Makamanda Polisi Mikoa Arusha na Mbeya wateremshwa vyeo

Mungi,
Taarifa za Andengenye kuandaliwa kuwa IGP zimezagaa sana mitaani hata kabla ya uteuzi huu. Lakini atambue kwamba hata kama atakuwa ameteuliwa kuwa IGP siku tukipandisha juu bendera ya ukombozi kwa mara ya pili basi hapo ni kama alivyofanya Rais Joyce Banda wa Malawi.

Hivi utaratibu wa kumpata IGP hauna uhusiano na Seniority in Service?
 
Yeah ni lazima police force ifanyiwe marekebisho.polisi wetu wanatia huruma ila na wao wanajisahau kama wanapigika kama raia wengine.Niliwaambia polisi Geita kwamba wasikubali kutumiwa na mabosi wao vibaya.Waige mfano wa wenzao Misri

Niliwaambia waone haya kutumiwa na wakubwa zao vibaya kuumiza watanzania wenzao huku wao waki-share bunduki na risasi(vitendea kazi).the guys are hustling for real....


Problems of the Tanzania police as i see them;

1.Employing of illiterate (poor communicating skill= poor understanding= poor implementation of directives)
2. indiscipline (the police is made up of persons that have questionable character and have very little respect for the rule of law)
3. No clear guideline (when arresting or releasing a person)
4. Poor handing of equipment and guns (have a close look at the vehicles allocated to the police and compare them with Army, custom civil defense etc)
5. poor welfare (not salary increase)

Likely solution (just a few)

1. Training to be handled by expatriates (General training on handing of guns and rule of engagement, character, dressing, presentation etc)
2. weeding out (those that fail to meet up with the standard required of the job be move to other less demanding job such as prison service, fire service or show the way out)
Ben .... kwenye red .... unaonaje marekebisho ya katiba yakaanzia hapo ....instead of Tanzania Police Force ikawa Tanzania Police Service
 
Last edited by a moderator:
Niliwahi kuopoa mrembo Triple A, baada ya siku chache nilikamatwa na traffic nikamkuta demu yupo traffic central
Tehe tehe tehee. Kweli siku hizi polisi wanashindana na Lundenga!
Tatizo ni kwamba hivi viWP havifananii na upolisi ukikutana navyo mitaani. Vinajirusha clubs kwa kwenda mbele na vinavaa nguo za ajabu ajabu kiasi ambacho huwezi kujua kama jeshi la polisi lina nidhamu ya mavazi!
 
Baada ya kusoma michango ya walionitangulia, inaonekana kwa ujumla Andengenye ana udhaifu/matatizo ya kiutendaji. Kwa hiyo ktk dhana na utamaduni wa (ccm/serikali) kulindana tatizo badala ya kushughulikiwa aidha linahamishiwa kwingeneko au linaahirishwa.

Ben kaainisha baadhi ya kasoro. Niongezee kuwa kasoro kubwa ziko:

1) Ktk sheria mama yaani katiba haisemi na kulazimisha kwa uwazi mambo kama (haki, wajibu, mipaka na adhabu) kwa kila raia (of coz polisi nao ni raia na wanapaswa kuwa chini ya sheria mama).

2) Kasoro ya pili kubwa iko ktk sheria za muundo wa jeshi lenyewe na hapo naanzia mafunzo mpaka teuzi za viongozi. Nyingi zililenga kukisaidia chama (ccm) kushika hatamu. Kwa ufupi sheria na mitaala yao imepitwa na wakati, na hazifai kutumika ktk mazingira ya sasa au yajayo.

3) Uwezo (autonomous) ya PT. Polisi iko chini ya Wizara ya mambo ya Ndani, na mara nyingi madudu yao yanaishia humo humo ndani!
Polisi inazo kashfa na kesi kibao za uhalifu, mauaji nk lakini hakuna uwazi mfano external overseer body to balance. So wakitekeleza amri za mabosi zao wa kisiasa wanajua mwisho wa siku hakuna atakayewawajibisha.

4) Tuweke kigezo cha mwenendo ktk usaili wa wanaoomba kujiunga na jeshi. Kwa makusudi naweka sifa ya tabia/mwenendo juu ya sifa ya elimu kwa sababu unaweza kuwa na jeshi/askari highly intellectual but equally undisciplined na hapo ukawa na matatizo ya aina nyingine kabisa.

5) Jeshi lolote hupimwa kwa utii na ufanisi wake. La kwetu utii ni kwa wanasiasa (hasa ccm) na ufanisi ni almost zero. So livunjwe liundwe upya kabisa!
 
Yule rpc aliyesababisha matatizo makubwa huko arsha kwa ajili ya kujikomba hatimaye amehamishiwa kwenye kitengo kipya makao makuu ya polisi dsm. Nafasi yake imechukuliwa na rpc liberatus anayetokea manyara kuja hapo arusha. Ni matumaini kuwa liberatus kama jina lake lilivyo atakuwa liberal na kutenda haki

source: Magazeti mengi ya leo jumapili
Mapolisi wote hwatofautiani, wote hutekeleza amri za CCM!
 
Yule rpc aliyesababisha matatizo makubwa huko arsha kwa ajili ya kujikomba hatimaye amehamishiwa kwenye kitengo kipya makao makuu ya polisi dsm. Nafasi yake imechukuliwa na rpc liberatus anayetokea manyara kuja hapo arusha. Ni matumaini kuwa liberatus kama jina lake lilivyo atakuwa liberal na kutenda haki

source: Magazeti mengi ya leo jumapili
Karibu jirani, kamanda liberatus,makamanda wa arusha si unajua tena ukiwapa ulinzi mambo yote poa...lakini mabomu ya machozi Lo!ni manukato kwao wataibuka kila kona,muulize adengenye.. hasa hasa rafiki yetu zuberi atakupa briefing....karibu,tushirikiane kujenga A town
 
mwema.jpg


SIKU mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko ya Baraza lake la Mawaziri, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema amefanya mabadiliko makubwa ya makanda wa Polisi Tanzania Bara na Zanzibar. Habari ambazo Mwananchi Jumapili inazo, baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa ama wamehamishiwa mikoa mingine au kurudishwa makao makuu huku maofisa wengine wakiteuliwa kuwa makamanda wapya. Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Advera Senso alisema jana kuwa mabadiliko hayo ni ya kawaida katika kuimarisha utendaji ndani ya jeshi hilo, pia kutekeleza maboresho (reforms) yanayoendelea kufanywa.

Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) wa Arusha,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Thobias Andengenye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Utawala na Rasilimali, Polisi Makao Makuu na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa RPC Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Liberatus Sabas.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Adolfina Chialo amehamishiwa Makao Makuu ya Upelelezi (CID – HQ) na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ilala, ACP Fautine Shilogile.

Mabadiliko mengine yamewagusa RPC Kilimanjaro, SACP Absalom Mwakyoma ambaye amehamishiwa mkoani Mara akibadilishana na
RPC Mara, ACP Robert Boaz ambaye amehamishiwa mkoa wa Kilimanjaro.

Senso alisema
RPC Ruvuma, SACP Michael Kamuhanda amehamishiwa mkoani Iringa kuchukua nafasi ya ACP Evarist Mangala ambaye amehamishiwa mkoa wa Shinyanga, wakati aliyekuwa kamanda wa Shinyanga, ACP Diwani Athumani amehamishiwa mkoani Mbeya kuendelea na wadhifa wake huo.

Aliyekuwa
RPC Mbeya, ACP Advocate Nyombi amehamishiwa Ofisi ya Upelelezi Makao Makuu katika kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini huku aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Ferdinand Mtui akiteuliwa kuwa mkuu wa kikosi hicho nchini, kuchukua nafasi ya SACP Anaclet Malindisa ambaye anastaafu.

Makamanda wa Polisi wapya wa mikoa walioteuliwa na mikoa yao kwenye mabano ni aliyekuwa Ofisa Mnadhimu mkoani Arusha, ACP Akili Mpwapwa (RPC Manyara), aliyekuwa
Ofisa wa Opareshini Mwanza, ACP Philipo Kalangi (RPC Kagera) aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Arusha, ACP Leonard Paul (RPC Geita) na aliyekuwa Ofisa Mnadhimu mkoa wa Dodoma, ACP Furgence Ngonyani (RPC Njombe).

Wengine ni Ofisa wa Oparesheni Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Marieta Minangi (RPC Ilala), ACP George Mwakajinga aliyekuwa Ofisa Mnadhimu Lindi anakuwa RPC Lindi, ACP Linus Sinzimwa kutoka CID Makao Makuu anakuwa RPC Singida na ACP Salum Msangi pia kutoka CID Makao Makuu anakuwa RPC Simiyu.

Senso alisema Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Kimataifa Makao Makuu ACP Dhahir Kidavashari anakuwa RPC Katavi, RCO Mwanza, ACP Deusdedith Nsimike anakuwa RPC Ruvuma, ACP Saada Juma Haji ambaye ni Ofisa Mnadhimu Ilala anakuwa Kamanda wa Kikosi cha Reli Dar es Salaamn na Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Arusha, ACP Amir Konja anahamia Dar es Salaam kuendelea na kazi hiyo.

Walioteuliwa kuwa wakuu wa vikosi vipya ni ACP George Mayunga kutoka CID Makao Makuu anayekuwa mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Mazingira, kikosi cha Ulinzi wa Watalii kitaongozwa na ACP Benedict Kitarika kutoka Kitengo cha Sheria na Utafiti Makao Makuu na ACP Deusdedith Katto kutoka Oparesheni Makao Makuu ataongoza Kikosi cha Ulinzi wa Migodi ya Madini.


Senso alisema mabadiliko hayo pia yamevigusa vyuo vya polisi ambapo aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam, SACP Elice Mapunda ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mafunzo Polisi Makao Makuu na nafasi yake kuchukukiwa na Mkuu wa Chuo cha Kidatu, ACP Ally Lugengo.

Mkuu wa Mafunzo katika Chuo cha Polisi Moshi, ACP Nasser Mwakambonja amehamishiwa Kidatu ambako anakwenda kuwa Mkuu wa Chuo hicho wakati aliyekuwa Mkuu wa Mafunzo SACP Abdulrahman Kaniki ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Utafiti cha Jeshi hilo.

Senso alisema maofisa wanaotarajiwa kustaafu utumishi wao ni Mkuu wa Mafunzo wa Kitengo cha Sheria na Utafiti, SACP Donald Kaswende na baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.

Makamanda hao na mikoa yao kwenye mabano ni SACP Henry Salewi (Kagera), ACP Sifueli Shirima (Lindi) SACP Celina Kaluba (Singida) na Mkuu wa Usalama Barabarani Kada Maalum ya Dar es Salaam, ACP Vitus Nikata.
 
Yawezekana ni agizo toka juu kwa Mkulu, maana makamanda hawa wa polisi wamelitia doa taifa na kumwaibisha mkulu.
 
Kwa Andengenye amepata "promotion" na sio "demotion" manake anaenda HQ kuchukua kitengo cha Utawala
 
Kwa Andengenye amepata "promotion" na sio "demotion" manake anaenda HQ kuchukua kitengo cha Utawala

Hiyo ni demotion by promotion. Ukiwa mkoani una mengi ya kupata na unaonekana mtawala. Lakini makao makuu kuna wa kupitia saluti na kuitikia shikamoo. Sawa na wafanyakazi wanaopenda zamu za usiku wakati uongozi haupo, lakini zamu za machana uongozi unazungukia sehemu za utendaji mara nyingi hukosa raha.
 
huyu mwema nae yuko kama bosi wake...anawabadilisha watu kazi badala ya kuwapiga chini..wafukuzeni kama utendaji wao mbovu alafu wale wa chini wawe promoted...mtu anakua kamanda wa polisi miaka 30 hii inazuia hata developments za wale maofisa wa chini kwa sababu huko juu mijitu inavoronga na haisimamishwi...:mad:
 
hivi kamanda ntobi yupo wapi siku hizi.....?
amesitaafu yuko nchini marekani kwenye mapumziko baada ya kulitumikia taifa lake kwa makini sana mara na arusha hawatamsahau milele alivyonyoosha mikoa hii na baada ya kutoka ujambazi umeibuka tena. Kama mara kuna vikundi vinajiita:-
  • mdomo wa furu
  • jamaika mokasi
 
Kichwa cha habari kinatueleza Uongo, hakuna waliyeteremshwa Vyeo

TAFADHALI REKEBISHA HIYO TITLE YAKO
 
Back
Top Bottom