BoT acheni majibu mepesi kwenye maswali magumu

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
BoT ACHENI MAJIBU MEPESI KWENYE MASWALI MAGUMU

BoT acheni majibu mepesi kwenye maswali magumu hasa hili la upungufu wa dola kwenye mzunguko wa uchumi, Ni kweli ukosefu wa dola ni janga la kidunia lakin kama wataalamu wa uchumi tuliowapa nafasi ya kutusaidia katika maswala yote ya fedha na uchumi mnapaswa kuja na masuluhisho ya kutoka hapa tulipo kama wataalam wa fedha na uchumi na sio kauli ya kutaka watu kutoa dolla mafichoni in fact ni hatua za kiuchumi zinapaswa kutumika ili kupelekea watu kutoa dola ndani na kuzirudisha kwenye mzunguko kuliko kutoa kauli zisizo tekelezeka na zenye kuongeza sintofahamu.

Kwa uhalisia uliopo sera za BoT juu ya dolla sio tu kwamba zinachochea watu kuficha dola lakin zinachochea ukuaji wa biashara haramu ya dola(Black forex market) kwa mfano utaratibu wa BoT kwa sasa ni maduka yote ya kubadilishia dola na taasisi za fedha kutokuvuka kiwango cha kununua au kuuza dola cha 2,500-2,550 wakat ukienda Kariakoo au mipakan dola inauzwa na kununuliwa kwa 2,700-2,800 kwa hali hii nani atauza dola kwenye mifumo ya fedha? lazima ipungue kwenye mifumo rasmi ya fedha kwa sababu hakuna atakae kubali kuuzia Bank dola kwa 2,500 wakat mtaani inanunulika kwa bei ya juu zaid, ni lazima kuweka utaratibu utakaopelekea watu kuziuzia taasisi za fedha dola na sio kutoa tamko tu, hii ni kanuni ya kawaida kabisa ya fedha.

Nilitegemea kuona BoT wanakuja na masuluhisho zaid mfano wastani kwa siku wanatoa hadi $5m kwenye mzunguko ambayo inasaidia uagizwaji wa mafuta, hii inasaidia kama asilimia 25% ya uhitaj wa soko hivyo wakiongeza wigo kwenye sekta zingine muhimu kama Afya, Kilimo n.k na kufikia asilimia 60-70 ya uhitaj wa soko ingepelekea bank kuwa na uwezo wa kuuza dola zaid Sokoni na kupunguza matumaini ya walioficha dola na wanaouza kwenye soko lisilo rasmi kukosa soko na kulazimika kuzirudisha kwenye mfumo rasmi.

Pia ipo njia ya udhibiti wa bidhaa tunazoagiza nje hasa kwa zile zinazozalishwa Nchini, Kutumia Nchi rafiki kuona uwezekano wa kufanya biashara kwa kutumia fedha yetu pamoja na fedha ya Taifa husika nk…

by Peter Msaki-Mjumbe wa Halmashaur Kuu Mkoa-Lindi

View attachment 2763709
 
Kaka nakubaliana na wewe coz sijui chochote kweny mambo ya fedha ila naulz tu,hauoni tukipandisha kiwango cha kuuza dollar pesa yetu inazidi kufa?na pia goverment lzm mda mwengne awe controler ktk uchumi inasadia kupunguza hz variation ambzo wafanya biashara wanaziweka.
 
Tunaporuhusu soko liwe total huru mfn tukubali bei ya dola iwe 2600 tunaiua shiling pia,mfumuko wa bei kwa bidhaa zitapanda zaid huo mkate hautanunulika,.nazani acha serikali ifanye lake wameshafanya tafiti.
 
Kuwaambia watu warudishe dollar sio suluhisho, BOT inatakiwa kuweka mazingira rafiki kwa kuwezesha watu kufanya miamala kwa uhalali, kwa sasa watu wako mipakani wanafanya biashara ya dollar kama kawaida na inahatarisha uchuni ya taifa, sasa kutoallow dollar kutumika ni kuupeleka uchumi mrama
 
Back
Top Bottom