Kifo - The Great Equalizer. Yaani hata uwe tajiri kiasi gani siku zako zikifika ni lazima uondoke tu. Waliobaki wataweka mbwembwe wee mara champagne, mara pesa, mara vito kama mafarao lakini you are dead!
Nimeona vimbwanga vya Ivan mume mwenza wa Mondi hapa. Yaani alikuwa anaagiza Fiji Water kwa ajili ya kuogea na alikuwa anadai ndicho kilichokuwa kinampa ngozi nyororo. Fiji Water inasemekana ndiyo maji safi zaidi duniani na kidogo ghali. Kachupa kamoja hako kanaweza kuuzwa mpaka dola 3. Imagine kujaza bathtub nzima tena mara tatu kwa siku. Ni kweli kula maisha kifo chaja. Apumzike kwa amani tajiri huyu kijana mwenye machachari!