Jenifa,
Mkuu nadhani hutakuwa unawatendea haki Watanzania ikiwa sababu unazotumia ni kile kinachomtokea Nape au viongozi wa CCM. Haiwezekanai watu wakimzomea mtu wako basi nawe unaanzisha zomea zomea bila sababu nyingine isipokuwa Uchama utafikiri tupo uwanja wa Taifa. Nape mara zote anakuja hapa kuzunguzia kazi yake, na amejikita ktk kuondoa nguvu ya Upinzani kiitikadi ktk kukisafisha chama..
Hii sii kazi ndogo hasa ikiwa chama kimefanya machafu mengi na Nape anakuwa bangusilo wa lawama za wananchi.. yeye kama mwanasiasa ni lazima azichukue hizi lawama kwa kufuta matusi hayo akilini na kuchukua mzizi wa fitna hizi kuwa kigezo cha kupambana na maadui wa chama ktk kusimamisha maadili..
Hivyo basi mashambilizi mengi ya wana JF kwa Nape yanatokana na uchafu wa viongozi wake ambao yeye amekuwa wakili kuwasafisha. Kazi ambayo sii rahisi kabisa isipokuwa unyenyekevu, kubali makosa na kuonyesha insanity ndio solution zaidi ya kurudisha matusi.. Na kama umemfuatilia Nape muda wote amekuwa wakili wa chama ktk kujivua Magamba akionyesha uwezekano wa kurudisha hadhi ya chama hata kama anazomewa..Pia ni jukumu lake kuonyesha mapungufu ya upande wa pili wa Upinzani ktk kuijenga imani ya watu dhidi ya vyama hivyo.
Mkuu wangu kama ndugu yako ameua ni lazima utakutana na watu watakao wazomea nyote watetezi wa mauaji hayo lakini itakuwa ujinga familia ya muuaji ikaanza nayo kuzomea watu kwa sababu tu wanazomewa wakitumia mifano ya - Mkuki kwa nguruwe!. Hii inaonyesha wazi wewe hufahamu uzito wa makosa yaliyotendeka na nachelea kusema kwamba wanaCCM wengi hawafahamu kiwango cha madhara ya utawala wa CCM kiuchumi isipokuwa wanatazama mavuno ya Ufisadi..
Dr. Slaa anakuja hapa kutujuza hali halisi ya kisiasa ndani ya chama chake na nje. Hakuna mahala popote Dr.Slaa amefikia kiwango cha kuzungumzia personal life ya Nape au viongozi wa CCM na wala sidhani kama kuna sehemu Nape kashambuliwa maisha yake binafsi na wanaJF..Hivyo jifunze sana kuwa mvumilivu kwa sababu Dr.Slaa yupo hapa kwa faida yetu sote bila kujali tofauti zetu za chama. Na kama sikosei maswali mengi yaliyowekwa hapa yametolewa na watu ambao sii wanachama wa CDM wala CCM..