Majimarefu wataje?

Kifulambute

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,539
755
Jana katika kikao cha bunge jioni Mbunge wa korogwe Prof. Maji marefu alisema anayo majina ya wabunge wanaosign na kuchukua posho kutoka mashirika mengine na wakifika bungeni wanadai hawataki posho.. alipoambiwa mwenyekiti wa bunge amsimamishe na awataje akasema asubiri kwanza. Hivi bunge ni la kusema uongo na mtu akatetewa? nilifikiri kama ni Zito amesema hivyo angeambiwa awataje maramoja.....Jamani awataje basi
 
hana hoja yule mchawi amefananisha umaarufu wa kisiasa na umaarufu wa kutibu kwa majini na mitishamba wapi na wapi eti kama watu maarufu duniani walioko bungeni tanzania yeye na nkamia ndio maarufu mweee
 
Huo ni utabiri inabidi akasome nyota kwanza au akacheze tunguli
 
hana hoja yule mchawi amefananisha umaarufu wa kisiasa na umaarufu wa kutibu kwa majini na mitishamba wapi na wapi eti kama watu maarufu duniani walioko bungeni tanzania yeye na nkamia ndio maarufu mweee

hhahahahah kweli kuna haja ya wabunge kuleta CV zao kabla ya kuteuliwa kugombea na sio uwezo wa kubwabwaja tu. bungeni siio mitishamba jamani.
 
kumbe kuna wabunge wanaopokea posho kwenye mashirika halafu wanajifanya hawazitaki posho.....NI UNAFIKI WA WANASIASA
 
anajikosha tu yule,hana lolote,eti naye ajengewe barabara na atangazwe km babu wa loliondo.crap
 
Jana katika kikao cha bunge jioni Mbunge wa korogwe Prof. Maji marefu alisema anayo majina ya wabunge wanaosign na kuchukua posho kutoka mashirika mengine na wakifika bungeni wanadai hawataki posho.. alipoambiwa mwenyekiti wa bunge amsimamishe na awataje akasema asubiri kwanza. Hivi bunge ni la kusema uongo na mtu akatetewa? nilifikiri kama ni Zito amesema hivyo angeambiwa awataje maramoja.....Jamani awataje basi

yule mwanamazingaubwe naye ni mbunge?du!mtatoka kweli?
 
hivi alipitaje ubunge.?? alichaguliwa au aliteuliwa...ni chama gani huyo jamaa. Ama kweli walioanzisha shule waliona mbali.!..Nini.??.eti hakuna mtu maarufu Tz kama huyo sijui nani,."profesa""!!??? maji yepi mpiga ramli.?? ana maanisha..mi ndo kwanza jana nimemuona, nlikuwa namckia tu...maskini ya Mungu bunge letu..!!
 
kumbe kuna wabunge wanaopokea posho kwenye mashirika halafu wanajifanya hawazitaki posho.....NI UNAFIKI WA WANASIASA
Wewe utakuwa mchawi kama alivyo majimafupi au ngumbalo kama yeye. Msomi hawez kukbali klchosemwa na huyo mganga wa kienyeji. Huyu mganga anawakilisha watu washrikina kama wewe.
 
Jana katika kikao cha bunge jioni Mbunge wa korogwe Prof. Maji marefu alisema anayo majina ya wabunge wanaosign na kuchukua posho kutoka mashirika mengine na wakifika bungeni wanadai hawataki posho.. alipoambiwa mwenyekiti wa bunge amsimamishe na awataje akasema asubiri kwanza. Hivi bunge ni la kusema uongo na mtu akatetewa? nilifikiri kama ni Zito amesema hivyo angeambiwa awataje maramoja.....Jamani awataje basi

Lazima aangalie majina kwenye mikoba kwanza ndio ayataje. Hili bunge la safari hii mmmnnhh haya. Imagine bunge lijalo mwenyekiti wa kamati ni huyu mganga wa kienyeji Prof. Maji marefu halafu katibu wake ni yule mrembo Wema Sepetu. Shuhuli ipo
 
Jana katika kikao cha bunge jioni Mbunge wa korogwe Prof. Maji marefu alisema anayo majina ya wabunge wanaosign na kuchukua posho kutoka mashirika mengine na wakifika bungeni wanadai hawataki posho.. alipoambiwa mwenyekiti wa bunge amsimamishe na awataje akasema asubiri kwanza. Hivi bunge ni la kusema uongo na mtu akatetewa? nilifikiri kama ni Zito amesema hivyo angeambiwa awataje maramoja.....Jamani awataje basi
Akawadanganye Korogwe,maana sehemu zingine huwezi kupigia kura mtu kama huyu!
 
Laitani mngelijua kama huyu Majimarefu ni mtu wa namna gani, wala asinge waumiza vichwa.....Wilaya ya Korogwe kuna sehemu inaitwa kilole,karibu na kituo cha Tanesco kuna mama mmoja anaitwa mama-Maria alikuwa anafanya biashara ya mamantilie,huyu Maji Marefu na jamaa mmoja anaitwa Rama kibonge walikula na kumkimbia huyu mama Maria...sasa mnategemea ataongea nini bungeni?
 
Back
Top Bottom