Majibu ya Dr. Slaa kwa maswali ya watanzania, Julai 2011

Kama Katibu Mkuu wa magwanda, inabidi awe na busara zaidi yenu, capacity ya mtu hujulikana katika maswali kama hayo ambayo nyinyi mnayaona yanawatatiza, hivi, hawa viongozi wanawaongoza watu wa aina fulani tu katika tabaka za jamii?

Na kama hatoyajibu ntajuwa kuwa na yeye "capacity" yake si ya uongozi wa Taifa, msishabikie maswali sio yenu, as Katibu Mkuu anatakiwa awe makini na sio mwenye papara kama nyie. Kaeni kimya mumuwache Slaa ajibu au akatae, msimsemee tafadhali.

Mbona hueleweki? Msingi wa hoja yako nini?
 
njia sahihi ni ipi?

1. Giza totoro na majibu rais ya mawaziri na rais - waambieni wabunge wenu watumie nafasi yao bungeni kuihoji serilkali, tena wanaweza kumuuliza Pinda hata alhamis ijayo( kama livyofanya Mbowe kama wiki mbili zilizopita)

2, Bahasha la Jairo - Hata sioni kwa nini unaliuliza kwa sababu hatua za kumsimamisha na CAG kuchunguza tuhuma zake zimetangazwa katika vyombo vyote vya afya, lakini kama bado unahitaji kujua kuhusu hili bahasha si vibaya pia kumuuliza waziri mkuu au kuihoji serikli kwa kupitia kwa wawakilishi wenu hungeni.

3. Kujivua gamba la Rostam - Hili linajibiwa kila uchao na CCM lakini pia muulize Nape akija hapa au kama unaharaka sana, mpigie mzee Mukama

4. Sakata la Madiwani Arusha - Hili kama unataka majibu ya ukweli, unaweza tu kwenda kwenye ofisi ya mkurugenzi pale arusha au kwa mabosi wake hapa TAMISEMI, lakini kama unataka majibu ya kisiasa muulize Slaa, yeye hana shughuli ya kumbana hivyo huwa anshinda sana hapa kijiweni, lakini pia kama unataka uongo muulize Nape akija.

5. Umasikini unaozidi kukua na gharama za maisha - Leo saa tatu kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV alijibu Beno Ndulu, unaweza pia kumuuliza wewe au kutumia wawakilishi wako bungeni wawaulize watawala.

N.B

Maswali yasipoelekezwa mahali husika mara nyingi yanaleta majibu yasiyo sahihi.
 
Nguluvi kwa taarifa yako, CDM tayari walishatolea tamko kuhusu muafaka wa Arusha kwamba- NI MUAFAKA BATILI- taratibu zinafuatwa kuchukuliwa kulingana na Katiba /ilani ya chadema.
Seal6 tamko lilitolewa na tumeliona sote. Hili jambo ni zito zaidi ya tamko na lina kitu kinaitwa political ramification. Maswali niliyomuliza Dr Salaa hakuna hata moja lililohusu tamko kama umeyarejea kwa uangalifu.

Kuna mambo mawili yanayojitokeza kwenye suala ili.
1. Muafaka:
Na hapo nimeuliza ulifikiwa katika mazingira gani ambayo yanaleta utata kati ya uongozi taifa, madiwani, mbunge na wanachama.
Je uongozi ulifahamu muafaka na ilikuwaje jambo hili lenye sura kubwa hadi kuvuka mipaka liachiwe mamlaka kama ya udiwani?
Je, chama katika ngazi ya wilaya na mkoa vilihusishwa na kwanini hakuna hatua dhidi yao. Je uongozi katika ngazi hizo upo na unawajibika?
Je, lengo la kuhamisaisha upingaji matokeo nchi nzima lilifikiwa? endapo maana nzima ilikuwa kugawana vyeo vya umeya na unaibu?

Yatokanayo na muafaka.
a)Kwanini taarifa hazikutolewa na Chadema na badala yake CCM wakatangaza. Na ilikuwaje uongozi wa taifa ukachukua zaidi ya wiki mbili tena katika shinikizo la vyombo vya habari na blogs na kutoa msimamo wa jambo hili.
b)Kwavile uongozi wa taifa ulijua jambo hili kamati ya mabere Marando ilienda kuchunguza nini na kwanini mkoa au wilaya hazikuhusishwa?
c)Kama chama kitaifa kinatofautiana na msimamo wa madiwani, je uongozi ni principles au personalities
d)Katika hali ya mkanganyiko kama huu tutarajie nini kuhusu uungwajwi wa misimamo ya Chadema siku zijazo?
e)Nini mapungufu yaliyoleta hali hii ya sintofahamu.

Nimelazimika kuyarejea na kufafanua maswali hayo ili nieleweke. Kama tamko peke yake linaweza kujibu maswali hayo basi nashukuru, vinginevyo suala hili litaleta sintofahamu katika wakati usiotakiwa na uisotarajiwa.

Seal, medani ya kisiasa inataka jambo liangaliwe kwa mtazamo mpana wenye suluhu ya kudumu na si kauli moja au mbili.
Kwa kuangalia haraka tu washiriki wa muafaka wamelitumia kama silaha dhidi ya misimamo ya Chadema na kukionyesha kama chama cha vurugu na kisichojua kinasimamia nini.

Kwa upande mwingine wanachama,wapenzi na mashabiki wametunduwaa kwa kutojua endapo suala lilikuwa kutafuta nafasi ya uongozi wa mtu mmoja au wawili. Zaidi ya hapo Chadema itawezaje kusimama kama chama kama hakina mizizi ya kuaminika katika wilaya na mkoa.
Na je taratibu za nidhamu zinazingatia mgawanyo wa madaraka.

Hayo ni mawazo yangu huru binafsi na yana lengo zuri tu la kuimarisha demokrasia na ustawi wa siasa katika taifa. Hayalengi kutoa uetetezi au kubana chama chochote zaidi ya kujenga na kuimarisha. Siasa inahitaji fikra pevu na si kauli moja au mbili watu wanazopenda kuzisikia.
 
Wakuu ktk swala la Madiwani nadhani tumekwisha limaliza la muhimu zaidi labda tumuulize Dr.Slaa hatua zitakazo chukuliwa na chama. Dr.Slaa ameeleza vizuri sana na hakika sijui kama balozi wetu UN akiitwa na rais na kuambiwa ajiuzuru kutokana na Tanzania kutokubaliana na maamuzi fulani basi balozi huyo ana haki ya kutumia maamuzi yake binafsi kama balozi.

Nitazidi kusisitiza kwamba diwani anawakilisha sera za chama na anafungwa na kanuni ktk utumishi wake kwa wananchi..Ni mtumishi wenu lakini kuna kanuni zinazoambatana na mamlaka alopewa na analazimika kuzifuata hata kama msimamo wa chama unatofautiana na maamuzi yake binafsi. Hawa madiwani wanapoteza nafasi zao ktk Halmashauri, hawapotezi wala hawalazimiki kupoteza Udiwani wao..

Nitawakumbusheni maneno ya Al Pacino ktk Godfather akimwambia kaka yake Fred - Never side with anyone against your family!.. haya maneno yana busara kubwa juu ya ngazi zote za kimaisha na hakika mnatakiwa kujifunza...
 
Serikali haijibu vichochoroni, tumia njia sahihi utayapata majibu.

Na wewe unafanya nini huku "vichochoroni"? Hawajibu "vichochoroni" lakini ikifika wakati wa kuomba kura, utawakuta wamejazana humo. Kwa kweli wewe unaonekana bado uko karne ya 19. Wakati akina Obama na Kagame wanatumia social media kuwasiliana na wananchi, wewe bado unaangalia traditional ways ya watawala kuwasiliana na watawaliwa. Grow up.
 
Seal6 tamko lilitolewa na tumeliona sote. Hili jambo ni zito zaidi ya tamko na lina kitu kinaitwa political ramification. Maswali niliyomuliza Dr Salaa hakuna hata moja lililohusu tamko kama umeyarejea kwa uangalifu.

Kuna mambo mawili yanayojitokeza kwenye suala ili.
1. Muafaka:
Na hapo nimeuliza ulifikiwa katika mazingira gani ambayo yanaleta utata kati ya uongozi taifa, madiwani, mbunge na wanachama.
Je uongozi ulifahamu muafaka na ilikuwaje jambo hili lenye sura kubwa hadi kuvuka mipaka liachiwe mamlaka kama ya udiwani?
Je, chama katika ngazi ya wilaya na mkoa vilihusishwa na kwanini hakuna hatua dhidi yao. Je uongozi katika ngazi hizo upo na unawajibika?
Je, lengo la kuhamisaisha upingaji matokeo nchi nzima lilifikiwa? endapo maana nzima ilikuwa kugawana vyeo vya umeya na unaibu?

Yatokanayo na muafaka.
a)Kwanini taarifa hazikutolewa na Chadema na badala yake CCM wakatangaza. Na ilikuwaje uongozi wa taifa ukachukua zaidi ya wiki mbili tena katika shinikizo la vyombo vya habari na blogs na kutoa msimamo wa jambo hili.
b)Kwavile uongozi wa taifa ulijua jambo hili kamati ya mabere Marando ilienda kuchunguza nini na kwanini mkoa au wilaya hazikuhusishwa?
c)Kama chama kitaifa kinatofautiana na msimamo wa madiwani, je uongozi ni principles au personalities
d)Katika hali ya mkanganyiko kama huu tutarajie nini kuhusu uungwajwi wa misimamo ya Chadema siku zijazo?
e)Nini mapungufu yaliyoleta hali hii ya sintofahamu.

Nimelazimika kuyarejea na kufafanua maswali hayo ili nieleweke. Kama tamko peke yake linaweza kujibu maswali hayo basi nashukuru, vinginevyo suala hili litaleta sintofahamu katika wakati usiotakiwa na uisotarajiwa.

Seal, medani ya kisiasa inataka jambo liangaliwe kwa mtazamo mpana wenye suluhu ya kudumu na si kauli moja au mbili.
Kwa kuangalia haraka tu washiriki wa muafaka wamelitumia kama silaha dhidi ya misimamo ya Chadema na kukionyesha kama chama cha vurugu na kisichojua kinasimamia nini.

Kwa upande mwingine wanachama,wapenzi na mashabiki wametunduwaa kwa kutojua endapo suala lilikuwa kutafuta nafasi ya uongozi wa mtu mmoja au wawili. Zaidi ya hapo Chadema itawezaje kusimama kama chama kama hakina mizizi ya kuaminika katika wilaya na mkoa.
Na je taratibu za nidhamu zinazingatia mgawanyo wa madaraka.

Hayo ni mawazo yangu huru binafsi na yana lengo zuri tu la kuimarisha demokrasia na ustawi wa siasa katika taifa. Hayalengi kutoa uetetezi au kubana chama chochote zaidi ya kujenga na kuimarisha. Siasa inahitaji fikra pevu na si kauli moja au mbili watu wanazopenda kuzisikia.
Nakufagilia mkuu Nguruvi3 kwa uwezo wako wa kuchambua maswali ili yapate majibu yaliyo sahihi.
Lakini kwa mambo yalivyo sioni kama majibu yatapatikana hapa ukizingatia kuwa CDM bado ni chama kichanga sana, tena sana.Na hii misuko suko itabainisha uchanga huo.
People are expecting too much from CDM, I am afraid it will not deliver as expected.
Hata hivyo this is what great thinking is all about.
 
Nakufagilia mkuu Nguruvi3 kwa uwezo wako wa kuchambua maswali ili yapate majibu yaliyo sahihi.
Lakini kwa mambo yalivyo sioni kama majibu yatapatikana hapa ukizingatia kuwa CDM bado ni chama kichanga sana, tena sana. Na hii misuko suko itabainisha uchanga huo.
People are expecting too much from CDM, I am afraid it will not deliver as expected.
Hata hivyo this is what great thinking is all about.

Mkuu samahani, naomba unieleweshe kidogo, uchanga wa chama unapimwa kwa vigezo gani? umri? au idadi ya wanachama? au kitu gani ili chama kiitwe kichanga hadi kushindwa kutoa majibu.

Kutokana na jinsi ulivyo'comments unamaanisha CCM ni chama kikongwe, mbona hawajitokezi walau kujibu maswali ya msingi kwa wananchi? au na CCM ni chama kichanga?
 
mkuu samahani, naomba unieleweshe kidogo, uchanga wa chama unapimwa kwa vigezo gani? umri? au idadi ya wanachama? au kitu gani ili chama kiitwe kichanga hadi kushindwa kutoa majibu.
kutokana na jinsi ulivyo'comments unamaanisha CCM ni chama kikongwe, mbona hawajitokezi walau kujibu maswali ya msingi kwa wananchi? au na CCM ni chama kichanga?

Ugwiji wa chama ni pamoja na uwezo na ustadi wa kujinasua kutoka kwenye matatizo ya kisiasa na bado chama kikawa intact.
Mimi sidhani kama CDM imefikia hali hiyo kwa sasa.

Wenzao CCM wana gamba gumu sana ambalo linatokana na uzoefu wa miaka mingi.
Migogoro inayoinandama CDM sasa hivi ni midogo sana lakini inaweza haribu taswira na mategeo ya wanachama wake.

Pamoja na positive impact ya CDM kwenye siasa za Tanzania kwa leo, ikiwa ni kupinga ufisadi, matumizi mabaya ya mali za umma na kucheck/balance maadili ya viongozi kisiasa, haya yote ni katika "kushambulia" siasa za nchini.

Hata hivyo kimuundo bado CDM haina ubavu mkubwa na base yake ni shaky.Inabidi ijitazame kujiimarisha kimuundo na misingi yake ili kipate nguvu zaidi ya "kushambulia" kisiasa.

Naomba nieleweke kuwa mashambulizi haya ya kisiasa ni chanya na yanakisaidia sana hata chama tawala kujisahihisha pale ambapo yenyewe vile vile kwa vikao vyake inashindwa kujinasua.
 
Back
Top Bottom