Makapuku Forum

Aksante sana
 
1939 - Meli ya MS St. Louis iliyokuwa imebeba wayahudi takribani 900 inakataliwa kuingia jimboni Florida nchini Marekani hivyo inageuza kurudi Ulaya ambapo Wayahudi 200 kati ya hao 900 wanaenda kuuwawa katika magerezaya mateso ya NAZI.

Walikuwa ni wakimbizi,walikuwa wanakimbia Mauaji waliyokuwa wanafanyiwa na Hitler na genge lake la NAZI
Walifuata tartibu ikiwepo kuomba VISA lakini wakakaushiwa na Rais wa USA enzi hizo Franklin D. Roosevelt akisingizia mdororo wa uchumi (Great Depression)
Hivyo kujikuta meli inageuza na kurudi huko kwao na Hitler kufanya yake
.....
 
So sad. Ingefanywa na Rais wa Nchi nyingine sidhani kama wangemsamehe!!
 
Aksante Fundi wa music!!
 
Duh, watu walijua utani!!
 
1979 - Luteni Jerry Rawlings anachukua madaraka ya Kuiongoza Ghana mara baada ya kupinduliwa kwa Jenerali Fred Akuffo katika Mapinduzi ya Kijeshi.
Alikuwa ni rubani kikosi cha anga Jeshi la Ghana
Wakati anafanya mapinduzi Alikuwa na umri wa miaka 32 tu
Baadaye anafanya Uchaguzi ili kujihalalisha kuwa Rais wa kidemokrasia na akawa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya 4 ya Ghana
........
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…