Makamanda Polisi Mikoa Arusha na Mbeya wateremshwa vyeo

Mkuu huyu mimi namfahamu kidogo ni mwongeaji kupita maelezo.Uzuri anajua nini tanzania ya leo wanachokihitaji. [pQUOTE=Mwita Maranya;3857773]Kwanini asichekecheke wakati kimepanda!?
Mpwapwa na Andengenye wametumika sana na ccm kuivuruga chadema lakini hatimaye nguvu ya umma imewashinda.

Sasa mumsubiri huyo Liberatus Sabas aliyekuwa Manyara muone kama naye atakuwa anatumiwa na magamba ama atakuwa mzalendo.[/QUOTE]
 
Issue sio Andendengenye! Hivi ile tume Igp aliyounda ya kuchunguza mauaji ya Arusha yalioongozwa na Ocd Zuberi itatoka lini? Au ndo imesahaulika coz Ocd ana refa? Huu ni utumiaji mbaya ya mali za umma! Inabidituombe kujulishwa ni kiasi gani kilitumika kwa tume zisizo na mrejesho na kujua kuna nini why ripoti inakuwa siri. Pia kama hamna majibu mazuri basi IGP awajibishwe
 
Polisi zamani walikuwa wana recruit Ma-WP wenye sura ngumu kweli! lakini siku hizi wanashindana na Lundenga kuchagua warembo.
Shughuli ipo!

Tehe tehe tehee. Kweli siku hizi polisi wanashindana na Lundenga!
Tatizo ni kwamba hivi viWP havifananii na upolisi ukikutana navyo mitaani. Vinajirusha clubs kwa kwenda mbele na vinavaa nguo za ajabu ajabu kiasi ambacho huwezi kujua kama jeshi la polisi lina nidhamu ya mavazi!
 
Kwenye hii thread watu wanaongelea dhuluma za polisi dhidi ya raia na hapo hapo wanaongelea kuwa RPC ni deal kwasababu kuna ulaji.

Hizi contradiction katika fikra zetu ndio zinatishia ile Tanzania bora ambayo wote tunaitaka.

Tatizo la TZ sio mtu mmoja mmoja bali mfumo mzima na culture ya sisi wananchi ya kufikiria deals badala ya kufikiria kazi na uwajibikaji.

Bila kuzingatia hayo tutaondoa Andengenye mmoja na kuleta Andengenye mwingine na tofauti pekee itakuwa sura na utii kwa wanasiasa tofauti.
 
Tuko pamoja kamanda.
Ninakubaliana na mapendekezo yako juu ya jeshi la polisi.
Observation zako ni za kweli hata recommendations zako zinaweza kuboreshwa kidogo kwa kuongezea na nyengine ili hatimaye tuwe na jeshi la polisi la wananchi wote wa Tanzania.

Nafiki kuna haja pia ya kulibadilisha jina, huenda kuitwa jeshi ndilo tatizo la msingi. Muda wote wanafikiria vurugu, kupiga virungu, risasi, mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Nadhani tuiite huduma ya polisi (Police service) kama ilivyo South Afrika. Kenya nao wamelibadili jeshi lao la polisi kuwa huduma ya polisi.

Ni kweli kamanda...mbaya zaidi tunaita police force.hilo neno force na lenyewe ni tatizo ndiyo maana mtu akikamatwa inakuwa kama vile vurugu.polisi wetu ni lazima wafunzwe ustaarabu na saikolojia.Tuko pamoja sana
 
Hivi ukiua wananchi unapandishwa cheo....

Crashwise,
Unakumbuka mauaji ya mahabusu katika gereza la mahabusu Rwanda Mbeya?

Unakumbuka mauaji ya wanacuf visiwani unguja na pemba jan 26 & 27, 2001?

Unakumbuka kashfa ya kamanda nzowa kumbambikia madawa ya kulevya mtoto wa Mengi?

Unakumbuka mauaji ya wananchi wa nyamongo?

Nadhani hadi hapo utakuwa umepata majibu ya swali lako.
 
Last edited by a moderator:
Andengenye hivi karibuni alikataza polisi kupiga watu mabomu hovyo. so it was expected

Na pia ushindi wa CDM Arumeru unaweza kuwa sababu pia. Maana alitakiwa kutumia propaganda za kipolisi kuhakikisha CCM inashinda sasa yeye akatenda haki.

Ila CDM wamwangalie huyu 2015 anafaa kupata highest post, kwani ni dhahiri kuwa aliyoyafanya Arusha hapo nyuma yalikuwa na shinikizo. Nafikiri Nchimbi kaanza kazi sasa. Ila aangalie watanzania wanazijua haki zao. Akianza kutumia polisi kama political weapon itamfanya JK awe mashakani sana kufika 2015 katika state iliyopo sasa. Tunaweza kwenda kwenye excited state very soon. Kazi ya polisi ni kuzuia uhalifu na kujenga harmone miongoni mwa jamii. Nadhani Andengenye alianza kujirudi na kuwa katika mstari.
 
Kwenye hii thread watu wanaongelea dhuluma za polisi dhidi ya raia na hapo hapo wanaongelea kuwa RPC ni deal kwasababu kuna ulaji.

Hizi contradiction katika fikra zetu ndio zinatishia ile Tanzania bora ambayo wote tunaitaka.

Tatizo la TZ sio mtu mmoja mmoja bali mfumo mzima na culture ya sisi wananchi ya kufikiria deals badala ya kufikiria kazi na uwajibikaji.

Bila kuzingatia hayo tutaondoa Andengenye mmoja na kuleta Andengenye mwingine na tofauti pekee itakuwa sura na utii kwa wanasiasa tofauti.

Mtanzania,
Enzi za IGP Mahita ilikuwa inasemwa wazi bila kificho kwamba ukipewa U-RPC ilikuwa lazima umjengee nyumba. Sasa unadhani fedha ilikuwa inatoka wapi?
Pamoja na kwamba mfumo ni mbovu lakini kuna baadhi ya individuals wana abuse mamlaka yao.
 
Last edited by a moderator:
Tehe tehe tehee. Kweli siku hizi polisi wanashindana na Lundenga!
Tatizo ni kwamba hivi viWP havifananii na upolisi ukikutana navyo mitaani. Vinajirusha clubs kwa kwenda mbele na vinavaa nguo za ajabu ajabu kiasi ambacho huwezi kujua kama jeshi la polisi lina nidhamu ya mavazi!

Kizazi hiki ndio kilivyo. Unataka waanze kutafuta wabaya wa sura ambao ni adimu?
Mavazi na muonekano vina mchango mdogo ktk utendaji na uelewa wa kazi.
 
Ha ha haaa. Nilikuwa nakaribia kushangaa kwamba Kimbunga hajatia maguu kwenye hii thread!
Huo ndio ukweli wenyewe mkuu lazima tufike mahali viongozi/maofisa wa juu wa jeshi la polisi watambue wajibu wao kwa wananchi. Wafanye kazi zao kwa weledi na miongozo ya jeshi la polisi, wajiepushe na kutumika kisiasa.

Mkuu Mwita Maranya mimi msimamo wangu ni vyombo vyetu vya usalama vifanye kazi bila upendeleo kwa kuwa nchi hii ni ya Watanzania si ya chama chochote cha siasa. Watu wanasema inabidi wawe na tujeshi twao kama green guards, blue guards ama red guards kwa kuwa vyombo vya usalama havifanyi kazi kwa weledi; hii ni hatari kwa ustawi wa usalama wa nchi yetu.
Pia mkuu naona haya mabadiliko yameenda sambamba na mabadiliko ya mawaziri wote waliokuwa wakishughulikia mambo ya usalama wa nchi yetu: Mwinyi, Vuai na Chikawe na wamekuja Vuai, Nchimbi na Mkuchika. Hii inaweza kuwa na ujumbe wowote juu ya utendaji wa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama?
 
Kimbunga,

Duh, mkuu Najua hapo kwenye red unanisema mimi.sijishtukii....lol
 
Mtanzania,
Enzi za IGP Mahita ilikuwa inasemwa wazi bila kificho kwamba ukipewa U-RPC ilikuwa lazima umjengee nyumba. Sasa unadhani fedha ilikuwa inatoka wapi?
Pamoja na kwamba mfumo ni mbovu lakini kuna baadhi ya individuals wana abuse mamlaka yao.

Mkuu Mwita Maranya na Mtanzania ni kwamba katika nchi hii ikiwa na madaraka ya kimkoa unakuwa fisadi kuliko wakurugenzi wako wa makao makuu. Kuna idara ukimwambia mkubwa wa mkoa aende makao makuu kuwa mkurugenzi unaweza kurogwa.
 
Last edited by a moderator:
Kimbunga,

Duh, mkuu Najua hapo kwenye red unanisema mimi.sijishtukii....lol

Mkuu Ben kwani wewe ni mkuu wa kajeshi mojawapo kati ya hivyo nilivyovitaja? Mkuu haya ni mawazo ya watu wwngi wanaounga mkono hivi vijeshi. Lakini hii ni reflection ya utendaji usio wa kieledi wa vyombo vyetu. Si hivyo tu hata hizi mob justice ambazo tunazipigia kelele kila siku zinareflect hali hiyo. Nadhani wenyewe wanalijua hili.
 
Last edited by a moderator:
Mi naona kama kapandishwa cheo,kapewa ukuregenzi utawala na rasilimali watu,anaweza kuwa IGP afta Mwema

Huenda ikawa kweli maana huyu kamanda alikuwa anasoma MBA pale SUA kabla hajahamishiwa Arusha. Na alipohamishiwa Arusha alikuwa bado hajamaliza. Manojua status ya MBA yake mtujuze humu jamvini.
 
Back
Top Bottom