Mazishi ya Bradley Lowery: Maelfu wafika kumuaga shabiki aliyegusa nyoyo za wengi....
.........Maelfu ya watu walijitokeza katika barabara za kuelekea nyumbani kwa Bradley Lowery, shabiki wa klabu ya Sunderland FC ya Uingereza, kutoa heshima zao za mwisho.
..
Ibada ya wafu ilifanyika katika kanisa la Mtakatifu Yusufu kijijini mwao, wengi wakimsifu sana mvulana huyo kwa ukakamavu wake na sifa alizojilimbikizia....
Maandamano yalikuwa sio ya nchii hiii..
Jermain Defoe aliyeonekana kutekwa na hisia, alikuwa amevalia jezi ya England yenye jina la Bradley

Meneja wa zamani wa Sunderland David Moyes alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri katika soka waliohudhuria mazishin hayo
Barabara za kuelekea kanisa la Mtakatifu Yusufu zilipambwa kwa puto na mabango yenye ujumbe wa kutoa heshima kwa Lowery.
Wengine waliacha ujumbe nje ya uwanja wa Sunderland wa Stadium of Light.
Waombolezaji walifika kwa wingi kanisani, hivi kwamba wengine walikaa nje.
Jamaa za Bradley walivalia jezi za soka, kukumbuka upendo aliokuwa nao kwa mchezo huo.
Mamake Gemma aliambia waliohudhuria mazishi hayo: "Alikuwa na tabasamu kubwa na la kupendeza hivi kwamba lilikuwa lingeangaza chumba chochote kile. Ni shujaa mwenye ujasiri, ametuacha.
"Aligusa nyoyo za wengi - aliwatia moyo watu wengi. Mwana wetu mpendwa, ndugu - nyota ya kupendeza.
"Ingawa wakati uliokuwa nasi ulikuwa mfupi, ni lazima una kazi ya kufanya huko mbinguni na malaika kwani Mungu amekuchagua wewe.
"Kwa sasa, mtoto wangu kwaheri, Hatu tutakapoonana tena shujaa wetu huko juu mbinguni."...
Ila kiukweli watu wameonesha upendo wa kiwango cha hali ya juu....zicheki picha watu walivoamua kufanya. .
Karibia kila barabara mtaani zilitumdikwa pichaa.
...moyes alikuwepooo
upendo uliojeee.....
Pumzika kwa amani kipenzi chetu....