Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,986
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 12,2022 na Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Pili Omary Mande aliyekuwa Afisa Mnadhimu namba moja mkoa wa Ruvuma anakuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi.
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marco Chillya ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi amehamishiwa mkoa wa Ruvuma akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Joseph Konyo ambaye amestaafu.
Aidha aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gaudianus Kamugisha amehamishiwa kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja, akichukua nafasi ya Kamishna Msaidizi wa wa Polisi (ACP) Abdallah Haji Seti aliyehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.