Makapuku Forum

Makapuku Forum

Wale wa simulizi twende woteee....


Sehemu ya 24....


"Haroo, mbona hamji kistaarabu kina nani nyinyi Ebo simameni haraka!" Aliuliza askari mmoja aliyekuwa na cheo cha Koplo huku akiwazuia kina Shebby. Pasipo kusema chochote Shebby alitoa kitambulisho na kuwaonesha. Wote walikakamaa na kutoa heshima stahiki. Moja kwa moja walikaribishwa na kusindikizwa kwa mkuu wa kituo kama jinsi alivyotaka Kamishna Shebby.
Bado kwa wakati huo Kimaro hakujua nini alichofikiria kukifanya kamishna Shebby na kwanini amekuwa mbogo kiasi kile.
Waliingia ndani kwa kasi ya mwendo wa mamlaka. Kwa bahati nzuri mkuu wa kituo alipoonana na Shebby tu walijikuta wote wakishangaana.
"Shebby!!!?"
"John!!"
"Aaagh! kweli milima haikutani kumbe upo huku?" Walipeana mikono Kamishna Shebby na yule mkuu wa Kituo ambaye ilitabanaisha ni watu wanaofahamiana kabla.
"Enhee, vipi familia tayari?" Aliuliza Shebby akiwa amepunguza munkari aliokuja nao. Alisogeza kiti na kukaa wakati huo wote Kimario alikuwa pembeni akitazama mazungumzo ya wakubwa zake licha ya kuwa wote kiumrii waliendana.\"Vipi familia kaka?" Alisaili Shebby.
"aaah! Shebby we acha tu habari za wanawake ndio sitaki kabisa kuzisikia" Alijibu mkuu wa kituo na kukivaa kile asemacho.
"Kivipi tena John hadi hutaki kusikia habari za wanawake?"
"Ndugu yangu yaliyonitokea ndio sitamani kabisa kutafuta familia kwa sasa we acha tu, nahisi nina mikosi sana kwa wanawake"
"Duh! John.. kwani kilikupata nini mshkaji baada ya kuachana kipindi kile? Si ulinambia ulitaraji kufunga ndoa siku si nyingi?"
"Ndugu yangu Shebby ni story ndefu sana ila nitakuhadithia kwa ufupi ilivyokuwa" Aliongea John ambaye alikuwa OCS kituo cha Mkuyuni akiwa na cheo cha Inspecta. Taratibu alikumbuka ilivyokuwa mara ya mwisho walipoachana na Shebby pindi walipokuwa kwenye kozi maalum ya uongozi na usimamizi ndani ya idara ya ulinzi wa ndani miaka minne iliyopita. John alianza kusimulia ilivyokuwa hadi kupelekea awe na msimamo wa kutohitaji kuwa na mwanamke hata familia.
"Ndugu yangu kiukweli kama ulikuwa hujui leo nitakwambia ujue wazi ukae ukijua kuwa wanawake ni watu wa ajabu sana inatakiwa uwe na akili nyingi sana jinsi ya kuishi nao.
Kumbuka siku ile ya mwisho tulipokuwa tunaagana kwenye ile tafrija baada ya kozi kuisha nilikuonesha kwenye simu yangu picha ya mwanamke niliyetaraji kumuoa baada ya kumaliza kozi. Basi baada ya kupandishwa cheo nilijua sasa maisha nitakuwa nishayaweka kwenye mstari tena kwa kuwa na mwanamke mzuri kama Tedy aaaah, nilijiona bonge la mjanja. Lakini! Daah! Sikia sasa ishu ilivyokuwa baada ya kuachana na kupoteana kipindi tulipomaliza kozi na kupewa likizo ya mwezi mmoja sikuamini nilichokikuta mtaani. Kumbe yule demu Tedy si alikuwa ananiigizia bwana! Muda wote naweka naye malengo hata nikawa najinyima na kumtumia pesa ili afungue mtaji wa saloon kama alivyonambia kumbe nae alikuwa anatumbua maisha na mpuuzi mmoja mchafumchafu mtoto wa mtaani na kunigeuza mimi chuma ulete.
Sio siri niliporudi almanusura niue mtu kwa hasira mara baada ya kupata umbea wote na nilipokuwa namuulizia kuhusu hiyo saloon aliishia kunizungusha. Lakini mwishowe walinasa kwenye mtego niliowatega ambapo kwa macho yangu niliwafuma wakiingia Guest moja huko Keko. Nilipompigia Tedy kumuuliza alipo alivyonambia ndio nilizidi kuchoka! Eti 'ooh, nimeenda kwa bibi vikindu anaumwa sana nitakupigia baadae'...... Nilichomjibu nikamwambia kuwa hiyo guest haiitwi vikindu inaitwa Mumbu na hapo nilikata simu na kufata ushauri wa mzee wangu tuliekuwa wote kwenye gari ambaye alinisihi mno nisipaniki wala kumchukia mwanaume aliyelala na mchumbaangu kwani mwenye makosa ni mchumbaangu. Nikakubaliana na mzee nikaachana na Tedy toka siku hiyo nikampiga stop tusijuane tena. Sasa hiyo tisa kumi ni Angelina au malaika ndivyo nilivyopenda kumwita mtoto kutoka Arusha aliyekuja kufanya kazi za ndani nyumbani kwetu kipindi hiko kabla sijahamishiwa hapa Mkuyuni na kuwa ocs. Angelina alikuwa mzuri mwenye adabu na heshima. Kila mtu nyumbani alimpenda kuanzia mzee, mama na dada hata tukashawishika tufanye mipango ili nimuoe awe mmoja wa familia yetu. Sasaa sijui niseme ujingaaa! au utaahira! yani nashindwa kuelewa hawa wanawake vichwa vyao vilivyo kwani kipindi chote tunafanya mipango na kuzungumza na mama yake huko kijijini walionesha hali ya kukubali kumbe yule mtoto Angelina alikuwa tayari mke wa mtu muda mrefu na alikuja Dar kufanya kazi za ndani kwa lengo la kumsubiri mumewe aliyekuwa huko migodini. Sio siri hii iliniuma mno nilipogundua na kushindwa kumuoa mwanamke ambaye tayari moyo wangu ulishaelekea kwake. Aliniangusha baada ya kusikia mumewe amerudi na mambo yamemuendea vizuri baada ya mgodi kutema na karudisha mapenzi kama kawaida. Hapo nilipagawa sana na ndipo baba yangu mzee Cyprian aliponihadithia kisa kimoja enzi zake kilichotaka kufanana na changu tena kutoka huko huko Arusha. Baba alisema siku moja alimuona bint mzuri walipokuwa kikazi na mwenzake. Alifanya mipango ya kuwa naye kupitia yule mwenzake ambaye alimzidi cheo. Lakin kumbe mwenzake akamzunguka kwa familia ya yule binti na zawadi mbalimbali.
Alipokuwa anaenda kule anajiwakilisha yeye ndiye mtakaji na zawadi zilitoka kwake. Mzee wangu alipokuja kugundua ilikuwa tayari kachelewa.
Akasalitiwa hata na binti mwenyewe ambaye pia alimjua mzee wangu ila akaamua kuwa na rafiki yake sijui kwanini. Yaani wanawake usiwaamini hata kidogo. Ila kwa dua za mzee na jinsi alivyosononeka kumkosa yule binti ndipo ikatokea safari iliyomfanya naye rafikiye amkose yule bint na kuchukuliwa na jamaa gani sijui ambaye mwishowe nasikia kumbe naye alikuwa na tamaa ya utajiri si akamuua kinyama yeye yule binti sambamba na mtoto aliyezaa nae na hapo ikawa si Mzee wangu wala yule rafiki ake aliyeweza kuishi na yule binti. Lakini yoooote yalisababishwa na binti mwenyewe laiti angekuwa na msimamo awali wa kumkataa yule rafikiake mzee aliyeanza kumchombweza na kumpondea mzee pengine yote yasingetokea hadi kuangukia mikononi mwa huyo bwana muuaji. Basi bwana ndio hivyo mzee hamasa zake nilizielewa na baada ya hapo kila mwanamke ninaemuona mbele yangu kuna muda namuona kama kinyago vile kwa jinsi walivyonipotezea malengo na pesa bila faida yoyote. Sasa hivi ishu yangu nikijisikia navuta cheche tu la bar basi tunamalizana kila mtu kimpango wake hahahahahaaaa.."
Alimalizia kwa kucheka ocs John na kumuacha kamishna Shebby katika taharuki kubwa kichwani. Hata Sajent Kimaro naye alikaa vizuri pindi alipokuwa anaisikiliza maneno ya ocs John.
"Enhee, Mkuu wangu safari hii wapi sasa na wewe uko wapi" aliuliza John
"Daah, nilikuja kwenye msiba huu uliotokea sehemu yako juu ya mganga wa kienyeji aliyekutwa amejichinja kibandani mwake sasa nilitaka kujua tafiti zenu mlipofikia na awali sikuwaza kama ningekutana na mtu tunayefahamiana kama wewe"
"Oooh! ni kweli bwana Dah! uchunguzi wetu bado unaendelea taratibu ila tuliruhusu mazishi yaendelee baada ya ripoti ya daktari kuthibitisha kuwa hakukuwa na kiashirio chochote kuwa marehemu alishambuliwa zaidi ilionekana ni msongo wa mawazo uliopelekea kujichinja. Ila tukiwa kama polisi bado uchunguzi wetu hatujaufunga rasmi."
"Sawa vizuri John" Aliongea Kamishna Shebby huku mawazo yake yakiipitia tena maneno aliyosimuliwa muda mfupi na ocs John hasa kwenye kipengele alichonukuu stori iliyomuhusu babaake kidogo ilimtia shaka. Hisia zilimvuta na kuona kuna vitu vinaingiliana na story ile ya Hussein kuhusu mkewe Zai. Alitamani kumuuliza zaidi lakini alitafakari njia ipi ya kumuingiza tena kwenye ile mada hadi afunguke zaidi kuhusu babaake! Lakini hakutaka amfanye ajue anachokitafuta wala amtilie shaka.
Ndipo Shebby alipoliacha lile na kurudi kwenye azma yake juu ya 'prove' aliyotaka kumuonesha Kimaro kuwa yule aliekufa si Mr.X japo alikuwa na kovu usoni.
"Sasa John hebu achana na ripoti ya daktari nihadithie kuhusu nyinyi mlivyopata taarifa ya kifo kile na mazingira mliyokuta hivi ni kweli yaliwapa picha kuwa yule mtu alijiua?" Aliuliza Shebby sasa akiwa kauvaa tena uso wa kazi kama alivyokuja na kumfanya hata ocs John kukaa makini kwa utulivu kabla hajatoa majibu. Alipoanza kuongea Ocs John tu, kama kawaida yake Shebby aliingiza mkono kwenye mfuko wa suruali kulipokuwa 'recoder' maalum aliyoitumia kwaajili ya kunasa sauti kwani ilikuwa na uwezo
"Ni hivi mkuu, tulipokea simu iliyoleta hiyo taarifa majira ya saa tatu asubuhi na vijana walipofika walichukua picha na kuhoji maswali mawili matatu ya msingi na katika maelezo waliyotupa raia hususani mtu wa kwanza kumuona marehemu ambaye alikuwa mwanae waliosaidiana kazi alisema kuwa babaake siku hiyo aliwahi mapema kwa nia ya kuandaa mazingira kuwa kuna mgeni wake mteja wa siku nyingi toka enzi za babaake angekuja lakini asubuhi ileile yule kijana alipofika na kuingia mule kibandani ndipo aliposhangaa kukuta babaake akiwa chini damu zimetapakaa huku mkononi akiwa na kisu."
"Sasa ukiwa kama ocs baada ya vijana wako kuleta taarifa hii ulichukua hatua gani zaidi"
"Kwanza mkuu niliwaamuru wapeleke mwili moja kwa moja hospitali kwa vipimo zaidi kama huenda alivamiwa na watu na kumchinja kisha kumshikisha tu kisu."
"wazo zuri sasa baada ya majibu kutoka kuonesha kuwa hakushambuliwa ndipo mkaungana moja kwa moja na ripoti ya daktari mkimaanisha hakuna tena upelelezi wowote si ndio?"
"Mmmh, hapana mkuu, kama nilivyosema awali bado tunafanya upelelezi wa chini kwa chini."
"Upelelezi gani John hivi ulifika hata eneo la tukio?"
"mh, hapana."
"Umeona sasa, unakikaribisha kitambi rafiki yangu usipende uheshimiwa wewe ni damu changa kama mimi bwana inabidi vitu vyengine tujiweke mstari wa mbele wenyewe tusipende kutuma tuma tu" Aliwaka kwa msisitizo Shebby guku akigonga meza iliyokuwa mbele. Polisi waliokuwa jirani na ocs walitega masikio ya umbea na kuzungumza chinichini kujua alichokuwa anazungumza Kamishna na ocs wao akituhumiwa uzembe. Kauli ya Shebby haikumshangaza tu ocs bali hadi Sajent Kimaro mwenyewe bado hakung'amua kamishna wake ana 'provement' zipi hadi imefikia kusema kwa kujiamini kiasi kile.
"Yaani, ndio hivyo ocs John nakuhakikishia kuwa yule mganga HAJAJIUA bali AMEUAWA." Aliekea msisitizo kabisa maneno yake Shebby na kuwafanya rafiki zake ocs John na sajent Kimaro kuachama midomo wasijue wamjibu nini kwa kuogopa kuwa huenda wakaeleweka vibaya mbele ya mkuu wao.
"Najua vichwa vyenu vinatamani kuniuliza nina uhakika upi hadi nasema hivi lakini haya majibu yangu kwenu yatawaongezea maswali kama nitawaambia kwa maneno tu. Na kwa sababu hiyo sitowapa mimi majibu ila kuna mtu mmefanya kosa sana kumuacha huru. Nahitaji aletwe hapa mara moja na nitamuhoji mimi mwenyewe na kila mtu hapa atapata picha kwanini nasema yule mganga hakujiua wala hakutingwa na mawazo bali ameuawa na aliyesababisha kifo chake ni mr. X"
"MR.X..!!?" Alishangaa sana ocs John mara baada ya kamishna Shebby kupitiliza maneno na kujikuta anaropoka jina la mr.X ambalo kwa upande wa ocs John lilikuwa geni kabisa.
"Usijali John, ni hadithi ndefu sana ila nitakuhadithia japo si leo kwanza nataka utume vijana wako akakamatwe huyu mtu mara moja."
"sawa Mkuu, nani mtu mwenyewe vijana wakaifanye hiyo kazi sasa hivi aletwe hapa."
"Nahitaji akakamatwe mtoto wa marehemu aliyekuwa msaidizi wake, huyo wa mwanzo kabisa kumuona marehemu."
"sawa Mkuu." Baada ya hapo ocs alimuita inspekta wake akusanye vijana saba haraka wachukue difenda kwenda kumkamata mtoto wa marehemu aliyejichinja ambaye pia ni mjukuu wa marehemu Mnyungunyungu aliyetarajiwa kuwa mganga atayefatia. Vijana wa polisi walipopewa agizo lile walitii haraka hasa walipogundua kuwa aliyetoa amri ile alikuwa ni Kamishna na walionesha ushupavu mbele yake ili wasionekane wachovu. Ndipo gari ilipochomoka kwa speed kama mshale kuwahi Mkuyuni stendi ili waelekee kule msibani kutimiza amri waliyopewa. Ukimya ulipita kituoni kwa zaidi ya saa zima wakisubiri vijana warudi na mshukiwa wa Shebby waone hiyo prove itayotumika kwenye mahojiano. Lakini ajabu toka waondoke wale vijana wa polisi walichelewa sana kurudi tofauti na haraka zao. Kibaya zaidi waliondoka pasipo kubeba mawasiliano yoyote hali iliyomtia hasira Kamishna Shebby.
"John....Kimaro sasa twendeni wenyewe hukohuko hatuwezi kusubiri tu." Alitoa amri Shebby na kunyanyuka kitini. Amri za Shebby ziliwafanya polisi wote kuwa kimya na kuwa makini sana katika kazi zao muda ule wakimuhofia sana na kumtafsiri kuwa yule kamishna ni mkali mno na mkorofi, bila kujua kumbe Shebby alikuwa mtu mwema sana tena mcheshi ila tu, kichwa chake kilivurugwa baada ya kujiingiza kwenye harakati za kesi ya Hussein na kumjua Mr X.
Walipofika nje kabla hawajaingia garini kupandisha Mkuyuni stendi ambako wangeacha gari na kushuka mabondeni kwa miguu, ndipo waliishuhudia difenda waliyoituma ikirudi kituoni na vijana kushuka haraka haraka. Macho ya Shebby yalishangaa kutomuona mtu aliyeagizwa zaidi aliwaona wamama wawili. Uso aliukunja jazba ikamvaa na kumwita inspector aliyeongoza wale vijana.
"Mbona mmechelewa sana inspekta pia hamkuja na muhusika! kulikoni?" Aliuliza kamishna Shebby.
"Mkuu tumefanya kila jitihada za kufanikisha kuja na mtuhumiwa lakini hatukufanikiwa kumpata baada ya kutoweka masaa machache kabla hatujafika."
"AMETOWEKA!!!?" wote watatu, Shebby, John na Kimaro walitaharuki na kuuliza pamoja.
......
 
UF ...
2cb96538819483afe5704b0901681d09.jpg
 
Muziki: Jumamosi Fleva


Ni jumamosi usiku sasa, lakini kama ilivyokuwa koloni la Malkia Liz, unaweza kuta ni saa sababu mchana sehemu fulani na wote tunaungana hapa KF kuburudika.

Usidanganywe na utando wa juu wa uji ukauparamia, juu umepoa ila ndani ni wa moto pasi mfano. Hii ndo hali ya leo humu KF, asanteni sana kwa mlioamua kupumzika. Mapumziko yenu tunayapenda na kipengele cha muziki kipo kuwaburudisha

Leo ni siku ya miziki ya kisasa zaidi na ni jambo zuri kwamba Makapuku Forum ni sehemu bora kabisa kuwa na hasa kwa kuwa wewe unayesoma segement hii u sehemu yake. Najua unajijua kuwa u mtu maalum kabisa pasi mfano si wale moja haikai mbili haiingii.

Kuna kolabo zinavutia kutazama wakiimba maana wote wanajua na utawafurahia. Sikiza kolabo hii ya komandoo pekee wa Tanzania ambaye huwa hakaribishwi sherehe za muungano kupasua matofari, yeah, Lady JayDee mkali mwenye sauti ya iliyopangika Kisababto na itakuvutia. Hapa anaungana Kidumu, unataka niongee nini kuhusu Kidumu. Tizama


Asanteee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom