Makapuku Forum

Makapuku Forum

WARUMI 8

37.Lakini katika mambo hayo yote tunashinda ;na zaidi ya kushindav,kwa yeye aliyetupenda.

38.Kwa maana nimekwisha kujua hakika kwamba ,wala mauti,wala uzima,wala malaika,wala yaliyopo ,wala yatakayokuwapo ,wala wenye uwezo,

39.Wala yaliyo juu wala yaliyochini ,wala kiumbe kingine chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu

Baba asante kwa upendo wako na kutuamsha salama ,tunashukuru kwa afya ,kazi ,familia na upendo usio mwisho tunajikabidhi mikononi mwako bariki kazi za mikono yetu ,ponya,huisha,simamia mipango yetu,ponya wagonjwa,na wanaopitia changamoto mbalimbali na Baba tunaomba tunayopitia yasitutenge nawe yatuimarishe na kufungua macho ya rohoni tuuone ushindi wetu.Tunaomba kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo
Amen

NAWATAKIA SIKU NJEMA MBARIKIWE
Amen

Ahsante sana mama mchungaji

Ubarikiwe
 
1044cd638b43766898ea0a71c0bb49f2.jpg
Aisee hawa wanasayansi
 
Katika dondoo za bbc

Mazungumzo ya Uingereza kujitoa katika umoja wa ulaya yanaendelea mjini Brussels, Ubelgiji

Tanzania yazindua Kamusi kuu ya kiswahili yenye maneno 45,000 yaliyopatiwa tafsiri tofauti na Kamusi nyingine

leo ni siku ya wakimbizi duniani.Kambi ya wakimbizi ya Dadaab ni kubwa kuliko zote ulimweguni na miezi iliyopita wakimbizi kutoka nchini somalia wamerejea nchini mwao ili kuanzisha maisha upya.

Tuelekee nchini Sudan Kusini ambapo kesi inayowakabili wanajeshi kumi na watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji na ubakaji wa wafanyikazi wa mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada, inaaza tena leo.

Makubaliano ya kusimamisha mapigano yamesainiwa mjini Rome Italia kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi ya waasi wa nchi hiyo.

Serikali Nchini Burundi imeanzisha kampeni ya kuwafundisha raia wake kuhusu sheria mpya inayo wakinga watu ambao wanafikwa na maovu au mateso kutokana na jinsi zao na pia adhabu zilizo andaliwa dhidi ya wahalifu hao

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramdhan unaoendelea, waumini wa kiislamu duniani hujizuia kula au kunywa kutekeleza ibada hiyo muhimu,Wanaspoti wa kiislamu huvumilia muda mrefu wa kutokula kukamilisha ibada hiyo.Je, wanaspoti hao hufanikiwa vipi kutimiza hilo
Hii ya kamusi niko nayo interesting nitaileta wote tuisome
 
Kwa vile huko anga za juu mazingira yake hayaeleweki, pengine mazungumzo ya kawaida yanaweza yasiwezekane. Teknolojia hii itasaidia sana katika mazungumzo ya binadamu katika sayari za mbali siku moja ukiachilia mbali kusaidia watu wenye matatizo ya kuzungumza hapa duniani (bubu, wenye celebral palsy na magonjwa mengineyo)
 
Kamusi Kuu ya Kiswahili yazinduliwa Tanzania
3002a82019f268b3b073be73f1193dfd.jpg


Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali yake inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa taifa na katika kulinda umoja wa kitaifa.

Ametoa kauli hiyo alipozungumza na wabunge, viongozi wa Serikali na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kamusi Kuu ya Kiswahili uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

"Serikali inatambua umuhimu wa lugha ya Kiswahili kwa ustawi wa nchi yetu na katika kulinda umoja wa kitaifa. Hakika lugha ya Kiswahili ndiyo inayotufanya tuwe Watanzania. Hivyo, tunaithamini na kwetu hii ni lulu na tunu ya Taifa," amesema.
578f1730386c723b03fb01149fcf4fc9.jpg

Waziri Mkuu katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake amesema uzinduzi wa kamusi hiyo unaenda sambamba na azma ya Serikali ya kutumia Kiswahili kwenye shughuli zote za kitaifa kama vile mikutano, mijadala, semina na ufundishaji shuleni.

Majaliwa amempongeza Rais John Magufuli kwa kuhimiza matumizi ya Kiswahili kwenye mikutano na matukio muhimu ya kitaifa, kama vile dhifa za kitaifa anazowaandalia wageni wake kutoka nje.

"Hata alipokuwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, Rais alitumia Kiswahili kuhutubia mkutano huo. Amekuwa akifanya hivyo, hata kwenye mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki lengo lake ni kuitangaza lugha hii ya Kiswahili," amesema.

Waziri Mkuu , amewasihi wazazi wahakikishe watoto wao wanapata kamusi hiyo kama moja ya nyenzo zao za kujifunza lugha ya Kiswahili."Ninashauri makundi mengine kama vile waheshimiwa wabunge, wanahabari, wakalimani, wafasiri, waandishi na wahariri wa vitabu, maofisa mawasiliano wa kwenye ofisi zetu, muone umuhimu wa kununua kamusi hii ili iwasaidie kujiimarisha kwenye matumizi ya Kiswahili fasaha na sanifu," amesema.

Awali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema Kiswahili ni lugha ya pili inayotumiwa na watu wengi zaidi barani Afrika lakini pia ni lugha ya 10 kati ya 6,000 zinazozungumzwa na watu wengi duniani.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita), Dk Seleman Sewangi amesema kazi ya kuandaa kamusi hiyo ilianza Agosti 12, 2011 na kukamilika mwaka 2015 na toleo la kwanza lilichapishwa.Amesema kamusi hiyo imekusanya maneno mengi makuu (vidahizo) kuliko kamusi zilizotangulia na kwamba ya sasa ina maneno 45,500.
 
WARUMI 8

37.Lakini katika mambo hayo yote tunashinda ;na zaidi ya kushindav,kwa yeye aliyetupenda.

38.Kwa maana nimekwisha kujua hakika kwamba ,wala mauti,wala uzima,wala malaika,wala yaliyopo ,wala yatakayokuwapo ,wala wenye uwezo,

39.Wala yaliyo juu wala yaliyochini ,wala kiumbe kingine chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu

Baba asante kwa upendo wako na kutuamsha salama ,tunashukuru kwa afya ,kazi ,familia na upendo usio mwisho tunajikabidhi mikononi mwako bariki kazi za mikono yetu ,ponya,huisha,simamia mipango yetu,ponya wagonjwa,na wanaopitia changamoto mbalimbali na Baba tunaomba tunayopitia yasitutenge nawe yatuimarishe na kufungua macho ya rohoni tuuone ushindi wetu.Tunaomba kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo
Amen

NAWATAKIA SIKU NJEMA MBARIKIWE
Amen

Asante kwa neno mama mchungaji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom