Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katika dondoo za bbc. ..


Kauli ya Rais wa Tanzania John Magufuli kwamba wasichana wanafunzi wanaopata ujauzito wasirudi shuleni imepingwa na baadhi ya wananchi na wanaharakati wakisema wasichana hawa wana haki ya kikatiba kuendelea na elimu.

Waziri mkuu wa Uingereza THERESA May amewasilisha mipango yake, kuhakikisha haki za raia wa Umoja wa Ulaya nchini Uingereza, baada ya kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

Leo ni siku ya wajane duniani. Mataifa mengi ya Afrika yamelaumiwa kwa kuwapuuza wajane. Tanzania ni miongoni mwa mataifa hayo.

Raia mjini kinshasa wawamwagia mzigo wa lawama wahubiri injili, mapasta pamoja na wamiliki wa baa kwa kusabisha kelele kwa jamii na kusababisha watu kukosa usingizi

Ujumbe wa waisilamu kutokea nchini Kenya upo nchini A-Kusini kuleta umoja baina ya raia wa A-Kusini kuweza kuelewa mahubiri ya dini ya kiisilamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani

Ukuaji wa teknolojia unaoenekana kushika kasi Nchini Kenya huku wanablogu wakizidi kuongezaka, hijabi bloggers ndo kivutio
Suala la mabinti hakika linahitaji mjadala,na aseme kilichojaa moyoni mwake huenda ikawa ni more personal,kitaifa,kikatiba kuzuia wasirudi shule....haimezeki

Wajane wakumbukwe hata vitabu vya Mungu vinazungumza yapo maandiko mengi mojawapobni hili

YAKOBO 1

27. Dini iliyo safi ,isiyo na taka mbele za MUNGU BABA ni hii,kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao ,na kujilinda na dunia pasipo mawaa.

MBARIKIWE
UF ....
35581a368a9a18499e83d43c00143190.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom