Makamanda Polisi Mikoa Arusha na Mbeya wateremshwa vyeo

Mungi,
Taarifa za Andengenye kuandaliwa kuwa IGP zimezagaa sana mitaani hata kabla ya uteuzi huu. Lakini atambue kwamba hata kama atakuwa ameteuliwa kuwa IGP siku tukipandisha juu bendera ya ukombozi kwa mara ya pili basi hapo ni kama alivyofanya Rais Joyce Banda wa Malawi.

Mwita Maranya

Hqapo kwenye red sasa tumekuja kwenye ukurasa mmoja.thanks kamanda...hakuna compromise na vibaraka wote kwanzia sasa wajue hilo
 
Mwita Maranya,

ofcourse hatuna tatizo na Jeshi la Polisi na ni kweli polisi wengi wanatuunga mkono.Wale waliotumia madaraka vibaya ni lazima washughulikiwe hakuna suluhu hapa.Kuna wale marafiki zangu wanaopenda kunipaka kwamba nina visasi lakini hapa ni kujenga nidhamu ya Jeshi.Matumizi mabaya ya dola ni lazima yashughulikiwe.Naunga mkono anachofanya michael Sata Zambia.Na bado kazi inaendelea

Huyu hata akiwa IGP ni lazima awajibishwe kwa matumizi mabaya ya nafasi yake.joyce Banda alimtimua IGP kazi ndani ya masaa 72.Inatakiwa sasa 2015 watu kama hawa siyo kutimuliwa tu ni lazima washitakiwe.

Mkuu mi nadhani kumwajibisha IGP peke yake haitatosha pindi CHADEMA watakapochukua utawala wa Tanzania.
Jambo la msingi inatakiwa mfumo mzima wa jeshi la polisi ubadilishwe from the roots. Tukiwa na jeshi linalojitegemea, ambalo haliingiliani na siasa nadhani itakuwa bora zaidi.
Nina imani na CHADEMA, baada ya uchaguzi watafanya siyo tu reshuffle, bali kubadili mfumo ili uendane na mahitaji ya jamii!
 
Akili Mpwapwa leo asubuhi nilikuwa naye kumbe ndiyo maana alikuwa anacheka cheka!

Kwanini asichekecheke wakati kimepanda!?
Mpwapwa na Andengenye wametumika sana na ccm kuivuruga chadema lakini hatimaye nguvu ya umma imewashinda.

Sasa mumsubiri huyo Liberatus Sabas aliyekuwa Manyara muone kama naye atakuwa anatumiwa na magamba ama atakuwa mzalendo.
 
Mwita Maranya,

ofcourse hatuna tatizo na Jeshi la Polisi na ni kweli polisi wengi wanatuunga mkono.Wale waliotumia madaraka vibaya ni lazima washughulikiwe hakuna suluhu hapa.Kuna wale marafiki zangu wanaopenda kunipaka kwamba nina visasi lakini hapa ni kujenga nidhamu ya Jeshi.Matumizi mabaya ya dola ni lazima yashughulikiwe.Naunga mkono anachofanya michael Sata Zambia.Na bado kazi inaendelea

Huyu hata akiwa IGP ni lazima awajibishwe kwa matumizi mabaya ya nafasi yake.joyce Banda alimtimua IGP kazi ndani ya masaa 72.Inatakiwa sasa 2015 watu kama hawa siyo kutimuliwa tu ni lazima washitakiwe.

Mi nakubaliana nanyi kuwa katika jeshi la polisi, wapo waliofanya blanders na wanastahili kushitakiwa. But kwa Andengenye, history will tell that he was a clean person. Tena mi nadhani kuhamishwa kwake ni recommendations zilizotolewa na Mkuu wa mkoa Magesa, kwani ameshindwa kumtumia...
 
Kabla ya 2015? Kwani Mwema amekaribia sana kustaafu?

By the way, naona Andengenye anafaafaa mwenye hiyo nafasi, in case...

Kufaa angeweza kufaa kama hakuna interference ya siasa. ila kwa mazingira aliyoonyesha Arusha Andengenye hafai hata kuwa OCS, japo kielimu amemzidi IGP mwema.
Andengenye kwenye sakata la Arusha CCM walimtumia kama Salama Kondom. yaani kuna Kipindi hata Mary Chatanda akimtuma anakwenda kuwapiga raia kwa mabomu.
 
Ben,
Kimsingi jeshi la polisi kama taasisi haina tatizo na Chadema, na kwahiyo sisi kama chama cha siasa hatuhitaji kuwa na ugomvi na taasisi ya jeshi la polisi kwani ushahidi uko wazi kabisa kwamba askari polisi wengi sana wanatuunga mkono.

Lakini ni muhimu ijulikane kwamba kuna baadhi ya maofisa wa juu wa jeshi la polisi wanatumika vibaya na ccm, ama wao wenyewe kwa utashi wao wanajipendekeza kwa ccm hadi wanafanya vitendo vibaya dhidi ya wanachama wenzetu pamoja na chama chetu kwa ujumla. Hao ni lazima watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, punde tu tutakapoikomboa nchi hii toka katika ukoloni wa ccm.

Mkuu Mwita Maranya ulivyosema watashughulikiwa nikaanza kuogopa ila ulipoongeza kwa mujibu wa sheria nikafarijika!
 
Last edited by a moderator:
Kamanda ni kweli kabisa, kwani uchaguzi uliopita 2010 line polisi kituo walichopigia kura familia za polisi (Kituo cha Mount Meru Hosp. Arusha) CHADEMA walipata kura nyingi sana.
Kivitendo polisi hatuko nao, ila ukweli wanaunga mkono mabadiliko. Tatizo kwa Polisi na Jeshi lipo kwa viongozi wao!
hii nimeipenda;inaonyesha ni kwa namna gani polisi nao walivyombele katika harakati za ukombozi.
 
Ben,
Kimsingi jeshi la polisi kama taasisi haina tatizo na Chadema, na kwahiyo sisi kama chama cha siasa hatuhitaji kuwa na ugomvi na taasisi ya jeshi la polisi kwani ushahidi uko wazi kabisa kwamba askari polisi wengi sana wanatuunga mkono.

Lakini ni muhimu ijulikane kwamba kuna baadhi ya maofisa wa juu wa jeshi la polisi wanatumika vibaya na ccm, ama wao wenyewe kwa utashi wao wanajipendekeza kwa ccm hadi wanafanya vitendo vibaya dhidi ya wanachama wenzetu pamoja na chama chetu kwa ujumla. Hao ni lazima watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, punde tu tutakapoikomboa nchi hii toka katika ukoloni wa ccm.
Mkuu sin mengi ya kuongeza zaidi ya kusema thank you!kiukweli umenena vizuri sana,ukweli ni kua askari wengi wa jeshi la polisi hawaungi mkono kabisa hiki chama cha c.c.m,sema ni wachache tu hasa wale maafisa wa ngazi za juu,ndio wanaowasulutisha askari wenzao na kulifanya jeshi la polisi kuchukiwa na wafuasi wengi wa vyama pinzani,nina sema hivyo kwa kua mimi nina rafiki zangu wawili masajenti wasaidizi wa polisi huku Moro,mara nyingi uwa nakunywa nao muda mwingine mpaka kwenye kambi yao ya magareza ambayo ina Bar pale karibu na njia panda ya kilakala,wengi wao uwa wanaweka wazi hawaitaki kabisa c.c.m,ila uwa hawana budi kufuata amri za maboss wao wakubwa wachache
 
Last edited by a moderator:
Andengenye hivi karibuni alikataza polisi kupiga watu mabomu hovyo. so it was expected

Ni kweli, kwenye uchaguzi wa Arumeru alikataa polisi kutumia nguvu. this can also be the reason.
Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba kiongozi aliyepewa dhamana na mamlaka halali ya kulinda maisha ya watu ana kila sababu ya kupinga baadhi ya amri ambazo hazina manufaa kwa jamii.
We all know that the government is there for the people's interests!

Kwa mtu kama Andengenye aliyesoma sheria hakutakiwa kuamrisha polisi kutumia risasi za moto kwa watu ambao hawana hata jiwe mkononi.

Andengenye will never fit for IGP position!
 
Mwita Maranya

Hqapo kwenye red sasa tumekuja kwenye ukurasa mmoja.thanks kamanda...hakuna compromise na vibaraka wote kwanzia sasa wajue hilo

Ben,
Hakuna kitu kinanikera sana kama kushuhudia watanzania wenzetu ambao wamekabidhiwa jukumu la kulinda na kudumisha usalama wa raia na mali zao, kujitoa akili na kuua ama kujeruhi wananchi wasio na hatia ili tu kuwafurahisha wanasiasa.

Na kuwawajibisha si suala la kulipa kisasi bali ni kuhakikisha askari polisi pamoja na watumishi wote wa umma wanawatendea kwa haki na usawa wananchi wote bila kutazama mafungamano ya mtu kisiasa.

Wale wanaokuona radical achana nao. Kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa akitusisitizia mara kwa mara juu ya umuhimu wa mtu kuwa na ''Principles'' katika maisha. Whether ni nzuri ama ni mbaya hicho ni kitu kingine!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tuko inawezekanaje?

Mkuu Kimbunga huo ndo uhalisia. Mwaombeji alikuwa anatumpokea maagizo direct kutoka makao makuu Dar, na alitumia mwanya wa ugeni wa Andengenye (akitokea Moro) kutimiza matakwa ya akina Ridhiwani, kupitia kigogo mmoja hapo makao makuu (Kagonja). Baada ya Andengenye kuzoea ofisi alianza kufuata taratibu na juhudi za akina Kagonja kumtumia zimegonga mwamba. Kutokuelewana kulianza Andengenye alipoacha mikutano ya CDM ifanyike, kuanzia ule wa kuadhimisha mwaka 1 tangu mauaji, na mikutano mingine ikiwemo ya juzi baada ya Lema kushindwa. Ridhiwani, kupitia kwa Magesa akaamuru Andengenye aandikiwe 'taarifa mbaya' na kulazimu Mwema amuhamishie Dar...
 
Mungi,
Kipindi kile tulidanganywa Ooh Tibaigana anaandiwa kuwa IGP. Mwisho wa siku ola! Sasa leo na wewe unatuambia nini?

TUMBIRI wa JF

Mkuu we subiri utakuja kuniambia. Tunafahamu kuwa hafai kuwa mkuu wa kitengo kinacholinda maisha na mali ya watu, lakini kwa kuwa amejitahidi kulinda maslahi ya ccm Andengenye atakuwa IGP
 
OCD yupo chini ya RPC. Kama aliona Mwombeji amechemka alitakiwa kumwajibisha.

Na ndicho alichofanya Andengenye, na ndicho kilichosababisha ahamishwe... Kule mwanzo (wakati wa mauaji), Andengenye alikuwa na miezi michache sana tokea amehamia Arusha, so Mwombeji alitumia mwanya huo...
 
Asa,huu ni ufinyu wa mawazo wa mleta thread au,mbona huyo andengenye ni kama amepandishwa cheo vile,maana anaenda kuwa mkuu wa kitengo ndani ya jeshi la police,huoni ka mwenzio anazidi kupepea tu?
 
Mkuu Mwita Maranya ulivyosema watashughulikiwa nikaanza kuogopa ila ulipoongeza kwa mujibu wa sheria nikafarijika!

Ha ha haaa. Nilikuwa nakaribia kushangaa kwamba Kimbunga hajatia maguu kwenye hii thread!
Huo ndio ukweli wenyewe mkuu lazima tufike mahali viongozi/maofisa wa juu wa jeshi la polisi watambue wajibu wao kwa wananchi. Wafanye kazi zao kwa weledi na miongozo ya jeshi la polisi, wajiepushe na kutumika kisiasa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu we subiri utakuja kuniambia. Tunafahamu kuwa hafai kuwa mkuu wa kitengo kinacholinda maisha na mali ya watu, lakini kwa kuwa amejitahidi kulinda maslahi ya ccm Andengenye atakuwa IGP

Sijui unamfahamu Andengenye kiasi gani Mkuu. Ila kiukweli huyu jamaa nimemfahamu kwa muda aliokuwa RPC Morogoro, sidhani kama ana kasoro kuwa IGP...
 
Back
Top Bottom