Makapuku Forum

Makapuku Forum

eb1ddc32ec50061b51744001e363eea1.jpg
 
Muziki: Penda Mwili Wako

Jumapili inaishiria wadau, naamini kabisa tumekuwa na siku nzuri. Kila mmoja na siku yake, wapo waloenda church leo, wapo walioenda kazini na wapo waliokuwepokuwepo tu, lazy sunday. Na kizuri zaidi ni kuwa bado tunakutana hapa na kubadilisha mawili matatu. Kapuku Forum ni jukwaa bora kabisa kwa sababu wewe u sehemu yake. Unalijua hilo.

Easy and lazy sunday ndivyo nilivyoiona leo mimi, na hata maongezi ya humu ndo yamekaa kirahisirahisi tu ilmradi tu kufanya siku iende vizuri.

Mambo ya simu ha hahahahaha, Tecno werevaa (whatever right?) ndo imeshika chati leo, hongera sana wenye tecno werevaa maaana naonaoga hata mnaweza kutuma maua. Mimi simu yangu ina simu ndani ya simu, cover la singsung, betry LG, supika za motorola, na keypads ni za tecno werevaa bila kusahau ni screen tach ya Itel6 (inafanana na Iphone). Mwisho wa siku ninaweza kuweka signature na kuingia JF kufurahia KF. Una tatizo na simu yangu?

Muziki wa leo: Penda mwili wako, yeah, love your body maana ni wewe na huwezi kuwa mwingine, kama una kakitambi ka bia na machalali basi endelea kuongeza michemsho, mwili ni wako utunze maana ni wewe unaumiliki. Fanya mazoezi ya kiaina ili uwe mwepesi, kula misosi ya maana sio kila siku wewe karanga na fanta orange.

Tuburudike na Ed leo, kuikamilisha Jumapili yetu na kuombeana kuwa wiki hii iwe ni nzuri na yenye mafanikio kwetu.


Asante Obe
 
Dondoo za bbc. ..



Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi, ametembelea mji wa Mosul kuwapongeza wanajeshi katika kile alichokiita ukombozi wa mji huo kutoka kundi la wapiganaji wa kiislamu

Usiku wa kumkai leo ilikuwa siku ya kwanza ya kutekelezwa kwa amri ya kutotoka nje wakati wa saa kumi na mbili unusu jioni hadi kumi na mbili unusu asubuhi kwa wakaazi wa maeneo kadhaa ya Lamu, Garissa na Tana River.

Tanzania ina adhma ya kuelekea katika uchumi wa viwanda ikiwa ni ajenda kubwa ya Rais John Magufuli.Mojawapo ya bidhaa zinazobuniwa na kutengenezwa nchini humo ni mpira wa miguu huku nchi hiyo ikiwa na uhitaji wa mipira laki 5 kwa mwaka.Na kwa wastani kijana mmoja huweza kutengeneza mipira minne kwa siku .

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amesema raia wake hawajutii uamuzi wao wa kupiga kura ya kujitenga na Sudan licha ya kuwepo mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo changa

Nchini Rwanda chama cha kisiasa cha PS Imberakuri kimemshtumu mwanadada Diane Rwigara aliyetangaza nia ya kugombea kiti cha urais kughushi nyaraka za chama hicho katika zoezi la kukusanya saini za wafuasi wake na kuapa kumpeleka mahakamani.

Nchini Tanzania baadhi ya wasichana na hata kina mama walioko maeneo ya vijijini, hukumbana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa za kujistiri ama sodo kwa lugha adhim kutokana na gharama, hivyo kufanya mahudhurio shuleni kuwa madogo kwa wanafunzi wa kike.

Wanariadha kutoka mataifa hamsini wameshawasili mjini Nairobi , Kenya tayari kwa michezo ya kumi na ya mwisho ya mashindano ya vijana ya shirikisho la riadha duniani IAAF
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom