Majibu ya Dr. Slaa kwa maswali ya watanzania, Julai 2011



Kasheshe,

..hizo ni propaganda za CCM tu.

...lakini mbona Nape,Sitta,Mwakyembe,na Kilango, wameandamana kule Mbeya na kwingineko?

..mbona wao hawaulizwi kama wanafanya military operations?

..hivi mmeona wapi operation za kijeshi zikafanyika mchana peupe?

NB:

..nawashauri CDM watembee na vitambaa vyeupe kwenye maandamano yao ili kuondoa dhana yoyote ile ya uvunjifu wa amani.


Vitambaa vyeupe havisaidii.mbona maandamano ya arusha walikuwa navyo lakini havikusaidia! Kabisa! 0 0
 
Umesahau juu ya conflict moja ya majukumu ya serikali na bunge.

Kuna huu mfuko wa maendeleo wa jimbo CDF . Binaffsi naona si sahihi sijui Dr slaa anasemaje. Pili sababu CDF io tayari basi Tumwombe Dr slaa awaagize wabunge wote wa CDM wawe wanachapisha matumizi ya pesa zile za majimbo yao kwenye magazeti kila baada ya miezi mitatu au sita. Hii itasaidia kuonyesha uwajibikaji wa wabunge wa CDM kwa wnanchi tofauti na wa CCM

Mkuu huo ushauri uliompa Dr Slaa sidhani kama ni sahihi. Kuwalazimisha wabunge wachapishe matumizi ya fedha ni sawa na kuhalalisha CDF ambayo imeanzihwa kimakosa. Ushauri wangu kwa serikali ni kufuta kabisa CDF. CDF tumenakili Uganda bila hata kufanya uchambuzi wa kutosha.

Kwa kifupi, CDF imekuwepo Kenya kuanzia 2003, Uganda tokea 2005 na Tanzania nafikiri 2008 kama sijakosea. CDF ilianzishwa Kenya kutokana na nguvu ya wabunge wa upinzani baada ya kuona kuwa majimbo yao yalikuwa hayapati fedha za maendeleo za kutosha toka serikalini kitu ambacho kilikuwa kinasabanisha maeneo hayo kuwa chini kimaendeleo na wananchi kukosa huduma muhimu. CDF ilianzishwa Uganda baada ya mikutano mingi kati ya Rais na wabunge kuwasaidia wabunge kutimiza ahadi walizowahaidi wapiga kura wao. Tofauti na Kenya, wabunge wa Uganda wao wenyewe walipokea cash ya sh milioni 10 za Uganda.

Rais Kikwete naye alisema CDF itaanzishwa kuwasadia wabunge kufanikisha projects za maendeleo na kupunguza kile alichokiita "daily nuisances" ambazo wabunge walikuwa wanakutana nazo majimboni mwao. Rais Kikwete alisema ni aibu kwa wapiga kura kuwataka wabunge wao wachangie kifedha kwenye shughuli za maendeleo wakati hawana fedha za kufanya hivyo. Hii ni pamoja na kuwa wakati wa kampeni wabunge wengi huwa wanatoa ahadi za kifedha.

Hata hivyo Rais Kikwete alisema wabunge wanaweza kusaidia majimbo yao kwa fedha zao kama kulipia watu ada za shule kama wakiombwa, lakini hili lisiwe jukumu lao. Badala yake wabunge waangalie zaidi kwenye masuala kama kuna shule na vifaa vya elimu vya kutosha majimboni mwao ili kuwawezesha watoto wapate elimu. Lakini ukiangalia wale wabunge wanaotetea posho wengi wao huwa wanasema kuwa hizo posho zinawasaidia sana wakiwepo majimboni mwao.

Ukiangalia model ya CDF ya Kenya ni tofauti na ya Uganda labda pia na ya Tanzania. CDF ya Kenya ilianzishwa kwa sheria iliyopitishwa na bunge, baada ya wabunge wa upinzani kulalamika bungeni kuwa majimbo yao yalikuwa yanaponjwa fedha za maendeleo kwa kuwa na wabunge wa vyama vya upinzani. CDF ya Uganda ni mazungumzo tuu kati ya Rais na wabunge fulani ambao nafikiri wapiga kura wao waliwajia juu kwa kushindwa kutimiza ahadi walizotoa. CDF ya Tanzania, Rais Kikwete ndio hivyo alisema itasaidia wabunge kuepukana na "daily nuisances" majimboni mwao.

Watu wanalalamika wabunge ku-manage CDF. Lakini wapo wanaosema kuwa suala zima la CDF is completely useless. Unless tu- abolish local governments, their role will be redundant. Ukiangalia nchi zilizoendelea, local government ndio iko responsible zaidi na local developments. Tatizo tulilonalo kwetu ni kutokuwepo kwa uhusiano wa kutosha kati ya ofisi ya mbunge jimboni na local governments. Sidhani kama CDF itasaidia, badala yake inaweza kuleta matatizo mengine. Utaenda kwa local government watakuambia nenda kwa mbunge wako anazo fedha, hasa pale kama mbunge mmoja huko Singida anaweza kugawa sh 50,000 sijui kwa walimu? (nisahihishe kama nimekosea).

Kuanzisha CDF ni sawa na kusema decentralisation (ambayo ni nzuri kulinganisha na ile ya Kenya) imeshidwa kuleta maendeleo kwa hiyo tutafute mbadala. Serikali kuu na wabunge inabidi wabakie kushughulikia masuala nyeti yanayoathiri system nzima kwa ujumla kupitia MKUKUTA au VISION 2025. Vinginevyo tutakuwa tuna "commercialise" siasa kwa kufanya wapiga kura wategemee misaada ya kifedha toka kwa wabunge kwa kuwapigia kura. CDF itafanya kura za wabunge ziwe zinauzwa.

Kwa nini serikali iwapatie wabunge fedha? Kwa nini wasipewe local governments au NGOs ambazo zinafanya kazi at the district level? Kama alivyosema mbunge mmoja huko Uganda suala la maendeleo ni la kitaifa, amabalo linabidi lipangwe na kutatuliwa kitaifa. Huwezi kutatua tatizo la mandeleo ya nchi kwa kuwapa baadhi ya individuals fedha kwa kutumia CDF. Hata kama ukimpa kila mbunge bilioni 10 hazitaleta maendeleo jimboni kwake.

Kazi za mbunge ni kupitisha sheria na ku-scrutunize matumizi ya serikali. Sasa kama mbunge ni mmoja wa watumiaji sijui ata-scrutunise kivipi matumizi. Kazi ya mbunge kwa mpiga kura sio kugawa fedha kwa wapiga kura wake. Kazi ya mbunge ni kusikiliza matatizo na maoni mpiga kura wake na kuya-channel kwenye vyombo husika.

Nim –quote pia Mzee Msekwa: "Inside his constituency, the MP is expected to carry out the normal duties of meeting and talking to constituents regularly...But again there have developed certain unscheduled expectations of treating their MP as a provider of financial assistance. This can and has created problems for those MPs who are unable to respond adequately to such expectations. For as the old adage goes, ‘members of parliament are men and women of high rank, [but] they have nothing in the bank!"

Alivyosema Msekwa ndivyo inavyotakiwa kuwa. Unfortunately, this is not the case. Wabunge wenyewe wana create unscheduled expectations majimboni kwa kutoa ahadi ambazo hawataweza kuzitimiza.

Sorry kwa post ndefu.
 
Mkuu huo ushauri uliompa Dr Slaa sidhani kama ni sahihi. Kuwalazimisha wabunge wachapishe matumizi ya fedha ni sawa na kuhalalisha CDF ambayo imeanzihwa kimakosa. Ushauri wangu kwa serikali ni kufuta kabisa CDF. CDF tumenakili Uganda bila hata kufanya uchambuzi wa kutosha. ........

Mkuu hata mimi nimeadika sikubalini na wabunge kuwa watendaji. na hili la CDF nalipinga Hilo tuko wote. Nilichomaanisha kipindi bado huo mfuko haujafutwa kisheria basi waonyeshe japo responsibility ya financial reporting. Financial reports za mikoa na halamashauria hazichapishwi wananchi wajue. Za CDF hawachapishi. Sasa ina maana gani


Tena Zitto kabwe kuna thread alisema atawasilisha hoja ya kuomba CDF ifutwe sijui kama chama chake kilimkubalia au imekuwaje. Inawezekana kwa kuwa hoja binafsi kaona hoja inaweza kukigawa chama .......sijui.
 
Mkuu huo ushauri uliompa Dr Slaa sidhani kama ni sahihi. Kuwalazimisha wabunge wachapishe matumizi ya fedha ni sawa na kuhalalisha CDF ambayo imeanzihwa kimakosa. Ushauri wangu kwa serikali ni kufuta kabisa CDF. CDF tumenakili Uganda bila hata kufanya uchambuzi wa kutosha. .

Yaan Dr Slaa akithubutu kuipinga hii CDCF nitamuona ni mnafiki kupindukia, nakumbuka mwaka 2009 wakati bunge linalazimisha kupitisha muswada huu, tulikwenda Dodoma na wanaharakati kutoka nchi nzima, tukiwa na matumaini na wabunge wa upinzani hasa Dr Slaa kutuunga mkono, lakini badala yake akishirikiana na wabunge wengine alitoa maneno ya kashfa sana kwa wanaharakati na kuutetea sana mfuko huu. yeye binafsi ni miongoni mwa wabunge walioshiriki katika kuupigania mfuko huu uanzishwe.(kumbu kumbu za tukio zima zipo policy forum I dare him kukanusha)
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Yaan Dr Slaa akithubutu kuipinga hii CDCF nitamuona ni mnafiki kupindukia, nakumbuka mwaka 2009 wakati bunge linalazimisha kupitisha muswada huu, tulikwenda Dodoma na wanaharakati kutoka nchi nzima, tukiwa na matumaini na wabunge wa upinzani hasa Dr Slaa kutuunga mkono, lakini badala yake akishirikiana na wabunge wengine alitoa maneno ya kashfa sana kwa wanaharakati na kuutetea sana mfuko huu. yeye binafsi ni miongoni mwa wabunge walioshiriki katika kuupigania mfuko huu uanzishwe.(kumbu kumbu za tukio zima zipo policy forum I dare him kukanusha)

Nakumbuka msuada ulivyowakilishwa bungeni Spika Makinda (wakati huo akiwa Naibu Spika) alisema waliokuwa wanapinga CDF walikuwa wana mislead the public. Kuwa wabunge wana majukumu mengi dhidi ya wapiga kura majimboni mwao na hawataweza kuyatimiza hayo majukumu bila kuwa na fedha. Mh Simbachawene (kama bado ni mbunge wa Kibakwe) alisema CDF itasaidia, pamoja na mambo mengine, wabunge kutembelea wapiga kura wao kujua matatizo na maoni yao. Hii inaonyesha wazi matumizi ya CDF yatakuwa ni yapi. Ndio maana nimesema ni inappropriate. Policy Forum walifanya utafiti juu ya faida na hasara za CDF Mombasa, Kenya. Mkuu unayo copy ya findings?
 
redio uhuru inamilikiwa na nani?

CCM, kama sijakosea, mhmm viwanja vya michezo vyote vya serikali walichukuwa kwa nguvu ila kasema, Sheria siunajuwa wao jamaa kwa kuvunja sheria ndio nambari one, hata rushwa sheria inakataza ila wao duh hadi yule mkubwa wao anatajwa yumo.
 
Maswala yote hayo sasa yanarudi mikononi mwa Kamati Kuu ambayo hivi Karibuni itatolea ufumbuzi swala la Madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chadema.
Nikushukuru tena kwa ufafanuzi ingawa yapo ambayo hayakujibiwa katika jibu la jumla. Kama kauli yako inavyosema ni vema kukatolewa maelezo ya kina kuhusu suala la Arusha. Yapo yanayoshtua kama kusikia madiwani wanachukua hatua au kuwasiliana na makao makuu bila uongozi wa wilaya au mkoa kuhusika. Ni mengi na endapo utakuwa na fursa tafadhali yatolee ufanunuzi maswali yaliyobaki kwa sababu impact yake inaweza kutoonekana sasa lakini ikawa na nguvu hasi siku za usoni.
1.Je lengo la maandamano ya Arusha na kwingineko limefikiwa?
2.Kama uongozi ulifahamu,kwanini wanachama na wapenzi hawakutaarifiwa hadi habari zilipoletwa na kiongozi wa CCM
3.Je,uongozi mzima wa Chadema katika ngazi ya wilaya na mkoa ulihusika katika majadiliano.
4.Kamati ya mabere iliundwa kuchunguza kitu gani uongozi wa taifa uliokuwa haukijui na matokeo ya uchunguzi huo yameleta tija ipi Chadema
5.Kama madiwani wanagomea maamuzi ya uongozi wa taifa, Chadema inajengwa kwa misingi(principles) au haiba(personalities)
6.Nini unadhani itakuwa uungwaji mkono katika base ya chama siku za usoni kutokana na jinsi suala hili lilivyoshughulikiwa(handled in general)
7.Unawaambia nini wanachama na wapenzi wa Chadema kuhusu hatima ya sakata hili baada ya uchunguzi na malumbano yanayoendelea
8.Je mapungufu(kama yapo) ya suala hili yametokana na nini

Nichangie pia kuhusu hoja ya mkuu EMT na wengine kuhusu CDF. Kadri nielewavyo mbunge ni mjumbe katika vikao vya maamuzi vya jimbo lake, halmashauri na vikao ngazi ya mkoa.
Mikoa na Halmashauri zote zinawajibika katika kukusanya mapato na kupanga matumizi ya sehemu husika kulingana na mahitaji.
Halmashauri zinafaidika na ruzuku kutoka serikali kuu kuendesha shughuli zao.

Katika ngazi za mkoa na wilaya kuna RC,DC,RAO,DAO,madiwani na watawala wengine ambao upana wa kazi zao unahushisha majimbo yenye wabunge.

Kwa muktadha huo, ni jambo gani ambalo mbunge anadhani uongozi wa Halmashauri, willaya hadi mkoa umeshindwa kutekeleza hadi yeye apewe pesa mkononi kwenda kuhamasisha maendeleo ya jimbo peke yake?

Je kuingia kwake kwenye vikao vya maamuzi na mipango ngazi ya mkoa na wilaya na halmashauri kuna maana gani endapo haamini kuwa maamuzi ya vikao hivyo ni kwa faida ya jimbo lake pia.
Kwa urahisi na ufupi, hela za CDF zinafanya nini zaidi ya kile kilichoshindikana na halmashauri,wilaya au mkoa??

Pili, kama mheshimiwa waziri mkuu alisema '...watu wapo nje wanashida inabidi uwape pesa' akimaanisha kuwa pesa za CDF ni pamoja na kutatua matatizo ya haraka ya wananchi.Swali ni kuwa itawezekanaje kwa CAG kufanya ukaguzi wa matumizi ya pesa hizo ambazo zingine zinagawiwa kama msaada bila utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na stakabadhi?
 
Nikushukuru tena kwa ufafanuzi ingawa yapo ambayo hayakujibiwa katika jibu la jumla. Kama kauli yako inavyosema ni vema kukatolewa maelezo ya kina kuhusu suala la Arusha. Yapo yanayoshtua kama kusikia madiwani wanachukua hatua au kuwasiliana na makao makuu bila uongozi wa wilaya au mkoa kuhusika. Ni mengi na endapo utakuwa na fursa tafadhali yatolee ufanunuzi maswali yaliyobaki kwa sababu impact yake inaweza kutoonekana sasa lakini ikawa na nguvu hasi siku za usoni.

Nichangie pia kuhusu hoja ya mkuu EMT na wengine kuhusu CDF. Kadri nielewavyo mbunge ni mjumbe katika vikao vya maamuzi vya jimbo lake, halmashauri na vikao ngazi ya mkoa.
Mikoa na Halmashauri zote zinawajibika katika kukusanya mapato na kupanga matumizi ya sehemu husika kulingana na mahitaji.
Halmashauri zinafaidika na ruzuku kutoka serikali kuu kuendesha shughuli zao.

Katika ngazi za mkoa na wilaya kuna RC,DC,RAO,DAO,madiwani na watawala wengine ambao upana wa kazi zao unahushisha majimbo yenye wabunge.

Kwa muktadha huo, ni jambo gani ambalo mbunge anadhani uongozi wa Halmashauri, willaya hadi mkoa umeshindwa kutekeleza hadi yeye apewe pesa mkononi kwenda kuhamasisha maendeleo ya jimbo peke yake?

Je kuingia kwake kwenye vikao vya maamuzi na mipango ngazi ya mkoa na wilaya na halmashauri kuna maana gani endapo haamini kuwa maamuzi ya vikao hivyo ni kwa faida ya jimbo lake pia.
Kwa urahisi na ufupi, hela za CDF zinafanya nini zaidi ya kile kilichoshindikana na halmashauri,wilaya au mkoa??

Pili, kama mheshimiwa waziri mkuu alisema '...watu wapo nje wanashida inabidi uwape pesa' akimaanisha kuwa pesa za CDF ni pamoja na kutatua matatizo ya haraka ya wananchi.Swali ni kuwa itawezekanaje kwa CAG kufanya ukaguzi wa matumizi ya pesa hizo ambazo zingine zinagawiwa kama msaada bila utaratibu wa kisheria ikiwa ni pamoja na stakabadhi?

Ndugu yangu Nguruvu3 nakubaliana kabisa na hoja yako. Kuna wakati waziri mkuu alikuwa akijibu hoja ya kuondolewa kwa 'sitting allowance' kwa wabunge.

Lazima nikiri wazi kuwa nilishtushwa sana na kauli ya anayejiita 'mtoto wa mkulima' aliposema kwamba wabunge wanazongwa mara kwa mara na wapiga kura wao wakiwa na shida mbalimbali ambazo baadhi zinaweza kutatuliwa papo kwa papo kwa kuwapatia fedha. Hii ina maana kuwa hata fedha za maendeleo ya jimbo ndivyo wanavyotarajia kutumia.

Swali langu ni kama ulivyouliza kwamba je, matumizi ya hovyo kiasi hicho yanawezaje kukaguliwa! Hakuna payment voucher, hakuna risiti au kithibitisho chochote cha mpokeaji hela, hakuna namna yoyote ya ufuatiliaji wa kuona kama mpokeaji fedha ametumia kama ilivyokusudiwa na kutimiza malengo, n.k. Kwa ujumla, fedha ya umma lazima iwe na mfumo fulani unazingatia kanuni ya uwajibikaji (accountability).

Vinginevyo, huo utakuwa ni ufisadi kama ulivyo wa Meremeta, Kagoda, Richmond, n.k.
 
Picha nzuri ni kwa Dr. Slaa kutokugombea jimbo la Igunga kwani baada ya uchaguzi mkuu 2010 jukumu kubwa ni kukiimarisha chama kwa ajili ya 2015 na sio kuingia Bungeni ili iweje?
 
Ahsante Dr Slaa, nina maswali machache yanayohusu suala la Arusha. Awali ya yote naomba nijenge hoja ili maswali yangu madogo na rahisi yaeleweke.

Sakata la Arusha lilikuwa katika msingi wa kupinga taratibu za uchaguzi wa meya zilizokiukwa kwa mujibu wa madai ya Chadema. Tuliona viongozi wakipigwa kwa mabomu, watu kupoteza maisha na wengine kubaki na vilema. Ni wazi suala hili lilichakua sura ya kitaifa kama si kimataifa kama lilivyoripotiwa na vyombo mbali mbali duniani. Ghafla tukasikia makubaliano ya madiwani Arusha(na muafaka ni jambo zuri siku zote). Ilichukua zaidi ya wiki mbili uongozi wa taifa kutolea ufafanuzi licha ya tambo na kejeli zilizokuwa zinatolewa na washirika wa muafaka.

Maswali
1.Je lengo la maandamano ya Arusha na kwingineko limefikiwa?
2.Je, uongozi taifa wenye dhamana tangu mwanzo ulifahamu kuwepo majadiliano baina ya madiwani?
3.Iweje suala zito kama hili liachiwe madiwani ikizingatiwa gharama kubwa iliyolipwa na wanachama
4.Kama uongozi ulifahamu,kwanini wanachama na wapenzi hawakutaarifiwa hadi habari zilipoletwa na kiongozi wa CCM
5.Je,uongozi mzima wa Chadema katika ngazi ya wilaya na mkoa ulihusika katika majadiliano.
6.Kamati ya mabere iliundwa kuchunguza kitu gani uongozi wa taifa uliokuwa haukijui na matokeo ya uchunguzi huo yameleta tija ipi Chadema
7.Kama madiwani wanagomea maamuzi ya uongozi wa taifa, Chadema inajengwa kwa misingi(principles) au haiba(personalities)
8.Nini unadhani itakuwa uungwaji mkono katika base ya chama siku za usoni kutokana na jinsi suala hili lilivyoshughulikiwa(handled in general)
9.Unawaambia nini wanachama na wapenzi wa Chadema kuhusu hatima ya sakata hili baada ya uchunguzi na malumbano yanayoendelea
10.Je mapungufu(kama yapo) ya suala hili yametokana na nini

Ahsante

Nguruvi
Nguluvi kwa taarifa yako, CDM tayari walishatolea tamko kuhusu muafaka wa Arusha kwamba- NI MUAFAKA BATILI- taratibu zinafuatwa kuchukuliwa kulingana na Katiba /ilani ya chadema.
 
Kama Katibu Mkuu wa magwanda, inabidi awe na busara zaidi yenu, capacity ya mtu hujulikana katika maswali kama hayo ambayo nyinyi mnayaona yanawatatiza, hivi, hawa viongozi wanawaongoza watu wa aina fulani tu katika tabaka za jamii?

Na kama hatoyajibu ntajuwa kuwa na yeye "capacity" yake si ya uongozi wa Taifa, msishabikie maswali sio yenu, as Katibu Mkuu anatakiwa awe makini na sio mwenye papara kama nyie. Kaeni kimya mumuwache Slaa ajibu au akatae, msimsemee tafadhali.
Tuna Imani na DR. Slaa katika kujenga na kujibu hoja zinazoelekezwa kwake ama chama. Hata wana JF humu jamvini ambao ni wafuasi na wapenzi wa CDM huja na majibu sahihi na yenye kuridhisha wana JF na Watanzania kwa ujumla. Ni tofauti kabisa na JK anavyokuwa anadanganywa na watendaji wake kisha anatoa majibu ya uongo kama Mawaziri na Manaibu wao wanavyolidanganya Bunge. Chadema na Viongozi wake wake makini.
 
Nimesoma maoni ya watu na Majibu ya Dr Slaa, nimefarijika kwamba Tanzania ina hazina kubwa ya watu wanaoweza kuikomboa hii nchi kiuchumi lakini wamewekwa pembeni na kikundi kidogo cha watu.

Nakushukuru Dr kwa majibu mazuri na yanayoeleweka, na wachangiaji wengi pia wamechangia vizuri sana, kuwa hapa JF ni sawa na kuwa Shule tena Shule kubwa.
 
Mwanzoni nilitoa wazo kuwa hayo maswali yanawahusu walio madarakani na sio walio nje ya madaraka,linalomhusu Dr ni hilo la madiwani na amelijibu vyema yeye kama katibu mkuu,chama tawala na serikali hawana majibu ndo maana wako kimya tu!
 
Heshima kwako Ndugu Slaa!

Naomba nimpate msimamo wa kisera wa chama juu ya suala la uraia wa nchi mbili 'dual citizenship'.
Pia faida na hasara ambazo suala hilo linaweza kuliletea taifa letu.

Asante.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom