Love balozii...Pamoja mdau
Mi nimezaliwa Kidatu kambini(ilivunjwa miaka ya1990 kugeuzwa kuwa Chuo Cha Kipolisi)
Hivyo nikiwa dogo nakumbuka kigaidi beaf,biskuti za jeshi,maharage ya kopo,kutibiwa hospitali za kijeshi n.k
Mambo ya JWTZ nayafahamu sana na wapo ndugu zangu waliorithi kazi ya msingi
Ila siku hizi hakunacha biskuti wala beef
........
Ni mkubwa kwangu kulingana na maelezo yakehahah eti kaka kwako
Kulikuwa na maduka ya jeshi(kantini) vitu bei chee,wajeda pia walikuwa wanapewa vitanda vya kukunja vya chuna vyenye spring,mablangeti n.kLove balozii...
Siku hiz ata bia za buku jero baraks kilwa road hupatiiii.
Ila tuyaachee kama yalivyo ...
Wajomba wamerudisha bei ya mtaaniLove balozii...
Siku hiz ata bia za buku jero baraks kilwa road hupatiiii.
Ila tuyaachee kama yalivyo ...
Kama utaki kwa hiari.... Subiri tukupige ya mkeka sasa.
Ndio hivyoAhaaaaaah
Siku hizi shedy anatuwekeaa story
Asante mkuu ShededeThe Little Magic angel
Sehemu ya tatu
Ndani ya Miami Beach
Ilipoishia
....
.....
.....
Kwa kuwa Chief Commander alijua kuwa anapambana na kiumbe asichokijua, kiumbe ambacho kinaaminika kuwa kimedondoka kutoka juu, aliwaza labda kiumbe hicho kinaweza kuwa alien; na kinaweza kuwa kiumbe cha ajabu na hatari. Alitumia ujuzi wa kijeshi kwa kujaribu kuwaambia wanajeshi wake wazime tochi pia wakae kimya. Alitaka kujua kama hicho kiumbe kinaona na kinasikia. Na kinatumia njia na silaha gani katika kujilinda? Hayo ndiyo yalikuwa mawazo ya haraka haraka ya Chief Commander McClaw.
Ukimya wa dakika tano bila kufanya chochote kile.sauti za watu waliokuwa wakiomba msaada zilisikika.
McClaw alilijua hilo alitambua fika kuwa watu wanaolia niwazi kuwa walijeruhiwa na kiumbe huyu ambaye mpaka sasa hawajajua ni nani?.
Haikuwa rahisi kuweza kujua nikiumbe gani sababu ya kiza kinene usiku ule.
McClaw alihisi labda kiumbe walichokuja kukabiliana nacho.
Kwa uweledi mkubwa alionao aliamua kufyatua risasi moja angani. lengo kujua kama kiumbe kipo maeneo hayo au kimeondoka?
Baada yakuona hakuna reaction yoyote ile iliyotokea aliaamulu kikosi chake kifanye upekuzi kwa kila kona ya Miami Beach.
Walifanikiwa kukuta miili ya watu 16 waliokwisha fariki na majeruhi 8.
McClaw alipiga simu hospital iliyo karibu na Beach hiyo.ilikuwa ni Mercy Hospital kuita gari ya wagonjwa kuweza kutoa msaada wa haraka kwa wahanga.
Majeruhi walikuwa na hali mbaya sana. Majeraha yao yalionekana ni kama yameunguzwa na moto mkali sana na sio risasi.
Hali hiyo ilimpa mawazo Chief Comander watu "wameunguzwa kiasi hiki na nikiumbe gani ambacho kinatumia moto kama siraha yake yakujikinga?"McClaw alikuwa akijiuliza
Alibaini wenda akawa ni Dragon au Dinosaur "lakini mbona wanyama kama hawa walitoweka dunia miaka mingi iliyopita"aliendelea kujiuliza bila majibu yoyote.
Alimwita kando Detective Kelvin Ago waongee kuhusu vita hii wasiyo ielewa.
"nimepigana na vita nyingi tokea nizaliwe lakini hii sijawahi kuiona"McClaw alifungua maongezi.
"Mkuu chakufanya hapa ni kuwa makini kwa kila hatua tunayopiga"Detective alijibu.
"hakika usiku umeingia sana pia nimechoka sana tukutane kesho asubuhi tupange mbinu mpya ya kupambana na hivi viumbe"alimpa maagizo kisha akapanda gari yake akaondoka.
Ndani ya San Francisco
Wakati Chief Commander anarudi nyumbani baada ya kazi ngumu ya usiku njiani gari yake ilipata tatizo(Jam)"shiiit"alilalama huku akishuka na vifaa kwa hasira hili alitengeneze.
Wakati anaendelea kulitengeneza uso kwa uso na kiumbe kinafanana kabisa na binadamu lakini ni kirefu(giant) sana na kinaonekana kuwa na hasira sana kanakwamba kimekula pili pili.
Je nini kiliendelea hapo usikose sehemu ya nne hapa hapa makapukuz
Ni vizuri akiendeleandio hii binamu aliniambia kawakatisha story haendelezi tena imekuaje tena anaendelea
ShukraniAsante mkuu Shedede
nilimiss habari za saa hivi haijaibiwa
Obe, makingilima na mahungulima tofauti yake ni nini
Hahaaa!Ni mkubwa kwangu kulingana na maelezo yake
Hivyo hakuna ubaya nilipomwita "kaka"
.......
Niko poa, Asante sana kwa ufafanuziPole mdau nimechelewa kujibu, hizi lugha za kibantu raha tupu, makingilima ni asubuhi sana/alfajiri na mahungumila ni jioni sana kabla ya usiku/machweo (kuna mawio na machweo, right?
Uko poa lakini?
Nalala sasa
Asante sana Obe ubarikiwe usiku mwema nimefurahia muziki ...asanteMuziki ni Kuwekeza.
Hivi kila ninapoandika haka kakipengele ni lazima nianze na salamu! Huna haja ya kujibu maana sijauliza swali. Habari za mihangaiko Makapuku wenzangu, najua wote tuko vema sana.
Ni tarehe moja na ndo inakatika, najua wapo ambao hawajarudi home maana mama/baba mwenye nyumba hajalala anasubiri kodi. Hongera kwa wamiliki wa nyumba wote mlio humu, na mtushukuru sana sisi wapangaji wenu tuliotulia tu humu, mngeitwaje baba/mama mwenye nyumba kama sio sisi? Heshima kwetu wapangaji 😀
Kiukweli leo niwe mkweli kwenu, sikupanga kuandika kitu kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Lakini kutokana na vitisho vya mjomba wangu lee empire kuwa nisipoandika atanitoa kwenye plan ya simu (kajiunga na jazwa ujwaze ya Tigo, kaunganisha line nne, anajazwa anatupunguzia salio sis family yake, ila uko makini kama makinikia kutofanya mchezo na Tanesco na plan yao ya 'acha kulipa,....., asante mjomba).
Kisa cha mimi kuandika leo ni 'matters of the heart' kwa sana na nikaona ana hoja ambyo siwezi kuipuuza, mimi sio mpuuzi. So, akaniambia sisi Makapuku ni family na mwenzetu anapofikwa na la kumfika iwe yeye mtu wake wa karibu nasi tukajua basi tunasema pole kwa pamoja. Na anapoondoka na kurudi basi tunafurahi kwa pamoja na ndicho ninachofanya leo kwa ajili ya Shunie nikiwajumuisha wote waliopatwa na ya kuwapata bila kupakatwa.
Kikawaida katika kuitafuta Furahiday huwa napenda kuweka kitu motomoto, kitu cha mikatiko kama si mitikisiko, praktaratumbaa. yeah, kitu Yondo sister na gitaa la Alain Nkounkou.
Lakini leo ninaweka kitu maalum kwa member wote wa Makapuku ambao kwa sababu tofauti waliondoka humu jukwaani na wamerejea tuko pamoja nao, karibuni na it is so good to see you back.
Nitamuelezea siku nyingine maana sitaki kuandika sana kuhusu yeye bali nakuacha ufurahie gitaa tamu na sauti nzuri toka kwa mkongwe Don Williams.
Karibu