Nimekukimbilia wewe Bwana nisiabike milele kwa haki yako uniponye
Unitegee sikio lako uniokoe hima uwe kwangu mwamba wa nguvu , nyumba yenye maboma ya kuniokoa
Ndiwe genge langu na ngome yangu kwa ajili ya jina lako uniongoze unichunge
Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri maana wewe ndiwe ngome yangu
Mikononi mwako naiweka roho yangu umenikomboa , Ee Bwana Mungu wa kweli
ZABURI:31:1:5
Mbarikiwe sana muwe na asubuhi iliyo njema