Makapuku Forum

Makapuku Forum

Ni kweli. Hasa ukizingatia kuwa hapa hatujuani personally. Uungwana huu unaonyesha kuwa he is a man of integrity and character, no matter what. Na hii inazidi kulipa heshima jukwaa hili.

==> Siku nyingi sijaona maoni yako kwenye mijadala ya kisiasa na mingine hapa. Jana wakati nikijibizana na mme wake na Shunie kuhusu ustahili wa rais wa sasa kutuongoza nilitamani kweli uingilie. Pengine ni pilika pilika kwa sababu hata topiki yako ya muziki kuna wakati huwa unaiahirisha. Tuko pamoja and good night!


Heshima kwako mdau, siku zinakimbia sana.

Niliona mchango wako kwenye maswali ya lee empire , ulijibu ukiwa very objective sana katika hli ambayo hukutaka kuja na jibu la JPM anastahili au hastahili halafu wengine waanze kukulabel kuwa uko upande usio wao.
Ulinikumbusha enzi hizo nasoma sana makala za jenerali Ulimwengu enzi za Rai halisi.

Pilika pilika zinabana na ndo maana unaona kuingia ni usiku sana au makingilima (asubuhi sana😀), nchi imevaa jeans kwa hiyo ni mwendo wa kujipanga kweli kweli.

Siasa ni maisha, huwezi kuikwepa, utaikuta kila mahali hata faraghani, utaikuta. Nitakuwa nashirikishiriki inapotokea.

Asubuhi njema.
 
kwahiyo ulijua mm mtawa cuzoo
00ccedc5660082cd03d768f95bf413a5.jpg


Ahaaaaaaaah wewe kibokoooo sio kwa swali hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom