Vitambulisho vya Taifa: Changamoto zinazowakabili wananchi na mwitiko wa Mamlaka (NIDA)

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1693926005110.jpeg
Je, umewahi kukumbana na Changamoto za Kupata Kitambulisho cha Taifa? Jiunge nasi katika Mjadala kuhusu Upatikanaji wa Vitambulisho vya Taifa Nchini Alhamisi hii, Septemba 7, 2023, kupitia 'X Spaces' ya JamiiForums

Tutaangazia Mchakato mzima wa Utoaji na Upatikanaji wa Vitambulisho ikiwemo Mafanikio, Changamoto wanazopata Wananchi na Mwitikio wa Mamlaka

'Link' ya Mjadala https://twitter.com/i/spaces/1MnxnpPbYNeGO
---
Mjadala Umeanza
BAADHI YA MASWALI NA HOJA ZA Wananchi
IVETA: Kiukweli hakuna vitambulisho vinavyotoka kwa siku 7 ni uongo, tumekuwa tukisubiri kwa zaidi Miaka 3 lakini hadi leo hakuna chochote hizo taarifa za siku 7 sio za ulimwengu huuHizo takwimu wanazotoa wawe wanaongea uhalisia kwa maana wanazosoma hazina ukweli wowote.

GEOFREY TENGENEZA (Afisa Habari - NIDA): Ni kweli kulikuwa na utaratibu wa kutoa Nakala ya Kitambulisho kwa wale ambao hawajapata Kadi lakini tulisitisha kutokana na matumizi mabaya ya Mfumo huoTuna taarifa pia kuna Watu wanawatapeli Wananchi kwa kuwaambia wanachapisha Nakala ya Kitambulisho, tunawaonya na tutawachukulia hatua kali.

MAGANGA: Mimi naomba kuuliza NIDA kwani watu wa Kigoma tuna shida gani? Maana kila tukitaka vitambulisho wanasema tukajaze Fomu za Uhamiaji ina maana huku Kigoma hakuna Watanzania wanaotakiwa kukaa huku.

MUSA: Nimejiandikisha tangu Mwaka 2016 hadi leo sijapata Kitambulisho nimepata Namba tu lakini Kadi nazungushwa tu sijapata, nawauliza NIDA changamoto nini ya kupatikana Vitambulisho?

DAIREKTA: Vijana wengi wamekuwa wakikosa kazi za pesa nyingi kwenye mitandao kutokana na kutokuwa na Kadi za Vitambulisho NIDA warudishe utaratibu wa kupata Nakala ya Kitambulisho ili kusaidia vijana wanaojihusisha na kazi za Kidigitali waweze kujiajiri

FAHAD: Nimepata fursa ya kusoma India lakini kuna changamoto kwenye Vitambulisho hakuna Anuani kwasababu huku vyuoni wanataka taarifa hizoPia, NIDA warudishe utaratibu wa Nakala za Vitambulisho vya Mtandaoni na waboreshe huduma kwa Wateja wanakuwa hawana majibu ya kueleweka tunapotaka msaada kwasisi tulio nje.

BABA MACHENGA: NIDA wamekuwa wakikosea majina ya Watu na wahusika wanapopeleka kwenye baadhi ya Taasisi wanapata changamoto, pia wanaporudi kwao NIDA wanawalipisha Fedha Sasa kwanini wasiweke mfumo unaoruhusu Watu kurekebisha Taarifa zao na kuweka Viambatisho wenyewe?

UFAFANUZI KUTOKA WA NIDA
GEOFREY TENGENEZA (Afisa Habari - NIDA): Sehemu ya majukumu ya NIDA ni kutambua na kusajili Watu wanaoishi Nchini, kutunza daftari la usajili wa watu, kutoa Vitambulisho kwa Wageni, Wazawa na kujenga utawala bora wa mamlakaShughuli rasmi za usajili zilianza Mwaka 2012 na mpaka sasa tuna Ofisi za Usajili 153 kwa Tanzania nzima.

Tumeanza kutoka katika matumizi ya ‘Card Reader’, NIDA tunazungumza na Taasisi nyingine ili kuwa na umoja wa kupata taarifa za Wateja au Mteja waoTumeanza hivyo katika Taasisi za Serikali ambapo wanatumia kanzidata ya NIDA kuweza kuwahudumia wateja wao, ili Mwananchi anapokwenda kupata huduma katika Taasisi husika anaenda na namba tu

Kitu muhimu ni Namba ya Utambulisho, kwenye Mataifa mengine wamefikia hatua ya kuwa hakuna haja ya kuwa na kitambulisho kwa maana lile ‘gamba’, namba pekee inatosha kumpatia Huduma na kumtambulisho

Kwa sasa hata kama itatokea unaambiwa upeleke Kitambulisho, bado muhimu ni Namba za Kitambulisho na si lile gamba, kutokuwa na kitambulisho haimaanishi haustahili kukosa Huduma.

Muda wa kupata Namba ya NIDA baada ya kujiandikisha huwa inategemea kulingana na matukio au uhalisia. Kuna muda kunakuwa na wimbi kubwa la watu wanaojiandikisha kwa wakati mmojaAidha, huwa tunafanya kazi na Taasisi nyingine kama UHAMIAJI ambao nao wanaweza kupitia ili kujiridhisha.

Kama hakuna matukio au mambo yanayosababisha msongamano, na taarifa za mhusika zikiwa hazina shida, Namba ya NIDA inatakiwa kupatikana ndani ya Siku 7 hadi 14Kama kukiwa na changamoto inaweza kuwa zaidi ya hapo.

Upande wa kupata kadi ya NIDA, baada ya kupitia mchakato wote ikiwemo kushirikisha Taasisi nyingine tunazofanyanazo kazi, Kukiwa hakuna matukio yenye msongamano kupata kadi ni ndani ya Wiki tatu hadi Mwezi mmoja, lakini kukiwa na changamoto inaweza kuwa zaidi ya hapo.

Tumesajili Watu milioni 24, Namba za Utambulisho ni Milioni 20 na Vitambulisho ambavyo vimechapishwa ni zaidi ya Milioni 17.

Tunakiri kuwa kulikuwa na changamoto ya kasi ya uchapaji wa vitambulisho, tulikuwa na changamoto ya mashine lakini kwa sasa tumepata mashine mpya na zimefungwa, kazi inaendelea.

Wakati wa #UVIKO19 tulipata changamoto katika uchapishaji wa kadi, uzalishaji ulisimama lakini baada ya UVIKO-19 mchakato ulirejeshwa na uzalishaji umeanza kwa kasi, tunavuka 50%.

Watanzania wote wenye Namba za NIDA hadi kufikia Januari 2024 kila Mwananchi mwenye namba husika atakuwa amepata Kitambulisho chake cha Taifa.

GEOFREY TENGENEZA (Afisa Habari - NIDA): Kama majina hayaendani na vyeti, nini kifanyike? Viambata muhimu wakati wa usajili ni pamoja na vyetiIkitokea inatakiwa abadilishe Majina au Taarifa zozote anatakiwa kuwasiliana na NIDA atasaidiwa lakini ni muhimu kuwa na nyaraka inayosapoti hayo mabadiliko.

Hakuna Rushwa wala Fedha ambayo Mwananchi anatakiwa kutoa ili apate kitambulisho anapofanya mchakato kwa mara ya kwanzaIkitokea anaenda kwa mara ya pili kama kufanya marekebisho, gharama zake ni Tsh. 20,000Ikitokea kuna Mtu anaombwa Rushwa ili afanikishe kupata Namba ya NIDA anatakiwa kutoa taarifa kwenye Mamlaka na Vyombo husika, hatua zitachukuliwa.

Kuna wakati Watu wanapenda njia za mkato kupata Huduma, inapotokea wanaangukia kwa vishoka na kuombwa Rushwa, baada ya hapo wanaona Watumishi wa NIDA wanaomba Rushwa.

Imewahi kutokea tukapata uthibitisho (wa rushwa) kwa Maafisa wetu wakati wa mchakato wa kupata Namba au Kadi ya NIDA na hatua zikachukuliwa.

DOREEN KAPWANI (Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - TAKUKURU): Tumewahi kupokea malalamiko katika Ofisi yetu ya Kinondoni kuhusu zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya NIDA

Pia, tulipata tuhuma kama hizo katika Ofisi ya TAKUKURU Manyara, hakukuwa na uthibitisho na tukarejesha mchakato kwa NIDA ili hatua zichukuliwe.

GEOFREY TENGENEZA (Afisa Habari - NIDA): Awali kulikuwa na utaratibu watoa huduma wengi walikuwa wanataka Kadi ya Kitambulisho lakini tumekaa na Taasisi nyingi na kuwaeleza kuwa wanatakiwa kutumia Namba ya Kitambulisho badala ya Kadi.

Bado tunaendelea kuwaelimisha baadhi ya Taasisi kuhusu hilo, na wale wanaotaka Kadi ni wale ambao hawajajiunga na Mfumo wetu wa Utambuzi NIDA.

Tunatoa rai kwa watoa huduma wengine ambao hawajajiunga na Mfumo wa NIDA wajitokeza ili kupata huduma hiyo Waje wasaini mikataba ili watumie Kanzidata ya Taifa.

Kuna mashahidi wakiwemo Taasisi za Benki wameona faida za kutumia Mfumo huo.
 
Thread Nzuri Sana Japo Ninacho Ila Watu Wengi Wana Number Tu Zaidi Wanaambulia Nenda, Rudi Ofisi Za NIDA Tanzania Nzima
 
Sijui kwann mkurugenzi wa Nida hatumbuliwii watu wanaangaikaa sanaa sanaa
 
Mimi siku moja nilienda ofisi za kata ya Wazo pale salasala ase nilikuta vitambulisho vingi sana kwenye mabox wenyew wanasema watu hawaji kuchukua sasa sijui hapo inakuaje.
 
Wanabidi kuhama kutoka Zama zao za zagiza Kubadilisha tu jina mnakuwa complicated hampo serious Nida
 
Kwa Nini vibali vinachelewa sanà kutoka?Kuna watu tumekosa namba Kwan vibali vinqchukua muda mrefu hadi mtu unajikatiq tamaa
 
Back
Top Bottom