Makapuku Forum

Makapuku Forum

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho pia anataka klabu hiyo kutoa dau la pauni milioni 60 ili kutaka kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier 23 (Mirror).
 
Manchester United hawatomuongeza mkataba Zlatan Ibrahimovic, 35, licha ya kumruhusu kuendelea kutumia uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wa Carrington wakati akiuguza jeraha lake la goti (Star).
 
ZABURI 100

1.Mfanyieni BWANA shangwe,dunia yote;

2.Mtumikieni BWANA kwa furaha;Njoni mbele zake kwa kuimba,

3.Jueni kwamba BWANA ndiye MUNGU Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake.,na kondoo wa malisho yake.

4.Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru;Nyuani mwake kwa kusifu;Mshukuruni ,lihimidini jina lake;

5.Kwakuwa BWANA ndiye mwema ;Rehema zake ni za milele;Na uaminifu wake vizazi na vizazi.

Asante BABA kwa mchana wa leo ,tunakushukuru,tunakutukuza ,tunakuabudu ,tunakuheshimu maana wewe ni mwema kwetu unatulinda,unatutunza unatutia moyo hata hatuangamii kwa mapito yoyote..asante kwa yote yanayoendelea mahali hapa tunakushukuru maana wewe ndiye unayawezesha yote,asante kwa ajili ya MAKAPUKU WOTE Endelea kutubariki BABA na kuimarisha Upendo uliopo .
Tunaendelea kukabidhi kazi zetu,mipango yetu,changamoto zote,wagonjwa na wenye shida mbalimbali nyoosha mkono wako maana mkono wako si mfupi ,gusa kila mmoja wetu akakuone MUNGU wetu na AMANI ITAWALE

TUNAOMBA NA KUSHUKURU AMEN

MCHANA MWEMA

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
Amen, nawe pia mchana mwema mama mchungaji
 
Manchester United bado hawajaweza kutoa kiasi wanachotaka Inter Milan ili kumsajili winga Ivan Perisic, 28, lakini wanatazamia kukamilisha mkataba wa pauni kati ya milioni 45 hadi 50 (Independent).
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger pia amedhamiria kutomuuza Alexis Sanchez, 28, ambaye hajasaini mkataba mpya na inadhaniwa anataka kwenda Manchester City (Independent).
 
Ukiwa unabugia ugali kibua mimi nakushushia tetesi za usajiliii kwa udhamini mnono wa kapuku hotel...

Twende sawa....

Hi Kapuku hotel mpishi hatendi haki kabisa anko, hivi ni lazima kila mchana tupikiwe ugali?

Wengine ni watu wa wali kwenda mbele, asubuhi tunaanza na vitumbua, mchana biriani , jioni walinazi. Kabla hakujakucha tunagonga kiporo
 
Chelsea wameweka kipaumbele katika kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, huku kukiwa hakuna uhakika na hatma ya Diego Costa, 28 (Guardian)
 
Meneja wa Leicester amekuwa na mazungumzo na winga Demarai Gray, 21, na anataka mchezaji huyo asiondoke huku Liverpool, Tottenham na Everton zikimtaka (Sky Sports).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom