Safari na Muziki
Ni usiku sasa hapa kwetu, lakini JF na hasa Makapuku ni kama himaya ya Muingereza enzi hizo. Unaweza kuta saa hizi ni saa sita mchana sehemu fulani na wote tumo humu humu Makapuku.
Jukwani humu leo kama tulivyoona kulikuwa na vioja, well, kuna kutukanana na sababu, lakini kama mtu anakuja tu anaanza kutukana basi ukimtukana utakuwa umempa heshima. Ila kwa namna tulivyowaaacha tumeonesha kweli humu si mahali pa mchezo mchezo. Asante kwetu.
Furahiday kama kawaida, siongei sana maana sichelewi kuandika yale ninayopenda kiukweli, In vino veritas, (kwenye mvinyo, kuna ukweli). Na maongezi mazuri ni pale mnapoongea wote lock zimeactivatiwa kiweekend.
Tumwangalie mpiga gitaa na muimbaji mzuri wa kiingereza Michael David Rosenberg almaarufu Passenger, mshindi wa Tuzo za Brit Award kwa wimbo 'Let Her Go'.
hebu burudika wakati naangalie utaratibu wa namna gani nitaondoka hapa maana sipaelewi elewi hapa nilipokaa.
Nikutakie wikend Njema sana na sitochoka kukwambia, Wewe ni Mtu Muhimu Sana Hapa Makapuku Forum. LLL
Nimemwangalia Passenger naye nimeona ana vidole sita au well, sijahesabu sawasawa. Wakati wenzangu wanaenda na visoda kufundishwa kuhesabu mimi nilikuwa nachunga tu mbuzi