Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,341
- 51,907
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Wapo wenzetu wenye mitazamo Duni linapokuja suala la ukabila u utaifa. Wapo wanaojiona ni Bora kuliko wengine lakini ukifuatilia Kwa umaskini ubora wanaojivunia ndio udhaifu wao. Na wapo ambao wanaojiona Duni lakini ukifuatilia uduni wao ndio ubora wao.
Kwa hapa nchini yapo makabila ambayo Watu Kutoka makabila hayo hujiona wao ni Bora kuliko wengine. Ingawaje sio wote lakini kasumba hiyo Ipo. Bila kumung'unya maneno naweza kutaja baadhi ya makabila hayo au maeneo ambayo wanatoka Watu hao, mathalani Wachaga, Wahaya, Wazanzibar, wanyakyusa miongoni mwa wengine. Zingatia sio wote.
Taikon Master nikasema embu ngoja nifuatilie na kuona huo ubora wanaojiona Bora kushinda wengine lakini nikagundua na Kiburi na majivuno ya wapumbavu tuu.
Niligundua Watu wa mataifa wote ni Sawa siku moja nilipokutana na Wayahudi Wakati Fulani nilipokuwa Rwanda. Tangu nikiwa mdogo nilikuwa nasikia Wayahudi ni Watu Bora na wenye Akili lakini siku nilipokutana nao haikunichukua siku Saba kugundua kuwa kuna Wayahudi wajinga, wapumbavu, na wenye Sifa dhaifu kama Watu wa mataifa mengine.
Wachaga nimeishi nao Kwa kitambo kirefu, wengine ni ndugu zangu, wengine na Baba zangu na sasa ni Wakwe zangu. Hivyo tangu utoto ninawajua. Hakuna maajabu yoyote ambayo yatawafanya wajione Bora kuliko wengine.
Wajinga wapo, walevi kupindukia wapo, wakatili wapo, Wasiojua kutafuta Pesa wapo, yaani kila Sifa dhaifu ambazo kwingine zipo nao wanazo.
Wazungu ni wateja wangu, ninachangamana nao Sana kwenye kazi zangu. Sikuona tofauti Ile kubwa ya kuonekana Bora kuliko wengine. Wapo Wazungu wenye Roho Mbaya, wapo Wazungu wanyanyasaji na wabaguzi, wapo Wazungu wenye tabia chafu ambazo zingine kuzisema sio Maadili. Hawana ule ubora ambao Watu wasiowajua huwaona.
Ninachotaka kusema, hakuna mtu Bora kuliko mwingine. Na hakuna taifa Bora kuliko taifa jingine. Na wala hakuna kabila Bora kuliko kabila jingine.
Ubora wa Watu hupimwa Kwa uadilifu, maadili, Haki, Wema, Upendo, Ukweli miongoni mwa mambo mengine.
Wakati tukiwa wadogo wale wote(wengi wao) waliokuwa wanajiona Bora kuliko wengine, wale wote wenye Kiburi na majivuno Kwa sababu yoyote Ile Kwa sasa ni Watu ambao wanatia huruma, Watu wakuhurumiwa tuu.
Usihangaike kuwa Bora dhidi ya wengine. Bali tafuta kuwa Bora juu yako mwenyewe na sio juu ya wengine. Jitahidi uwaone wengine Bora kuliko wewe hiyo itakupa nafasi ya kuona umuhimu wa wengine na umuhimu wako kuonwa na wengine.
Usipoona ubora wa wengine jua hata wewe ubora wako hauonekani.
Pumzika sasa Taikon wa Fasihi
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam