Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20170620-WA0006.jpg
 
Katika dondoo za bbc

Mazungumzo ya Uingereza kujitoa katika umoja wa ulaya yanaendelea mjini Brussels, Ubelgiji

Tanzania yazindua Kamusi kuu ya kiswahili yenye maneno 45,000 yaliyopatiwa tafsiri tofauti na Kamusi nyingine

leo ni siku ya wakimbizi duniani.Kambi ya wakimbizi ya Dadaab ni kubwa kuliko zote ulimweguni na miezi iliyopita wakimbizi kutoka nchini somalia wamerejea nchini mwao ili kuanzisha maisha upya.

Tuelekee nchini Sudan Kusini ambapo kesi inayowakabili wanajeshi kumi na watatu wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji na ubakaji wa wafanyikazi wa mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada, inaaza tena leo.

Makubaliano ya kusimamisha mapigano yamesainiwa mjini Rome Italia kati ya serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati na makundi ya waasi wa nchi hiyo.

Serikali Nchini Burundi imeanzisha kampeni ya kuwafundisha raia wake kuhusu sheria mpya inayo wakinga watu ambao wanafikwa na maovu au mateso kutokana na jinsi zao na pia adhabu zilizo andaliwa dhidi ya wahalifu hao

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramdhan unaoendelea, waumini wa kiislamu duniani hujizuia kula au kunywa kutekeleza ibada hiyo muhimu,Wanaspoti wa kiislamu huvumilia muda mrefu wa kutokula kukamilisha ibada hiyo.Je, wanaspoti hao hufanikiwa vipi kutimiza hilo
Asante kwa BBC nasubiri kuiona kamusi niitumie.

Uingereza umoja umewashinda kwanini

Mungu awasaidie wakimbizi duniani,na alete maridhiano Amani ipatikane makwao,ni kazi ngumu kuwa mkimbizi,kuanza maisha mapya mahali papya,kuwtengana na familia tunawaombea waliorudi kwao amani itawale pawe mahali pazuri na salama kuishi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom