Makabila haya yanaongoza kwa kuwekana wao kwa wao kwenye nafasi za Umma

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,081
kuweka watu wa kabila lako kwenye kampuni yako ama biashara yako binafsi ni ruksa maana mwisho wa siku hata hasara ni yako mwenyewe, Lakini ajabu mambo haya yanafanyika serikalini kwenye mjumuiko wa taifa zima bado mtu anaweka kipaumbele kwenye jamii anayotokea hata kama wapo wenye sifa chache

1. Wachaga.
2. Wasukuma
3. Wanyakyusa
4.Wahaya
 
kuweka watu wa kabila lako kwenye kampuni yako ama biashara yako binafsi ni ruksa maana mwisho wa siku hata hasara ni yako mwenyewe, Lakini ajabu mambo haya yanafanyika serikalini kwenye mjumuiko wa taifa zima
bado mtu anaweka kipaumbele kwenye jamii anayotokea hata kama wapo wenye sifa chache

1. Wachaga.
2. Wasukuma
3. Wanyakyusa

Wahaya at least
Bila kusahau wazanzibar
 
makabila matatu yenye hizo sifa ni haya haya yenye kulima ndizi kwa wingi:
MCHAGA, MHAYA, MNYAKYUSA

Wasuku wameanza hivi karibuni.

Nakumbuka miaka flani Pale NIC-Shirika la bima, kinyakyusa ilikuwa kama lugha ya rasmi ya shirika
 
kuweka watu wa kabila lako kwenye kampuni yako ama biashara yako binafsi ni ruksa maana mwisho wa siku hata hasara ni yako mwenyewe, Lakini ajabu mambo haya yanafanyika serikalini kwenye mjumuiko wa taifa zima
bado mtu anaweka kipaumbele kwenye jamii anayotokea hata kama wapo wenye sifa chache

1. Wachaga.
2. Wasukuma
3. Wanyakyusa

Wahaya at least
Wanyakyusa tunasakamwa eeh?
 
Hapo unazungumzia simulizi. Toa mfano.

Wachaga wasomi ni wengi. Hata darasa la watoto 30 huko Lindi si ajabu ukakuta wachaga wako 5 hadi 10.

Wanyakyusa wameshika ofisi ipi na ipi, na wamemsaidia nani?

Wasukuma kwa idadi ni wengi, waliosoma ni wengi, ingawa ambao hawajasoma ni wengi zaidi.

Hayo makabila, wachaga, wasukuma yameshika nafasi nyingi, si kwa sababu wanapendeleana. Wenye shule wako wengi. Wanyakyusa, unawasingizia. Labda enzi za Nsekela na Mwaikambo. Wanyakyusa hata kusaidiana ni kugumu, watu wote watokao nyanda za juu kusini hawapendi kubebana.
 
Hoja ya ukabila haihusiani na kwamba wangapi wamesoma au la.
Kwanini ofisi ikiwa na viongozi labda wangoni au wahehe tusikute wahehe au wangoni wamejazana? Ni kwamba hawajasoma?

Sasa tuje kwa makabila hayo yaliyosemwa kwamba wamesoma. mfano ofisini kiongozi akiwa ni mnyakyusa wanajjazana wanyakyusa kwamba wachaga na Wahaya kwa ofisi hiyo wanakua hawajasoma au ni ukabila?

Ofisini akiwa mhaya ni Kiongozi makabila yote mengine Hadi hao wachaga na wanyakyusa na makabila mengine wanakua hawana elimu sasa ndio maana wamejaa Wahaya.

Nadhani kuna shida ya ukabila ambayo haisemwi wazi ila ipo shida ya ukabila na udini nchi hii.

Miaka ya Leo uniambie kuna kabila halina wasomi lipo hilo?

Kwamba unaajiri watu wa usafi wakabila lako mpaka walinzi kwasababu wamesoma mbona hoja inakataa kabisa, zaidi ya ukabila hakuna lingine hapo.

Kuna tasisi mpaka za serikali zinajulikana ni za kabila flani au dini flani walau baada ya Utumishi kuweka utaratibu mpya kumeanza kuwa na mabadiliko.
 
Back
Top Bottom