikia maongezi ya yule Ninja na kuhisi kwa asilimia tisini kuwa mchumba wa Shebby waliyeenda na Hussein bubu kukutana nae ndie yule Ninja aliyemsaidia pale lakini hakutaka kumwambia haraka Kamishna Shebby kwa kuwa alijua kuwa yule Lady Ninja alitumiwa kimakosa na Mr X kwa kuwa alikuwa katika mlolongo wa watu waliotakiwa kupotezwa na Mr X.

* * * * * *

Alirudi Asha na kufanikiwa kuibuka chumbani kwake pasi na mtu yeyote kujua.
Alijiangalia kwenye kioo cha chumbani kwake mara baada ya kuvua mask yake ya Kininja na kuchukua sindano aliyoichoma dawa ya kuzuia maumivu na kujidunga eneo lile la tumboni.
Na bada ya nusu saa maumivu yalikata kwa nguvu ya ile dawa hapo ndipo alipochojoa mavazi yake ya kininja na kubaki na nguo ya ndani kisha alichukua visu maalum vya oparation vilivyokuwa chumbni kwake mule na kujituliza mbele ya kioo na kuanza kujichana huku akijibinya kwa nguvu kuondoa kile kisu kwenye nyama zake za tumbo.
Kitendo alichokuwa anakifanya Asha kilikuwa si cha kitoto kwani ilihitajika ujasiri wa hali ya juu sana kufanya kama alivyokuwa anafanya Asha tena huku akijiangalia kwenye kioo mpaka akafanikiwa kutoa kile kibisu cha kininja kilichonasia kwenye nyama za tumbo lake.

Baada ya hapo Lady Ninja Asha alianza kujishona taratibu sehemu ile ya jeraha kwa umakini mkubwa mpaka akafanikiwa kumaliza kabisa na kubaki na alama ya mshono eneo lile la chini kidogo ya tumbo.
Ndani mwa Dk, Asha ilikuwa nusu ya hospitali kwani kila kitu muhimu kilikuwepo na aliandaa haya yote kwa kujua kuwa katika kazi zake siku moja inaweza kumpata balaa na kujisaidia mwenyewe na ndivyo ilivyokuwa siku hiyo.
Alijifunga bandage yenye dawa maalum eneo lile la mshono na kuizungushia kiunoni ambapo ilibana vizuri kisha alisafisha eneo lote lililokuwa na dam dam na kujilaza chali kitandani akiwaza nini hatma yake ya baadae na huyo Mr. X

("Hivi yule aliyenisaidia ni nani hasa? Na kwanini alikuja eneo lile Mh! Inaonekana ni mtu hatari sana tena sana lakini kwanini alikuwepo pale? Au anajua kinachoendelea pale ? Natamani ningemjua nimuulize lakini sidhani kama anaweza kuwa salama kwangu")
Aliendelea kuwaza Asha akiwa pale kitandani wakati huo tayari ilikuwa inaingia alfajiri na maumivu ya mshono yakaanza upya na kumuongezea zaidi mawazo kwani alijua kabisa vile visu vinakuwaga na sumu ndani yake pindi vikiingia kwenye nyama ya binaadam.
Japo aliweza kukitoa lakini aliamini tayari mwilini mwake ana sumu ya Invisible knife na itakuaje endapo atajulikana kuwa na jeraha atadanganyaje? au hiyo ndoa kama itapangwa haraka ataolewaje...?
Alifikiria Asha na kujiuliza maswali haya yaliyomfanya chozi limtoke kwa mara nyengine.
Hakujisikitikia yeye kama atakufa mapema kwa sumu iliyo mwilini mwake bali alisikitika endapo atakufa kabla ya kumuua Mr X. .......


Twambie nani Mr X na wapi alipo?"
lilikuwa ni swali toka kwa Kamishna Shebby akimuuliza mateka wao yule ambae ni Tyga.
"Sijui unazungumzia nini"
alijibu Tyga kwa kujiamini mbali na kuwa uso wote ulikuwa umechakaa hata hakuweza kuona vizuri kutokana na uvimbe na damu zilizokuwa bado zinamvuja.
"Narudia twambie wapi Mr X alipo na ni NANI??"
"Nimeshasema sijui unamaanisha nini wala sijawahi sikia hiko kitu"
bado aliendelea kutia ngumu Tyga wakati huo Cj4 alikuwa anasikia kile alichokuwa anajibu Tyga lakini alimuacha Shebby aendele kumuhoji huku upande wake binafsi alikuwa na mtu mmoja akimuhabarisha kinachoendelea nae si mwengine ni mkuu wa majeshi tu.
"Nani Mr X??????"
"SI-JU-I"
Mabishano yaliendelea ambapo safari hii Cj4 aliamua kutoka kule nje alipokuwa na kurudi speed hadi kwa Tyga bila kumuuliza kitu chochote alichomoa kisu chake cha kikomandoo na alipomfikia Tyga tu alikamata sikio na kulikata lote palepale mbele ya Kamishna Shebby aliyekuwa anatumia maneno mengi kumuhoji Tyga.
"Aaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhhhhhhh"
Alipiga yowe la maumivu Tyga mara baada ya Cj4 kumpangusa sikio na kulieka mbele yake pasi na huruma.
"Sasa Muulize tena kama atakuwa hasikii vizuri au haelewi nakuja baada ya dakika kumi kumalizia la upande wapili"
Aliongea Cj4 na kunyanyuka tena kwenye sehemu ile waliyoiandaa mapema kipindi wanasuka mchezo wao wa kumnasa Mr X hivyo ndani ya lile gofu haikumaanisha tu waliingia kwa dharula ama walibahatisha. bali walikuwa walipaandaa mapema kwa kujua lazima Mr X atatuma mtu wake wa kummaliza Hussein bubu.

Kitendo cha Cj4 kumkata kwanza sikio Tyga bila kutumia muda wa kubembeleza kumsemesha wala kumuuliza kidogo kilimstaajabisha Shebby ambae yeye hasira zake muda wote zilikuwa kwa Ninja wa kike ambae Cj4 alimuacha aende.
Maumivu yalikuwa makali sana kwa Tyga lakini bado msimamo wa kumficha Mr X ulikuwa palepale hali iliyomtia hasira zaidi na Shebby aliyeamua kumzibua sehemu za sikio zilezile zilizokuwa zinarusha damu na kupelekea Tyga kupoteza fahamu.
"Huyu atasema kweli?"
aliuliza Shebby kwa kuhisi kuwa yule mateka wao anaonesha yuko tayari kabisa kufa kuliko kusema ukweli kuhusu mr X
"Kwa kuwa ana mdomo atasema tu kile anachokijua kweli, ukimshindwa utanambia nije nimsemeshe"
alijibu kwa kujiamini Cj4 na kuingia tena mmule ndani alipozimia Tyga.
Lakini alipokuwa anamsogelea kumkaribia pale chini alisikia mlio wa kitu mithili ya alarm ya saa ya kimulimuli ikibeep kwenye mavazi ya Tyga ambapo alimpekua harakaharaka ndipo alipostuka baada ya kugundua kumbe kwenye lebo ya nyuma ndani ya kola ya gwanda ile ya kininja aliyovaa Tyga kulikuwa na maneno madogo ambayo kumbe yalishonewa na wire wenye signal maalum za bomu la kuendeeshwa na rimoti... Yaani lile vazi zima la Kininja lilitengenezwa kwa nyuzi maalum za baruti nyeusi ikiwa na maana combat aliyovaa Tyga lilikuwa ni bomu.
Hii ilimstua na kumshangaza Cj4 kwa kuhisi kuwa hata yule Ninja mwenyewe hakuwa anajua kama amevaa bomu muda wote na sasa namba zake zimeingizwa kwenye systim na rimoti imewashwa na ishaanza kuhesabu japo pale haikuwaonesha itahesabu kwa dakika ngapi.
"Tokaaaa Shebby Rukia nje harakaa Tokaaaaa"
alikimbia Speed kutoka nje Cj4 na kumkamata Kamishna Shebby kuruka nae kwa nje ya ile nyumba pindi alipokuwa anashangaa Cj4 alipokuwa anampigia kelele za kutaka arukie nje wakimbie eneo la kile kibanda.

Waliangukia mita kumi na lile gofu huku Shebby akiwa bado haelewi, Cj4 alimshika tena mkono na kuanza kukimbia nae pamoja kuelekea mbali zaidi na lile gofu.
"CJ....Vi....."
alitaka kuongea kitu Shebby lakini kabla hajamalizia alistushwa na kishindo cha mlipuko kutokea nyuma yao na alipogeuka hakuamini kuona gofu lile alilokuwemo mateka wao likisambaratika kwa moto.

"Shiit Cj4 ina maana umeamua kumlipua!!?"
aliuliza kwa mshangao Kamishna Shebby pindi alipokuwa anashuhudia ule mlipuko uliowasha moto ghafra kule kwenye gofu walilomfunga mateka wao Tyga.
"Huu sio muda wa kuuliza Kamishna bado tupo kwenye mchezo wa Mr X japo na sisi tumeanzisha mchezo wetu ndani yake tuondoke hapa haraka."
aliongea Cj4 na kukimbilia kule ilipo gari yao sambamba na Shebby na kujitoma ndani yake ambapo safari hii dereva alikuwa Cj4 mwenyewe.
"Lakini kwa nini umemlipua?"
"Mimi sie niliyemlipua ila ni Mr X mwenyewe"
"Mr X?? Kamlipua lipuaje sasa"
"Kwa kutumia akili za siku nyingi kabla hajatafuta wachezaji nyota wa kuucheza mchezo wake"
majibu ya Cj4 si kwamba yalikuwa yanamsaidia Shebby kutatua maswali aliyokuwa nayo, bali ndio kwanza yalikuwa yanampa maswali mapya ambayo yalikuwa yanamuonesha mwanga jinsi ya kutafuta majibu pasi na kuuliza tena.
"So what is Next..?"
aliuliza Shebby japo alihisi wanaenda kwa Hussein bubu ila alitaka kujua kama itawalazimu wamuhamishe ama waendelee kumtega palepale lakini jibu la Cj4 lilizidi kuonesha tofauti baina ya KOMANDOO wa JESHI na KAMISHNA wa POLISI.
"Next mimi nitadili na Hussein wewe pitiliza alfajiri hii hii kwa mchumbaako na umuhamishe pale anapoishi haraka kwa usalama zaidi"
"Mchumbaangu? Ina maana dokta Asha?"
"Ndio hivyo, all the best Kamishna"
Alijibu maneno haya Cj4 wakati huo tayari gari ilifika pale Mbagara karibu na ile hoteli kulipoonekana kun mkusanyiko wa watu na maaskali polisi hususani sehemu ile ya nyuma kwenye bustani.
Alishuka Cj4 na kumuachia usukani Shebby ambae alikuwa bado anayatafutia ufumbuzi majibu ya maswali ya Cj4 huku akipiga gia kuelekea kwa mchumbaake kwa kufata kauli ya mtu aliyeamini kwa moyo mmoja kuwa amemzidi mbinu na akili ya vita.

Lakini ukweli ni kua Cj4 alibaini mchezo uliotegwa na Mr X kwa wale Maninja wake hasa alipowaona wanapambana usiku wake sare zao zilishabihiana karibu kila kitu na kubaini kuwa matereo ndio yaleyale na system ndio ile ile hivyo kuna uwezekano mkubwa na yule Ninja mwengine akalipuliwa na mavazi yake ambayo aliamini wazi kuwa hajui kama ni bomu.
Na kwa kuwa alihisi kwa asilimia kubwa kuwa yule Ninja ni mchumbaake Shebby aliyevaa kivuli cha Dokta Asha na yote hayo aliyabaini kupitia maongezi yao wenyewe pindi walipokuwa wanapambana bustanini.
Hivyo aliamini kama asipoenda mtu kumtoa kule basi maisha yake nayo yatakuwa hatarini.

* * * *

Aliamka asubuhi ile Asha na kujichoma tena sindano ya kuua maumivu kabla hajatoka kuelekea chini akiwa na maana ya kufanya mazoezi ya kutembea kwa kupandisha ngazi na kutroti kidogo ili kukipa shurba kidonda chake kibichi kisijivute na kumfanya astukiwe na watu kama alikuwa na jeraha mwilini mwake.
Alivaa full tracksuit na kwa jinsi alivyokuwa anatembea kwenye ngazi mara baada ya kutoka chumbani kwake ilikuwa ni vigumu mno kumtambua kama ana jeraha la mshono mwilini mwake.
Mazoezi ya kupanda na kushuka ngazi yaliendelea wakati huo bado mamaake alikuwa hajaamka na kutoka chumbani kwake.

Akiwa anafanya yale mazoezi mepesi ya kupanda na kushuka vingazi mulemule ndani bado mawazo yalikuwa mengi sana kichwani mwake Asha hususani kuhusu kifo cha Mr X.
Hakuwahi kumuona alivyo wala kujua wapi alipo hata historia yake alikuwa haijui zaidi alichojua kipindi cha nyuma kuwa mr X ni mtu mwenye kutetea haki za watu na kuwasaidia na kuwafichua wabaya na ndio sababu ya kuwa na maadui waliokuwa wanataka afe ili akosekane mtu wa kuwafichua na kusaidia wengine.
Awali aliamini hayo lakini sasa ameujua ukweli kuwa wote waliokuwa wanamtafuta mr X kwaajili ya kumuua walikuwa sahihi kabisa.
Lakini ugumu unakuja ni kugundua picha halisi ya mr X na jina lake halisi ama hata wadhfa aliowahi kuwa nao kwani ingesaidia kumgundua na kumpata kiurahisi.
"Mwisho wako unakuja... Mwisho wako ndio huu, Mwisho wako unakuja , Mwisho wako ndio huu"
aliongea haya maneno Asha kwa hisia huku akiwa kama anaimba pale alipokuwa anapandisha ngazi na kushuka.

Lakini mara akiwa bado anapandisha na kushuka pale kwenye ngazi ndipo aliposikia mlio wa kitu cha alarm ukitokea chumbani kwake kama vile alivyokuwa anasikia Cj4 na kumfanya Asha asijue Alarm ile ni ya nini kwa kuwa yeye hajawahi kuset alarm yenye mlio kama ule.
Alianza kupandisha taratibu kurejea chumbani kwake kuangalia hiyo alarm ilikuwa ya nini, lakini akiwa anapandisha kabla hajaufikia mlango wa chumbani mwake alijikuta moyo unamuenda mbio na kusita kuingia kwanza na kusimama mlangoni kusikilizia akiwa anajishauli inapotokea hiyo alarm na kupata hisia ni pale kitandni alipozivua nguo zake za Kininja usiku aliporudi na hapo kidogo alijipa moyo kuwa hakuna kitu kibaya na ndipo alipotaka kufungua mlango lakini Hamaaaaaadiiiii.......!!! Alirushwa yeye na Mlango baada ya mlipuko wa ajabu kutokea ghafra mule chumbani na kumstua hadi mamaake aliekuwa analala chumba cha chini.
''Aaaaaaaaaaaaaaaaaghhhhhh''
 
Uf...
99a035ccf4bef69dce0a60dc5bdc939d.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom