Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Rose anapita kwenye moto Mkubwaaa..

Kuna mahojiano kwenye gazeti flani anasema matatizo yalianza baada ya kiongozi Mkubwa flani kumtaka kingono, hiyo ilikuwa baada ya kumsaidia kurekodi nyimbo, alipokataa ndio zikaanza tuhuma za utapeli.

Anasema anakamatwa na polisi anapigwa hadi anazimia akiwa hapo Dodoma, mtu huyo Mkubwa anaushirikiano na viongozi wa dini, kashfa zikaanza, Mara katoa mimba n.k

Waliposhindwa zikaanza vita ya nguvu za Giza, kwanza akapata ajali kubwa akapona, akaumwa na joka kubwa nadhani hadi sasa ana bandeji,

Waliposhindwa magonjwa yakaanza yasiyoonekana hospitali...

Lakini vipigo vya polisi ndivyo vilivyomfanya akimbie nchi
Daa kama ni kweli Mungu amkumbuke
 
Unachosema ni kweli lakini Rose alikuwa mwislamu, hajui misingi ya ukristo, kakutana na wanaojinufaisha tu kwa mgongo wake, hajawahi kupata mafundisho ya ukristo achilia mbali wokovu, kakutana na upentekoste njaa ambao unaokoka asubuhi, jioni umejaa Roho kesho unaenda kuhubiri.

Ila Nina hisia mbaya kuwa wewe ni miongoni mwa maagenti wa devil, MNA mission ya kuangusha wote waliosimama katika Kweli kama alivyokuwa Rose, na sasa mnachekelea kwamba " mission accomplished " . umeleta mada hii kumdhihaki...

Andiko linasema, " usifurahi ee adui yangu niangukapo nitasimama tena"

Sasa mnamvua nguo na kumtoboa macho kama Samsoni, lakini najua mwisho wake utakuwa Mkuu kuliko mwanzo wake.
Yaani wanamdhiki hawajui kwanini yupo mpaka sasa, Mungu anamakusudi gani naye, pole yake dada Rose
 
Mkuu Mshana Jr! Nimefurahi kukucheki hapa kwenye mambo ya injili,nimezoea kukucheki kwenye: 'Mada maalum kwa walevi na wanywa pombe'...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mimi ni future pastor
 
watu wa Mungu lazima tubebe LAWAMA kwenye hili. HAIWEZEKANI siliha ya kumsifu Mungu wetu inaangamia watu tupo kusubiri kutoa hukumu badala ya kumsaidia. Biblia inasema chukuliananeni kwa upole. yaani mpaka anafika hatua hiyo watu tupo tu !
Ndiyo binadamu wasasa tunawazidi hata mafarisayo wa kipindi cha Yesu Kristo
 
shida ya nabii ilikuwa kutapa watu zaidi baada ya Dada yetu kupona. Lakin ukiangalia kwa jicho LA rohoni Dada yetu anashida ya kisaikolojia tu na pengine si ya kiroho(mapepo). Kwani yeye mwenyewe tayari anajua ujumbe wa mapepo.
 
Chonde chonde waimba injili, msitamani kuingia siasani. Injili haitaki uchafu wa siasa. Injili iko juu ya siasa. Siasa zina rafu kushindana na washindani. Kuiga wanamuziki wa kidunia waliopenya siasani kwa kutumia miziki yao ni tofauti muimba injili kufanya hivyo. Injili ni utakatifu haitaki kuchanganywa na siasa moja kwa moja. Wanasiasa waache kuwatumia waimba injili kwenye matukio yao ya kisiasa watawaharibu vibaya karama zao.
Hakika
 
Hivi Rose Mhando si alikuwa na management yake?? Imekuwaje Management ambazo zilikuwa zikinufaika na Uimbaji wake zimuache atumbukie kwenye hayo madhira??

Pole nyingi kwake, ingawa kuna umuhimu wa kujifunza kwa Bahati Bukuku ambaye tangu ameanza kuimba Gospel sijabahatika kusikia skendo chafu kumuhusu ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.
Mungu aendelee kumpigania hasa kwenye hiki kipindi kigumu anachopitia( Zaburi 23).
Msama alimchoka kwa utapeli wake,kilichomlostisha Rose ni kutoaminika na Mapromota!Hata hiyo issue ya Polis asimsingizie Kigogo yeyote itakua alikula hela za Show na akuonekana ndio akapelekwa Polisi
 
Bado ni wadogo zetu kwa mbali ila walituokoa sana kipindi kile cha mapito
Walituokoa sana kwa kweli maana tulikuwa tunaishi na madukuduku yetu moyoni pasipo pa kuyasemea, lakini ujio wa Jf ndani ya Kenya talk ilitufanya kutua mizigo iliyokuwa imetuelemea vifuani
 
Sehemu moja nilipojua hakuna ukweli ni pale kisket alichovaa kupanda juu huku pepo likiwa limeshapanda akawa anashusha ile sket namanisha anajifunika vizur

Ukiwa na pepo huwi vile, na kilichofanyika unakua huna kumbukumbu nacho kabisa tena kama ni kustiriwa vzr wanakustiri wanaokusaidia kuondoa hilo pepo

Hapo ndio nikajua hamna kitu ni kiki
Hii ndio point ya msingi kuelezea kwamba kweli dada Rose ametuchezea. Nilishangaa kumuona anabana miguu ili asikae uchi na kuishusha sketi yake!!
 
Me nmeiangalia ile crip Mara mbilimbili adi nikabaki najichekea mwenyewe.kila kama kaka Mkubwa nawe umeliona ilo basi Niko sawa na tunaenda sawa
 
Back
Top Bottom