Makala: Haya ya Rose Muhando ni mapito au anguko?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Wasalam waleikhum..!

Kidogo tumepumzishwa kwenye zile sinema zetu.... Tumepata msimu mdogo wa mwanadini muimba nyimbo za injili mwanadada na mama wa watoto Rose Muhando.

Hii inaweza kuwa mada ya NNE kumhusu... Japo nyingine zilizotangulia zikimjadili Rose wa sasa kama celeb na kile kinachomtokea...

Kwanza itambulike kuwa hii ni vita ya kiroho, falme za giza dhidi ya falme za nuru, wakuu wa mbingu dhidi ya wakuu wa anga...

Rose ni catalyst tu katika vita kubwa ya kiroho na ya kidunia... Nuru dhidi ya giza... Alikuwa jemadari msimu wa kwanza akapambana vilivyo, akazishinda falme za giza katika maeneo mengi.. Lakini kwakuwa ana mwili wa damu na nyama, alilemewa... Akazidiwa akampa adui nafasi... Sasa anatengenezwa...!

Rose Muhando ni nani?

Kwa wale waliobahatika kusoma habari zake huko nyuma... Aliingia kwenye uimbaji wa nyimbo za injili akitokea kwenye ndoa iliyojaa mateso (kwa mujibu wake) akiwa na karama ya uimbaji na mahitaji ya nyakati kumbeba aliibuka kuwa mmojawapo wa nyimbo za injili mwenye kipaji na mafanikio mengi... Lakini mafanikio yake yalikuwa kwenye hatari kubwa kwakuwa aliyapata kwa kupambana na shetani (kimtazamo)

Kuna wakati tunaweza kusema kwa hakika Rose alikuwa mlokole kamili na nyimbo zake zikiwaokoa na kuwabariki wengi....

Misukosuko ilipoanzia

Zaburi ya 23 kuna mstari unasema... Nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti....! Kila mmoja wetu ana mapito yake ... Hata waimbaji wenzake walishapitia anayopitia... Si wa kwanza yeye na hatakuwa wa mwisho... Shida iko hapa, je unapopitia kwenye mapito unasimama upande gani? Wa nuru au giza? Anguko lako ama kusimama tena vitategemea ulikuwa upande gani... I mean upande gani uliupa airtime kubwa....! Ni wazi Rose alipojaribiwa aliingiwa na upofu na kumpa Mungu wake kisogo akaenda kufanya kolabo na upande wa giza... Sasa anasulubiwa.. Msimu huu wa pili anamsaidia adui.. Na huu ndio ushindi uliokuwa unatafutwa na falme za giza

Imekuwaje aibukie Kenya?

Kwanza kiuhalisia Rose ni kweli kabisa anaumwa na hayupo sawa.. Ni kama mwaka sasa tumekuwa hatusikii habari zake nzuri.. Amepitia mapito mengi, amechapwa akachapika.. Anaonekana live ana POP mkononi vidonda na makovu.. Na kwa maneno yake mwenyewe kwa takriban siku 90 alikuwa hajui anatoka wapi anaenda wapi... Amekuwa kama chizi fresh, zinatoka zinarudi... Alifikaje Kenya kwa hali ile? Alipelekwa? Alifikaje kwa yule mtume nabii?
Kisanga kinaanzia hapa!

Dunia ya leo watu hupenda kuyatumia matatizo ya wengine kujinufaisha ama kuwatumia wao wenyewe pia...

Rose Muhando ni jina kubwa Afrika mashariki. Habari zake zikisikika popote ndani ya jumuiya hii si jambo geni

Mtume na nabii kwa kuiona fursa... Anamuahidi kumsaidia Rose kwa masharti hasa la kutaka amuombee mbele ya waumini wake kukiwa na camera zinazochukua video na picha.. Lakini la zaidi anamfundisha cha kuongea..

Nimeangalia kwa makini video ile.. Sijui misa ilianzaje lakini anaonekana mtumishi wa Mungu akimwita Rose aliyechoka na kuanza kumuombea.

Ghafla Rose anaanguka na mapepo yanaaza kuongea kuwa kuna wivu juu ya mafanikio yake, hawataki aimbe, wamechukua magari yake wanataka kumuua nknk... Lakini ni wakati huu mapepo yakiongea Rose ana ufahamu wa kuondoa mkono wa mtumishi mdomoni mwake aweze kuongea vizuri....

Baada ya maombi mafupi mapepo yanatimka na hapo hapo Rose anazinduka na kuanza kuongea yaleyale yaliyokuwa yakiongelewa na mapepo... Halafu anaendelea kuelezea changamoto za familia yake, watoto kukosa ada nk.. Halafu anamalizia kwa kumshukuru Mungu...

Rose, Mungu hadhihakiwi... Mapepo hayatoki kivile na fahamu hazirudi kivile.. Nguvu ya pepo kutoka si ya kitoto (nitaelezea kwenye mada nyingine)

Umetumika vibaya kwenye mapito yako... Angalia wanaokutumia wasikuongoze kwenye anguko kuu
 
Kwani tatizo ni lipi? Mbona imekuwa big deal, Hivi bahati bukuku au Shusho akiombewa hapa bongo akaanguka tutasema ana mapepo? Au ingekuwa topic kama ilivyosasa endapo dada yetu huyu angeanguka hapa bongo.

Mi naonaga Hizi ni mambo za kawaida sana kwa wanamama maana kuanguka ni kawaida sana kwao. Sema kwa kuwa ni abroad ndio maana imekuwa big deal. Tumsubiri arudi nayeye atupe wanchi wanchii za hayo mambo huko
 
Ilifikia mahali Rose akialikwa kuimba nyimbo za dini anachukua pesa halafu hatokei siku ya kuimba kwake.
Yaani ni full utapeli hadi wenzake wakamsusa kumpa mialiko iliyokuwa inamwingizia pesa.
Arudi kuomba msamaha kwa aliowakwaza ninauhakika watamsamehe na kumpokea, wahenga walisema.
Ujanja mwingi mbele giza.
 
Hakunaga kitu ambacho naamin hakinaga mwisho mzuri kama UJANJA UJANJA katika kutafuta mafanikio, yan bora uwe shari to shari kuliko kuish kwa kutegemea ujanja ujanja. Haya maneno niliambiwa nikaanza kuyafanyia tathmin nikaamini. Mtu huyo huyo alieniambia hayo maneno aliniambia pia "Kuna mstari mwembamba sana unaomtenganisha mjanjamjanja, dalali na tapeli" haya nayo nayatathmini, akili kumchwako, za kuambiwa changanya na zako
 
Sehemu moja nilipojua hakuna ukweli ni pale kisket alichovaa kupanda juu huku pepo likiwa limeshapanda akawa anashusha ile sket namanisha anajifunika vizur

Ukiwa na pepo huwi vile, na kilichofanyika unakua huna kumbukumbu nacho kabisa tena kama ni kustiriwa vzr wanakustiri wanaokusaidia kuondoa hilo pepo

Hapo ndio nikajua hamna kitu ni kiki
 
Back
Top Bottom