Nini Kauli ya Serikali Kuhusu Makato ya Tozo na Mtandao Kutokufanya Kazi Vizuri

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MBUNGE KUNTI MAJALA - NINI KAULI YA SERIKALI KUHUSU MAKATO YA TOZO NA MTANDAO KUTOKUFANYA KAZI VIZURI

Mhe. Kunti Majala Mbunge wa Viti Maalum amemuuliza swali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kupitia Wizara ya Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka kwenye mfumo wa Analogia kwenda kwenye mfumo wa Kidigitali.

"Serikali iliamua kuanzia mfumo wa malipo wananchi kuanza kulipa kwa njia ya kielektroniki. Mfumo huu umekuwa na changamoto kubwa sana ya makato makubwa na Mawasiliano ya mtandao kutokuwa sawa" - Mhe. Kunti Majala

"Nini mkakati wa Serikali; (1) Kupunguza makato na (2) Kuhakikisha unaboresha mfumo wake ili mfumo uweze kufanya kazi kwa uthabiti kutokana na kadhia kubwa wanayoipata watanzania kwa namna ambavyo mtandao unavyofanya kazi" - Mhe. Kunti Majala

"Tanzania kutokana na maendeleo ya TEHAMA, Serikali imeanza kutekeleza mifumo mbalimbali kwa ajili ya kurahisisha utendaji kazi ndani ya Serikali ikiwemo na ukusanyaji wa mapato kwa mfumo wa kielektroniki" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimeanza kutekeleza mifumo mbalimbali kielektroniki na tunapitia nyakati za mafanikio na changamoto tunapoelekea kujiimarisha, ukusanyaji wa mapato kielektroniki unaendelea vizuri" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Ili kukabiliana na changamoto hizi yapo maelekezo thabiti yaliyofikiwa na Serikali ikiwemo kuanzisha Wizara Maalum inayoshughulikia Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa lengo la kupitia kwa kina mifumo na kuimarisha TEHAMA na kusimamia kampuni za Mawasiliano" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Tozo kuwa kubwa na mtandao kutokufanya kazi vizuri. Suala la tozo hili ni wale walioamua tozo kuwepo na haya tunayafanyia kazi maana tumewasikia wabunge mara kadhaa na wananchi pia kuitaka Serikali ipitie makato au tozo zinazotozwa maeneo mbalimbali. Hilo linafanyiwa kazi" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Suala la mtandao Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari atakuja kuwasilisha mpango wa bajeti na kazi utakaofanya kazi mwaka 2024 na kuomba ridhaa ya fedha. Moja ya mambo nitakayomuagiza hapa ni kuja kueleza nini Wizara inafanya katika kuimarisha mifumo hasa mitandao bila kukatika" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Upande wa Serikali tunapata hasara sana na baadhi ya watu wanaopata vitendea kazi vya kielektroniki kwa kuzima na kusingizia kuwa mtandao haupo na kujipatia mapato. Tunataka kuimarisha eneo hili ili tuwe na mfumo mzuri wa mtandao kupitia taasisi zetu zinazosambaza mitandao" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu

"Serikali inaimarisha tozo mbalimbali ili kuleta unafuu kwa watanzania. Malengo yetu tunapokwenda kwenye maendeleo ya Teknolojia tuwe na TEHAMA inaweza kumhakikishia mtanzania kuitumia katika shughuli zake" - Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-05-12 at 16.17.19.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-12 at 16.17.19.jpeg
    67.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-05-12 at 16.17.21(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-12 at 16.17.21(1).jpeg
    71.3 KB · Views: 1
Back
Top Bottom