Uncle Araali
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 946
- 1,260
UKIACHA WABUNGE,KUNDI JINGINE LINALOILA KEKI YA TAIFA KISAWASAWA NI HILI HAPA...
Wasalaam,
Nawasalimu kwa Jina la JMT...
# Kazi na Iendelee
Ndugu zangu WaTanzania,wakati Mchezo wa Mpira wa miguu ukiendelea, Makosa makubwa yanaonwa na mashabiki/watizamaji walio nje,na syo wachezaji waliopo ndani ya uwanja.
Moja ya Mtizamo wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kuwahimiza Viongozi wengine,wananchi na Taasisi mbalimbali za kiserikali na Zisizo za kiserikali kuwa huru na kuwakosoa sawasawa wanapokosea au wanaona mambo yanaenda ndivyo-sivyo..kwa Watawala/Viongozi wa juu wa Kiserikali,ni kwa sababu sisi watizamaji tulioko Nje huenda tunaona Makosa/Madhaifu yenye kuhitaji marekebisho ambayo wao viongozi wakuu huenda hawayaoni Ndani ya Ulingo.
Kwa Mantiki hyo basi,Napenda nianze na kuichambua kidogo sana Clip ya video ya Mbunge wa jimbo Furani aliyekuwa anadai POSHO za ubunge ziongezwe maana hazitoshi.
Mbunge huyu anaweza kulaumiwa sana kama yy ingawa aliomba kitu kinachotamaniwa na kila Mbunge wa bunge la JMT..lakini hawataki kusema tu.
Hakuna mtu asiyependa Pesa,ila ktk kupenda ndyo tunatofautiana kwa viwango, kuna anaetamani apate 1000,kuna wa elfu 10,kuna wa laki,milioni,mamilioni au Bilioni n.k.
Mimi na wewe tukiwa kwenye harakati za kupambania UGALI tu tena wa leoleo,wenzio wanahangaikia Makampuni ya Bilioni kadhaa,.
Wakati Mwalimu wa daraja la III A,au mtumishi wa kima cha chini cha mshahara wa serikali akihangaika na 300,000 yake kabla ya MAKATO kwa mwezi,kuna Mbunge anaona milioni 12 kwa mwezi Ndogo.
hapo lazima kuwa kuwe na Mtikisiko wa Amani ya Moyo hata kama ya Nchi ipo imara kwa Nje. Na si mmoja tu aliyenukuliwa akiomba nyongeza nadhani ni wabunge wote wanaona hivyo tu kwa ndani ya moyo yao..maana kama kuna mtu mmoja Mzalendo angekuwa anaona hyo ni nyingi ukilinganisha na kazi zake,basi angesikika akipiga kelele mizigo ipunguzwe.
Kundi hili linaloitafuna sawasawa KEKI ya Taifa la watu masikini,wakati wa uchaguzi unapowadia,wanatumia hadi Milioni 400,000,000 au zaidi kuhakikisha wanawarubuni walalahoi kwa kujua zitarudi tu,sasa kwa kulinganisha kinachoingia na kile kilichomtoka,anaona kabisa biashara aliyofanya huenda akapata nusu hasara au hasara kabisa ndyo sababu kelele zinaongezeka kwa madai ya kuongezwa posho.
Ktk Bunge la 11,kuna Mbunge mmoja tu wa Upinzani kutoka Mkoa wa Kigoma ndo peke yake aliomba posho zipunguzwe pamoja na mshahara ili zipelekwe kuwasaidia watu masikini mojakwamoja lakini aliambulia za USO pasipo kuungwa mkono na mbunge yoyote...au wa chama chochote.
Mwingine Aliyekuwa kiongozi wa KUB akakataa Shangingi vieitee...kuwa hawezi kulitumia maana ni gari la Anasa sana na lina matumizi makubwa ya anasa ukilinganisha na umasikini wa kunuka unaowakabili waTz..ila huyu kwakuwa alikuwa anaigiza ili kupata sifa,baadae uzalendo ukamtoka,akaendelea kula Viyoyozi tu na kulitumia hilo VXR V8.
Sasa basi,
Ukiacha kundi hilo la Wabunge/Waheshimiwa linalotumia Takribani BILIONI 45 kila mwezi kwa posho,mishahara,matumizi ya Magari,mafuta na kulipa wasaidizi wao wakiwemo Madereva...kila mwezi huku idadi yao ikiwa ni 393 tu..sawa na asilimia 0.00006% ya waTanzania wote, huku kukiwa na wananchi ambao hawana uhakika wa kupata mlo mmoja kwa siku ...Kundi la pili LISILOJULIKANA kwa Macho Makali sana ni la WAKUU WA IDARA Chini ya Halmashauri zote 187 za nchi yetu.
Ifahamike kuwa watu wanalogana usiku na mchana kupata UKUU wa IDARA.
Kwanini? Twende pamoja hapa.
Kwa kila halmashauri kuna idara zisizopungua 12.
Idara hizi zina viongozi wake. Viongozi hawo ndyo wanaitwa wakuu wa idara ambao ni mara zote wanakuwa wajumbe wa Mkutano wa Council kama ilivyo kwa MAWAZIRI mle bungeni.
Idara hizo ni pamoja na..
Idara ya..
1: Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji.
2: Elimu Msingi.
3: Elimu Sekondari.
4: Afya
5. Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa jamii na vijana
6. Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
7. Mifugo na Uvuvi
8. Ardhi
9. Utumishi na Utawala
10. Maji
11. Fedha na Biashara
12. Ujenzi
Idara hizi zaweza kuongezeka au kupungua kulingana na mahitaji ya halmashauri husika..pia zaweza kuwa na Majina tofauti kutokana na kurahisisha mahitaji ya kiutawala..
Wakuu wa Idara -wana-ila vipi keki ya Taifa?
Fuatana na mimi hapa
● Mshahara wa Mkuu wa idara=2.7M hadi 3.4.(wasitani wa 3M)
● Posho ya Pango/kodi ya nyumba=600,000 kwa mwezi, yaani inatoka 1.8M baada ya miezi 3.
● Posho ya Simu/Mawasiliano 300,000..kila mwezi.
● Posho ya Maji/nyumbani 200,000 kwa mwezi.
● Usafiri toka home kwenda kazini 300,000.
● Chai ya Kazini 180,000 kwa mwezi kwa maana ya 6,000 kwa siku..
Hapo sijagusia posho za vikao vya Halmshauri ambavyo ndugu zangu nyinyi mnajua vinafanyika karibia kila siku iendayo kwa MUNGU, na mle ndani hawakai bure, analetewa chai NZITO na mayai ya kienyeji, na baadae msosi wa nguvu na ikifika usiku kama kikao ni kirefu sana, wanajiongezea posho ya ziada, yaani ikifika saa 9:31 tu za alasiri,basi syo 90,000 tena, inakuwa Double.
Sasa hizo posho za vikao tuachane nazo kwanza.
Chukua Mshahara na Takataka nyingine ukizileta pamoja unapata Tshs. 4,580,000/- kila Mwezi.
Tuna Halmshauri za wilaya 187.
Ukizidisha hapo unapata jumla ya Wanufaika 2244
Yaani tuna jumla ya wakuu wa Idara elfu mbili, mia mbili na arobaini na nne elfu nchi nzima.
Chukua hesabu rahisi sana ya darasa la 4B,
Chukua 4,580,000×2244.
Hapo utapata..
Bilioni 10,277,520,000
Yaani zaidi ya BILIONI 10 zinatumika na maboss 2244 tu kila mwezi kwenye Nchi yenye watu Wanaofikia milioni 55..
Hapo sijawagusa maboss wa hao jamaa ambao ni maDED. Hao jamaa ndyo mwisho wa matatizo sasa kwa kujipangia matumizi.
Hayo mamilioni hapo juu, wao ndyo wanayaidhinisha kuwalipa wenzao,sijui wao wanajilipaje wakifanya kazi hadi usiku jamani.
Kuna baadhi ya watu mnaweza kunishangaa kwa Calculations hizo hapo juu, lakini mie nitawaona wa ajabu kwa kuwa wasahaurifu wa mambo rahisi sana.
Rais Mzalendo wa awamu ya 5,Hayati Dr.John Pombe Magufuli, alipoingia tu Madarakani alianza na sera yake ya Kufanya Standardization ya Mishahara.
Mbali na kujipunguzia mshahara au Posho yake mwenyewe kama Rais,alisema Rank ya mwisho ya Mshahara ni ya Waziri Mkuu na akataja waziwazi kuwa mshahara huo wa PM hauwezi kuzidi 9M.
Nini kilikuwepo kabla ya Mzalendo kupunguza mshahara wa Baadhi ya Maboss wa Nchi?
Wakurungenzi wa baadhi Mashirika ya UMMA walikuwa wanajilipa hadi Milioni 45 kwa mwezi.
Yaani pesa ambayo mtendaji wa kata akistaafu hawezi kuifikia kwa wakati huo ilichukuliwa kila mwezi na mkurugenzi wa Shirika furani ikiwemo mashirika ya BANDARI, TANAPA, TRA, NDEGE, NYUMBA (NHC)n.k..
Fikiria kuna Mtanzania ana mshahara wa 285,000 halafu kuna Jamaa ambalo linafanya kazi kwa kuweka sahihi tu kwenye mafaili huku likilipwa hadi posho ya watoto wake nyumbani lina mshahara wa 45,000,000. Fikria hapo halafu jibu baki nalo mwenyewe.
Ukishindwa kunielewa na hapo, nakupa mfano hai wa Mwisho.
Kuna mkurugenzi wa Kituo cha uwekezaji na uwezeshaji yaani TIC alikula mabilioni akatumbuliwa.
Aliyekuwa Rais wa Nchi kwa wakati huo hakuona mtu mwingine ndani ya Nchi, yaani wasomi na Maprofesa wooote waliomo nchini hawakuwa na Sifa, ktk kuangaza huku na kule alienda kumwona Dada Mmoja Ukoo wa Kina KAIRUKI huko Afrika kusini, huyo dada aliombwa aje Tanzania kwa maelewano kuwa angelipwa mshahara unaokaribiana na ule aliokuwa akilipwa huko South Africa.
Binafsi alidai alikuwa analipwa kiasi kilicho sawa na 35M per Month.
Kwakuwa Tanzania ndyo nchi ya Wazazi wake,aliombwa alipwe 20M lakini akakataa, akasema walau alipwe 30M, Awamu ya NNE ikaamua kumlipa 25M per Month akakataa katakata.
Basi,
Wakaamua kumlipa 25,000,000 kila mwezi lakini hakuwa radhi kuzichukua kwenye acc.yake kwa zaidi ya miaka 2 akidai mshahara ni mdogo sana.
Aliendelea kuwa Mkurugenzi wa TIC huku akigomea mshahara hadi TingaTinga JPM alivyoingia Ikulu ya Magogoni 2015.
Wakati wa kukatakata mishahara,na yy JULIETH KAIRUKI kwenye idara yake ya TIC panga likampitia, Rais akasema yaani pamoja na kulipwa 25M anaona ni kidogo anataka 30M, Sasa namlipa chini ya 9 kama Hataki aondoke.
Yule dada akataka kufungua kesi na serikali, kabla ya kufanya hivyo, Akatumbuliwa.
Kwahyo, tusiwatupie macho ya Hasira waheshimiwa wabunge tu, tunawaonea bure, hii nchi inaliwa na wengi na walio wengi hawadhaniwi kama wanaIFYONZA sawasawa hii nchi.
Wanaoangaliwa ni wabunge tu na wakurugenzi wa mashirika ya umma na walio chini yao.
Hali ilivyo serikalini ni kwamba,
Mishahara kama mishahara kwa kigezo cha Danganyatoto kilichopo ni midogo sana kuliko posho wanazozitolea macho..
Kipato cha Mkurugenzi wa (W) kwa mwezi ukiacha Dili feki na zile 25% za wazabuni ni mala 3-5 ya mzigo wa mbunge anaokunja mfukoni kwa mwezi,,,ndyo maana Mbunge nae anatamani awe mkurugenzi...ndo ujue uzalendo imebaki jina tu,watu wanataka shekeli..
Ndyo maana watu wapo tiari kuacha ukuu wa Mkoa ili akawe DED wa halmashauri furani..
Kuna Spika wa bunge la Nchi Mojawapo za Afrika Mashariki,mke wake ni Mkurugenzi wa halmashauri furani,yupo tiari akose hata huo uspika ili tu mke wake aendelee kuwa Mkurugenzi..
Sasa leo nimesemea Kundi moja tu la wakuu wa idara,lakini Nchi hii kuna watu wanaInyonya hatari yaani hawa ndyo hawataki kusikia watu wanalalamika kuhusu shida zao zinazowakabili,
Ukilalamika tu,unaweza kuitwa Mchochezi au Unataka Kuvuruga Amani ya Nchi..
Hawa ndyo wanaoongoza kusema Nchi yetu ina Amani na hawapendi amani ivurugike...
Amani syo hyo unayoijua wewe,ni ile Amani ya Matumbo yao..
Ushauri:
Serikali ifute posho,kuwe na mshahara tu,maana kuna majamaa yapo tiari kulipwa laki moja kama posho ya watendaji wa vijiji ili tu liendelee kufaidi zile stahiki za Kulipiwa Nyumba,Maji,Umeme,Simu/Mawasiliano,Bima kubwa,Nauli na watoto wakiugua,mke akijifungua n.k kama ilivyo kwa WAKUU WA IDARA zote ambao kwa YAKINI hata kazi na majukumu yao hufanywa na walio chini yao kwa maana ya wasaidizi huku wao wakibaki na kazi moja tu ya KUTIA SAHIHI,Lakini ndyo wanaotafuna Nchi vizuri sana kuliko wenzao na Bado wataweka Posho ya Kwenda Msalani ya haja ndogo au kubwa..maana ndyo iliyobaki..
MUNGU ibariki Tanzania.
Sukari,GS.
Mwanhuzi-Meatu
SIMIYU.
0742111113
0719111113.