Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Kila jambo lina asili
Akiwa kwenye ngazi za kuelekea mafanikio, akaanza taratibu kuacha kutunga na kuimba nyimbo zenye uchaji, akaanzisha style ya kucheza kidunia na nyimbo zisizo na uvuvio wa kimungu, ikawa sasa ni kama bongo fleva yenye mashairi ya dini
Hapa ndio shetani alipewa nafasi ya kuketi barazani kwake... Kipenga kikapulizwa kwa kashfa za ngono... Shetani huanzia hapo, baadae starehe (tuhuma za kutumia madawa ya kulevya) halafu ikaja kutojali na utapeli.... Mpaka kufikia hapa shetani alikuwa keshamaliza kazi
Yaliyofuatia yote yalikuwa ni finishing tu mkuu wa anga amteke mazima... Na kuangukia mikononi mwa hawa madalali wa shetani kwa jina la unabii... Kazi imekamilika
Ajaye baada ya sasa ni Rose wa kuhangaika kwenye makanisa ya hawa manabii na mitume... Na kila atakapofika atatolewa mapepo yasiyotoka.. Yakisikia pepo toka, yanacheka na kujificha yakinyuti kimya kabisa... Kwakuwa yanafahahamu mchezo wote hayana pressure
Unachosema ni kweli lakini Rose alikuwa mwislamu, hajui misingi ya ukristo, kakutana na wanaojinufaisha tu kwa mgongo wake, hajawahi kupata mafundisho ya ukristo achilia mbali wokovu, kakutana na upentekoste njaa ambao unaokoka asubuhi, jioni umejaa Roho kesho unaenda kuhubiri.

Ila Nina hisia mbaya kuwa wewe ni miongoni mwa maagenti wa devil, MNA mission ya kuangusha wote waliosimama katika Kweli kama alivyokuwa Rose, na sasa mnachekelea kwamba " mission accomplished " . umeleta mada hii kumdhihaki...

Andiko linasema, " usifurahi ee adui yangu niangukapo nitasimama tena"

Sasa mnamvua nguo na kumtoboa macho kama Samsoni, lakini najua mwisho wake utakuwa Mkuu kuliko mwanzo wake.
 
Wasalam waleikhum..!

Kidogo tumepumzishwa kwenye zile sinema zetu.... Tumepata msimu mdogo wa mwanadini muimba nyimbo za injili mwanadada na mama wa watoto Rose Muhando.

Hii inaweza kuwa mada ya NNE kumhusu... Japo nyingine zilizotangulia zikimjadili Rose wa sasa kama celeb na kile kinachomtokea...

Kwanza itambulike kuwa hii ni vita ya kiroho, falme za giza dhidi ya falme za nuru, wakuu wa mbingu dhidi ya wakuu wa anga...

Rose ni catalyst tu katika vita kubwa ya kiroho na ya kidunia... Nuru dhidi ya giza... Alikuwa jemadari msimu wa kwanza akapambana vilivyo, akazishinda falme za giza katika maeneo mengi.. Lakini kwakuwa ana mwili wa damu na nyama, alilemewa... Akazidiwa akampa adui nafasi... Sasa anatengenezwa...!

Rose Muhando ni nani?

Kwa wale waliobahatika kusoma habari zake huko nyuma... Aliingia kwenye uimbaji wa nyimbo za injili akitokea kwenye ndoa iliyojaa mateso (kwa mujibu wake) akiwa na karama ya uimbaji na mahitaji ya nyakati kumbeba aliibuka kuwa mmojawapo wa nyimbo za injili mwenye kipaji na mafanikio mengi... Lakini mafanikio yake yalikuwa kwenye hatari kubwa kwakuwa aliyapata kwa kupambana na shetani (kimtazamo)

Kuna wakati tunaweza kusema kwa hakika Rose alikuwa mlokole kamili na nyimbo zake zikiwaokoa na kuwabariki wengi....

Misukosuko ilipoanzia

Zaburi ya 23 kuna mstari unasema... Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti....! Kila mmoja wetu ana mapito yake ... Hata waimbaji wenzake walishapitia anayopitia... Si wa kwanza yeye na hatakuwa wa mwisho... Shida iko hapa, je unapopitia kwenye mapito unasimama upande gani? Wa nuru au giza? Anguko lako ama kusimama tena vitategemea ulikuwa upande gani... I mean upande gani uliupa airtime kubwa....! Ni wazi Rose alipojaribiwa aliingiwa na upofu na kumpa Mungu wake kisogo akaenda kufanya kolabo na upande wa giza... Sasa anasulubiwa.. Msimu huu wa pili anamsaidia adui.. Na huu ndio ushindi uliokuwa unatafutwa na falme za giza

Imekuwaje aibukie Kenya?

Kwanza kiuhalisia Rose ni kweli kabisa anaumwa na hayupo sawa.. Ni kama mwaka sasa tumekuwa hatusikii habari zake nzuri.. Amepitia mapito mengi, amechapwa akachapika.. Anaonekana live ana POP mkononi vidonda na makovu.. Na kwa maneno yake mwenyewe kwa takriban siku 90 alikuwa hajui anatoka wapi anaenda wapi... Amekuwa kama chizi fresh, zinatoka zinarudi... Alifikaje Kenya kwa hali ile? Alipelekwa? Alifikaje kwa yule mtume nabii?
Kisanga kinaanzia hapa!

Dunia ya leo watu hupenda kuyatumia matatizo ya wengine kujinufaisha ama kuwatumia wao wenyewe pia...

Rose Muhando ni jina kubwa Afrika mashariki. Habari zake zikisikika popote ndani ya jumuiya hii si jambo geni

Mtume na nabii kwa kuiona fursa... Anamuahidi kumsaidia Rose kwa masharti hasa la kutaka amuombee mbele ya waumini wake kukiwa na camera zinazochukua video na picha.. Lakini la zaidi anamfundisha cha kuongea..

Nimeangalia kwa makini video ile.. Sijui misa ilianzaje lakini anaonekana mtumishi wa Mungu akimwita Rose aliyechoka na kuanza kumuombea.

Ghafla Rose anaanguka na mapepo yanaaza kuongea kuwa kuna wivu juu ya mafanikio yake, hawataki aimbe, wamechukua magari yake wanataka kumuua nknk... Lakini ni wakati huu mapepo yakiongea Rose ana ufahamu wa kuondoa mkono wa mtumishi mdomoni mwake aweze kuongea vizuri....

Baada ya maombi mafupi mapepo yanatimka na hapo hapo Rose anazinduka na kuanza kuongea yaleyale yaliyokuwa yakiongelewa na mapepo... Halafu anaendelea kuelezea changamoto za familia yake, watoto kukosa ada nk.. Halafu anamalizia kwa kumshukuru Mungu...

Rose, Mungu hadhihakiwi... Mapepo hayatoki kivile na fahamu hazirudi kivile.. Nguvu ya pepo kutoka si ya kitoto (nitaelezea kwenye mada nyingine)

Umetumika vibaya kwenye mapito yako... Angalia wanaokutumia wasikuongoze kwenye anguko kuu

Mshana Jr Jana nimeangalia ile Video my thoughts were 100% like whatever you have written here

Ila kiukweli huyu mama anatia huruma sana
 
[emoji15][emoji848][emoji848] [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha hii mada mshana jr ni agent wa shetani?
 
1. Hii hutokea kwa mwanamke ambaye ni single au ameachika

2. Atajishughulisha na kuwa na miradi mikubwa na mafanikio

3. Wasaidizi wake wengi wanakuwa vijana wa kiume tena

4. Huyu mama alikuwa mwimbaji maarufu

5. Ma dancer au ma stage show ambao wlikuwa wananogesha muziki wake wa kasi ambao huwezi kuucheza ukiwa na akili timamu bila ya kuwa na kamzuka fulani ni vijana wa kiume masela wa mtaani

6.Yawezekana na ukiangalia video zake wale vijana walikuwa kawaokota mtaani watumia ndumu ama ngada.

7.Yawezekana aliwauliza ni nini sababu za kuchangamka ama walikuwa wanamuomba fedha boss wao huyo kabla ya show ili waondoe nishai na kweli baada ya kuwapatia stim stage iliwaka moto

8.Yawezekana akapatikana mmoja akawa karibu na boss zaidi na zaidi na mahusiano na kumfundisha boss wake naye kuondoa soo kabla ya kupanda jukwaani..

9. Yawezekana boss kwa ukaribu na kijana wake wa shoo naye akajaribu ili waende sambaba

10. Yawezekana boss akawa addicted mpaka kila kitu sasa kimeharibika
 
Mshana Jr Jana nimeangalia ile Video my thoughts were 100% like whatever you have written here

Ila kiukweli huyu mama anatia huruma sana
Yuko kwenye mateso makali na setbacks za maisha... Na ni katika kipindi hiki shetani hujiinua na kuidhihaki imani na misimamo yako huku akijifanya rafiki mwema sana kumbe rohoni anashangilia ushindi na kukukebehi sana
CC: nabiidaniel
 
kwanini binadamu tunafikiri au kuwaza kwamba kuna ufalme mwingine unapambana na Mungu?
Huyu huyu aliyeziumba mbingu na nchi? huyu huyu aliyetengeneza na kufanya kila kitu katika uso wa nchi?
Lazima tunamatatizo ya kimtazamo pia hatupendi kuwaza zaidi ya hadithi tunazopigiwa na wajanja janja....
Tuwe serious japo kidogo.
 
Soma habari za Lucifer, kisha kasome kitabu cha ufunuo... Haya ni mambo ya kiimani si kila mmoja anaweza kuelewa
 
Uhujumu uchumi ndio nini?
Ni mambo ya kutembelea nyota za watu na watu hawajui kama zina expirations date walahi
Maana lazima zitarudi kwa mwenyewe tu walahi
Na watu wa sanaa nao pia wamo katika ilo wimbi. Sasa hivi naona kibao kimegeuka, kina wema wako hoi, wafanya biashara nao hoi walahi
Yusuf Manji na wengine ingekuwa sio rahisi waingie kwenye msukosoko, lakini sasa wako uchi tunaona wazi mambo yao ya kuhujumu nchi yetu walahi
Zamani tulikuwa gizani lakini sasa MAMA TANZANIA ameamka na hasira kuu kwa maadui zake na baraka na rehema kwa wanao mpenda kwa dhati walahi
 
Nimeangalia video Ile ya dakika Saba, lakini kuna kitu kimenishangaza sekunde ya 26 akiwa tayari pepo limeshika fahamu zake, ameweza kusogeza skert yake ili asijifunue, hapa ndipo nilipoacha kuangalia video nzima.
Wasalam waleikhum..!

Kidogo tumepumzishwa kwenye zile sinema zetu.... Tumepata msimu mdogo wa mwanadini muimba nyimbo za injili mwanadada na mama wa watoto Rose Muhando.

Hii inaweza kuwa mada ya NNE kumhusu... Japo nyingine zilizotangulia zikimjadili Rose wa sasa kama celeb na kile kinachomtokea...

Kwanza itambulike kuwa hii ni vita ya kiroho, falme za giza dhidi ya falme za nuru, wakuu wa mbingu dhidi ya wakuu wa anga...

Rose ni catalyst tu katika vita kubwa ya kiroho na ya kidunia... Nuru dhidi ya giza... Alikuwa jemadari msimu wa kwanza akapambana vilivyo, akazishinda falme za giza katika maeneo mengi.. Lakini kwakuwa ana mwili wa damu na nyama, alilemewa... Akazidiwa akampa adui nafasi... Sasa anatengenezwa...!

Rose Muhando ni nani?

Kwa wale waliobahatika kusoma habari zake huko nyuma... Aliingia kwenye uimbaji wa nyimbo za injili akitokea kwenye ndoa iliyojaa mateso (kwa mujibu wake) akiwa na karama ya uimbaji na mahitaji ya nyakati kumbeba aliibuka kuwa mmojawapo wa nyimbo za injili mwenye kipaji na mafanikio mengi... Lakini mafanikio yake yalikuwa kwenye hatari kubwa kwakuwa aliyapata kwa kupambana na shetani (kimtazamo)

Kuna wakati tunaweza kusema kwa hakika Rose alikuwa mlokole kamili na nyimbo zake zikiwaokoa na kuwabariki wengi....

Misukosuko ilipoanzia

Zaburi ya 23 kuna mstari unasema... Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti....! Kila mmoja wetu ana mapito yake ... Hata waimbaji wenzake walishapitia anayopitia... Si wa kwanza yeye na hatakuwa wa mwisho... Shida iko hapa, je unapopitia kwenye mapito unasimama upande gani? Wa nuru au giza? Anguko lako ama kusimama tena vitategemea ulikuwa upande gani... I mean upande gani uliupa airtime kubwa....! Ni wazi Rose alipojaribiwa aliingiwa na upofu na kumpa Mungu wake kisogo akaenda kufanya kolabo na upande wa giza... Sasa anasulubiwa.. Msimu huu wa pili anamsaidia adui.. Na huu ndio ushindi uliokuwa unatafutwa na falme za giza

Imekuwaje aibukie Kenya?

Kwanza kiuhalisia Rose ni kweli kabisa anaumwa na hayupo sawa.. Ni kama mwaka sasa tumekuwa hatusikii habari zake nzuri.. Amepitia mapito mengi, amechapwa akachapika.. Anaonekana live ana POP mkononi vidonda na makovu.. Na kwa maneno yake mwenyewe kwa takriban siku 90 alikuwa hajui anatoka wapi anaenda wapi... Amekuwa kama chizi fresh, zinatoka zinarudi... Alifikaje Kenya kwa hali ile? Alipelekwa? Alifikaje kwa yule mtume nabii?
Kisanga kinaanzia hapa!

Dunia ya leo watu hupenda kuyatumia matatizo ya wengine kujinufaisha ama kuwatumia wao wenyewe pia...

Rose Muhando ni jina kubwa Afrika mashariki. Habari zake zikisikika popote ndani ya jumuiya hii si jambo geni

Mtume na nabii kwa kuiona fursa... Anamuahidi kumsaidia Rose kwa masharti hasa la kutaka amuombee mbele ya waumini wake kukiwa na camera zinazochukua video na picha.. Lakini la zaidi anamfundisha cha kuongea..

Nimeangalia kwa makini video ile.. Sijui misa ilianzaje lakini anaonekana mtumishi wa Mungu akimwita Rose aliyechoka na kuanza kumuombea.

Ghafla Rose anaanguka na mapepo yanaaza kuongea kuwa kuna wivu juu ya mafanikio yake, hawataki aimbe, wamechukua magari yake wanataka kumuua nknk... Lakini ni wakati huu mapepo yakiongea Rose ana ufahamu wa kuondoa mkono wa mtumishi mdomoni mwake aweze kuongea vizuri....

Baada ya maombi mafupi mapepo yanatimka na hapo hapo Rose anazinduka na kuanza kuongea yaleyale yaliyokuwa yakiongelewa na mapepo... Halafu anaendelea kuelezea changamoto za familia yake, watoto kukosa ada nk.. Halafu anamalizia kwa kumshukuru Mungu...

Rose, Mungu hadhihakiwi... Mapepo hayatoki kivile na fahamu hazirudi kivile.. Nguvu ya pepo kutoka si ya kitoto (nitaelezea kwenye mada nyingine)

Umetumika vibaya kwenye mapito yako... Angalia wanaokutumia wasikuongoze kwenye anguko kuu
 
Kwa sisi tuliokuwa na uzoefu wa kiroho.

Rose Mhando ameonesha maigizo makubwa. Ni kweli ana matatizo makubwa. juzi juzi nilimuona Dodoma na jamaa akaniambia umemuona Rose Mhando? kwa kweli nilvyomuona sikuamini kabisa kama ni yeye.

Kwa ufupi ni kwamba mapepo yanapozungumza pale yanapokemewa, yule mwenye mapepo (nafsi) huwa hana habari na kile kinachozungumzwa na yale mapepo, Huwa anakuja kusimuliwa kile kilichokuwa kinaendelea. lakini Rose anaibuka na kusema complete/exactly kile mapepo walichokuwa wanasema. HUO NI UIGIZAJI MKUBWA.

FUNZO:
Kwa sisi tunayemfahamu Umaarufu wa Rose uliibuliwa na Mwalimu pale alipo mualika katika mkutano/semina yake dodoma katika viwanja vya mashujaa miaka ya 1990....

Inasemekana baada ya kupata umaarufu mkubwa siku nyingine walimualika tena katika mkutano/semina na kuwajibu anataka alipwe pesa ndio atahudumu. (waandaaji walimshangaa sana kwa kutoza pesa wakati wengi wanalilia waalikwe kwenye mikutano hiyo na kwamba yeye alipata promo kupitia semina hizo).

SINA UHAKIKA kwamba habari zilipomfikia Mwalimu alishangaa na kuishia kwamba Rose ataimba na kupata pesa nyingi na utajiri alafu atapiga muziki wake mpaka vilabuni kwenye pombe. (Its done now!)

Wasanii na waimbaji wa Injili Mungu hazihakiwi umepewa bure toa bure. hao waliokualika wanajua una watoto, una familia na una matumizi mengine. Hii tabia ya kumtoza Mungu gharama ili muhudumu muiache.
Ni mwalimu yupi huyo aliyemwalika kwenye mkutano/semina?
 
Mgibeon

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2011
rep.png
8,322
like.png
11,074
point.png
280
Today at 5:36 AMNew #7
Mshana Akili kubwa! UnaKINA kwenye kila nyanja ya maisha! Nawaza siku JF ikifungwa tutapotezana na watu kama wewe Doh, Mwenyezi Mungu aepushie mbali kabisa.
Mkuu nmekopy na kupaste Id na comment yako........hebu tuanzishe mjadala mpana wa jinsi ya kufanya ili tusiwapoteze watu wenye kariba ya Mshana Jr
 
Nakumbuka mwaka 2005 mzee Malecela alimtumia Rose Muhando kufanya tamasha la nyimbo zake za injili pale hotel ya Golden Tulip iliyopo Masaki, Dar na wengi tukahudhuria. Mzee alimtumia ikiwa ni sehemu ya kujijenga kisiasa kuelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huo ambapo hata hivyo chama chake kilimpiga chini.
 
Ha ha ha ha aiseee.. Nimeangalia hii video clip, imebidi nicheke, maana sio kwa usanii huu.. Hapo baada Rose kuanguka sketi yake ikapanda juu kidogo, nimeshangaa pamoja na kuwa amepandwa na mashetani, lakini akakumbuka kuivuta sketi chini ili ikae sawa, kisha akaendelea na kupandwa na mapepo..!
 
Soma habari za Lucifer, kisha kasome kitabu cha ufunuo... Haya ni mambo ya kiimani si kila mmoja anaweza kuelewa
Please bro, niambie hizo habari za Lucifer amekuapa nani? kama Mungu alikushukia akakuhadithia story za Lucifer andika hiyo experience yako. lakini kama umesoma mastory na simulizi za watu wengine trust me you have bamboozled na hicho kitabu cha ufunuo kimeandikwa na wajanja janja kushika akili zenu.... na ndio maana tamthilia zinaendelea leo Rose Muhando next year huyo huyo mchungaji aliyemuombea naye wenzake watampa episode.
 
Back
Top Bottom