Dondoo za bbc. ..

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametembelea mji wa Mosul kuwapongeza wanajeshi katika kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu

Usiku wa kumkai leo ilikuwa siku ya kwanza ya kutekelezwa kwa amri ya kutotoka nje wakati wa saa kumi na mbili unusu jioni hadi kumi na mbili unusu asubuhi kwa wakaazi wa maeneo kadhaa ya Lamu, Garissa na Tana River.

Tanzania ina adhma ya kuelekea katika uchumi wa viwanda ikiwa ni ajenda kubwa ya Rais John Magufuli.Mojawapo ya bidhaa zinazobuniwa na kutengenezwa nchini humo ni mpira wa miguu huku nchi hiyo ikiwa na uhitaji wa mipira laki 5 kwa mwaka.Na kwa wastani kijana mmoja huweza kutengeneza mipira minne kwa siku .

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema raia wake hawajutii uamuzi wao wa kupiga kura ya kujitenga na Sudan licha ya kuwepo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo changa

Nchini Rwanda chama cha kisiasa cha PS Imberakuri kimemshtumu mwanadada Diane Rwigara aliyetangaza nia ya kugombea kiti cha urais kughushi nyaraka za chama hicho katika zoezi la kukusanya saini za wafuasi wake na kuapa kumpeleka mahakamani.

Nchini Tanzania baadhi ya wasichana na hata kina mama walioko maeneo ya vijijini, hukumbana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa za kujistiri ama sodo kwa lugha adhim kutokana na gharama, hivyo kufanya mahudhurio shuleni kuwa madogo kwa wanafunzi wa kike.

Wanariadha kutoka mataifa hamsini wameshawasili mjini Nairobi , Kenya tayari kwa michezo ya kumi na ya mwisho ya mashindano ya vijana ya shirikisho la riadha duniani IAAF