Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katika dondoo za bbc. ..


Kauli ya Rais wa Tanzania John Magufuli kwamba wasichana wanafunzi wanaopata ujauzito wasirudi shuleni imepingwa na baadhi ya wananchi na wanaharakati wakisema wasichana hawa wana haki ya kikatiba kuendelea na elimu.

Waziri mkuu wa Uingereza THERESA May amewasilisha mipango yake, kuhakikisha haki za raia wa Umoja wa Ulaya nchini Uingereza, baada ya kuondoka katika Umoja wa Ulaya.

Leo ni siku ya wajane duniani. Mataifa mengi ya Afrika yamelaumiwa kwa kuwapuuza wajane. Tanzania ni miongoni mwa mataifa hayo.

Raia mjini kinshasa wawamwagia mzigo wa lawama wahubiri injili, mapasta pamoja na wamiliki wa baa kwa kusabisha kelele kwa jamii na kusababisha watu kukosa usingizi

Ujumbe wa waisilamu kutokea nchini Kenya upo nchini A-Kusini kuleta umoja baina ya raia wa A-Kusini kuweza kuelewa mahubiri ya dini ya kiisilamu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani

Ukuaji wa teknolojia unaoenekana kushika kasi Nchini Kenya huku wanablogu wakizidi kuongezaka, hijabi bloggers ndo kivutio
Mi naona magu yuko sawa tu
 
ZABURI 71

8.Kinywa changu kitajazwa sifa zako ,na heshima yako mchana kutwa

9.Usinitupe wakati wa uzee,Nguvu zangu zipunguapo usiniache.

BABA Asante kwa asubuhi ya leo ,asante kutuamsha salama Sifa ,Shukurani,Heshima Na Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.
Tunaomba toba kwa mambo yote tuliyokosa kwa mawazo maneno na matendo turehemu twakusihi.
Ponya wagonjwa ,waliovunjika moyo,wasio na kazi Baba waangalie kwa wema wako,wafiwa ,wajane yatima wafariji waguse wakuone wewe na wakutegemee daima.

Tufundishe kusamehe zaidi,kupenda zaidi,kutoa zaidi ili tupate kusamehewa,kupendwa na kupokea.

Siku ya leo tushike mkono tuongoze katika safari hii njema ya maisha ambayo umetupa kama zawadi iliyo njema tuifurahie na kila wakati tuhesabu baraka ulizotujalia,tusinung'unike,tusikate tamaa na wala tusirudi nyuma tukaze mwendo huku tukikutegemea wewe tu ili tuuone utukufu wako.

Bariki kila mmoja katika kundi dogo hili la MAKAPUKU awe msaada kwa mwenzie,awe faraja awe mfano bora na kumbukumbu njema kwa kila mmoja na kuifanya dunia uliyojaa changamoto kuwa mahali pema na pazuri pa kuishi.

Asante kwani utatupa kushinda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Amen

MUWE NA SIKU NJEMA MBARIKIWE
Amen mamii
 
3f9c186e5cacf486d58a4182f81256e2.jpg
 
Kuna wakati unahisi umebaki peke yako kwa kuwa ndugu jamaa n'a marafiki wamekutenga lakini nikuambie ni kweli watakutenga lakini yuko mmoja tu ambaye hatakutenga naye ni Mungu muumba wa mbingu n'a ardhi Mungu wa Abraham Isaka n'a yakobo

Huyu pekee atakurudishia tena hao waliokutenga

Asubuhi njema makapuku forum
 
Kuna wakati unahisi umebaki peke yako kwa kuwa ndugu jamaa n'a marafiki wamekutenga lakini nikuambie ni kweli watakutenga lakini yuko mmoja tu ambaye hatakutenga naye ni Mungu muumba wa mbingu n'a ardhi Mungu wa Abraham Isaka n'a yakobo

Huyu pekee atakurudishia tena hao waliokutenga

Asubuhi njema makapuku forum
Asante mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom