Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nilifanikiwa ila wewe kwa nini ulienda sasa kwa yule dada wa kiarabu muuza shurubati? Hivi ni mwarabu au mpemba yule maana si kwa mbwembwe zile
Sasa bhinamuu mambo ya muuza shurubati wetu yamekujajee apa ?? Naulizaa tu

kesho ninae ila mm nimeona nimuite mwarabu mpemba vijana wanasema sio wa nchii hii

Ndoa ndogo bado changa ujue
 
5557fc4916a8040bec99461fdd92b39d.jpg
 
Muziki: KKB

Leo napata ugumu kusalimia kwa maneno, tupeane tano ngumu ngumu kuashiria kuwa tumekuwa na siku nzuri kabisa siku ya leo bila kujali nini kilijiri kwa uzuri au ubaya. Nitakuwa faster leo maana mchana mzima beki zimekuwa hazikabi ipaswavyo hivyo imebidi kocha niingie uwanjani dakika za majeruhi angalau kutafuta droo, yeah, sio droo utie nguo na makorokoro bali sare angalau asubuhi staftahi ipatikane.

Ni bahati mbaya sana kusikia member mwenzetu keshakuwa mwendazake (RIP), ndo maisha hayo nasi hatuna cha kuzuia maana ardhi ni kubwa sana, akizikwa yeye si kwamba atatumalizia nafasi, makaburi hayajajaa kutufanya sisi tusife. Inauma sana. Pole kwetu

Sijui ni upepo wa kusi au kasi umepita nami leo nilitaka kuweka nyimbo ya 'kitotototo' yaani kucheza mwanzo mwisho unaelewa huelewi ilimradi tu vyombo vya muziki vinaposikika unajisikia kutingisha mwili na hasa mguu, usitingishe kiuno, bado ni mapema sana na ada zinazidi kupanda kila siku. Sakayo asante kwa uchaguzi huu

Mr Nice na si Mr Noise ndiye atakayetuburudisha leo, sina mengi juu yake maana ukiona Diamond ang'ara leo jua kuwa Mr Nice aliisimamisha Afrika Mashariki na Kati, hakuacha hata kitongoji kimoja katika nchi saba zinazotuzunguka. Wazazi iliwabidi watunge maneno ili kuwaelewesha watoto kuwa kuku akipanda baiskeli ujue anaenda kuchinjwa.

Hadi wakati mwingine. Nakupenda kapuku mwenzangu sababu wewe ni mtu muhimu humu, heshima yako sana



KKB- Kuku kapanda Baiskeli

Aisee Asante Obe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom