Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170623-WA0007.jpg
 
ZABURI 71

BABA Asante kwa asubuhi ya leo ,asante kutuamsha salama Sifa ,Shukurani,Heshima Na Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.

Tufundishe kusamehe zaidi,kupenda zaidi,kutoa zaidi ili tupate kusamehewa,kupendwa na kupokea.

Siku ya leo tushike mkono tuongoze katika safari hii njema ya maisha ambayo umetupa kama zawadi iliyo njema tuifurahie na kila wakati tuhesabu baraka ulizotujalia,tusinung'unike,tusikate tamaa na wala tusirudi nyuma tukaze mwendo huku tukikutegemea wewe tu ili tuuone utukufu wako.

Bariki kila mmoja katika kundi dogo hili la MAKAPUKU awe msaada kwa mwenzie,awe faraja awe mfano bora na kumbukumbu njema kwa kila mmoja na kuifanya dunia uliyojaa changamoto kuwa mahali pema na pazuri pa kuishi.

Asante kwani utatupa kushinda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Amen

MUWE NA SIKU NJEMA MBARIKIWE

Asante kwa maombi, uwe na siku njema
 
ZABURI 71

8.Kinywa changu kitajazwa sifa zako ,na heshima yako mchana kutwa

9.Usinitupe wakati wa uzee,Nguvu zangu zipunguapo usiniache.

BABA Asante kwa asubuhi ya leo ,asante kutuamsha salama Sifa ,Shukurani,Heshima Na Utukufu ni kwako Mfalme wa Amani.
Tunaomba toba kwa mambo yote tuliyokosa kwa mawazo maneno na matendo turehemu twakusihi.
Ponya wagonjwa ,waliovunjika moyo,wasio na kazi Baba waangalie kwa wema wako,wafiwa ,wajane yatima wafariji waguse wakuone wewe na wakutegemee daima.

Tufundishe kusamehe zaidi,kupenda zaidi,kutoa zaidi ili tupate kusamehewa,kupendwa na kupokea.

Siku ya leo tushike mkono tuongoze katika safari hii njema ya maisha ambayo umetupa kama zawadi iliyo njema tuifurahie na kila wakati tuhesabu baraka ulizotujalia,tusinung'unike,tusikate tamaa na wala tusirudi nyuma tukaze mwendo huku tukikutegemea wewe tu ili tuuone utukufu wako.

Bariki kila mmoja katika kundi dogo hili la MAKAPUKU awe msaada kwa mwenzie,awe faraja awe mfano bora na kumbukumbu njema kwa kila mmoja na kuifanya dunia uliyojaa changamoto kuwa mahali pema na pazuri pa kuishi.

Asante kwani utatupa kushinda sawa na mapenzi yako katika jina la Yesu Amen

MUWE NA SIKU NJEMA MBARIKIWE
Ameeeeeeiiiiiiniiiii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom