Majibu ya Serikali Kuhusu Vitambulisho vya NIDA Vyenye Ukomo na Visivyo na Ukomo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
944
WhatsApp Image 2023-05-17 at 20.41.11.jpeg

SERIKALI KUANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU VITAMBULISHO VYA NIDA VYENYE UKOMO NA VISIVYO NA UKOMO

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha Wafanyakazi Nchini anayetokea Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Janejelly James Ntate ameuliza swali lililoelekezwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuhusu vitambulisho vya NIDA ambalo lilijibiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira na Muungano) Mhe. Khamis Hamza Khamis

"Je, wale waliopewa namba za NIDA kabla ya tangazo la GN96 ya mwaka 2003 vitambulisho vyao vitatoka vikiwa na ukomo au vikiwa havina ukomo"? - Mhe. Janejelly James Ntate

"Je, Serikali imejipangaje kuleta uelewa kwa wananchi ili wajue kwamba vitambulisho vyao ambavyo vimekaribia kuwa na ukomo na ambavyo vina ukomo havitawaathiri ili kupunguza taharuki Iliyo kwa wananchi sasa?" - Mhe. Janejelly James Ntate

"Vitambulisho ambavyo vitakuja baada ya tangazo hili havitakuwa na ukomo. Vitambulisho ambavyo vitakuja na tangazo lilishatoka kabla wataendelea kwa sababu lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi hawakosi huduma za muhimu na vitambulisho vilivyokwisha muda vitaendelea kutumika kuwapatia wananchi huduma mpaka pale Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi itakapotoa maelekezo mengine" - Mhe. Khamis Hamza Khamis

"Wananchi watafikiwa na taaluma, kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Waziri ameshatoa tangazo kupitia TV, Radio na Magazeti. Tumeshatoa maelekezo na muda wowote tunaweza kuanza mafunzo kwa Watendaji wote wa NIDA ili waanze kuwafundisha wananchi ili wajue mchanganuo wa kipi kimekwisha ukomo, kipi hakitakwisha ukomo na kipi kitatumika" - Mhe. Khamis Hamza Khamis
 
Vitambulisho Gani vinajadiliwa wakati ni zaidi ya miaka 7 watu hawajapata vitambulisho bado. Hii kazi ingepewa private sector tu maana wangelipwa kutokana na nakala wanazochapisha so wangekua speed. Ila Hawa NIDA Wana mishahara so wachapishe wasichapishe hakuna hasara wanapata.

Wanakera sana..... Hata JPM aliwashindwa kabisa licha ya ubabe wake.
 
Yaan mm tangu 2019 mpaka Leo kitambulisho bado tu najiuliza inapofikia mtu kumpa no Mana yake mchakato umekamilika Ila wao ss eti nlipewa no kitambulisho mwaka wa nne ss hakijatoka
 
Yaan mm tangu 2019 mpaka Leo kitambulisho bado tu najiuliza inapofikia mtu kumpa no Mana yake mchakato umekamilika Ila wao ss eti nlipewa no kitambulisho mwaka wa nne ss hakijatoka
Usikute pesa iliyotengwa kwa ajili ya kitambulisho, mkurugenzi husika anaizungusha kwenye biashara na miradi yake.
 
ID,ina number na hiyo number ndio jina lako ambalo serikali yako imekupa ,sasa itakuaje jina liwe na ukomo?hii ni shithole country yenye ukomo wa jina,ID number unazaliwa nayo na kufa nayo, Tanzania tumechelewa sana ,inabidi tuanze upya na tuanze na watoto wanaozaliwa, kila mtoto kabla hajawa discharged ni lazima awe na birth certificate yenye number, na number hii lazima iongee kwenye systems nzima ya nchi
 
Vitambulisho Gani vinajadiliwa wakati ni zaidi ya miaka 7 watu hawajapata vitambulisho bado. Hii kazi ingepewa private sector tu maana wangelipwa kutokana na nakala wanazochapisha so wangekua speed. Ila Hawa NIDA Wana mishahara so wachapishe wasichapishe hakuna hasara wanapata.

Wanakera sana..... Hata JPM aliwashindwa kabisa licha ya ubabe wake.
Yaani uchukue Data za raia wa nchi yako umpe let say Masumin Printing?? Hiyo Database atakua kaiweka kwenye ofisi zake au za serikali?? Ushawahi kujaza form ya Nida ukoana information za siri unazozijaza??

Kuwa serious basi ficha 7TLis6zundgjxykdhitzf wako
 
Hivi unakuta hawana wino, au karatasi za kuprintia? Mambo ya NIDA inafikirisha sana...wanapeleka mambo yao taratibu utafikiri wale wataalam wanaofanyia tafiti dawa ya ukimwi...
 
Yaan mm tangu 2019 mpaka Leo kitambulisho bado tu najiuliza inapofikia mtu kumpa no Mana yake mchakato umekamilika Ila wao ss eti nlipewa no kitambulisho mwaka wa nne ss hakijatoka
2019 hapo juzi tu mkuu, mimi tangu 2013 hadi leo sijapata.
 
Yaani uchukue Data za raia wa nchi yako umpe let say Masumin Printing?? Hiyo Database atakua kaiweka kwenye ofisi zake au za serikali?? Ushawahi kujaza form ya Nida ukoana information za siri unazozijaza??

Kuwa serious basi ficha 7TLis6zundgjxykdhitzf wako
Mpuuzi kweli wewe kwani tunavyo apply vyuo binafsi au tunapoomba visa na scholarship huko nje hatujazi hizo taarifa? In fact hata benki Zina access ya taarifa za NIDA mfano CRDB wamewahi niprintia copy ya NIDA sababu Wana access system ku retrieve taarifa zangu. Sasa kama CRDB Wana access taarifa Kuna Nini Cha ajabu wakapewa private sector kuprint.

Kumbuka hata hiyo mifumo ya NIDA imetengenezwa na kampuni za huko nje na ndio wanafanya hata maintenance ya system. Sasa kama mabeberu wanatutengenezea mifumo ndio sembuse washindwe kuihack kama wanataka taarifa?

Karatas za uchaguzi tu za kuamua Rais tunaprint nje, mitihani ya taifa tunaprint nje, silaha za kivita na ndege za serikali, material ya Noti za BOT zote zinaagizwa nje Tena kwa private companies ndio sembuse kitambulisho tu?

Kama huna unalojua Bora ukae kimya tu.
 
Back
Top Bottom