Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki ni Kuwekeza.

Hivi kila ninapoandika haka kakipengele ni lazima nianze na salamu! Huna haja ya kujibu maana sijauliza swali. Habari za mihangaiko Makapuku wenzangu, najua wote tuko vema sana.

Ni tarehe moja na ndo inakatika, najua wapo ambao hawajarudi home maana mama/baba mwenye nyumba hajalala anasubiri kodi. Hongera kwa wamiliki wa nyumba wote mlio humu, na mtushukuru sana sisi wapangaji wenu tuliotulia tu humu, mngeitwaje baba/mama mwenye nyumba kama sio sisi? Heshima kwetu wapangaji 😀

Kiukweli leo niwe mkweli kwenu, sikupanga kuandika kitu kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Lakini kutokana na vitisho vya mjomba wangu lee empire kuwa nisipoandika atanitoa kwenye plan ya simu (kajiunga na jazwa ujwaze ya Tigo, kaunganisha line nne, anajazwa anatupunguzia salio sis family yake, ila uko makini kama makinikia kutofanya mchezo na Tanesco na plan yao ya 'acha kulipa,....., asante mjomba).

Kisa cha mimi kuandika leo ni 'matters of the heart' kwa sana na nikaona ana hoja ambyo siwezi kuipuuza, mimi sio mpuuzi. So, akaniambia sisi Makapuku ni family na mwenzetu anapofikwa na la kumfika iwe yeye mtu wake wa karibu nasi tukajua basi tunasema pole kwa pamoja. Na anapoondoka na kurudi basi tunafurahi kwa pamoja na ndicho ninachofanya leo kwa ajili ya Shunie nikiwajumuisha wote waliopatwa na ya kuwapata bila kupakatwa.

Kikawaida katika kuitafuta Furahiday huwa napenda kuweka kitu motomoto, kitu cha mikatiko kama si mitikisiko, praktaratumbaa. yeah, kitu Yondo sister na gitaa la Alain Nkounkou.

Lakini leo ninaweka kitu maalum kwa member wote wa Makapuku ambao kwa sababu tofauti waliondoka humu jukwaani na wamerejea tuko pamoja nao, karibuni na it is so good to see you back.

Nitamuelezea siku nyingine maana sitaki kuandika sana kuhusu yeye bali nakuacha ufurahie gitaa tamu na sauti nzuri toka kwa mkongwe Don Williams.

Karibu




Asante Binamu yangu ubarikiwe sana
 
Sijamsikia, itabidi nikae chini nimsikize, au kaniharibia! Maana huyu mjombaangu full matatizo si kaenda kumwambia BH kuwa tuliendaga kwa mganga wa kienyeji kuangalia nyota, huku akijua kabisa BH na wapiga ramli ni kitumbua na mchanga.
 
1/September 11 attacks
4492f209df9b7a082b7163b4f734323e.jpg
85eb17287ac636fa1cdb4f1df55c4008.jpg
0017238d93527e85b463a69794b3ffda.jpg

Hhi wala siandiki maneno mengi...kila mtu anajua alichokifanya Osama Bin Laden mwaka 2001 lakini mwisho wa siku akasakwa na kuuawa
Watu karibia 3k (2996) walifariki huku zaidi ya 6000 wakijeruhiwa
.
.
.
.
.
.
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane kesho
..........
Asante mkuu tumepata na kujikumbusha matukio haya
 
Mwaka huu ndo hivyo unapuyanga wapendwa. Tayari tumefikia nusu. Ati, malengo uliyokuwa umejiwekea kwa mwaka huu yanaendeleaje? Umeyakamilisha kwa asilimia ngapi?

Hata kama unajikongoja kama mimi, hakuna haja ya kukata tamaa. Bado nusu nzima inakusubiri. Rekebisha unapoona hapakwenda sawa hata kama ikiwa ni kupunguza muda wa kushinda hapa Makapuku, kuamka saa moja mapema zaidi n.k. Yote kwa yote mkumbuke na kumshukuru Mungu kwa yote, chapa kazi kwa bidii, endelea kutenda mema na mengine yote yatajitosheleza kwa wakati wake. Mbarikiwe sana!
a917790c44d235a8082fe1cf3a018561.jpg
 
Sijamsikia, itabidi nikae chini nimsikize, au kaniharibia! Maana huyu mjombaangu full matatizo si kaenda kumwambia BH kuwa tuliendaga kwa mganga wa kienyeji kuangalia nyota, huku akijua kabisa BH na wapiga ramli ni kitumbua na mchanga.
Bhinamu kipenz kwanza nikukumbushe ile simu uliyotaka ubadirishe ntaileta panapo majaliwa Mungu akijaliaa ...shaka ondoa

Asante kwa nyuzi ya leo make najua umejazwa vilivyo na bando za tigo na ni matumaini yangu ata BH umempigia kwa viber make nilikufundisha wasiwasi wangu sijajuaa kama ulikumbuka kuzima data make kila siku unadai simu inakata chaja haraka ...

Anyway mama mchuchu wala usiofu make imeandikwa samehe saba na 77 japo hesabu ya kuzidisha table sikumeza ilikuwa inaaishia 12..

Kuhusu kumwambia Mama mchuchu mambo ya mganga mbona ilikuwa zaman ata viroba havijakatazwa yawezekana nilikuwa nishafungua lock ...

Asante Mama mchuchu wa obe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom